Wapi Jeikei wa ukweli,dar es salaam na kibunango kuchangia mada hii adhimu ???
Tanzania, on Africa's east coast, is one of the poorest states in the world, formerly controlled in turn by Arab slavers, German colonists and the British.At the time of the radar deal, life expectancy was 45.
Tanzania was forced to apply for debt relief from the west and was heavily dependent on aid. It is ravaged by HIV/Aids and its GDP per head is just $723 (£465).
President Benjamin Mkapa, whose regime did the deal, was succeeded in 2004 by his political colleague Jakaya Kikwete.
Tanzania, which has no air force, bought the military air defence radar from BAE in 2001 for £28m.
It was claimed the Commander system, which was portable and festooned with anti-jamming devices, could also be used for civilian air traffic control.
The country borrowed the cost from Barclays, adding to its debt burden. Both the World Bank and the International Civil Aviation Organisation called the purchase unnecessary and overpriced.
In London, the then development secretary, Clare Short, temporarily blocked aid payments in protest. "It stank," she now says of the sale.
She urged an export licence be withheld, but was overruled by Tony Blair himself. Robin Cook, then foreign secretary, recorded bitterly in his diary that Dick Evans [of BAE] seemed to have "the key to the garden door of No 10 [Downing St]".
In January 2007 the Guardian disclosed that BAE had used an offshore front company, Red Diamond, to secretly pay £8.4m, 30% of the radar's ostensible price, into a Swiss account.
The account was controlled by Tanzanian middleman Sailesh Vithlani. His "consultancy" agreement was, it is alleged, formally signed off in London by Evans.
Nilichosema ni kwamba Rais hataki kuruhusu uchunguzi wa maofisa waandamizi wa serikali au mtu yeyote yule kufanywa kwa kuegemea katika minongono au ushahidi dhaifu, kwa sababu kwa kufanya hivyo, serikali inaweza kuwa katika hatari ya kulipa fidia kubwa kama watuhumiwa watashinda kesi mahakamani, alidai Dk. Hoseah katika taarifa yake jana.
TAARIFA zilizovuja za mtandao wa Wikileaks, ambazo zilizotoka kwa Serikali ya Marekani, zimemgusa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (Takukuru), Dk. Edward Hoseah, na kwa haraka, amekanusha kuwa Rais Jakaya Kikwete amekuwa ni kikwazo cha utendaji wa taasisi hiyo, kama alivyonukuliwa humo.
Dk. Hoseah, anadai katika taarifa za mtandao huo zilizoripotiwa jana na gazeti la The Guardian la Uingereza kueleza kuwa Rais Kikwete alikuwa anakwamisha kuchunguzwa kwa vigogo wa serikali wanaotuhumiwa kwa vitendo vya rushwa, na pia madai kuwa anahofia maisha yake kama Mkuu wa Takukuru.
Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana, Dk. Hoseah anakiri kukutana na ofisa wa Marekani ofisini kwake Julai 2007, lakini katika mazungumzo yake, anakanusha kuwa hakuna mahali popote alipoeleza kuwa Rais Kikwete alikuwa hataki sheria ichukue mkondo wake katika kuwachunguza vigogo wanaotuhumiwa kwa rushwa.
Nilichosema ni kwamba Rais hataki kuruhusu uchunguzi wa maofisa waandamizi wa serikali au mtu yeyote yule kufanywa kwa kuegemea katika minongono au ushahidi dhaifu, kwa sababu kwa kufanya hivyo, serikali inaweza kuwa katika hatari ya kulipa fidia kubwa kama watuhumiwa watashinda kesi mahakamani, alidai Dk. Hoseah katika taarifa yake jana.
Kuhusu madai ya hofu ya maisha yake, alisema anakumbuka kuulizwa na ofisa huyo kama anahofia uhai wake au la, akiwa ni Mkuu wa Takukuru, na kwamba jibu lake lilikuwa rahisi, ndio, wakati unaposhughulika na vigogo au matajiri, ni lazima uwe mwangalifu na tahadhari na maisha yako.
Lakini hakuna mahali popote nilipotamka kuwa nina mpango wa kukimbia nchi kwa sababu maisha yangu yalikuwa hatarini. Ni jambo la kushangaza kwa mara nyingine, Ofisa huyo wa Ubalozi wa Marekani amenikariri kinyume na ukweli na sijui nia yake hasa ilikuwa nini.
Dk. Hoseah alisema kupokea vitisho ni sehemu ya kazi yake kwa sababu anawachunguza watu matajiri na wenye nguvu, lakini kwa kuwa kila kitu kinafanyika kulingana na sheria iliyopitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hakuna cha kuhofia sana kwa sababu kila kitu kiko katika sheria.
Aliihakikishia jamii kwamba ingawa kazi yao ni ngumu, wataendelea na dhamira yao ya kupambana na rushwa katika ngazi zote kwa kushirikiana na wadau wote nchini.
Tunaamini kwa pamoja tutashinda vita hii, lakini tukigawanyika, itakuwa kazi ngumu kufikia dhamira yetu.
to make things better, we need local wikileaks as well