Candid Scope
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 11,897
- 6,933
Kweli Tanzania hatutaendelea, watawa wanafanya njama za kuua kwa ajili ya pesa eti unawaita wahuni.
Ama kweli Tanzania italiwa kwelikweli, maana maliasili zinaondoka bado tunawatetea wahalifu.
Hiyo skandali ni kweli kabisa na shirika ndio lililokuwa linamiliki mgodi, hapa hakuna kumunya munya. Kwenye hili hakuna siri. Juu ya mauaji ya Prof sijui.
Subirini CHADEMA washinde migodi yote itamilikiwa na Shirika wakisaidiwa na Ujerumani. Hapa ndio mwisho wa Tanzania.
Wewe vilevile you're guilty sababu una-propagate na ku-sensationalize upuuzi kama huu. Kama hii habari ungeiacha kule Raia Mwema, sidhani kama kuna mtu angehangaika nayo, maana ni ujinga mtupu.
Nikilinganisha hizi habari, Raiamwema siwaelewi kabisa
Rwanda yatajwa kifo cha Prof. Mwaikusa | Gazeti la MwanaHalisi
Habari hiyo imeshanukuliwa na vyombo vingi.
Kunyamazia upuuzi huu maana yake kushabikia vyombo hivyo vya habari viendelee kufanya upuzi ule ule, lazima kieleweke na wafanye tathmini ya kutosha kabla ya publication. Tukinyamaza kesho watafanya mabaya zaidi ya hili. Unachotaka mwanao anapoharibi kitu ni kunyamazia tu badala ya kufanya jitihada kuonya asirudie makosa hayo.
Mkuu wa Shirika la Peramiho Benedictine Fathers (OSB) Abate Lambert kwenye picha hiyo aliyeko mbele mstari wa nyuma mpenda watu, mleta maendeleo na usitawi wa wananchi wengi ukanda wa Ruvuma na Kusini nyanda za juu kwa wengi wanashangazwa na habari hiyo toka Raia Mwema yenye taswira ya kuchafua badala ya ukweli halisi.
Bahati nzuri siku za nyuma nilipokuwa mwanahabari nilifanikiwa kuwepo kikazi maeneo hayo mwenyeji wangu akiwa Ahmed Jongo. Baadhi ya watajwa nawafahamu si kitu cha kawaida kufanya jambo kama hilo ukitilia maanani ninavyomfahamu Abate Lambert Dor na anavyoheshimika katika Jimbo la Songea na majimbo yandokando na naendeleo kwa wananchi. Hospitali ya St. Joseph Peramiho ndio kimbilio kubwa ukanda huo. Shule ya sekondari Peramiho imetoa wasomi wengi wa kike nchini. Kuna mengi naona wasioijua Peramiho ndio wanaoweza kuzusha mambo yasiyo na kichwa wala miguu, flagment.
Kwa hiyo inaonekana nia yako ya kubandika maada hii is just so that kwamba wewe mwenyewe, pekee yako na kwa juhudi zako binafsi, uweze ku-refute every single issue mentioned in the story, au siyo? Waingereza wana msemo "Dont bite more than you can chew". Sasa una kazi kubwa sana, maana kuna watu wa kila aina humu ndani wenye backgrounds and convictions za kila namna. Jee, unaweza kuwaridhisha wote kwa maandishi yako pekee yake?
UKIINGIA KWENYE BIASHARA UNAKUWA UMETOKA KWENYE UTAKATIFU. sishangai sana kama wakihusishwa.biashara maana yake faida.faida ni kwa njia yeyote ikiwemo kukwepa kodi, magendo, kuua yeyote anaye kukwamisha kupata faida n.k
Nijuacho ni kuwa prof aliuawa na watu wanaozaniwa ni toka burundi na rwanda nse prof alikuwa anasimamia baadhi ya kesi
Hii ya leo ndo nashangaa ila kama wanahusika hao watawa mbona wangetumia mbinu zingine kutekeleza hayo bse prof aloshindiliwa risasi za kutosha na mpaka leo kimya
Taarifa inasema aliuwa na majambazi akiwa ndani ya gari mbele ya get la nyumbani kwake, wakati anajiandaa kuingia ndani, 'majambazi' hao walikimbia mara baada ya tukio hilo bila ya kuchukua kitu chochote. Hiyo ni taarifa Polisi kwa mujibu wa mlinzi. Sasa hapa sijui ni documents zipi walizopora na je wanasheria huzurula na documents halisi au vivuli?
Taarifa nyingine, nje ya jeshi la Polisi na mlinzi iliihusisha serikali ya Kagame na mauaji yale, na nyingine ikaihusisha serikali ya Tanzania, kuwa ilitelekeza hayo kwa lengo la kufukia ukweli juu ya suala la balali.
Na sasa hv tena kuna wachunguzi wanakuja na taarifa zao kuhusu uhusika wa shirika la kitawa.
Inawezekana kabisa ikawa hivyo, lakini msingi wa vielelezo vinavyojengwa ni dhaifu sana kubeba tuhuma.
Inafahamika kuwa prof Mwaikusa aliuwawa na serikali ya kagame nd hili linahusishwa sana na yeye kujiingiza na siasa za mauaji ya kimbarik nchini Rwanda...Raia mwema
chini ya uenyekiti wa Jeneral Ulimwengu
wana interest na ukaribu na rwanda na hapa wanajaribu kupotosha
Nikilinganisha hizi habari, Raiamwema siwaelewi kabisa
Rwanda yatajwa kifo cha Prof. Mwaikusa | Gazeti la MwanaHalisi