Kwanza unaonekana unafatilia sana mambo ya jikoni!Una moyo mgumu sana duu Mimi nisingeweza kumuweka ndani shemeji Yangu tena sababu ya chakulaaaa ....hapo tatizo ni njaaa .mmh we kweli jasusi!
Ni wazi unatatizo kubwa na mkeo.
Unacho takiwa kufanya ni kukaa na mkeo chini na kumueleza ukweli kuwa na yeye aanze kuchangia na swala la kuwasaidia ndugu zake mnaweza kukaa chini na kuangalia jinsi ya kuwasaidia bila kuingia kwenye mikwaruzano.
Kama ndugu zake hawana kazi basi jitahidi muwatafutie kibarua na ni vyema mka kaa na mkeo mkajua jinsi ya kufanya!
Halafu ni wazi hili swala umeligeuza kama uadui ndio maana mkeo anafanya hivyo bila kukushirikisha!
Hebu jaribu kukaa na mkeo muongee kuhusu hili swala na uchukulie kama huo ni mzigo wako pia!