WHO inatakiwa izijibu hoja za Rais Magufuli kwa umakini mkubwa. Tropical diseases kama TB, Malaria kwanini hazina chanjo na zinaua sana?

Mamabo ya maajabu kabisa. Yaani, jiwe anauliza WHO wajieleze kuwa wameshindwa na chnjo ya malaria na TB na kuna watu waku staajabisha kabisa. "eti who wajibu masuala" kabla kutuletea vaccine. huu ni mtihani kweli kweli. Huku tunakufaaaa. Zanzibar tunakufa maana kuna watu wanamuabudu Jiwe na hawshughuliki na kujikinga. Tunaambiwa tu pneumonia wakati ni korona. Pneumonia inatibiwa kwa antibiotics. Corona haina dawa. Hata ukivuta BANGI unakufa tu.
 
Viongozi wa afrika ni alinacha sana kwahiyo anataka kutuambia amekumbuka shuka wakati kumekucha
 
kwa hiyo mabeberu wanawaonea wivu upcoming superpowers kwa kuwaletea chanjo ya covid 19
Ila chanjo nyingine hawawaonei wivu....
Inahitaji uwe na akili ya mwendawazimu ili kukuelewa
 
U

Umeliweka vizuri sana. Tuna kiongozi Mkuu mropokaji. Nitamlaumu Kikwette milele kwa chuki yake dhidi ya Lowassa na kumg'ang'ania Membe hadi tukaingia kwenye huu mkenge.
Mungu aliruhusu jambo hilo kutokea ili waTZ watoke usingizini na kuchukia ujinga.
Utatawaliwa na mtu yeyote wa sisiem hata kama hana akili sawasawa hiyo ni lazima penda usipende siyo ombi.
Sisiem itatawala tanzania mpaka mwisho wa dunia
 
Me sidhani kama ni sahihi sana mpaka sasahivi kulaumu athari za ukoloni au ukoloni mamboleo,, kama tunatambua ukoloni na ukoloni mambo leo basi tunajielewa kwa nini tuendelee kulaumu na kushindwa kufanya mambo yetu ikiwepo kufanya tafiti na chanjo mbalimbali? Tusipokuwa na mifumo ya elimu inayoangalia maslahi yetu hatutafika popote.China na North Korea wamefika hapo leo kwa sababu ya kutengeneza mifumo yao bora ya elimu,leo hii badala ya kuanzisha somo la historia Tanzania ambayo tayar lipo lingeongezewa baadhi ya mambo kwa maboresho lakini nguvu kubwa tungeweka kwenye science.Mfano mwanafunzi anaeweza biology na brunches zake asome kuanzia darasa la nne mpaka Chuo kikuubadala ya kumjazia mwanafunzi rundo la masomo ambayo anasoma juujuu.
 
Chanjo na dawa nyingi hazitengenezwi na serikali bali makampuni binafsi. Makampuni haya yanafanya biashara na sio huduma. Kwa sababu hiyo yanajikita katika chanjo na dawa za magonjwa yanayowasumbua watu wa magharibi kwa sababu wanajua wanaweza kuwauzia na kupata faida. Magonjwa yanayosumbua nchi maskini hazipewi priority kwa sababu wanajua hazina uwezo wa kuzinunua kwa bei itakayofidia gharama za utafiti na utengenezaji. Ndio maana utafiti wa chanjo na tiba ya magonjwa kama malaria au sleeping sickness, magonjwa ambayo hayapo katika nchi za magharibi unafadhiliwa na taasisi kama za wakina Bill and Melinda Gates Foundation ambazo hazina utaalam na resources za kutosha kuwekeza katika tafiti zote zinazohitajika za maradhi yanayopatikana katika nchi zetu.

Kwa kifupi tukitaka chanjo kwenye haya magonjwa tunatakiwa tuunganishe juhudi za nchi zetu kwa kushirikiana na taasisi rafiki kufanya utafiti ili tupate chanjo. Njia nyingine ni kuongeza juhudi kuyatokomeza hayo magonjwa badala ya kutegemea chanjo. Shida ni kuwa hatuna nia za kisiasa katika suala hili na mzigo tumewatwika wakina Bill Gates.

Amandla...
 
Paragraph ya pili ni UONGO ili kuhalalisha hoja yako. Kama wadau walivyotangulia kusema, huo wivu wa mabeberu kwa nini tusiuone kwenye chanjo za polio, TB, dawa za ARV nk
Nakubaliana na hoja ya kujiridhisha na ubora wa chanjo, lakini hoja ya eti mabeberu wana wivu na sisi, ina ukakasi mkubwa kwa sababu kila tulichonacho, siyo sisi pekee tunavyo(madini, rasilimali za asili, bahari, maziwa nk)!
 
Paragraph ya pili, PROPAGANDA TUPU, hivi ni kwa faida ya nani?
 
Mi bado sijaelewa lengo la kutumia chanjo za polio, TB au dawa za ARVs kama counterargument kwamba ubeberu wanatumia pandemic ya corona kujineemesha zaidi kupitia vaccines zao. Ni kweli chanjo ya polio ilitusaidia, ni kweli dawa za ARVs zimesaidia sana tu. Ni makosa makubwa ya kimkakati kwamba hatukujifunza kutengeneza dawa zetu na kwamba miaka mingi baadaye bado tunaendelea kuwategemea wazungu kwa ajili ya afya za watu wetu.

Magufuli anachosema, au ninachojaribu kukisoma kupitia attitude ya Magufuli (na wale wanaomsupport) kuhusiana na corona, ni kwamba enough is enough! -- Tanzania haitaki kuendelea kuwa tegemezi wa Magharibi kwenye mambo yanayohusu afya ya watu wake, na kwenye mambo mengineyo pia. Hatua ya kwanza ni kusema HAPANA kwenye inshu ya chanjo ya corona. Kusema hapana huku, kutatufanya, kwanza, tupambane na corona kwa namna yetu iliyo ndani ya uwezo wetu. Pili, kutatujengea uzoefu wa nini cha kufanya janga kama hili likitokea tena. Kama miongoni mwa uzoefu huo ni kuona umuhimu wa kujijengea uwezo wa kutengeneza chanjo zetu wenyewe, well and good!

Kitu ambacho watu kama nyie mnakiadvocate ni kuendelea kuitazama magharibi kama baba yenu na Mungu wenu kwenye mambo yanayohusu mambo yenu. Yaani mmeifanya Marekani na Ulaya kama one-stop-shop kwa matatizo yenu yote, na kwenda kinyume na kile wanachokifanya, au wanachokisema basi unaonekana umekosea, dah! Maana halisi ya uhuru ni doing your own thing eti. Viongozi wa nchi hii wenye fikra kama zako ndio wameirudisha hii nchi nyuma sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…