Who is Benson Bana?

Who is Benson Bana?

To be fair, Bana could just be a victim of the current system (like most Tanzanians in the country) in which a measure of loyalty to the rulers is essential if you are to make any headway in a public sector career, business and even mere survival in whatever socio-economic engagement you're in. Remember Saddam's Iraq and Baathism? No need to be too harsh on his intellectual endowment. Under different circumstances, he could be a different person - for the better!
 
Hi wanajamvi naomba ,nipe details za huyu prof je ni kweli ni fake, ktk mjadala ITV kapwaya full anajibu ugoro hado wapiga simu wamemstukia. Nani ana details za usomi wake huyu jamaa mpaka imeniuma sana
 
Fake kwa maana upeo wake wa kuchambua ni feki au taaluma yake haijatulia? Anyway ndio mshauri wa rais katika masuala ya siasa hivyo simjui.
 
Kashachakachuliwa na CCM thats why unamuona alivyo, Hajui kama anajishusha huyu
 
Hi wanajamvi naomba ,nipe details za huyu prof je ni kweli ni fake, ktk mjadala ITV kapwaya full anajibu ugoro hado wapiga simu wamemstukia. Nani ana details za usomi wake huyu jamaa mpaka imeniuma sana

Kumbe keshazawadiwa u professa na Mkandala?
 
Sioni kama ana deserve hiyo hadhi aliyonayo. Nimekuwa nafuatilia hoja zake katika mijadala mbalimbali na nimeona hazina mshiko, na huwa ana kajazba furani na sometimes anakuwa preemptive i.e kujudge mabaya hata kama hayatakuwepo. Kwa mfano, alijua watu wata ponda utafiti wake kuhusu kuchagulika kwa JK nikamsikia ile siku akitangaza utafiti huo siku chache kabla ya uchaguzi wa 2010 alisema" Huu ni utafiti wetu, japo tunajua watu watema hivi na vile kwa kutoridhika" Na hapo ndipo nilipokosa imani na REDET
 
Na kumbukeni keshafundisha watu kibao hapa TZ kwa maana ya waliopitia UDSM! Kwa hiyo na wenyewe tuna mashaka na taalum zao! Kama Mhadhiri wao ndo yuko hivyo wao wakoje? Poleni sana bandugu!
 
Bana is straight forward and progressive fellow. He is not what you have been lamenting here. I wish you would have worked with him.
 
binadamu tunabadilika sana, mimi nimefundishwa na Dr. Bana, ni mwalimu mzuri sana, haya yanayotokea sasa ni matokeo ya pesa na mapendo ya madaraka
 
Jana nilitazama kipindi cha Kiti Moto cha ITV na niliumia sana kuona kuwa msomi kama Dr.Benson Bana akizidiwa nondo na dada ambaye ana shule ya kawaida, Ketty! Aliniacha hoi Dr. Bana alipoponda uamuzi wa wabunge wa CHADEMA kutoka nje ya Bunge wakikwepa kupiga kura ambayo walijua wazi kuwa,kwa idadi yao isiyofikia ya Wabunge wa CCM na wa vyama vyao shirikishi Bungeni, wangesaidia kuhalalisha uamuzi wa Bunge ulio kinyume na msimamo wao.

Wasomi wa kweli wanajua kuwa CHADEMA walitoka nje ikiwa ni hatua ya mwisho kabisa (last resort) ili isijengeke picha kwamba uamuzi walioupinga wa kuunganishwa kwa lazima kwa watu kucheza na kanuni, yalipigiwa kura na wote wakiwemo hao wabunge wa CHADEMA na hivyo uamuzi huo ni wa wote,yaani wa Bunge zima.

Dr Bana alisema kwamba wabunge hao wa CHADEMA walifanya vibaya kuchukua hatua hiyo aliyoitafsiri kuwa baadaye itakuwa ya kufuatwa na kila kundi la watu watakaopinga maamuzi ambayo hawakukubaliana nayo. Mpaka hapo sikuona tatizo la shule yake kwa hoja yake.Lakini alikuja nichosha aliposema walichopaswa kufanya wabunge wa CHADEMA ni kukomaa mjengoni na kupambana kwa hoja kutetea kile walichoamini kuhusu jambo lililokuwa liamuliwe dhidi ya msimamo wao badala ya kutoka nje kuikimbia hoja.

Daktari wetu huyu wa Falsafa ina maana kishasahau kwamba wabunge hao wa CHADEMA walishapambana kwa nguvu zote za hoja ndani ya mjengo kupinga walichoona si haki kutendewa katika suala hilo katikati ya miguno,kejeli,kauli kali kupitia vipaza sauti bila Mheshimiwa Spika kukemea waliofanya utoto huo huku "miongozo ya spika" ikiombwa hapa na hapa! Dr Bana alichotaka wabunge hao wa CHADEMA wazipige kavu kavu ndani ya mjengo na wapinzani wao baada ya Mheshimiwa Spika kutupilia mbali hoja zao na kuamua kura ipigwe?

Huyu ni Daktari wa Falsafa wa namna gani asiyelitazama suala kwa mapana na kuzama kwenye ushabiki wa kisiasa? Hivi taasisi yake inayotoa takwimu za kisiasa inapaswa kuendelea kuaminiwa kweli wakati yeye ameshajibainisha anashabikia upande gani katika staili isiyo tofauti na ya ushabiki wa Yanga na Simba usioona mazuri ya upande mwingine?

To me, PH D ya Dr. huyu ni very questionable.
 
Huyo shahada yake ya udaktari ilishanunuliwa na CCM. Hivi anaona vitu kwa kutumia miwani ya CCM. Kama msomi anashindwa kujinasua toka kwenye mitego ya kundi fulani la watu bora akae kimya kuliko kuzungumza kama alivyozungumza Dr. Bana.
 
Jamani miye lazima niwe mkweli, msomi yeyote anayemsupport mkwere huwa napata wasiwasi kuhusu uhalali wa usomi wake!
 
Huyu kiukweli ni dk ila mfumo umeshamharibu. Hata kina dk kitila, mvungi n.k wangekuwepo ccm si ajab tungewashangaa
 
Mamluki wa ccm huwa hawaoni hata kama watu watakufa, hukumbuki matamko wakati wa vurugu za arusha? Hukumbuki migomo ya vyuo walidai cdm ndo wanachochea wakati wao wenyewe hawatoi huduma kwa wakati.
 
Mh! Kila mtu anauhuru wa kutoa mawazo yake.Benson alisema alichoona kwa ufahamu na uzoefu wake.Halafu wewe kama msomi si kila hoja lazima uikubali lakini pia sio kilahoja iliyo nje ya upeo wako au mawazo yako basi ni mbovu,hapa lazima uchuje.Kwa upande wangu mimi namuunga mkono Bana.
 
Jana nilitazama kipindi cha Kiti Moto cha ITV na niliumia sana kuona kuwa msomi kama Dr.Benson Bana akizidiwa nondo na dada ambaye ana shule ya kawaida, Ketty! Aliniacha hoi Dr. Bana alipoponda uamuzi wa wabunge wa CHADEMA kutoka nje ya Bunge wakikwepa kupiga kura ambayo walijua wazi kuwa,kwa idadi yao isiyofikia ya Wabunge wa CCM na wa vyama vyao shirikishi Bungeni, wangesaidia kuhalalisha uamuzi wa Bunge ulio kinyume na msimamo wao.

Wasomi wa kweli wanajua kuwa CHADEMA walitoka nje ikiwa ni hatua ya mwisho kabisa (last resort) ili isijengeke picha kwamba uamuzi walioupinga wa kuunganishwa kwa lazima kwa watu kucheza na kanuni, yalipigiwa kura na wote wakiwemo hao wabunge wa CHADEMA na hivyo uamuzi huo ni wa wote,yaani wa Bunge zima.

Dr Bana alisema kwamba wabunge hao wa CHADEMA walifanya vibaya kuchukua hatua hiyo aliyoitafsiri kuwa baadaye itakuwa ya kufuatwa na kila kundi la watu watakaopinga maamuzi ambayo hawakukubaliana nayo. Mpaka hapo sikuona tatizo la shule yake kwa hoja yake.Lakini alikuja nichosha aliposema walichopaswa kufanya wabunge wa CHADEMA ni kukomaa mjengoni na kupambana kwa hoja kutetea kile walichoamini kuhusu jambo lililokuwa liamuliwe dhidi ya msimamo wao badala ya kutoka nje kuikimbia hoja.

Daktari wetu huyu wa Falsafa ina maana kishasahau kwamba wabunge hao wa CHADEMA walishapambana kwa nguvu zote za hoja ndani ya mjengo kupinga walichoona si haki kutendewa katika suala hilo katikati ya miguno,kejeli,kauli kali kupitia vipaza sauti bila Mheshimiwa Spika kukemea waliofanya utoto huo huku "miongozo ya spika" ikiombwa hapa na hapa! Dr Bana alichotaka wabunge hao wa CHADEMA wazipige kavu kavu ndani ya mjengo na wapinzani wao baada ya Mheshimiwa Spika kutupilia mbali hoja zao na kuamua kura ipigwe?

Huyu ni Daktari wa Falsafa wa namna gani asiyelitazama suala kwa mapana na kuzama kwenye ushabiki wa kisiasa? Hivi taasisi yake inayotoa takwimu za kisiasa inapaswa kuendelea kuaminiwa kweli wakati yeye ameshajibainisha anashabikia upande gani katika staili isiyo tofauti na ya ushabiki wa Yanga na Simba usioona mazuri ya upande mwingine?

To me, PH D ya Dr. huyu ni very questionable.
Kila raia ana uhuru wa kutoa mawazo yake! Na sio kila raia lazima awe mshabiki wa CHADEMa! Dr.Bana aliongea vizuri sana Chadema tujifunze kupokea maoni mbalimbali na sio kutaka kusifiwa kwa kila jambo! Ulikua mtazamo tu wa Dr Bana!
 
Umeongea vizuri sana ila Tatizo la wanachadema usipokubaliana nao utabandikwa kila jina nia na madhumuni kukushushia hadhi yako. Vilevile kutokana na mapenzi yao ya chama basi hata ukweli hawauoni.
 
Mh! Kila mtu anauhuru wa kutoa mawazo yake.Benson alisema alichoona kwa ufahamu na uzoefu wake.Halafu wewe kama msomi si kila hoja lazima uikubali lakini pia sio kilahoja iliyo nje ya upeo wako au mawazo yako basi ni mbovu,hapa lazima uchuje.Kwa upande wangu mimi namuunga mkono Bana.

Na ndiyo maana kuna mahali niliandika "Mpaka hapo sikuona tatizo la shule yake kwa hoja yake" nikizingatia uhuru wa kutoa mawazo.Lakini utakuwa upuuzi kama mtu ataiita rangi nyekundu kuwa bluu na kuachwa bila kusahihishwa eti kwa sababu ana uhuru wa kusema! Alichowalaumu Wabunge wa CHADEMA Dr. Bana ni kuacha kuendelea kupigania hoja yao Bungeni na badala yake kutoka nje wakati ukweli ni kwamba Wabunge hao walipigana kwa hoja bila mafanikio mpaka kufikia hatua ya kupiga kura kupitisha hoja hiyo ambayo hawakuikubali.Walichokataa na kutoka nje ni kukwepa kushiriki kupiga kura ambayo wangeshindwa kutokana na uchache wao. Dr. Bana angefuatilia tukio hilo kama msomi angeuona ukweli huo. But he spoke out his minds without making prior research. As is widely known,no research,no right to speak. That is why I think his being academician is drastically tainted. Mtu ana uhuru wa kutoa mawazo yake lakini si sahihi kutoa mawazo ya uongo.Mbaya zaidi mtu huyo akiwa msomi.
 
Back
Top Bottom