Who's the hell is Lewis Makame? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Who's the hell is Lewis Makame?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ng'wanangwa, Oct 19, 2010.

 1. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #1
  Oct 19, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,179
  Likes Received: 895
  Trophy Points: 280
  Huyu mtu ni nani katika nchi hii?

  Nilimnukuu kwenye clip moja ya ITV jana akisema hata kama kuna utata kwenye matokeo utakaosababisha mawakala wa vyama kugoma kusaini form za kukubali matokea, "hiyo haitabadili matokeo ya kituo husika".

  Huu ni ubabe, kiburi, kulewa madaraka au ni kitu gani?

  Mbona kila mtu ni Amiri Jeshi nchi hii?
   
 2. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #2
  Oct 26, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0


  Wakati zimebakia siku nne tu kabla ya uchaguzi, Watanzania wengi wanajiuliza endapo NEC hii ya Makame ina uwezo wa kuepusha ghasia kubwa. Sasa hivi mustakabli wan chi uko katika mikono ya mtu mmoja tu, Judge Lewis Makame – kama vile mustakabali wa Kenya ulivyokuwa kwa Samuel Kivuitu katika kipindi kile.

  Kivuitu aliamua kuitumbukiza nchi katika machafuko makubwa na kuleta mauaji ya wengi – bila shaka kwa kutokana na kutotenda haki.

  Hapa kwetu yalishatokea kule Visiwani, baada ya uchaguzi wa 2000 – kutokana na maamuzi ya hovyo ya tume ya uchaguzi kule – ZEC.

  Kwa hiyo Lewis Makame atambue kwamba Watanzania sasa hivi wanamtazama yeye tu na namshauri akalifahamu hili.
   
 3. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #3
  Oct 26, 2010
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  kwani uchaguzi ni tarehe 29?
   
 4. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #4
  Oct 26, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0

  Mkuu, nimerekebisha.
   
 5. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #5
  Oct 27, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Tume ya uchaguzi ambayo ipo chini ya ccm imekuwa ikifanya kazi kwa maelekezo ya ccm katika vipindi vya chaguzi kama hivi.

  Ikumbukwe kwamba pale kenya yule mkuu wa Tume ya Uchaguzi KEC aliamua kusoma matokeo ya kura anayoyajua yeye wala hakufuata mtiririko wa matokeo ya kura yalivyojiri hivyo akaiingiza nchi kwenye machafuko kwa UJASIRI WAKE WA KIJINGA.


  Endapo kaka yangu Lewis makame na komredi mwenzake Rajab Kiravu wakijijasirisha kufanya kama wafanyavyo miaka yote basi wajue kwamba pamoja na mtawala wa sasa kufanyiwa booking The Hague, Lewis atakuwa ndiye mtuhumiwa namba moja endapo kutatokea hamaki ya wananchi kukataa kuchakachuliwa kura zao.


  Yes Mtuhumiwa namba moja ni Lewis Makame, orodha inaendelea.
   
 6. Mpambalyoto

  Mpambalyoto JF-Expert Member

  #6
  Oct 27, 2010
  Joined: Mar 26, 2010
  Messages: 752
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hawayaoni ya Tarik Aziz huko Iraq siyo? Au hawatishwi na The Hague maana hakuna vitanzi huko? Kama wanafikiri Watanzania ni wale wa 1995, watajibeba!
   
 7. Mtende

  Mtende JF-Expert Member

  #7
  Oct 27, 2010
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 4,072
  Likes Received: 338
  Trophy Points: 180
  we muache atoe macho kama kakamatwa ugoni siku ya kupanda kizimbani ikifika ataisoma namba
   
 8. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #8
  Oct 27, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Kuna daraja la watu hapa nchini wanadhani wao wanalindwa na sheria hata wakifanya madudu yeyote yale.
  Hatuombei vurugu zitokee bali tunawasihi TUME wakae mbali na any night-shift inayowatoa kwenye day-light job za haki

  Hawajifunzi hawa, we waache tu waichezee amani yetu
   
 9. GFM

  GFM JF-Expert Member

  #9
  Oct 27, 2010
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 708
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  kwakeli Tanzania inabidi tuamke tu sasa, tunachekwa kila kona ya Africa mashariki kwamba sisi ni makondoo
   
 10. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #10
  Oct 27, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Watanzania kumbukeni kuweka ushahidi hata wa picha kwa kila tukio mabalo siyo jema wakati wa uchaguzi maana hawa jamaa wanadhani endapo wananchi watatoana macho wao haiwahusu.....
   
 11. Zed

  Zed JF-Expert Member

  #11
  Oct 28, 2010
  Joined: Mar 28, 2009
  Messages: 359
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Hata mtandao wao nec.go.tz una leta wasiwasi kama kweli NEC ni chombo kitakachotuhakikishia uchaguzi huru na wa haki. Hivyo ndivyo mtandao wao unavyo-share IP na mmoja wa wagombea uraisi! Kwa namna hii maswali ni mengi sana... kwanini? Na kama ni IP ni ya serikali kwa nini campaign team ya mgombea itumea IP hiyo? je huku si kukiuka sheria za uchaguzi? Wasiwasi wangu ni hapo ndipo kura zinaweza kuchakachuliwa! Lazima tuchunge kura zetu katika kila stage
  [​IMG]
   
 12. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #12
  Oct 28, 2010
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 9,003
  Likes Received: 585
  Trophy Points: 280
  jamaa hata usoni linaonekana lichawi, pamanina zake.
   
 13. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #13
  Oct 28, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Mkuu umenifumbua macho ajabu.
  sasa hebu ona hii nduluge,
  ni kiashiria kwamba kuna mutual agreement ya kubadilishana mawasiliano hapo.
  I am soooo doubtful na hili NEC la lewis na kiravu ambao tangu imeanzishwa wao wapo madarakani kutokana na uzoefu wao kuwafaa sana ccm na si taifa
   
 14. R

  Rugemeleza Verified User

  #14
  Oct 28, 2010
  Joined: Oct 26, 2009
  Messages: 668
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Hii ni hatari sina imani hata kidogo na hawa watu wa NEC kwani wanaganga njaa na kulinda wale waliobadilisha katiba ili waendelee kuongoza NEC.
   
 15. M

  MULANGIRA Member

  #15
  Oct 28, 2010
  Joined: Oct 10, 2010
  Messages: 74
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  @font-face { font-family: "Times New Roman"; }@font-face { font-family: "ArialMT"; }p.MsoNormal, li.MsoNormal, div.MsoNormal { margin: 0in 0in 0.0001pt; font-size: 12pt; font-family: "Times New Roman"; }table.MsoNormalTable { font-size: 10pt; font-family: "Times New Roman"; }div.Section1 { page: Section1; } Jaji Mstaafu Makame na Tume heshimuni na lindeni uamuzi wa Watanzania

  Na
  Mwandishi wetu

  Ibara ya 74(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977 inatangaza kuundwa kwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Tume hii ni chombo muhimu sana katika kusimamia demokrasia nchini. Kwani kimepewa jukumu zito la kusimamia mchakato mzima wa kuwachagua viongozi wa nchi yetu yaani Raisi, wabunge na madiwani. Ni jukumu ambalo si tu kwamba ni zito bali pia takatifu ambalo wale ambao wamevikwa dhamana hiyo lazima wawe watu huru, wasiotiliwa shaka na watu, na ambao wataheshimu kwa dhati, ukakamavu na ushujaa mkubwa uamuzi wa wa wananchi wa Tanzania kupitia zoezi la uchaguzi mkuu.

  Kwa bahati mbaya utendaji wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo inaongozwa na Jaji Mstaafu Lewis Makame unatia mashaka makubwa kama kweli itakuwa tayari kuheshimu matakwa ya Watanzania. Kwamba utendaji wake unatia mashaka ni kunatokana na kuvurugwa kwa uchaguzi mkuu wa mwaka 1995 ambako ilibidi zoezi zima la uchaguzi katika Jiji la Dar es Salaam lifutwe na kurudiwa. Huku majimbo mengine ya mikoani watu wakiruhusiwa kuendelea kupiga kura kwa zaidi ya siku mbili. Vituo mbalimbali ambavyo watu walipiga kura kule mikoani vilitoa matokeo ya ajabu kuwa wagombea wa upinzani walipata kura sifuri hata katika vituo vile ambavyo wao walipiga kura!

  Hakuna aliyechukuliwa hatua kwa kuvurugwa kwa uchaguzi huo. Kulikuwa na kesi nyingi sana mahakamani. Dawa ya kesi hiyo ilikuwa si nyingine bali kutunga sheria ambayo iliweka vikwazo dhidi ya kufunguliwa kwazo ikiwemo na lile la kulipa shilingi milioni tano kwa kila mdaiwa kama kinga ya gharama za kesi. Aliyetoa pendekezo hilo si mwingine bali aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Tume hiyo, Augustine Ramadhani, ambaye hivi sasa ni Jaji Mkuu.

  Utendaji wa Tume hii uliendelea kujionyesha kuwa unatekeleza amri za CCM na Serikali pale uchaguzi mdogo wa ubunge wa Temeke ulivyofanyika mnamo mwaka 1996. Nguvu nyingi sana zilitumika huku Tume ikikaa na kuachia mambo yaende ilivyotaka. Kama si umakini wa mawakala na wafuasi wa NCCR-Mageuzi mwaka huo Mrema asingeshinda. Makosa ya Tume yalikuwa makubwa zaidi mwaka 2000 ambapo hata Mkuu wa Jeshi la Polisi Omari Mahita alitoa vitisho kwa CUF na kuwaambia kuwa kama wao ni Ngangari basi yeye ni Ngunguri. Na kuwa siku ya uchaguzi hakuna hata ndege atakayewika. Udanganyifu uliofanyika mwaka huo ulikuwa mkubwa lakini tume haikuona kasoro yoyote ile.


  Hali hiyo iliendelea mwaka 2005 ambapo mgombea wa CCM na kile kinachoitwa ushindi wa kishindo hakikuwa kweli kwani vurugu, wizi wa kura na kuongezwa kwa kura katika vituo ndiko ambako kulitawala. Kwamba katika kesi ya dhidi ya Wilbroad Slaa Mahakama Kuu ilithibitisha kuwa Dr. Slaa aliibiwa kura zaidi ya 5,000 ni ushahidi kuwa wizi wa kura umetawala na unabarikiwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi ambayo inaongozwa na Jaji Mstaafu Lewis Makame. Je kuna hatua ambazo Tume ilichukua dhidi ya watendaji wake wezi wa kura? Hapana. Tume iliendelea kuonyesha udhaifu mkubwa sana katika uchaguzi mdogo kule Tarime, Busanda na Biharamulo. Vitendo vya utumiaji nguvu na rushwa vilikithiri lakini Tume imekuwa ikivifumbia macho na hakuna hata mtendaji wake hata mmoja aliyeadhibiwa au kuwajibishwa.

  Hapa ndipo ninaomba nizungumzie juu ya mashaka makubwa ambayo mtu mwenye akili nzuri na timamu anayoweza kuwa nayo juu ya nia ya kweli ya viongozi wa Tume hii. Jaji Mstaafu Makame amekuwa Mwenyekiti wa Tume hii kuanzia mwaka 1993. Sifa kubwa ya mtu kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ilikuwa ni lazima awe Jaji wa Mahakama Kuu au Jaji wa Mahakama ya Rufani. Wakati ile ya Makamu Mwenyekiti wa Tume ilikuwa ni kwamba awe mtu anayeshika, aliyewahi kushika au anayestahili kuteuliwa kushika madaraka ya Jaji wa Mahakama Kuu au Jaji wa Mahakama ya Rufani. Hizo ndizo sifa zilizochangia kuchaguliwa kwa Majaji Lewis Makame na Augustine Ramadhani kwani wote wawili walikuwa ni majaji katika Mahakama ya Rufani.

  Ajabu yake pale Jaji Lewis Makame alipokuwa anafikia umri wa kustaafu serikali ilipeleka muswada ya Mabadiliko ya Kumi na Nne ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mnamo tarehe 7 Februari mwaka 2005. Miongoni mwa ibara zilizobadilishwa ilikuwa ni ibara ya 74. Hii ilibadilisha sifa za Mwenyekiti na Makamu wa Mwenyekit wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi. Ibara hiyo hivi sasa inasomeka:

  74 (1) (a) Mwenyekiti ambaye atakuwa ni Jaji wa Mahakama au Mahakama ya Rufani au ni mtu mwenye sifa ya kuwa wakili na amekuwa na sifa hizo kwa muda usiopungau miaka kumi na mitano.

  Ibara ya 74(1) (b) inarudia sifa hizo kwa Makamu Mwenyekiti wa Tume. Mabadiliko haya yalikubaliwa na Raisi Benjamin Mkapa mnamo tarehe 6 Aprili 2005. Kutokana na mabadiliko haya Jaji Mstaafu Lewis Makame ameendelea kuiongoza Tume hiyo. Hapa ndipo mtu anaweza kujiuliza je kwa nini sifa hizo zilibadilishwa kama si kwa lengo la kuhakikisha kuwa Jaji Lewis Makame anaendelea kuingoza Tume hiyo? Je, kwa nini amechaguliwa kuiongoza Tume hiyo licha ya utendaji na usimamizi mbovu wa Tume hiyo? Jibu li wazi ni kwamba waliomteua wanaridhika na utendaji huo kwani wananufaika nao.

  Ni kwa minajili hii uadilifu na kuaminika kwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Jamhuri ya Muungano ni vitu ambavyo havipo. Katika nchi ambazo watu wanaheshimu utumishi wa umma na kuepuka mgongano wa masilahi Jaji Mstaafu Lewis Makame na Mkurugenzi wake Rajabu Kiravu walitakiwa wajiuzulu. Lakini si kwetu watu hawa wameshupalia nafasi zao kwa sababu ambazo wao wanazielewa.

  Licha ya hayo yote ni kauli yangu kuwa wana jukumu kubwa la kuhakikisha kuwa wanaheshimu matakwa ya Watanzania kwani hivi sasa wananchi hawatavumilia kuona kuwa matakwa yao yanakiukwa. Ni lazima wawe wasimamizi wa haki na waheshimu uamuzi wa Watanzania. Mashaka ambayo yanazunguka uteuzi wao yanatosha kuwafanya waelewe kuwa Watanzania si watu wajinga na pale watakapoona matakwa yao yanakiukwa basi watachukua hatua zifaazo dhidi yao. Tafadhali Jaji Mstaafu Makame na wajumbe wa Tume heshimu uamuzi wa Watanzania na hakikisheni kuwa unakuwa huru, wa haki na ukweli.
   
 16. M

  MULANGIRA Member

  #16
  Oct 28, 2010
  Joined: Oct 10, 2010
  Messages: 74
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  @font-face { font-family: "Times New Roman"; }@font-face { font-family: "ArialMT"; }p.MsoNormal, li.MsoNormal, div.MsoNormal { margin: 0in 0in 0.0001pt; font-size: 12pt; font-family: "Times New Roman"; }table.MsoNormalTable { font-size: 10pt; font-family: "Times New Roman"; }div.Section1 { page: Section1; }
  Makame ni mnufaika wa mabadiliko ya Katiba

  Hadi Februari 2005 sifa za Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zilitajwa na Ibara ya 74 (1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa zifuatazo:

  Tume ya Uchaguzi
  74.-(1) Kutakuwa na Tume ya Uchaguzi ya Jamhuri ya Muungano ambayo itakuwa na wajumbe wafuatao watakaoteuliwa na Rais:-
  (a) Jaji wa Mahakama Kuu au Jaji wa Mahakama ya Rufani, ambaye atakuwa mwenyekiti;
  (b) Makamu Mwenyekiti ambaye atakuwa mtu anayeshika, aliyewahi kushika au anayestahili kuteuliwa kushika madaraka ya Jaji wa Mahakama Kuu au Jaji wa Mahakama ya Rufani;

  (c)wajumbe wengine watakaotajwa na sheria iliyotungwa na Bunge.

  Lakini ili kumlinda Jaji Makame aendelee kushika nafasi hiyo sifa hizo zilibadilishwa katika Mabadiliko ya Kumi na Nne ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yaliyofanywa tarehe 7 Februari 2005 na kukubaliwa na Raisi Mkapa mnamo tarehe 6 Aprili 2005.

  Ibara ya 74 (1)(a) na (b) hivi sasa inasomeka:

  74 (1) (a) Mwenyekiti ambaye atakuwa ni Jaji wa Mahakama au Mahakama ya Rufani au ni mtu mwenye sifa ya kuwa wakili na amekuwa na sifa hizo kwa muda usiopungua miaka kumi na mitano (Nimeongeza msisitizo)

  (b) Makamu Mwenyekiti ambaye atakuwa ni Jaji wa Mahakama au Mahakama ya Rufani au ni mtu mwenye sifa ya kuwa wakili na amekuwa na sifa hizo kwa muda usiopungau miaka kumi na mitano (Nimeongeza msisitizo)

  Kwa minajili hiyo ni wazi kuwa Jaji Lewis Makame amenufaika na mabadiliko hayo na kwa hiyo ndiyo maana anaendelea kuibeba CCM katika utendaji wake. Ni lazima kuyasema hayo na kumtaka yeye na Tume kuthibitisha uadilifu na kuaminika kwao.
   
 17. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #17
  Oct 28, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0

  Makame asituletee yale aliyokuwa akitaka kuleta mwenyekiti wa tume ya uchaguzi wa Ivory Coast katika uchaguzi wa mwaka 2000 pale alipotaka kumpa ushindi wa chee aliyekuwa rais mwanajeshi Robert Guey. Kilichotokea tunakijua -- hali ya kisiasa nchini humo haijatulia hadi leo.
   
 18. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #18
  Oct 28, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Mtuhumiwa mwingine ni Rajab KIRAVU. huyu ndiye injini ya MAKAME kwenye ishu zao za kuzidunduliza kura
   
 19. Ngisibara

  Ngisibara JF-Expert Member

  #19
  Oct 28, 2010
  Joined: Jan 2, 2009
  Messages: 2,083
  Likes Received: 431
  Trophy Points: 180
  Hii link ya kushea IP ya NEC na Kikwete inahitaji maelezo ya kina otherwise Mwanakijiji azidi kutufafanulia ni jinsi gani bado ni vigumu kura kuibiwa
   
 20. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #20
  Oct 28, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Hawajui kwamba tunajua ila wakishagundua kuwa tunajuwa watajiju
   
Loading...