Who's the hell is Lewis Makame?

Who's the hell is Lewis Makame?

@font-face { font-family: "Times New Roman"; }@font-face { font-family: "ArialMT"; }p.MsoNormal, li.MsoNormal, div.MsoNormal { margin: 0in 0in 0.0001pt; font-size: 12pt; font-family: "Times New Roman"; }table.MsoNormalTable { font-size: 10pt; font-family: "Times New Roman"; }div.Section1 { page: Section1; } Jaji Mstaafu Makame na Tume heshimuni na lindeni uamuzi wa Watanzania

Na
Mwandishi wetu

Ibara ya 74(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977 inatangaza kuundwa kwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Tume hii ni chombo muhimu sana katika kusimamia demokrasia nchini. Kwani kimepewa jukumu zito la kusimamia mchakato mzima wa kuwachagua viongozi wa nchi yetu yaani Raisi, wabunge na madiwani. Ni jukumu ambalo si tu kwamba ni zito bali pia takatifu ambalo wale ambao wamevikwa dhamana hiyo lazima wawe watu huru, wasiotiliwa shaka na watu, na ambao wataheshimu kwa dhati, ukakamavu na ushujaa mkubwa uamuzi wa wa wananchi wa Tanzania kupitia zoezi la uchaguzi mkuu.

Kwa bahati mbaya utendaji wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo inaongozwa na Jaji Mstaafu Lewis Makame unatia mashaka makubwa kama kweli itakuwa tayari kuheshimu matakwa ya Watanzania. Kwamba utendaji wake unatia mashaka ni kunatokana na kuvurugwa kwa uchaguzi mkuu wa mwaka 1995 ambako ilibidi zoezi zima la uchaguzi katika Jiji la Dar es Salaam lifutwe na kurudiwa. Huku majimbo mengine ya mikoani watu wakiruhusiwa kuendelea kupiga kura kwa zaidi ya siku mbili. Vituo mbalimbali ambavyo watu walipiga kura kule mikoani vilitoa matokeo ya ajabu kuwa wagombea wa upinzani walipata kura sifuri hata katika vituo vile ambavyo wao walipiga kura!

Hakuna aliyechukuliwa hatua kwa kuvurugwa kwa uchaguzi huo. Kulikuwa na kesi nyingi sana mahakamani. Dawa ya kesi hiyo ilikuwa si nyingine bali kutunga sheria ambayo iliweka vikwazo dhidi ya kufunguliwa kwazo ikiwemo na lile la kulipa shilingi milioni tano kwa kila mdaiwa kama kinga ya gharama za kesi. Aliyetoa pendekezo hilo si mwingine bali aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Tume hiyo, Augustine Ramadhani, ambaye hivi sasa ni Jaji Mkuu.

Utendaji wa Tume hii uliendelea kujionyesha kuwa unatekeleza amri za CCM na Serikali pale uchaguzi mdogo wa ubunge wa Temeke ulivyofanyika mnamo mwaka 1996. Nguvu nyingi sana zilitumika huku Tume ikikaa na kuachia mambo yaende ilivyotaka. Kama si umakini wa mawakala na wafuasi wa NCCR-Mageuzi mwaka huo Mrema asingeshinda. Makosa ya Tume yalikuwa makubwa zaidi mwaka 2000 ambapo hata Mkuu wa Jeshi la Polisi Omari Mahita alitoa vitisho kwa CUF na kuwaambia kuwa kama wao ni Ngangari basi yeye ni Ngunguri. Na kuwa siku ya uchaguzi hakuna hata ndege atakayewika. Udanganyifu uliofanyika mwaka huo ulikuwa mkubwa lakini tume haikuona kasoro yoyote ile.


Hali hiyo iliendelea mwaka 2005 ambapo mgombea wa CCM na kile kinachoitwa ushindi wa kishindo hakikuwa kweli kwani vurugu, wizi wa kura na kuongezwa kwa kura katika vituo ndiko ambako kulitawala. Kwamba katika kesi ya dhidi ya Wilbroad Slaa Mahakama Kuu ilithibitisha kuwa Dr. Slaa aliibiwa kura zaidi ya 5,000 ni ushahidi kuwa wizi wa kura umetawala na unabarikiwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi ambayo inaongozwa na Jaji Mstaafu Lewis Makame. Je kuna hatua ambazo Tume ilichukua dhidi ya watendaji wake wezi wa kura? Hapana. Tume iliendelea kuonyesha udhaifu mkubwa sana katika uchaguzi mdogo kule Tarime, Busanda na Biharamulo. Vitendo vya utumiaji nguvu na rushwa vilikithiri lakini Tume imekuwa ikivifumbia macho na hakuna hata mtendaji wake hata mmoja aliyeadhibiwa au kuwajibishwa.

Hapa ndipo ninaomba nizungumzie juu ya mashaka makubwa ambayo mtu mwenye akili nzuri na timamu anayoweza kuwa nayo juu ya nia ya kweli ya viongozi wa Tume hii. Jaji Mstaafu Makame amekuwa Mwenyekiti wa Tume hii kuanzia mwaka 1993. Sifa kubwa ya mtu kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ilikuwa ni lazima awe Jaji wa Mahakama Kuu au Jaji wa Mahakama ya Rufani. Wakati ile ya Makamu Mwenyekiti wa Tume ilikuwa ni kwamba awe mtu anayeshika, aliyewahi kushika au anayestahili kuteuliwa kushika madaraka ya Jaji wa Mahakama Kuu au Jaji wa Mahakama ya Rufani. Hizo ndizo sifa zilizochangia kuchaguliwa kwa Majaji Lewis Makame na Augustine Ramadhani kwani wote wawili walikuwa ni majaji katika Mahakama ya Rufani.

Ajabu yake pale Jaji Lewis Makame alipokuwa anafikia umri wa kustaafu serikali ilipeleka muswada ya Mabadiliko ya Kumi na Nne ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mnamo tarehe 7 Februari mwaka 2005. Miongoni mwa ibara zilizobadilishwa ilikuwa ni ibara ya 74. Hii ilibadilisha sifa za Mwenyekiti na Makamu wa Mwenyekit wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi. Ibara hiyo hivi sasa inasomeka:

74 (1) (a) Mwenyekiti ambaye atakuwa ni Jaji wa Mahakama au Mahakama ya Rufani au ni mtu mwenye sifa ya kuwa wakili na amekuwa na sifa hizo kwa muda usiopungau miaka kumi na mitano.

Ibara ya 74(1) (b) inarudia sifa hizo kwa Makamu Mwenyekiti wa Tume. Mabadiliko haya yalikubaliwa na Raisi Benjamin Mkapa mnamo tarehe 6 Aprili 2005. Kutokana na mabadiliko haya Jaji Mstaafu Lewis Makame ameendelea kuiongoza Tume hiyo. Hapa ndipo mtu anaweza kujiuliza je kwa nini sifa hizo zilibadilishwa kama si kwa lengo la kuhakikisha kuwa Jaji Lewis Makame anaendelea kuingoza Tume hiyo? Je, kwa nini amechaguliwa kuiongoza Tume hiyo licha ya utendaji na usimamizi mbovu wa Tume hiyo? Jibu li wazi ni kwamba waliomteua wanaridhika na utendaji huo kwani wananufaika nao.

Ni kwa minajili hii uadilifu na kuaminika kwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Jamhuri ya Muungano ni vitu ambavyo havipo. Katika nchi ambazo watu wanaheshimu utumishi wa umma na kuepuka mgongano wa masilahi Jaji Mstaafu Lewis Makame na Mkurugenzi wake Rajabu Kiravu walitakiwa wajiuzulu. Lakini si kwetu watu hawa wameshupalia nafasi zao kwa sababu ambazo wao wanazielewa.

Licha ya hayo yote ni kauli yangu kuwa wana jukumu kubwa la kuhakikisha kuwa wanaheshimu matakwa ya Watanzania kwani hivi sasa wananchi hawatavumilia kuona kuwa matakwa yao yanakiukwa. Ni lazima wawe wasimamizi wa haki na waheshimu uamuzi wa Watanzania. Mashaka ambayo yanazunguka uteuzi wao yanatosha kuwafanya waelewe kuwa Watanzania si watu wajinga na pale watakapoona matakwa yao yanakiukwa basi watachukua hatua zifaazo dhidi yao. Tafadhali Jaji Mstaafu Makame na wajumbe wa Tume heshimu uamuzi wa Watanzania na hakikisheni kuwa unakuwa huru, wa haki na ukweli.

Ilisemwa siku nyingi kuwa Makame hastahili kuwa mwenyekiti wa hiyo tume hata kidogo. Kiravu umri wake wa kustaafu umefika na ameongezewa muda kigezo cha kuongezewa muda kilikuwa nini??? Je hakukuwa na watu wanaofaa kwenye nafasi hiyo. Kuna majaji wastaafu watatu ambao ni wajumbe wa tume je ilikuwa ni lazima wawe pale, hakukuwana watu competent kujaza hizo nafasi? Kiukweli hawa wote watamtetemekea aliyewapa ajira na aliyewa ajira ni, Raisi a Jamhuri ambaye ni Mgombea wa Uraisi.

Katika hali kama hii Unategemea nini?
 
Ilisemwa siku nyingi kuwa Makame hastahili kuwa mwenyekiti wa hiyo tume hata kidogo. Kiravu umri wake wa kustaafu umefika na ameongezewa muda kigezo cha kuongezewa muda kilikuwa nini??? Je hakukuwa na watu wanaofaa kwenye nafasi hiyo. Kuna majaji wastaafu watatu ambao ni wajumbe wa tume je ilikuwa ni lazima wawe pale, hakukuwana watu competent kujaza hizo nafasi? Kiukweli hawa wote watamtetemekea aliyewapa ajira na aliyewa ajira ni, Raisi a Jamhuri ambaye ni Mgombea wa Uraisi.

Katika hali kama hii Unategemea nini?
Mkuu tumesema sana hilo lakini serikali ya sisiemu ambayo ndiyo inateua majaji wa mahakama ya rufaa wameweka pamba masikioni.
Neno lako nitalizungumza kwenye sanduku la kura hapo jumapili
 
we muache atoe macho kama kakamatwa ugoni siku ya kupanda kizimbani ikifika ataisoma namba
Wayasalimishe hayo mabox fake tunayoelezwa kutua huko ngerengere kabla hali haijabadilika. Sasa hivi hatuwaoni usoni, this is a new era.
 
Mzee una nafasi kubwa ya kuweka historia na kurudisha heshima yako iliyopotea.

Uwe tayari kuweka historia pale utakapotangaza rais mpya kabisa wa chama kipya kabisa nchi hii.

Kuvuruga uchaguzi kama miaka iliyopita is not acceptable and you may pay for that!

For me kura is not a secret issue, sijaona popote ilipoandikwa sheria kuwa iwe siri! upinzani wana kura zangu zote!!!!! Ila asiposhinda mtu wangu nitakaa chini na kujiuliza swali hili zito
Why on earth did upinzani decided to go for election knowing than NEC is belong to CCM??

Baada ya uchaguzi nadhani ni muda mwingine wa wale wote mnaojiita wanachadema kukaa chini humu ndani na kusafisha jukwaa ambalo limeoza kwa upupu wenu wa ushabiki na kushindwa kujenga hoja zenye mshiko! hakuna hoja, point, utetezi wote wa maana ulio na akili ya wazi unaofanywa na baadhi ya wanachadema inayoweza kuwafanya watu waseme JF ina great thinkers. I may forgive you because of stress and panic this time, but your mess is there! you will need to clean it ASAP whether Slaa will be president or not!

Chadema hoyee!
 
Haya wakuu.
kwa yaliyotokea kwenye vituo vya kupiga kura hayatoshi kuongezea kwenye fomu ya mashtaka dhidi ya makame and the gang?
 
Ucheleweshaji wa kutangaza matokeo unaashiria kuwa Lewis Makame anakaribia kuwa Kivuitu. Hali ninavyoiona si nzuri sana. Je jaji Makame atazinduka na kuacha matokeo ya uchaguzi yawe sawasawa na maamuzi ya Watanzania badala ya CCM na NEC?
 
Pengine tatizo ni uzee! Kuna vijana wengi tu wanaoweza kuendesha NEC kwa uzuri zaidi
 
Ishu ni kumtokezea tu huyu!
Kwanini hakemei mambo mazito hivi?
Nasikia Makamba yuko Shinyanga kujaribu kununua jimbo pale...sijui itakuwaje!
 
Hawa watu wanataka kuleta balaa hapa!!!

I wonder!!!:doh:
 
Hawa watu wanataka kuleta balaa hapa!!!

I wonder!!!:doh:

Tatizo NEC na CCM hawajifunzi. Wamejaa kiburi cha kifisadi, hawajui kuwa nchi siyo ya NEC wala CCM ni ya Watanzania. NEC na CCM wanataka kujaribu kuwachagulia Watanzania wabunge wao na Rais wao. Kama Watanzania wamemkataa JK na kumchagua Dr. Slaa ndivyo wanavyotaka na walivyoamua nchi yao iongozwe na si vinginevyo.
 
Mchakato wa kujenga demokrasia ya vyama vingi haufanikiwi kwa sababu ya matukio kama haya yanayaoendelea. Hapa ndiyo umuhimu unaonekana dhahiri kuwa iteuliwe Tume ya Uchaguzi ambayo wajumbe wake watapendekezwa na vyama vyote vya siasa ambayo ndiyo itakuwa na jukumu la kusimamia uchaguzi.

Tume ya Uchaguzi inatiliwa shaka na vyama vya upinzani kuwa inapendelea upande wa chama cha Mapinduzi. Haki inaonekana haitendeki kabisa. Vyama vya upinzani na wananchi kwa ujumla wake hawana imani na Tume ya Uchaguzi. Kuna umuhimu wa kuwa na Tume ya Uchaguzi ambayo haitiliwi shaka hata kidogo.

Tazama, mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi anateuliwa na Rais ambaye naye ni Mwenyekiti wa chama Tawala CCM, anaingia katika kinyang'anyilo na wenyeviti wa vyama vingine. Uongo umebaridiri sura, zama hizi ni sawa na zile zama za Mwalimu ambapo, watu walikua wakiwekewa sura ya mtu na mgombea kivuli alaf wanaambiwa wanaambiwa wafanye uchagizi.

Laiti ningekua mimi ni Jaji Makame ningejuzuru katika wadhifa huo kuliko kutumika vibaya kama anavyotumika hivi sasa.
 
Hekima na busara vikitawala anaweza fanya ivyo otherwise atakomaaa mpaka 2015
 
Silipendi hili lizee mpaka basi na mwenzie kiravu wanafiki wakubwa.
 
Kwa uelewa zaidi,ni sawa na mechi ya simba na yanga then timu moja ndio inamchagua refa wake,kwa sababu zake na vigezo ambavyo si vya maridhiano na timu pinzani.Hapo ni wazi aliyemchagua refa ndio atashinda.Huyu Makame alishastaafu,lakini bado akateuliwa kuja kutuibia kura.Prof Mwesiga Baregu ambaye ni mtaalamu wa siasa aliyekwa akifundisha Udsm na mchango wake ulikuwa muhimu wa haki na maendelea saana katika nyanja ya elimu tena chuo chenyewe kilisema hana mbadala na kuna upungufu mkubwa wa wataalam hivyo huduma yake inahitajika sana.Serekali ikasitisha mkataba wake eti muda wa kustaafu umefika,wa muhim uhapa yupi?mwizi makame au mhadhiri BareguNafikiri hii serekali imekuwa sawa na wale wayahudi waliotaka Yesu asulubiwe mpaka kufa,na aachiwe baraba,muovu aliyekuwa kifungoni.Sasa hawa CCM wanatupeleka wapi? Nafikiri wadau wameliona na wakiingia mjengoni nafikiri swala moja wapo ni kuhakikisha swala la tume huru inayokubalika pande zote linafanyiwa kazi ipasavyo.
 
Back
Top Bottom