William J. Malecela
R I P
- Apr 27, 2006
- 26,584
- 10,466
hata mimi nakubaliana nawe katika hili.. Salim muda wake uimeshapita hawezi tena mitulinga ya nchi hii hasa baada ya Kikwete. Utawala unaofuata sasa hivi lazima apatikane mtu kuyafanya yale aliyoshindwa Kikwete na sio kurudi nyuma tena kama vile nchi iko shwari.
Mkuu Mwanahabari,
Ni kweli Mwandosya alikuwa amefanikiwa kwa kiasi fulani lakini hakuwa tajiri wa kutanua. Matanuzi yameonekana kuongezeka alipokuwa PS ambapo u-consultant ulikuwa haupo tena. Huko wizarani ndio alipoona utamu wa siasa na kuamua kwenda kugombea ubunge ili asiwe tu PS bali awe ndio waziri kabisa. Na kati ya alivyotuletea pamoja na utaalamu wake wa electronics ni hiyo ndege na radar. Hivi vyote alivitetea bungeni.
Nijuavyo mimi ni kuwa ile ndege ni pre-owned, maana GS 550 bei yake ni zaidi ya $50million, ni ndege ya anasa. Boeng 737-600 mpya kutoka kwenye makaratasi, Boeng wenyewe wanaweza wakakupa kwa bei sawa na ya GS 550. Sasa kwa ukonsaltanti wa Mwandosya kwa nini hakuishauri serikali vizuri wakati national airline ilikuwa inarusha Boeng 737-200 ambazo hata uundwaji wake umesitishwa? Huyu bwana ana maswali mengi ya kutujibu.
_________________________
Kaka ukitoa suala la kiitikadi, vita kubwa ya wamarekani ilikuwa ni role yake katika kuhakikisha China inaingia katika umoja huo na kuwaondoa Taiwan ambao walikuwa na hadi sasa ni wafuasi wa wamarekani.
Salim na Tanzania ndio walikuwa wakiongoza mchakato wa kuhakikisha China inapewa uanachama na pia ile hadhi ya uanachama wa kudumu. Salim na wenziwe waliingia wakicheza ngoma ukumbini kufanikiwa hilo na siku ileile Bush akiwa kama balozi wa marekani UN alimpatia ujumbe kuwa ajiandae kupambana nao. Mpambano ambao uliendelea hadi wakati wa uchaguzi wa 2005.
Lingine lilikuwa ni role yake katika harakati za ukombozi wa mataifa ya kusini mwa afrika. Yeye akiwa hapo alikuwa frontman muaminifu wa Mwalimu katika harakati zake za ukombozi barani Afrika.....
Hujaongelea msimamo wake kuhusu Palestina..
Ukweli ni kuwa mpambano ulikuwa mkubwa na vita bado inaendelea kama ambavyo harakati za uchaguzi wa 2005b zilivyonyesha.....
omarilyas
Hizi habari nili zisikia tu kwa maana zina tokea wengine watoto au hatuja zaliwa.. Nime pata kusikia kuwa miaka ya themanini...........................
MwanaFalsafa,
Ni kweli kabisa; wengine tulikuwa ndio kwanza tumejiunga secondary school wakati Salim Ahamed Salim alipotikisa dunia kule UN na kidogo awe katibu mkuu wa UN.
Mpambano mkali ulikuwa kati yake ni Kurt waldheim ambaye alikuwa ndiye katibu mkuu na alitaka kuendelea. USA walikuwa wanamuunga mkono yeye na waliamua kumpinga Salim kwa nguvu zote. Wote wawili walikuwa na kura za kutosha kuwa katibu mkuu ila USA ili veto kwa Salim na China ku veto kwa Waldheim.
Baada ya round tatu Waldeim akaamua kujitoa na Salim akabaki peke yake bado USA ili veto na hivyo na yeye kulazimika kujitoa na Pereze Cuellar akachaguliwa kirahisi kuwa katibu mkuu.
Balozi wa USA aliyekuwa anamlima Salim muda wote alikuwa ni Jeane Kirkpatric chini ya rais Reagan. Tena kwenye mazungumzo alikuwa anafurahisha kwa kusema anampenda sana Salim kama binadamu lakini kwa amri ya nchi yake ataendelea kupiga veto. Rais Reagan alikuwa ndio kwanza ameingia madarakani na siasa zake za ubabe. Labda Carter angelikuwa bado rais huenda Salim angeshinda.
Wakati huo tulikuwa tunashinda kwenye radio kusubiri mwana wa Tanzania Salim Ahmed Salim atangazwe katibu mkuu, lakini bahati haikuwa yetu. Nashangaa siku hizi eti kuna watu wana hata nguvu ya kusema Salim sio Mtanzania.
Bora wewe ulikuwa walau una akili mkuu. Wengine hata hatukuwa tuna tarajiwa. Kwa hiyo walitoa sababu gani za kumpinga? Au ndiyo mambo ya vita baridi na walikua hawana haja ya kutoa sababu za msingi? Je Salim alikuwa na uwezo wa kikazi wa kupewa nafasi hio?
Sasa nimeanza kupata picha. Je una taarifa yoyte kuhusu huyo Waldheim in regards to his qualifications? Ukilinganisha yeye na Salim nani ali stahili? Na je Pereze Cuellar alikua na uwezo kuhusu hawa jamaa wawili au ndiyo hivyo tena he was a compromise choice only?
Ukitoa na suala la sifa na itikadi za Kurt pia kulikuwa na suala la yeye kuwa mfuasi wa Hitler wakati fulani tena katika level nyeti. Hili lilifichwa na kukandamizwa na wamarekani lakini lilikuwa wazi miongoni mwa mataifa ya dunia ya tatu (G77). Suala hili liliibuka rasmi aliporudi Austria na kugombea nafasi ya u-chancellor na kulazimika kujitoa ama kujiuzulu hapo baadae.
Kuhus Salim, nimekuwa nikifanya uchunguzi kuhusiana na UN...ukweli ni kuwa kila niongeaye naye na kujitambulisha kuwa ni mtanzania ni majina matatu hujirudia na kupambwa sana...Mwalimu Nyerere, Salim Ahmed Salim na Balozi wetu wa sasa huko, Dr Augustine Mahiga.
Ukiangalia kamati za umoja wa mataifa ambazo Salim alikuwa akiongoza ukitoa suala la uenyekiti wa baraza la usalama ambao kila taifa linaloweza kupata uanachama huko uwe wa miaka miwili ama wa kudumu hupewa nafasi hiyo kwa mwezi mmoja na urais wa Baraza kuu (GA), Salim alikuwa mstari wa mbele sana katika shughuli zingine haswa zile za ukombozi, mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi, na hata ajenda za kiuchumi za nchi za dunia ya tatu.
Ukiwa balozi wa nchi changa kama Tanzania yenye kiongozi asiyeaminiwa na hata kuchukiwa mabepari na wafuasi wao duniani kote kama Mwalimu Nyerere, ni wazi lazima ukubalike sana miongoni mwa wawakilishi wa mataifa mbalimbali katika umoja huo ili upate nafasi za kuongoza kamati na ajenda mbalimbali huko.
Hata hivyo ni lazima tukumbuke kuwa kushabihiana kimitazamo na ajenda kati ya Salim na Nyerere ambaye wakati huo ndio alikuwa wizara ya mambo ya nje na kila kitu, na pia imani ambayo MWALIMU aliyokuwa nayo kwake, ni wazi kulimsaidia sana katika kufanikisha utendaji wake huko.....
omarilyas
Mwanafalsafa1,
..Dr.Kurt Waldheim alikuwa UN SG tayari na alikuwa anagombea kwa kipindi cha 3.
..kwa kawaida UN SG hugombea vipindi viwili tu. kuna wengine,kama Dr.Botrous Ghali wa Egypt, ambao walipata matatizo na kuondolewa ktk nafasi hiyo baada ya kipindi kimoja.
Mtanzania,
..kwa upande wangu naona kama Tanzania tulikuwa overly ambitious, au naive, na siasa za uchaguzi wa UN SG.
..msimamo wetu ktk siasa za kimataifa za wakati ule ulikuwa umetuweka ktk upande tofauti na interest za wakubwa--USA na UK.
..ilitupasa kuelewa kwamba mgombea yeyote yule toka Tanzania angepingwa na mataifa hayo mawili makubwa, lakini haswa haswa USA.
..kuna mahali nilisoma kwamba alikuwepo MLIBERIA ambaye alikuwa mtumishi wa muda mrefu wa UN. inasemekana AFRICA ingempendekeza huyo at least kulikuwa na uwezekano angeungwa mkono na USA.
NB:
..kampeni za kugombea UN SG zina gharama kubwa sana.
..wakati ule tulikuwa na hali mbaya sana ya kiuchumi.
..sijui ni nani alikuwa akilipa gharama hizo, labda CHINA.
Another element katika veto ya Wamarekani ni ile ninayoita "missed opportunity." Kama alivyosema Mtanzania Jean Kilkpatrick kweli alikuwa ana affection na Salim kwa sababu walishafanya kazi naye pale UN. Katika juhudi za kumsaidia Salim alifanya mpango akutane na Alexander Haig wakati huo ndiye aliyekuwa Secretary of State. Mkutano ukapangwa na Salim akakubali. According to Balozi Bomani, a day before the meeting Alexander Haig alipata safari ya ghafla kwenda Middle East akamwachia deputy wake jukumu la kukutana na Salim. Lakini Salim aliposikia Haig yuko out of town alikataa kwenda Washington licha ya Balozi Bomani kumsihi. So as they say, the rest is history. Wamerikan wakatranslate the no show ya Salim kama snub huku Salim naye akitranslate kuondoka kwa Alex Haig kama snub. That was the end of it. Mwanafalsafa, kwa kawaida Marekani haitoi sababu inapopiga veto against a SG.