Why did i get married??

Why did i get married??

mnhh hapo kazi ipo..
yeye anapenda nini?
mpira?kwenda mziki?
anzia na hobbies zake
tazama nae mpira,..mfuate bar akiwa anataka kurudi...

wengi hawapendi kufwata huko, kiukweli kuna wakati ndoa inaboa kichizi, na kuirudisha mahala pake inahitaji moyo haswa, mana umeshaanza kumchukia fulani, akisema hiki anakuboa, akitaka hivi anakuboa, kazi kweli kweli.
 
kama kweli umeolewa angalia sana shetani atakuwa anainyemelea ndoa yako. hebu fikiria upendo wa kwanza pindi mnaoana huo ndo uwe platform ya kuona ni nini kimekoseka. mm huwa naamini kama ndoa imekaa say five years hata mitatu kuna mambo mengi ambayo mmefanya so inapotokea ume quit naona unapoteza vingi kuliko utakavyopata. maana naamini kama umeamua kuachana tu bila sababu ya msingi kama uzinzi na kifo(ambazo kibiblia ndo zimeruhusiwa kuachana) basi ujue utachuma laana tu maana mwisho wa siku utakuwa na mwanaumme mwingine wakati mme wako wa ndoa yu hai hivyo haitakuwa afya kwako na maisha yako yote!
 
Hapo ndo nilikuwa napataka kwenye kugrow togather, narudi kule kule why did I get married? Yaani hata sielewi kwasababu nikianzisha idea lets do this itapingwa na itaishia hewani na mimi natafuta idea ingine itachambuliwa na kuonekana ni uharibifu wa hela na nyingine kutafutiwa sababu kwamba haifai haya ukisema yeye basi alete any idea so that we can go together anakwambia sina idea yoyote. ukinifatilia nilishaomba mtu anayejua kuogelea anifundishe hiyo ilikuwa moja ya idea ya kujilkep busy nikamuomba tujifunze wote week ends tuwe tunaogelea nikaambiwa nataka kumuua na maji akiwa mtu mzima wakati yeye hajui kuogelea nikaishia hapo maan ukiendelea sana inakuwa ugomvi kiufupi ni tabu bin shida looh
Pole sana Mkunde Original . Mwanaume mwenye tabia za aina hii ni kazi sana kuishi nae lkn Mungu akusaidie upate hekima itakayoweza kumbadilisha au Mungu akusaidie uweze kupotezea tabia zake. Nakosa hata cha kukushauri manake wengi washakupa mawazo mazuri naomba niungane na Mentor ktk kukuombea ili Mungu aifanye upya ndoa yako. Ukipata mabadiliko tujuze ili tumshukuru Mungu
 
Last edited by a moderator:
Mkunde Original ungefunguka zaidi anakufanyia nini mpaka uko so down namna hiyo. Anakunyima kupiga naye show, au ni mlevi kupindukia, je ni mgomvi, halali nyumbani kwake?
 
wengi hawapendi kufwata huko, kiukweli kuna wakati ndoa inaboa kichizi, na kuirudisha mahala pake inahitaji moyo haswa, mana umeshaanza kumchukia fulani, akisema hiki anakuboa, akitaka hivi anakuboa, kazi kweli kweli.
Hayo yote mkichunguza kwa makini tatizo linaweza kuwa limeanzia kwenye kutopeana Papuchi na dushelele kwa ufasaha. Wakati mwingine mkijaribu kusawazisha hapo mambo mengine yote hunyooka nakuwa kama siku ya Honey moon yenu.
 
i wish i could hug you right now..(naona these days nakua sentimental kidogo)
kukata tamaa na jambo ambalo unaamini kuna a way (hata chance iwe ndogo vipi)is a crime (kwangu)
siko kwenye ndoa ila naamini kama relationships ni kama 24hrs jobs na inahitaji moyo wa ziada kwa sasa ili ndoa yako isimame,am not a fan of divorce maybe pale kunapokua hakuna nafasi kabisaaaa ya kujenga tena
i also believe on fasting and praying kwa kitu unachohitaji,Mungu sio kiziwi
fanya kila kitu ukiwezacho,ukishindwa just let it be..hutajuta baadae.pole
 
Dah pole sana inaelekea umechanganyikiwa kweli , lakini ndoa inataka uvumilivu, Kaeni mzungumze mmalize tofauti zenu, na wewe mbona umejikataa mwenyewe, yaani umekata tamaaa sana, haitakiwi kukata tamaa,

Asante nshapoa hope litapita salama.
 
Habari zenu za week end MMU??

Nimejikuta najiuliza hili swali jioni hii bila jibu, najua kuna movie ya kimarekani inaitwa hivi na nilishawahi kuangalia ila nimekosa jibu ilikuwaje kuwaje nikaolewa memory imekata kabisaaaa hapa nilipo sielewi hat kwa nini bado niko ndani ya hii ndoa. May be am not a good wife and nimejisahau sitimizi majukumu yangu kama mke ila kwa nini haniachi? If I examine myself yeah ninamapungufu ila na siwezi kuwa mkamilifu kama malaika am trying my level best but sioni mwisho wa hii ndoa. Kifupi nimechoka na sina guts za kutoka mwenyewe hadi nifukuzwe yaani akithubutu tuu kunitimua hata usiku wa manane atakuwa kanipa ahueni but at the same time am not sure if I can at all survive on my own thats why sithubutu kutimka on my own. Ila kwa nini inakuwa tabu bin shida kila leo na yaleyale ndo yanajirudia? Nahisi uvumilivu wangu unaelekea negative sijui nikiwa dataz wife itasaidia yaani niwe sijali lolote niwe bora liende kwangu yote yawe sawa..........................????
Mkiona hivi kama ujue maji yamenizidi nguvu na nahisi kuzama na nikiangalia kulia, kushoto mbele na nyuma hakuna hata kijiti cha kushikilia walau kunisupport nisizame.
Am so down Mkunde mimi..........

Mbona hujasema shida nini,? Anakupiga, anacheat, katoka na housegirl au halali nyumbani au mlev, hana bullet???
 
chini ya miaka 5 tuna mtoto mmoja.

Hiyo ndoa hata haijaanza unataka kuivunja mama? Nakwambia utakuja kuifurahia mkijitahidi mkafika angalau 15th anniversary. Sasa hivi ndio mnaanza kujuana mlivyo kiuhalisi (sio imaginary mlivyokuwa mnatongozana). Ongeeni na wala msiwahusishe watu, utakuja kuniambia ukifanya hayo. All the best!
 
Hayo yote mkichunguza kwa makini tatizo linaweza kuwa limeanzia kwenye kutopeana Papuchi na dushelele kwa ufasaha. Wakati mwingine mkijaribu kusawazisha hapo mambo mengine yote hunyooka nakuwa kama siku ya Honey moon yenu.

mie niliboreka kwa mambo mengine kabisa, hata hiyo kitu nilikuwa siihitaji kivile, nilikuwa naona usumbufu tu, lakini sasa hivi tunaenda sawa.
 
kama kweli umeolewa angalia sana shetani atakuwa anainyemelea ndoa yako. hebu fikiria upendo wa kwanza pindi mnaoana huo ndo uwe platform ya kuona ni nini kimekoseka. mm huwa naamini kama ndoa imekaa say five years hata mitatu kuna mambo mengi ambayo mmefanya so inapotokea ume quit naona unapoteza vingi kuliko utakavyopata. maana naamini kama umeamua kuachana tu bila sababu ya msingi kama uzinzi na kifo(ambazo kibiblia ndo zimeruhusiwa kuachana) basi ujue utachuma laana tu maana mwisho wa siku utakuwa na mwanaumme mwingine wakati mme wako wa ndoa yu hai hivyo haitakuwa afya kwako na maisha yako yote!

Asante kwa maneno yako ya farajana kutia moyo.
 
kila siku zinavyosogea moyo wa kuolewa unapotea kabisaaaa, maybe this will change someday ila nahisi hali hii inaweza kunipata.
 
Pole sana Mkunde Original . Mwanaume mwenye tabia za aina hii ni kazi sana kuishi nae lkn Mungu akusaidie upate hekima itakayoweza kumbadilisha au Mungu akusaidie uweze kupotezea tabia zake. Nakosa hata cha kukushauri manake wengi washakupa mawazo mazuri naomba niungane na Mentor ktk kukuombea ili Mungu aifanye upya ndoa yako. Ukipata mabadiliko tujuze ili tumshukuru Mungu

Asante kwa maombi nitawapa mrisho nyuma baada ya kikao, mbarikiwe wana wa mungu.
 
Kuna uwezekano kuwa mwenzako ni 'baby husband'(mummy's boy) kitu ambacho hukukigundua toka mwanzoni na sasa kinaanza kujitokeza. Hii husababisha mifarakano isiyo na kichwa wala miguu katika mahusiano..Kama ni hivi kuna njia mbalimbali za kukabili hali hii.
 
Mkunde Original ungefunguka zaidi anakufanyia nini mpaka uko so down namna hiyo. Anakunyima kupiga naye show, au ni mlevi kupindukia, je ni mgomvi, halali nyumbani kwake?

Ni kutokuelewana vitu vidogo vidogo tuu ambavyo unakuwa unavipuuzia lakini vikijaa chungu ndo hapo najikuta nimechoka na sina hamu ya kuendelea, kupishana kiswahili tuu pia kunaweza leta ugomvi, waweza uliza swali au kusema kitu mwenzio akatafsiri vingine na kumaanisha vingine ukishangaa kwa kutabasamu wakati ukimwambia mbona mie sijamaanisha hivo anachukia kuwa unamdharau na kumcheka wakati yeye kachukia basi ni vitu vya namna hiyo.
Nashukuru dhambi ya kutokulala nyumbani haipo ni vijimambo tuu vidogovidogo vinavokera.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom