Why did I call you?

Why did I call you?

Fixed Point

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2009
Posts
11,304
Reaction score
12,753
hilo ni swali ambalo nimeulizwa dakika chache zilizopita toka kwa rafiki yangu.
Huyu mtu hatupo close saana, ila naweza kusema ni rafiki. huwa tunaongea once in a while na mara nyingine kuombana ushauri.
Leo alinipigia akiwa na hasira sana, na kunihadithia jinsi watu fulani walivyom-treat vibaya baada ya kumaliza kuwafanyia kazi yao. kwa bahati mbaya/nzuri kazi ilishafanyika, sasa kachanganyikiwa sana hajui hata awafanye nini hawa watu.
baada ya kumsikiliza maelezo yake yoote, nikaanza kumshauri, na kwa kweli nilifanikiwa kumfanya achukulie kila kilichotokea in a positive way, na mwisho wa mazungumzo akajikuta hasira zake zote towards wale watu zimeisha kabisa...... akabaki ananiuliza "why did I call you?" nikamwuliza kwa nini? akaniambia nilitamani kuongea na mtu ambaye ataniongezea hasira ili nipate nguvu za kugombana na hawa jamaa ili haki itendeke. sasa wewe umenifanya the opposite. nikabaki nacheka tu.
tunapotokewa na watu (wawe wa karibu sana na sisi au mtu ambaye umekutana naye tu) wakatuambia makwazo yao, mimi naamini lengo lao kubwa ni kupata faraja kwa kile wanachokipitia, na siyo kumfanya ajisikie dunia inamwangukia. hata kama unaona kwa hali yoyote ile huwezi kutatua tatizo lake, the least thing you can do ni kumfanya angalau aone it is not the end of the world...... umuweke awe positive na kila kitu kitajipanga kadiri muda unavyoenda, wanasema time heals.
Nawatakia siku njema wapendwa wangu
 
Ni kwa wakubwa tu wanaoweza fanya hivyo(simaanishi ukubwa wa miaka ama umbo, ukubwa wa akili)

Kuna vitu vingi vinafanya umpe mtu ukweli wake, level of confidence and trust kati yenu.
Na ukiona mtu anakukumbuka wakati yupo down/hasira, jua uko special kwake.
 
why didn't l call you?

maana jana niliact kwa hasira, ningekupigia labda nisingefanya niliyoyafanya.
mambo ni aje rafiki?
poa rafiki, pole sana.....
of all the people, wewe? kwa nini hukuni-call? lol!
usijilaumu, wakati mwingine tunafanya vitu ili tujifunze rafiki. ukiona unajutia ujue kuna kitu umejifunza kutukana na tendo ulilolifanya.... naamini halitarudia tena.
 
Ni kwa wakubwa tu wanaoweza fanya hivyo(simaanishi ukubwa wa miaka ama umbo, ukubwa wa akili)

Kuna vitu vingi vinafanya umpe mtu ukweli wake, level of confidence and trust kati yenu.
Na ukiona mtu anakukumbuka wakati yupo down/hasira, jua uko special kwake.
Ni kweli Kongosho....
sometimes huwa nashangaa watu wanaoniambia vitu vyao wala sipo close nao kihivyo....
yaani utakuta ni rafiki wa rafiki yangu, au rafiki wa ndugu, najishangaa tu, mbona hakumwambia fulani anakuja kuniambia mimi?
 
there are times mtu unaweza kujisikia hasira ukahitaji
someone to listen to you,share ur tears with,someone to understand....,......

ukipata bahati ya kukutana na watu kama FP it really helps
 
Wee naye una hasira?

hahahah, umenikumbusha rafiki yangu wa A'level aliyewahi sema "yaani mimi Kaunga akinifokea, inakuwa kama ananiambia tu". Kweli nilikasirika, niece wangu ambaye ana kitoto hata mwezi haujatimia keshaanza kupuyanga mitaani, anamuacha mtoto na housegirl kweli ni fair????
 
Kumwamini mtu si lazima muwe karibu kila saa mnaongozana
Kuna watu unawaambia vitu fulani sababu una hakika uko salama kwao
Au unaweza mwambia mtu kitu sababu unahisi ana upeo huo wa kushauri hicho ulichomwambia.

Kuna mtu aliwahi niomba ushauri/maono yangu juu ya jambo fulani, nilishangaa, niliona ni too sensitive
Hapo hapo ni mtu mzima kwangu na ana mke, nikajiuliza kwa nini asimwulize mkewe, sikupata jibu.

Kuna siku nikamsikia anapiga story tu ila akasema 'wakati mwignine unakosa wa kuuliza nyumbani sababu unakuta mwenza hana upeo huo'. Mie nikajikonektia dot na lile aliloniuliza, nikabaki 'mmh!'

Ni kweli Kongosho....
sometimes huwa nashangaa watu wanaoniambia vitu vyao wala sipo close nao kihivyo....
yaani utakuta ni rafiki wa rafiki yangu, au rafiki wa ndugu, najishangaa tu, mbona hakumwambia fulani anakuja kuniambia mimi?
 
Unataka akang'olewe koromeo?

Mmh, mimi nikiombwa ushauri na mwanamme huwa nakuwa makini sana, hasa kama ana hasira

Unaweza sababisha watoto wa watu kuwa yatima, au mwanamke mmoja kuwa mjane

Hujamtendea haki huyo jamaa....lol!

Kwa nini hukubadilisha na kumpa dozi kidogo ya hasira??

Babu DC!!
 
ila FP kuna watu wengine ni ngumu kuwa define..Anakuja kwako kwa ushauri unajitahidi kumshauri in a positive way, akitoka hapo bado anakwenda kulianzisha halafu kujuta baadae...
 
Last edited by a moderator:
Sio hata kidogo, huyo mtoto alizaa mwenyewe? Duh mwezi, hata njia haijakauka vizuri:shock:. Ulikuwa na haki kwa kweli, hata kama hayupo under your roof.

Mie naogopa kukasirika, napata taabu sana handle my anger.

hahahah, umenikumbusha rafiki yangu wa A'level aliyewahi sema "yaani mimi Kaunga akinifokea, inakuwa kama ananiambia tu". Kweli nilikasirika, niece wangu ambaye ana kitoto hata mwezi haujatimia keshaanza kupuyanga mitaani, anamuacha mtoto na housegirl kweli ni fair????
 
ila FP kuna watu wengine ni ngumu kuwa define..Anakuja kwako kwa ushauri unajitahidi kumshauri in a positive way, akitoka hapo bado anakwenda kulianzisha halafu kujuta baadae...
watu kama hao pia wapo Marejesho, lakini wewe unakuwa ulishafanya kazi yako..... hutajilaumu.
Ila kuna watu ukienda kumwomba ushauri ndo yale anakuambia "yaani kakufanyia hivyo? yaani huyo jamaa ni wa kumkodia ndundiko kwenda kumsuta, hafai kabisaaaa"..... hapo unafanyaje? si unajiongezea hasira?
 
Back
Top Bottom