WikiLeaks: Tanzania official fears for his life!

Anachosema Dr. Hoseah ni kwamba for some reason, ofisa wa ubalozi wa Marekani anamsingizia. Huyo ofisa atakuwa na interest gani ya kuwadanganya viongozi wake kule Washington na kwenye issue kama hiyo. Kama alivyosema Nyambala hapo juu hawa wakuu wetu hawatakiri hata siku moja.

Sasa hivi tunamwona huyu Mkuu akijitahidi kulinda maslahi yake badala angekuwa mjasiri akasema yes ndiyo hivyo nilivyohisi wakati ule. Sidhani kama kuna mtu ambaye angemlaumu kama angesema hivyo lakini tunavyojua, hawa viongozi wetu wanaona ni lazima wajikombe kwa viongozi wao.
 
Hosea anadangnya nn watanzania wakati kila kitu kiko wazi, ushahidi uko wazi wameshindwa no wameogopa kumtia Chenge mahakamani.

hizo hela za chenge inwezekanaka

  • kazirudisha kwa serikali kwa mapatano na serikali ili asishtakiwe - JK's way of dealing with mafisadi
  • Ni za CCM . Chenge alizihifadhi kwa sabu ya wadhifa aliokuwa nao wa mwanasheria mkuu.

Hosea afuatilie kesi inavyoendelea UK ndo atajua. Jaji Uk amesema dili lina rushwa. Yeye mwenyewe kasema hivyo.

  • Je amefanya nn?
  • Hao Maofisa wa ngazi ya juu jeshini ni kina nani
 
Sidhani hapa kuna janja janja ya maneno, very likely hivi ndivyo anavyo-perceive kuhusu mkuu wake na kuna ukweli ndani yake!

"He told us point blank ... that cases against the prime minister or the president were off the table ..." The cable then details allegations against former leaders and their inner circles, saying they would be "untouchable".

"He noted that President Kikwete does not appear comfortable letting the law handle corruption cases which might implicate top-level officials." The cable then says Kwitke "does not want to set a precedent" by going after any of his predecessors.

- Wewe ungekua mkuu wa kazi wa Hosea ungemfukuza kazi kusema hayo maneno empty? I mean kipi kipya hapo ambacho wananchi wa hili taifa hatukujui na ni neno gani hapo la maana sana linaweza kumfungisha kiongozi yoyote wa taifa letu kwenye sheria hata za huko majuu?

- I mean tizama Wikileaks za huko majuu hasa US, jina kwa kitendo Mfalme wa Saudia anaitaka US iitundike mabomu Iran boom kwenye sheria hapo anaondoka mtu, kwanza hata nina wasi wasi sana na hii Wikileaks iliyoitaja bongo na kina Hosea kama ni for real, naiona kama imefinyangwa na mafisadi kutuzuga wananchi, Wikileaks za kweli huwa ni clear hazina maneno ya ujanja ujanja kama hiii yetu, it is simply fake sio ya Assange mzee wa datas original!

William.
 
Hivi mlitegemea aseme nini? Ukweli umeshamwagwa kwenye Wikileaks kwa hiyo lazima ajishaue.
 
Dk. Edward Hoseah, na kwa haraka, amekanusha kuwa Rais Jakaya Kikwete amekuwa ni kikwazo cha utendaji wa taasisi hiyo, kama alivyonukuliwa humo.

Dk. Hoseah anakiri kukutana na ofisa wa Marekani ofisini kwake Julai 2007, lakini katika mazungumzo yake, anakanusha kuwa hakuna mahali popote alipoeleza kuwa Rais Kikwete alikuwa hataki sheria ichukue mkondo wake katika kuwachunguza vigogo wanaotuhumiwa kwa rushwa.

"Nilichosema ni kwamba Rais hataki kuruhusu uchunguzi wa maofisa waandamizi wa serikali au mtu yeyote yule kufanywa kwa kuegemea katika minong'ono au ushahidi dhaifu, kwa sababu kwa kufanya hivyo, serikali inaweza kuwa katika hatari ya kulipa fidia kubwa kama watuhumiwa watashinda kesi mahakamani," alidai Dk. Hoseah katika taarifa yake jana.

Kuhusu madai ya 'hofu ya maisha yake', alisema anakumbuka kuulizwa na ofisa huyo kama anahofia uhai wake au la, akiwa ni Mkuu wa Takukuru, na kwamba jibu lake lilikuwa rahisi, "ndio, wakati unaposhughulika na vigogo au matajiri, ni lazima uwe mwangalifu na tahadhari na maisha yako."

Mimi sioni sehemu aliyokanusha, zaidi ya yote amekubaliana na "cable" ya WikiLeaks:
- Nilikutana na Ofisa wa Ubalozi (Julai 2007)
- Rais Kikwete hataki uchunguzi ufanyike dhidi ya maofisa waandamizi wa serikali (sijui role ya Rais ilikuwa ipi hapa?)
- Ni kweli maisha yake yako hatarini na anahitaji kuchukua tahadhari wakati wote
-
 
Nilichosema ni kwamba Rais hataki kuruhusu uchunguzi wa maofisa waandamizi wa serikali au mtu yeyote yule kufanywa kwa kuegemea katika minong'ono au ushahidi dhaifu, kwa sababu kwa kufanya hivyo, serikali inaweza kuwa katika hatari ya kulipa fidia kubwa kama watuhumiwa watashinda kesi mahakamani," alidai Dk. Hoseah katika taarifa yake jana.
Kama kweli rais alisema haya basi ama hajui utaratibu wa kisheria au ni mbabaishaji. Mtu hawezi kuishtaki serikali kwa kufanyiwa uchunguzi. Sababu pekee rais anaweza kuzuia fulani asichunguzwe ni kwa sababu tayari anajua yatakayogundulika na hataki yagundulike.

Watanzania wote si mazezeta kiasi hiki
 
Nilichojifunza righ away ni kwamba Hosea ni mbabaishaji... unfortunately to him, we hvae wikileaks these days, tungejuaje anajikanganya hovyo na yeye ndiye mwenye dhamana

i am very sorry but ninaamini wikileaks kuliko hosea... he is note trustworthy
 
I love Wikileak, ndio maana jamaa kasingiziwa kesi ya kubaka ili wampoteze kwenye uso wa duania Lol! halafu bila haibu wanakanusha wakati wenyewe kwa midomo yao waliwahi kusema nanukuu maneno yao wenyewe hapa

Rais Kikwete "Tuwaache wazee wetu wapumzike kwa amani"

Hosea "EPA ni issue kubwa ambayo tusipoangalia inaweza kutingisha nchi"

IGP "Nchi hipo mikononi mwa wana EPA kwahiyo tuwe makini na kushughulikia swala hili"

ukiangalia na Wikileak ilichosema kuna tofauti gani na maneno yao wenyewe hapa

Hakuna dhamira sahihi ya kutaka kumaliza rushwa kubwa ndani ya Tanzania, wanaokamatwa kwa Rushwa ni akina yahe waliokula sh. milioni moja mpaka kumi lakini wanaoibia serikali mabilioni wanakuwa huru, angalieni kesi zote za EPA, hakuna mtu atakayefungwa kwa kuwa ushaidi hakuna, ukiweka ushaidi unataka kuwausisha wakubwa na hizi kashifa wakati Rais ameagiza wakubwa wasiguswe

Hii ndio sababu ya watu kama Malegesi mpaka leo hawajawahi kukamatwa kwa EPA wakati wanajulikana ni jinsi gani walivyochukua pesa kwa hira kutoka BOT
 
Dk Hoseah adaiwa kufichua siri za JK

MKURUGENZI Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Dk Edward Hoseah, anadaiwa kufichua siri za Rais Jakaya Kikwete kwamba kiongozi huyo wa nchi asingependa vigogo serikalini kufikishwa mahakamani kwa tuhuma za rushwa. Kadhalika, mkuu huyo wa Takukuru anadaiwa kushindwa kuwafikisha mahakamani vigogo waliohusika na kashfa ya rada kwa sababu anahofia usalama wake, gazeti la The Guardian la Uingereza liliripoti juzi.

Mbali na hofu hiyo, gazeti hilo pia lilieleza juzi kuwa Dk Hoseah alipewa maelekezo maalumu na Rais Kikwete kutoshughulikia kesi za rushwa zinazowahusu vigogo katika serikali yake na hasa marais waliomtangulia. The Guardian lilitoa taarifa hiyo likiunukuu mtandao wa habari wa WikiLeaks uliojizolea umaarufu duniani kwa kutoa habari za kiuchunguzi hasa baada ya mwasisi wake, Julian Paul Assange, kutiwa matatani.

Kwa mujibu wa habari hiyo, Dk Hoseah, alisema hayo Julai 14 mwaka 2007, alipokuwa akizungumza na mwanadiplomasia wa Marekani, Purnell Delly jijini Dar es Salaam. Alisema uchunguzi wa kashfa ya rada ni hatari kwake kwa kuwa vigogo nchini, hawaguswi kwa tuhuma na kwamba "tayari alikuwa ameanza kupata vitisho".

Akizungumza kwa huzuni na kusononeka, Dk Hoseah alidai kuwa kwa ari na utashi alionao katika vita dhidi ya ufisadi, angeweza kuwafungulia mashtaka watuhumiwa wa ufisadi, lakini ameshindwa kwa kuwa kesi hiyo inawagusa vigogo kadhaa, wakiwamo marais na waziri mkuu mstaafu na ndani ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ). "Biashara hiyo chafu iliwahusisha maafisa kuanzia ngazi ya Wizara ya Ulinzi na afisa mmoja au wawili wa ngazi za juu ndani ya jeshi, The Guardian lilieleza likinukuu vinasa sauti vya ubalozi huo.

Dk Hoseah alitumia mkutano huo kueleza mafanikio ya Tanzania katika mapambano dhidi ya rushwa na kueleza kuwa matumaini yake ya awali kusimamia mkakati huo, yamevunjwa moyo. "Alituambia waziwazi (rais) kwamba tuhakikishe kesi inayomhusu rais au waziri mkuu na viongozi waliomtangulia, tusiziguse na ziwekwe chini ya meza," lilieleza gazeti hilo katika taarifa yake.

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na sheria zake ndogondogo, mtu yeyote aliyewahi kuwa rais wa nchi hawezi kufikishwa mahakamani kwa tuhuma zozote zinazomkabili.

Lakini, wadau kadhaa wa masuala ya siasa, sheria, haki za binadamu na utawala bora wamekuwa wakiendesha harakati za kudai katiba mpya ambayo pamoja na mambo mingine, wametaka iondoe kinga ya rais ya kutoshitakiwa mahakamani hata mara baada ya kustaafu kwenye nafasi hiyo.

"Kuna taarifa za ufisadi ndani ya Beki Kuu ya Tanzania (BoT). Pia Visiwani Zanzibar kuna mambo mengi yanayohusiana na rushwa na ufisadi,"alinukuliwa Dk Hoseah ambaye alieleza kuwa anaamini "maisha yake yatakuwa hatarini" iwapo atathubutu kuendesha uchunguzi huo.

Taarifa hizo kutoka kumbukumbu za vinasa sauti vya ubalozi wa Marekani nchini, zimeeleza kuwa katika mazungumzo hayo, Dk Hoseah alikuwa anarudia na kusisitiza kuhusu usalama wake, akisema anaamini maisha yake yapo hatarini kwa sababu alishapokea ujumbe wa vitisho kupitia simu yake ya mkononi na barua. "Amesema (Dk Hoseah) amekuwa akikumbushwa mara kwa mara kwamba katika vita hiyo ya ufisadi, anapigana na matajiri na wenye nguvu katika vita dhidi ya ufisadi,"gazeti The Guardian lilimnukuu Delly, afisa huyo wa Marekani aliyekuwa akizungumza na Dk Hoseah.

Imeelezwa katika taarifa hiyo kuwa sababu kubwa ya Dk Hoseah kujaribu kutia mguu kwenye sakata la rada ni taarifa ya uchunguzi wa Taasisi ya Kuchunguza Ufisadi ya Uingereza (SFO), ambayo ilieleza kinagaubaga kuhusu kesi hiyo. Delly alisema, Hoseah amekuwa akionywa katika vitisho hivyo kwamba anaweza akaiona chungu nchi yake ikiwa ataendelea na mapambano hayo.

"Alisema (Dk Hoseah), ukihudhuria mikutano ya ndani na vigogo wa serikali, wanataka wakuone ukijihisi kwamba wao ndio wamekuweka katika cheo chako, lakini ukiwa mbishi wa kushikilia misimamo yako tu, basi uko katika hatari," gazeti hili lilimnukuu Delly. Awali akizungumza na gazeti hili, Dk Hoseah alikiri kupata vitisho vinavyohatarisha maisha yake kutokana na mapambano yake dhidi ya rushwa, lakini akasema hajaiona habari hiyo iliyonukuu mazungumzo yake na mwanadiplomasia huyo wa Marekani.

Hata hivyo, mtendaji huyo wa Takukuru alisema ni kawaida yake kukutana na mabalozi wa nchi mbalimbali kila mwaka na kujadiliana nao mambo mengi kuhusu Tanzania. Alisema mabalozi ni wadau wakubwa katika bajeti ya Tanzania na hivyo huwa wanakutana kila mwaka kujadili mambo mbalimbali ya kuhusu kusaidia bajeti ya serikali. "Mimi huwa nakutana na mabalozi wa nchi mbalimbali kwa sababu wao ni wadau katika mradi wa ‘government budget support' (Mpango wa kusaidia bajeti ya serikali), hivyo hilo sio tatizo," alisema Dk Hoseah.

"Msimamo wangu ni kwamba mapambao dhidi ya ufisadi ni endelevu hadi hapo tutakapofanikiwa kumaliza tatizo hili," alisema Dk Hosea na kukiri: "Vitisho vipo vingi tu, kutoka kwa watu wanaotuhumiwa, lakini si hata ninyi waandishi mnamwagiwa ‘tindikali' katika mapambano yenu, hivyohivyo hata mimi napata vitisho." Alisisitiza kuwa pamoja na vitisho hivyo, hawezi kurudi nyuma katika mapambano ya rushwa na ufisadi.
"I'm Tanzanian I will die in Tanzania, it is my country' (mimi ni Mtanzania, nitakufa Tanzania, ni nchi yangu), siwezi kuhama nchi kwa vitisho vya watu wachache wanaotuhumiwa kwa ufisadi na rushwa," alisisitiza Dk Hoseah. "Hilo la kwamba nafikiria kuhama nchi wametia chumvi si unajua magazeti? Sijafikiria kuhama nchi licha ya vitisho, mimi naona ni changamoto na jambo la kawaida katika mapambano," aliongeza Dk Hoseah.

Kuhusu Rais Kikwete kukwamisha mapambano ya ufisadi kama alivyonukuliwa na gazeti hilo la The Guardian, Dk Hoseah alipiga chenga kulijibu badala yake akaeleza: "Ili umpeleke mtu mahakamani si lazima umtuhumu na kumfanyia uchunguzi? Lakini pia lazima tujenge utamaduni wa kuwaheshimu viongozi wetu." Lakini baadaye saa 9:30 alasiri jana,Takukuru ilituma taarifa iliyoeleza kuwa Dk Hoseah ameshangazwa na Ofisa wa Ubalozi wa Marekani kumnukuu vibaya huku akisema hajui ana lengo gani.

Katika taarifa hiyo, Dk Hoseah alikiri kukutana na ofisa huyo wa Ubalozi wa Marekani ofisini kwake Julai mwaka 2007, lakini, akasema ripoti ya mazungumzo yao aliyoipeleka nchini kwake imechakachuliwa. "Kwa mfano haikutokea katika mazungumzo yetu kusema kwamba Rais Jakaya Kikwete hakutaka kuruhusu sheria kuchukua mkondo wake, kuwashitaki vigogo wote wanaotuhumiwa kwa ufisadi kama ilivyodaiwa na Ubalozi wa Marekani," ilisema taarifa hiyo iliyotolewa na idara ya mahusiano ya Takukuru.
"Nilichosema ni kwamba Rais hayuko tayari kuruhusu kushitakiwa kwa vigogo wa serikali au mtu mwengine yeyote kwa tuhuma za uvumi au kwa ushahidi dhaifu, kwa sababu kufanya hivyo, serikali itakuwa hatarini kwa kulipa gharama kubwa ya fidia ikiwa mtuhumiwa huyo atashinda kesi mahakamani," ilisema taarifa hiyo na kuongeza.

Kuhusu hofu ya maisha yangu, nakumbuka niliulizwa na Ubalozi wa Marekani kwamba je, naogopea maisha yangu au la, nikiwa Mkuu wa Takukuru? Na jibu langu lilikuwa rahisi kwamba ‘bila ya shaka' unapopambana na wakubwa na matajiri kama hao wanaotuhumiwa unapaswa kuwa makini na maisha yako. Lakini hata siku moja sikusema kwamba napanga kuhama nchi kwa sababu maisha yangu yapo hatarini.

Ni mshangao kuona kwa mara nyengine ofisa wa Ubalozi wa Marekani ananinukuu mimi vibaya au nje ya mada na sielewi kabisa lengo lao lilikuwa nini." Alsema rekodi yake, akiwa Mkuu wa Takukuru iko wazi kabisa wakati wowote anapokuwa na ushahidi wa kutosha dhidi ya mtuhumiwa yeyote wa ufisadi hawaogopi lolote isipokuwa ni kumburuza mahakamani bila ya kujali cheo chake.

Naye Mkurugezi wa Mawasiliano ya Rais, Salva Rweyemamu, hakupatikana jana kuzungumzia suala hilo kutokana na simu yake kuita bila kupokelewa muda wote. Kwa upande wa msaidizi wake, Premi Kibanga aligoma kuzungumzia suala hilo kwa kile alichoeleza kuwa hajaisoma habari hiyo iliyochapishwa na gazeti la The Guardian la Uingereza.
"Mimi sijaiona wala kuisoma habari hiyo, hivyo siwezi kuzungumzia kitu ambacho sijakiona. Sina uhakika kwamba Dk Hoseah amesema hayo, pengine umemuelewa vibaya," alisema Kibanga. Juhudi za kumpata Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Alphonso Lenhardt, kuzungumzia suala hilo hazikufanikiwa baada ya simu yake ya mkononi kutokuwa hewani kila ilipopigwa.
 
Hii inanifanya nianze kuamini uvumi kuwa Balali shaidi namba moja yupo hai na hajafa unless waje na reason nyingine, maana Balali akipatikana viongozi wetu wote wanaishia mahakamani. kweli tuna genge la mafia ndani ya nchi yetu na watanzania wamelala tu mbumbumbu bila hata kuchukua hatua
 
"Nilichosema ni kwamba Rais hataki kuruhusu uchunguzi wa maofisa waandamizi wa serikali au mtu yeyote yule kufanywa kwa kuegemea katika minong'ono au ushahidi dhaifu, kwa sababu kwa kufanya hivyo, serikali inaweza kuwa katika hatari ya kulipa fidia kubwa kama watuhumiwa watashinda kesi mahakamani," alidai Dk. Hoseah katika taarifa yake jana.

Kuhusu madai ya ‘hofu ya maisha yake', alisema anakumbuka kuulizwa na ofisa huyo kama anahofia uhai wake au la, akiwa ni Mkuu wa Takukuru, na kwamba jibu lake lilikuwa rahisi, "ndio, wakati unaposhughulika na vigogo au matajiri, ni lazima uwe mwangalifu na tahadhari na maisha yako."

"Lakini hakuna mahali popote nilipotamka kuwa nina mpango wa kukimbia nchi kwa sababu maisha yangu yalikuwa hatarini. Ni jambo la kushangaza kwa mara nyingine, Ofisa huyo wa Ubalozi wa Marekani amenikariri kinyume na ukweli na sijui nia yake hasa ilikuwa nini."

Hatuhitaji ushahidi mwingine............Dr. Hosea aliongea nao.........na wamareakani hawana sababu ya kuongopa......................

Na vita dhidi ya ufisadi inakwamishwa na JK na Takukuru kwa pamoja ila Hosea alichofanya ni kumsukumia bosi wake lawama.................Safari hii watamalizana wenyewe............ukweli unajionyesha watuhumiwa wa madawa ya kulevya ni kimya chenye mshindo mkuu................Dowans/ Richmond hakieleweki...........................Radar hatujui faili limepotelea wapi.....................Sasa Hosea anakanusha nini?

Huyu jamaa ni tapeli wa kimataifa na hata familia yake iko marekani......................labda anajipendekeza huko ili wasimfutie viza ya kuvinjari majuu kwa mabwana zake anaowaabudu.....................tunasikia ana nyumba za kifahari huko majuu....................
 
Nafikiri kuna haja ya kusoma taarifa yote yote kutoka kwenye cable, link hii hapa Cable Viewer , Hii inaonyesha ni jinsi gani viongozi waandamizi wa serikali wanavyojua kuwa kikwete ni weak, lakini wanvumilia tu kwa sababu ya matumbo yao. Tusubiri tutaona Mengi
 
hosea hayo uliyaongea na balozi wa marekani yana ukweli sema sasa unakanusha, coz kitumbua chako kishamwangiwa MCHANGA, so unamwogopa mkwere, ndo maana unakanusha, kuwa hujasema haya ''Nilichosema ni kwamba Rais hayuko tayari kuruhusu kushitakiwa kwa vigogo wa serikali au mtu mwengine yeyote kwa tuhuma za uvumi au kwa ushahidi dhaifu, kwa sababu kufanya hivyo, serikali itakuwa hatarini kwa kulipa gharama kubwa ya fidia ikiwa mtuhumiwa huyo atashinda kesi mahakamani,"

my take siku zote hukweli hujitenga na uongo, muda si mrefu hayo yaliyosemwa na wikileak YATAZIBITISHWA, na hapo ndio utakapo ona AIBU
 



WikiLeaks cables: Tanzania official investigating BAE 'fears for his life'

Prosecutor Edward Hoseah voiced safety fears over inquiry into 'dirty deal' involving sale of radar system to government


  • David Leigh
  • Sunday 19 December 2010 21.30 GMT
    President-Jakaya-Kikwete--007.jpg
    President Jakaya Kikwete, pictured with George Bush in 2008, had his commitment to fighting corruption questioned, according to the cables. Photograph: Jim Watson/AFP/Getty Images The Tanzanian prosecutor investigating worldwide misconduct by BAE, Britain's biggest arms company, confided to US diplomats that "his life may be in danger" and senior politicians in his small African country were "untouchable".

    A leaked account of what the head of Tanzania's anti-corruption bureau, Edward Hoseah, termed the "dirty deal" by BAE to sell Tanzania an overpriced radar system, is revealed in the US embassy cables.
    BAE is to appear in court in London tomorrow, when their system of making secret payments to secure arms contracts, exposed by the Guardian, will be officially detailed for the first time.

    Every individual involved in the BAE scandal in Britain and Tanzania has escaped prosecution.

    But the arms giant agreed with the UK Serious Fraud Office (SFO) to pay £30m in corporate reparations and fines, provided the word "corruption" did not appear on the indictment. A corruption conviction would debar the company from EU contracts.

    The former overseas development secretary, Clare Short, said at the time: "It was always obvious that this useless project was corrupt."

    Hoseah met a US diplomat, Purnell Delly, in Dar es Salaam in July 2007, and claimed (unrealistically it turned out) he would be able to prosecute guilty individuals in the BAE case. The US cable reports: "He called the deal 'dirty' and said it involved officials from the Ministry of Defence and at least one or two senior level military officers."

    Hoseah spoke gloomily about the prospects for Tanzania's anti-corruption struggle and his original hopes to prosecute the "big fish" of corruption.

    "He told us point blank ... that cases against the prime minister or the president were off the table ..." The cable then details allegations against former leaders and their inner circles, saying they would be "untouchable".

    "He noted that President Kikwete does not appear comfortable letting the law handle corruption cases which might implicate top-level officials." The cable then says Kwitke "does not want to set a precedent" by going after any of his predecessors.

    There were "widespread rumours of corruption within the Bank of Tanzania", Hoseah said, and the island region of Zanzibar was also "rife with corruption".

    The diplomat noted: "Hoseah reiterated concern for his personal security ... saying he believed his life may be in danger ... He had received threatening text messages and letters and was reminded every day that he was fighting the 'rich and powerful'."

    He might have to flee the country. He warned: "He said quietly: 'If you attend meetings of the inner-circle, people want you to feel as if they have put you there. If they see that you are uncompromising, there is a risk.' "

    The US embassy noted in a "cynical" aside, that probably the only reason Hoseah felt obliged to attempt a BAE prosecution was because the SFO had presented him with "a fully developed case file, brimming with detailed evidence".

    Today's court appearance by BAE is the culmination of lengthy attempts to bring the company to justice since the Guardian exposed its worldwide secret payment system.

    The prime minister at the time, Tony Blair, intervened in 2006 to halt an SFO investigation into payments to members of the Saudi royal family.

    The US department of justice has had more success than the SFO, forcing BAE to pay $400m (£260m) in penalties under the US Foreign Corrupt Practices Act.

    £28m radar deal 'stank'


    Tanzania, on Africa's east coast, is one of the poorest states in the world, formerly controlled in turn by Arab slavers, German colonists and the British.At the time of the radar deal, life expectancy was 45.
    Tanzania was forced to apply for debt relief from the west and was heavily dependent on aid. It is ravaged by HIV/Aids and its GDP per head is just $723 (£465).

    President Benjamin Mkapa, whose regime did the deal, was succeeded in 2004 by his political colleague Jakaya Kikwete.

    Tanzania, which has no air force, bought the military air defence radar from BAE in 2001 for £28m.
    It was claimed the Commander system, which was portable and festooned with anti-jamming devices, could also be used for civilian air traffic control.

    The country borrowed the cost from Barclays, adding to its debt burden. Both the World Bank and the International Civil Aviation Organisation called the purchase unnecessary and overpriced.

    In London, the then development secretary, Clare Short, temporarily blocked aid payments in protest. "It stank," she now says of the sale.

    She urged an export licence be withheld, but was overruled by Tony Blair himself. Robin Cook, then foreign secretary, recorded bitterly in his diary that Dick Evans [of BAE] seemed to have "the key to the garden door of No 10 [Downing St]".

    In January 2007 the Guardian disclosed that BAE had used an offshore front company, Red Diamond, to secretly pay £8.4m, 30% of the radar's ostensible price, into a Swiss account.

    The account was controlled by Tanzanian middleman Sailesh Vithlani. His "consultancy" agreement was, it is alleged, formally signed off in London by Evans.
 
Judge questions BAE deal over payments for Tanzania contract

Mr Justice Bean tells Southwark Crown court it appeared that BAE had paid 'whatever was necessary' to get contract



  • Rob Evans and David Leigh
  • http://www.guardian.co.uk/ Monday 20 December 2010 21.26 GMT <li class="history">
    BAE-007.jpg
    BAE has steadfastly argued that it did not make corrupt payments to secure a contract from the Tanzanian government. Photograph: Murdo MacLeod for the Guardian A controversial deal between prosecutors and Britain's biggest arms firm, BAE, was today challenged by a judge who said the company appeared to have been engaged in bribery.
    BAE had reached a deal with the Serious Fraud Office earlier this year in which it agreed to plead guilty to a relatively minor accounting offence. BAE steadfastly argued that it did not make corrupt payments to secure a £28m contract from the Tanzanian government.
    But today, Mr Justice Bean questioned the heart of the agreement, repeatedly saying that payments originating from the company appeared to be "corrupt" and for "bribing decision-makers in Tanzania". He told Southwark crown court that it appeared that BAE had paid "whatever was necessary to whomever it was necessary" to get the Tanzanian contract. He added that it appeared that the payments were disguised so that BAE "would have no fingerprints on the money". "They just wanted the job done &#8211; hear no evil, see no evil," he said. The judge is due to sentence BAE tomorrow .
    In February, BAE struck the plea deal with the SFO and American prosecutors to end years of corruption investigations into its business methods. The arms giant agreed to pay £30m in corporate penalties in return for admitting accounting irregularities over a radar contract with Tanzania. Anti-corruption campaigners have argued that the deal is too lenient and cosy.
    Today, Victor Temple, the QC for the SFO, told the court that BAE had set up a system of "covert" and "overt" agents to sell their arms around the world. The "overt" advisers "conducted their work openly as BAE's in-house representatives", he said, while the "covert" agents' work was "highly confidential".
    He said Sir Richard Evans, BAE's chairman, had "personally approved" the use of a businessman, Sailesh Vithlani, as its "covert" agent to secure the Tanzanian radar contract. Approval was also given by Mike Turner, then a board member who later became BAE's chief executive.
    Temple said BAE paid $12.4m (£7.7m) to Vithlani between 2000 and 2005 &#8211; around a third of the radar contract's value.
    BAE had paid much of this money through its front company based in the British Virgin Islands (BVI), known as Red Diamond, to a Panama-based company controlled by Vithlani.
    Today the court heard that the SFO and BAE had agreed a series of "carefully- worded" statements to put before the judge. These included:
    &#8226; The admission by BAE that "there was a high probability that part of the $12.4m would be used &#8230; to favour BAE" while the contract was being negotiated;
    &#8226; "It was not now possible to establish precisely what Vithlani did with the money which was paid to him";
    &#8226; That the SFO did not say that any of this money was "in fact improperly used";
    &#8226; That the SFO accepted that BAE had not engaged in corruption.
    The judge called these statements the "critical part" of the case, repeatedly asking barristers for the SFO and BAE what the money had actually been used for.
    He said: "I have to establish what has happened. If there is no money to be used for corrupt practices, why is 97% of it paid through a BVI company controlled by BAE to another [offshore] company controlled by Vithlani?"
    When Temple said Vithlani had been hired to lobby for BAE, the judge questioned why the businessman was paid so much for his work.
    Temple said that lobbying was legitimate work. "To lobby is one thing, to corrupt another".
    Temple added that BAE had committed the accounting offence as Vithlani had been recorded in its books as performing "technical services", but he had no knowledge of any technical matters.
    David Perry, QC for BAE, argued that the firm had not admitted any corruption and should only be sentenced for the one offence they had confessed to in the plea bargain.
    The judge had threatened to call witnesses to testify as he wanted to established the purpose of the payments, but later decided to go ahead with passing sentence tomorrow.
 
Dr. Hosea ni mnafiki sana - yote ni kweli tunafahamu; na matokeo ya mkutano na ubalozi alikwenda Marekani kwa semina; na zaidi ya yote Hosea ana nyumba Marekani na familia imekuwa huko kwa muda mwingi - ni hofu ya maisha yake.
 
Wapi Jeikei wa ukweli,dar es salaam na kibunango kuchangia mada hii adhimu ???
 
The judge had threatened to call witnesses to testify as he wanted to established the purpose of the payments, but later decided to go ahead with passing sentence tomorrow.

Huu unaweza kuwa ni nafasi ya mafisadi wetu uchwara kupumua........................
 
Back
Top Bottom