Who is Salim Ahmed Salim?

hata mimi nakubaliana nawe katika hili.. Salim muda wake uimeshapita hawezi tena mitulinga ya nchi hii hasa baada ya Kikwete. Utawala unaofuata sasa hivi lazima apatikane mtu kuyafanya yale aliyoshindwa Kikwete na sio kurudi nyuma tena kama vile nchi iko shwari.

Ahsante mkuu Bob, kwa kunielewa hoja yangu kwamba Salim ni kweli ana CV nzito sana, lakini kwa siasa za Tanzania, ni too much kwake kwa sasa hivi, kusema kwamba eti atakuja kumshinda Kikwete akiwa rais tayari wewe unajua better kuwa hilo halitakuja kutokea,

Mimi ninaheshimu uamuzi wake wa kujitoa kabisa na siasa za bongo, lakini bado Salim ni one of our best represantantives huko nje kama sio all the time.
 
kubwajinga,mwanahabari,

..napendekeza Prof.Mwandosya aliondolewa Wizara ya Nishati na kupelekwa viwanda baada ya kuonekana kwamba ni kikwazo kwa ufisadi uliokuwa ukiendelea pale.

..Prof alitaka kukataa tranfer hiyo na kujiuzulu lakini wapo watu wazima waliomsihi asifanye hivyo.

..mwaka 1995 wana mtandao walijaribu kumchongea Msuya kuwa ndiye aliyesababisha Mwandosya aondoke serikalini. ukweli ni kwamba waliochefua Mwandosya na civil service ni Mzee Mwinyi na Kikwete.

..suala la rada lilianza toka wakati wa Mzee Mwinyi. kwa hiyo tusubiri tuone huu uchunguzi utaishia wapi.

..kuhusu ununuzi wa ndege ya Raisi hapo naamini kabisa Prof.Mwandosya anawajibika kujibu tuhuma zote zinazojitokeza.

Mkandara,

..nina maswali kuhusu zile pickup za jeshi. kuna habari mitaani kwamba ilikuwa ni "zawadi" aliyopewa SAS binafsi.

..kuna sheria inayodhibiti zawadi wanazopewa watumishi wa umma. kwa msingi huo SAS alifuata sheria kama ni kweli Waarabu walimpa zawadi ya pickups zaidi ya 70.

..swala linalojitokeza hapa ni kwanini Waarabu wale wampe magari 70. tena yote yawe ni pickup toyota landcruiser.

..Waarabu walimpa magari yote yale wakitarajia akafanye nayo nini? hivi haiwezekani kwamba serikali ndiyo iliyoomba msaada huo?

..pia WAARABU waliotoa magari yale ndiyo hao hao walioshia kumilikishwa eneo la mbuga ya LOLIONDO?

GAME THEORY,

..watu kama Salim Salim ndiyo wamefaidi matunda ya Uhuru na kuwa mabalozi wa Tanzania.

..wakati akiwa Balozi serikali ilikuwa inasomesha watoto wa mabalozi kuanzia chekechea mpaka yule wa University.

..Kwa kifupi mabalozi wanalipiwa gharama zote za maisha isipokuwa mavazi yao.

..ukiteuliwa Ubalozi Tanzania hiyo ndiyo tiketi yako out of poverty.

FMES,

..hata mimi nakubali kwamba CV ya SAS ni ya nguvu kwelikweli.

..lakini sidhani kama tunahitaji Raisi mwenye CV kama ile aliyonayo SAS.

..Kwa kweli Tanzania ya leo inahitaji Raisi atakayesimamia shughuli za maendeleo, na siyo Raisi "kiguu-na-njia" anayeshugulika na international policy na diplomacy.

..wakati umefika kwa Tanzania kusifiwa kutokana na bidhaa zake, shule na vyuo vyake, bararabara zake, bandari, reli etc etc.

..Sifa kubwa ya Tanzania huko nje ni kwamba it is the birth place of Dr.Julius Nyerere. wasiwasi wangu ni kwamba mtu kama SAS anaweza kuiga international activism ya utawala wa Mwalimu. We do not need that in this era.
 
Mkuu Mwanahabari,
Ni kweli Mwandosya alikuwa amefanikiwa kwa kiasi fulani lakini hakuwa tajiri wa kutanua. Matanuzi yameonekana kuongezeka alipokuwa PS ambapo u-consultant ulikuwa haupo tena. Huko wizarani ndio alipoona utamu wa siasa na kuamua kwenda kugombea ubunge ili asiwe tu PS bali awe ndio waziri kabisa. Na kati ya alivyotuletea pamoja na utaalamu wake wa electronics ni hiyo ndege na radar. Hivi vyote alivitetea bungeni.

Nijuavyo mimi ni kuwa ile ndege ni pre-owned, maana GS 550 bei yake ni zaidi ya $50million, ni ndege ya anasa. Boeng 737-600 mpya kutoka kwenye makaratasi, Boeng wenyewe wanaweza wakakupa kwa bei sawa na ya GS 550. Sasa kwa ukonsaltanti wa Mwandosya kwa nini hakuishauri serikali vizuri wakati national airline ilikuwa inarusha Boeng 737-200 ambazo hata uundwaji wake umesitishwa? Huyu bwana ana maswali mengi ya kutujibu.

_________________________

G550 ilikuwa Mpya Kabisa, na Tanzania Govenrment FLight Agency walikuepo Marekani wakisimamia na kuifanyia majaribio Savannah Georgia ambako they build the Gulfstream. Ilikuwa Custom Made to Tanzanian Specifications including APU design and other performance settings, na walikabidhiwa ndege na CEO wa Gulfstream kiwandani ----> Ongea na CEO TGFA/John Mkony Pilot wa Rais, Alikuwepo kule na atakupa uthibitisho zaidi.

Kuhusu Air Tanzania, ile ni Shirika la kibiashara ambalo management mbovu ya miaka mingi, hata wangepewa ndege mpya, ni shirika ambalo serikali ishauriwe itupiliwe mbali, uza kila kitu, hata wabunge wengi walisita kuongezea hela lile kampuni.

Yeye ni consultant wa mambo ya Engineering na mazingira, na kuhusu ndege mambo yote ya negotiations za bei, na mikataba yanashughulikiwa na Attourney General na Wizara ya Fedha. Wizara ya Mawasiliano inahusika na Certifying na registering the plane na uchunguzi wa kitaalamu kupitia TGFA (na rada kupitia watu wa CIvil aviation). Yeye kama waziri anawasilisha reports anazopewa na watu wake wizarani bungeni na kwenye baraza la mawaziri ili ipitishwe, hawezi tu kusimama na kusema nunueni 737-600 wakati wataalam wametoa recommendation ya G550 baada ya kupitia ndege nyingi tu ikiwemo Boeing BBJ, na baraza la mawaziri kupitia kabla haijawasilishwa bungeni , na wabunge kupitisha.

Kama vilikuwa havihitajiki, Bunge lisingepitisha. Kuhusu Rada, malipo yalikuwa yameshaanza kutolewa wakati yeye anaingia Uwaziri hata ukisoma Hansard za bunge anakupa timeline na kwanini Rada ilihitajika (sasa kama wakina CHenge walikula dili wakati wanagawa pesa, hiyo ni issue ya kuchunguza), kuhusu Gulfstream you have to look at the Cost of it spread over 50 yrs, thats 1 million US a yr, Ikulu ya JK tayari imetumia zaidi ya dola Millioni 54 (thats just for a quarter of 2006/2007 3 mnths!!!)kwa sababu tofauti zikiwemo safari zake ambazo hatumii hii ndege.

Tanzania Government Flight linaendesha ndege za Serikali mbili ambazo ni Fokker (the company doesnt even exist anymore) na ile anayotumia Rais F28 ilinunuliwa 1978! G550 imenunuliwa ili itumike sawa sawa for more than 50 years, ina moja performance na range kubwa kuliko ndege nyingi sasa, ikitumiwa sawasawa its cheaper to use over the years kuliko kutumia commercial. Sasa Kama raisi wa sasa hataki kuitumia na kusafiri na Emirates and the rest first class na team ya watu 50 ambayo gharama zake zinatisha, hilo ni chaguo lake. Ndege ilinunuliwa ili itumike. Ndege mpya was the right choice.

G550 can fly 18 (yetu nadhani up to 20 people) passengers up to 6,750 nautical miles (12501 kilometers) nonstop at a cruising speed of .885 Mach and at an altitude of up to 51,000 feet. uwezo wa kutua viwanja vidogo ambavyo 737 haiwezi, this means kwasababu za kiusalama kiongozi anaweza kutumia viwanja vidogo na rahisi kumsafirisha kiongozi kuliko kutumia commercial airport.

Mwisho I agree, Maswali mengi ya kujibu.
 
Jokakuu,
Mkuu nimeshindwa kuelewa ulichotaka kufahamu toka kwangu.

Ikiwa Salim alipewa hizo gari 70 na akazipeleka jeshini, mimi nitasema kitu gani zaidi..hata kama ilikuwa deal la serikali ni lazima kuna mtu aliyepeleka maombi hayo. hata deal la rada wapo wahusika kamili ambao leo tunataka wafikishwe mahakamani hatuwezi kusema ilikuwa ni serikali hivyo hakuna mhusika.

Sielewi kama alipewa yeye hizo gari kama zawadi ama ni ktk kuiwakilisha serikali lakini la muhimu hapa ni kwamba magari hayo yalipatikana bure bila kuigharimu serikali yetu. Who was the man behind?...
 
Hizi habari nili zisikia tu kwa maana zina tokea wengine watoto au hatuja zaliwa.. Nime pata kusikia kuwa miaka ya themanini Salim Ahmed Salim alikua front runner katika kuwa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa.

Nikaendelea kusikia kuwa kwa ajili sisi tulikua na mfumo wa ujamaa Warusi wali support Salim kupewa lakini Wamarekani na ubepari waka pinga hili. Ikawa zuta niku vute mpaka waka amua kumpa mtu neutral ambae ange kubalika na Wamarekani na Warusi. Je kuna mwenye taarifa ili kuaje kuaje ili sisi wengine tuelewe vizuri zaidi?
 
Kaka ukitoa suala la kiitikadi, vita kubwa ya wamarekani ilikuwa ni role yake katika kuhakikisha China inaingia katika umoja huo na kuwaondoa Taiwan ambao walikuwa na hadi sasa ni wafuasi wa wamarekani.

Salim na Tanzania ndio walikuwa wakiongoza mchakato wa kuhakikisha China inapewa uanachama na pia ile hadhi ya uanachama wa kudumu. Salim na wenziwe waliingia wakicheza ngoma ukumbini kufanikiwa hilo na siku ileile Bush akiwa kama balozi wa marekani UN alimpatia ujumbe kuwa ajiandae kupambana nao. Mpambano ambao uliendelea hadi wakati wa uchaguzi wa 2005.

Lingine lilikuwa ni role yake katika harakati za ukombozi wa mataifa ya kusini mwa afrika. Yeye akiwa hapo alikuwa frontman muaminifu wa Mwalimu katika harakati zake za ukombozi barani Afrika.....

Hujaongelea msimamo wake kuhusu Palestina..

Ukweli ni kuwa mpambano ulikuwa mkubwa na vita bado inaendelea kama ambavyo harakati za uchaguzi wa 2005b zilivyonyesha.....

omarilyas
 
Asante sana mkuu. Bado uelewa wangu ni mdogo kuhusu swala hili kwa usi shangae kama niliacha baadhi ya vitu. ndiyo nia ya kuianzishia thread nijue zaidi. Je Salim isinge kuwa tofauti za kiitikadi angepewa? Kwa maana uchapaji wake kazi ulikuwa una kubalika? Au hiyo nafasi ya katibu mkuu siku zote ni vita za kiitikadi na maslahi tu?
 
Hizi habari nili zisikia tu kwa maana zina tokea wengine watoto au hatuja zaliwa.. Nime pata kusikia kuwa miaka ya themanini...........................

inaonekana wewe ni kijana mdoogo sana!
na unazifuatilia siasa kwa level KUBWA!

keep it up mdogo wangu,utaenjoy
 
MwanaFalsafa1,

Ni kweli kabisa; wengine tulikuwa ndio kwanza tumejiunga secondary school wakati Salim Ahamed Salim alipotikisa dunia kule UN na kidogo awe katibu mkuu wa UN.

Mpambano mkali ulikuwa kati yake ni Kurt waldheim ambaye alikuwa ndiye katibu mkuu na alitaka kuendelea. USA walikuwa wanamuunga mkono yeye na waliamua kumpinga Salim kwa nguvu zote. Wote wawili walikuwa na kura za kutosha kuwa katibu mkuu ila USA ili veto kwa Salim na China ku veto kwa Waldheim.

Baada ya round tatu Waldeim akaamua kujitoa na Salim akabaki peke yake bado USA ili veto na hivyo na yeye kulazimika kujitoa na Pereze Cuellar akachaguliwa kirahisi kuwa katibu mkuu.

Balozi wa USA aliyekuwa anamlima Salim muda wote alikuwa ni Jeane Kirkpatric chini ya rais Reagan. Tena kwenye mazungumzo alikuwa anafurahisha kwa kusema anampenda sana Salim kama binadamu lakini kwa amri ya nchi yake ataendelea kupiga veto. Rais Reagan alikuwa ndio kwanza ameingia madarakani na siasa zake za ubabe. Labda Carter angelikuwa bado rais huenda Salim angeshinda.

Wakati huo tulikuwa tunashinda kwenye radio kusubiri mwana wa Tanzania Salim Ahmed Salim atangazwe katibu mkuu, lakini bahati haikuwa yetu. Nashangaa siku hizi eti kuna watu wana hata nguvu ya kusema Salim sio Mtanzania.

China ilikuwa inalipa fadhila za kuiunga kuingia UN na ilisema itaendelea ku veto candidate mwingine yeyeote mpaka labda Salim ajitoe. USA walikuwa wanaona Salim ni Mkomunist.
 
MwanaFalsafa,

Ni kweli kabisa; wengine tulikuwa ndio kwanza tumejiunga secondary school wakati Salim Ahamed Salim alipotikisa dunia kule UN na kidogo awe katibu mkuu wa UN.

Mpambano mkali ulikuwa kati yake ni Kurt waldheim ambaye alikuwa ndiye katibu mkuu na alitaka kuendelea. USA walikuwa wanamuunga mkono yeye na waliamua kumpinga Salim kwa nguvu zote. Wote wawili walikuwa na kura za kutosha kuwa katibu mkuu ila USA ili veto kwa Salim na China ku veto kwa Waldheim.

Baada ya round tatu Waldeim akaamua kujitoa na Salim akabaki peke yake bado USA ili veto na hivyo na yeye kulazimika kujitoa na Pereze Cuellar akachaguliwa kirahisi kuwa katibu mkuu.

Balozi wa USA aliyekuwa anamlima Salim muda wote alikuwa ni Jeane Kirkpatric chini ya rais Reagan. Tena kwenye mazungumzo alikuwa anafurahisha kwa kusema anampenda sana Salim kama binadamu lakini kwa amri ya nchi yake ataendelea kupiga veto. Rais Reagan alikuwa ndio kwanza ameingia madarakani na siasa zake za ubabe. Labda Carter angelikuwa bado rais huenda Salim angeshinda.

Wakati huo tulikuwa tunashinda kwenye radio kusubiri mwana wa Tanzania Salim Ahmed Salim atangazwe katibu mkuu, lakini bahati haikuwa yetu. Nashangaa siku hizi eti kuna watu wana hata nguvu ya kusema Salim sio Mtanzania.

Bora wewe ulikuwa walau una akili mkuu. Wengine hata hatukuwa tuna tarajiwa. Kwa hiyo walitoa sababu gani za kumpinga? Au ndiyo mambo ya vita baridi na walikua hawana haja ya kutoa sababu za msingi? Je Salim alikuwa na uwezo wa kikazi wa kupewa nafasi hio?
 
Salim alikuwa na uwezo; kumbuka alishakuwa rais wa baraza la usalama la umoja wa mataifa mwaka 1976 na pia mwaka 1979 alikuwa rais wa UN general assembly. Hizo nafasi ni ishara tosha kwamba alikuwa na uwezo mkubwa.

Mwaka 1980, Nyerere alimrudisha TZ kuwa waziri wa mambo ya nchi za nje kama njia ya kumwandaa kugombea nafasi ya katibu mkuu.

Kikwazo kilikuwa siasa za wakati ule za mlengo wa kulia na kushoto. Pia jeuri ya Nyerere ilikuwa ni kikwazo kikubwa. Kumbuka Reagan na Thatcher ndio marais ambao kila Nyerere akihutubia walikuwa wanageuka kwingine na kucheka. Nyerere kwa watu kama hao alikuwa kama alivyo rais wa Iran kwa sasa.

Pia uhusiano wa Tanzania na China ulikuwa sababu moja wapo ya kumsaidia Salim maana China walisema wataendelea kumwunga mkono mpaka apite.

Uwezo haikuwa sababu ya kukataliwa Salim; kumbuka alishakuwa na kura za kutosha kuwa katibu mkuu, ila huwezi kuwa katibu mkuu kama kuna nchi moja yenye veto inakupinga na hicho ndio kilitokea.
Bora wewe ulikuwa walau una akili mkuu. Wengine hata hatukuwa tuna tarajiwa. Kwa hiyo walitoa sababu gani za kumpinga? Au ndiyo mambo ya vita baridi na walikua hawana haja ya kutoa sababu za msingi? Je Salim alikuwa na uwezo wa kikazi wa kupewa nafasi hio?
 
Sasa nimeanza kupata picha. Je una taarifa yoyte kuhusu huyo Waldheim in regards to his qualifications? Ukilinganisha yeye na Salim nani ali stahili? Na je Pereze Cuellar alikua na uwezo kuhusu hawa jamaa wawili au ndiyo hivyo tena he was a compromise choice only?
 
Ukitoa na suala la sifa na itikadi za Kurt pia kulikuwa na suala la yeye kuwa mfuasi wa Hitler wakati fulani tena katika level nyeti. Hili lilifichwa na kukandamizwa na wamarekani lakini lilikuwa wazi miongoni mwa mataifa ya dunia ya tatu (G77). Suala hili liliibuka rasmi aliporudi Austria na kugombea nafasi ya u-chancellor na kulazimika kujitoa ama kujiuzulu hapo baadae.

Kuhus Salim, nimekuwa nikifanya uchunguzi kuhusiana na UN...ukweli ni kuwa kila niongeaye naye na kujitambulisha kuwa ni mtanzania ni majina matatu hujirudia na kupambwa sana...Mwalimu Nyerere, Salim Ahmed Salim na Balozi wetu wa sasa huko, Dr Augustine Mahiga.

Ukiangalia kamati za umoja wa mataifa ambazo Salim alikuwa akiongoza ukitoa suala la uenyekiti wa baraza la usalama ambao kila taifa linaloweza kupata uanachama huko uwe wa miaka miwili ama wa kudumu hupewa nafasi hiyo kwa mwezi mmoja na urais wa Baraza kuu (GA), Salim alikuwa mstari wa mbele sana katika shughuli zingine haswa zile za ukombozi, mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi, na hata ajenda za kiuchumi za nchi za dunia ya tatu.

Ukiwa balozi wa nchi changa kama Tanzania yenye kiongozi asiyeaminiwa na hata kuchukiwa mabepari na wafuasi wao duniani kote kama Mwalimu Nyerere, ni wazi lazima ukubalike sana miongoni mwa wawakilishi wa mataifa mbalimbali katika umoja huo ili upate nafasi za kuongoza kamati na ajenda mbalimbali huko.

Hata hivyo ni lazima tukumbuke kuwa kushabihiana kimitazamo na ajenda kati ya Salim na Nyerere ambaye wakati huo ndio alikuwa wizara ya mambo ya nje na kila kitu, na pia imani ambayo MWALIMU aliyokuwa nayo kwake, ni wazi kulimsaidia sana katika kufanikisha utendaji wake huko.....

omarilyas
 
Last edited:

Asante sana mkuu. Kuna kitu kingine nili sikia sijui kama ni kweli. Nili sikia Nyerere ali push Salimu awe katibu mkuu U.N. ili asi gombee uraisi kabisa Tanzania. Yani ali taka aende mbali kabisa. Hii ina ukweli wowote?
 
Kwa wana CCM Kikwete anafaa zaidi kuliko Salim A. Salim!

Tunakoenda lazima kizazi cha sasa kitatukanwa waziwazi na wajukuu zetu!
 
Mwanafalsafa1,

..Dr.Kurt Waldheim alikuwa UN SG tayari na alikuwa anagombea kwa kipindi cha 3.

..kwa kawaida UN SG hugombea vipindi viwili tu. kuna wengine,kama Dr.Botrous Ghali wa Egypt, ambao walipata matatizo na kuondolewa ktk nafasi hiyo baada ya kipindi kimoja.

Mtanzania,

..kwa upande wangu naona kama Tanzania tulikuwa overly ambitious, au naive, na siasa za uchaguzi wa UN SG.

..msimamo wetu ktk siasa za kimataifa za wakati ule ulikuwa umetuweka ktk upande tofauti na interest za wakubwa--USA na UK.

..ilitupasa kuelewa kwamba mgombea yeyote yule toka Tanzania angepingwa na mataifa hayo mawili makubwa, lakini haswa haswa USA.

..kuna mahali nilisoma kwamba alikuwepo MLIBERIA ambaye alikuwa mtumishi wa muda mrefu wa UN. inasemekana AFRICA ingempendekeza huyo at least kulikuwa na uwezekano angeungwa mkono na USA.

NB:

..kampeni za kugombea UN SG zina gharama kubwa sana.

..wakati ule tulikuwa na hali mbaya sana ya kiuchumi.

..sijui ni nani alikuwa akilipa gharama hizo, labda CHINA.
 
Kwa nini ali ruhusiwa kugombea term ya tatu kama ilikua kinyume na sheria? Hiyo si ilikua ukiukwaje wa katiba wa wazi wazi kabisa? Mataifa mengi haya kupinga hali hiyo? Na je ukatibu mkuu si una zunguuka kimabara?

Kwa maana hiyo ilikua zamu yetu Afrika so kwa nini wagombea wasio waafrika waka jitokeza?
 
Another element katika veto ya Wamarekani ni ile ninayoita "missed opportunity." Kama alivyosema Mtanzania Jean Kilkpatrick kweli alikuwa ana affection na Salim kwa sababu walishafanya kazi naye pale UN. Katika juhudi za kumsaidia Salim alifanya mpango akutane na Alexander Haig wakati huo ndiye aliyekuwa Secretary of State.

Mkutano ukapangwa na Salim akakubali. According to Balozi Bomani, a day before the meeting Alexander Haig alipata safari ya ghafla kwenda Middle East akamwachia deputy wake jukumu la kukutana na Salim. Lakini Salim aliposikia Haig yuko out of town alikataa kwenda Washington licha ya Balozi Bomani kumsihi. So as they say, the rest is history.

Wamerikan wakatranslate the no show ya Salim kama snub huku Salim naye akitranslate kuondoka kwa Alex Haig kama snub. That was the end of it. Mwanafalsafa, kwa kawaida Marekani haitoi sababu inapopiga veto against a SG.
 
Mtanzania,
Just a point of correction. Rais wa Marekani hakaagi na kusikiliza hotuba za viongozi wa mataifa mengine UN. Actually he is among the first speakers when the General Assembly opens. Akimaliza kutoa hotuba yake huondoka na vikao vyake na viongozi wengine hufanyia kwenye hoteli ambayo inatumika kama residency ya US ambassador to the UN. Ni kweli Reagan hakumpenda Nyerere, lakini hakuwahi kuwepo general assembly when Nyerere gave a speech.
 
Another element katika veto ya Wamarekani ni ile ninayoita "missed opportunity." Kama alivyosema Mtanzania Jean Kilkpatrick kweli alikuwa ana affection na Salim kwa sababu walishafanya kazi naye pale UN. Katika juhudi za kumsaidia Salim alifanya mpango akutane na Alexander Haig wakati huo ndiye aliyekuwa Secretary of State. Mkutano ukapangwa na Salim akakubali. According to Balozi Bomani, a day before the meeting Alexander Haig alipata safari ya ghafla kwenda Middle East akamwachia deputy wake jukumu la kukutana na Salim. Lakini Salim aliposikia Haig yuko out of town alikataa kwenda Washington licha ya Balozi Bomani kumsihi. So as they say, the rest is history. Wamerikan wakatranslate the no show ya Salim kama snub huku Salim naye akitranslate kuondoka kwa Alex Haig kama snub. That was the end of it. Mwanafalsafa, kwa kawaida Marekani haitoi sababu inapopiga veto against a SG.

Picha ninayo pata ni kwamba U.N. ni taasisi yenye elements zaki upendeleo na ubaguzi sana. Taasisi imekaa kisiasa zaidi ilivyo kidiplomasia. Ni kama vile nchi kubwa za duniani(sasa Marekani tu nadhani) wanai tumia as a way to serve their interests internationally.

Because of the U.N. naiona kama an extention of the U.S. Foreign Department.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom