Whatsapp na Mgogoro wa Familia

Whatsapp na Mgogoro wa Familia

tatizo familia ya mumeo inaonyesha wana character za uswahili, kupenda umbea na majungu, sasa kwenye familia za hivyo ukiwa wa tofauti hutaweza kuishi manake wote watakuona kama hufai, una ringa, watakutenga na kufanyiwa mambo mengi ya kukuumiza, na mbaya zaidi inaonyesha na mumeo nae lake moja na ndugu zake kwahiyo hata yeye anakuona na kukuchukulia kama wanavyokuchulia watu wengine kwenye familia yake na hiyo ni mbaya sana, manake at least mume anaposimama upande wako familia yake wanakuwa hawana nguvu sana ya kukutenda. Me nazani mtu wa kukaa nae na kuongea nae ni huyo huyo mumeo muweke chini mueleze yoooote anayofanya na unayofanyiwa na ndugu zake na jinsi gani yanavyokuumiza matokeo ya hapo ndo yatakupa picha ya uchukue hatua gani next
 
Pole sana jitoe tu ktk Group lao. Kaa kivyako kuomba talaka sio suluhisho, na isitoshe nadhani mna watoto sasa kaa kimy na "Mute" wote watakoma umbea wao. Na wakikurudisha jitoe tena.
 
najua inaandikwa pia....hahahahah, sasa unafikir hapo kuna furaha gan ya ndoa, mana ukienda kwa wakwe kero, wake wenzio ndo yarabi toba! mumeo nae ndo akili kashikiliwa mkononi.... alaf kama masikin ya mungu hana wazazi ndo utaomba mwisho wa dunia uwe kesho! tabu nyingine hizi! sasa angekua peke yake yangekuepo yote haya....?? mi bora niwe single tu kwakweli, mambo ya kuolewa wake wengi hapana

Nadhani hujamuelewa , wake wenza anaomaanisha ni wake wa wadogo zake mumewe.
 
Mmmhhh
Wanaume wengine? majanga!!!!
Pole
Vumilia
Jitoe tena kwenye hilo group then mwambie kuwa hutaki kuwe na mipaka sometimes!!!!heegh
Kwani ndoa jehanam!?

Jamani Munkari unaendeleaje mgonjwa..? poleee..
 
Last edited by a moderator:
pata kitu roho inapenda. Kim nana sijamuona kwenye huu uzi.

ha ha ha ha ha ha

kwa kweli uke wenza una tabu huyu Marijani Rajabu aliimba wakati mziki hauna pesa siku hizi wanakatika viuno wanapata hela kibao
hawana cha kuimba bora mie wa kujisikilizia nyimbo hizooo
 
Last edited by a moderator:
Miss Chagga nimeshajitoa huko lakini najua atanirudisha tena, ila hii hali tu inanikwaza sana, yaani sijui niseme nini nieleweke lakini maisha ya ndoa yamekuwa magumu

Dawa ni kumblock ili ajitambue ana kosea sana lkn ukimya ni dawa kubwa wadharau tu ipo cku wataxhoka usimuache mme wako utawapa kichwa yatakwisha
 
Pole sana dada naima79 umesema mume wako anayajua yote,kabla sijatoa ushauri wangu naomba majibu ya haya maswali samahani lakini....
je huwa ana respond vipi katika vile vituko ambavyo familia inakufanyia,huwa ana kushauri nini? Je huwa mkali sana? Au? Alishawahi kukukaripia sana jambo lolote uliloenda kinyume na familia yao? Je uliongea naye kuhusiana na hiyo picha aloweka,na amekupa majibu gani? Naomba majibu ntakuambia nini ufanye.
 
Last edited by a moderator:
Pole,huyo mumeo atakuwa hajitambui, kwa jifupi ni limbukeni fuata ushauri wa Cleverking kujitoa kwenye hiyo group
 
poleee dada angu.
ila duuuhhh
w.ume tunatofautiana kwa kweli.
kama iyo kesi unavoelezea ni kweli, nathubutu kusema mumeo ana matatizo, tena makubwa, mumeo alipaswa yeye kukwambia toka kwenye grp kama ilo lakin yeye ndo kwanza admin tena ana kuadd kw nguvu,...nna wasi wasi na akili za mmeo, im vty sorry.
mimi katika maisha yangu, madhaifu na makosa ya mke wangu, nitajitahd kadri ya uwezo wangu niyakingie kifua ikiwezekana niyabebe mie mbele ya ndugu,marafiki na jamaa zangu ili mke wangu awe msafi aonekanwe mtu haswaaa, kila mtu amsifu kwa sifa njema.
na napata huzuni ikitokezea watu wanamsema wife wangu kw mabaya.

the same case kwa ndugu zngu, ntajtahd kadri ya uwezo wangu ndugu zangu wawe watu wazr mbele ya wife.,
na ikitokezea kua hawana maelewano ntawasuluhisha with very care, nkihisi hawapatani ntajitahd kuwatenganisha bila kuacha athari kwa yoyote bila kupendelea kw yoyote, mwisho wa siku mke wangu anahaki na mimi zaidi, unless niproove kw ushahidi kua mke wangu ndio mwenye matatizo
 
Za siku wana MMU?

Ni hivi; kwa kifupi mimi na familia ya mume wangu hatuko vizuri sana
kama mwanzoni, na hii yote imesababishwa na fitina ya mmoja wa mke wa
mdogo wa mume wangu kuwa na mambo ya umbea, urongo na unafiki na
anapenda kutupaka matope wake wenzake siku zote.

Kwa vile ni familia ya kusikiliza maneno, huwa wanampokea vizuri na
wanamfurahia, sasa mimi sikulelewa katika maisha hayo nilichoamua kuwa
mbali kidogo na maneno yao yaani ni pamoja na kupunguza sana visiting ya
ukweni maana wenzangu wengine watatu wote wanakaa pamoja na mama mkwe
yaani bado hawajaamua kutoka nyumbani.

Sasa nyumba imekuwa na matatizo, yaani wengine hapo hatufai kabisa na
anaefaa ni huyo mwenye hulka ya maneno, hii imeweza kutujengea ukorofi
kwa kila tunalolifanya liwe zuri liwe baya utaonekana mbaya tu mzuri ni
huyo mmoja.

Tukija katika point ni hivi, mume wangu ame-create family group
whatsapp. Hiyo group ni mipasho, manyanyaso na masimango tu, sio group
ya kupeana taarifa muhimu. Kukiwa na shida ndani basi sehemu ya
kukusemea ni katika group. Sasa jana ka-share hiyo picha hapo na ndugu
zake wote wakawa wanaisupport na kuifurahia, na hiyo yote kwasababu pia
hawanipendi na wananisemea vibaya kila siku japo nasikia ila nanyamaza
kwa vile sitaki shari.

Mume wangu anafahamu hayo yote, mimi binafsi nimeona hii ni kejeli kubwa
kwa sababu waliomo kwenye group ni watu ambao wanatamani nipate shida,
watafurahia wakisikia nanyanyasika, watafurahia wakisikia nimeyumba.

Sasa kwa mfano ningeweka mimi picha labda inasema husbands are always
selfish and cheaters, vipi yeye asingeona namdhalilisha? Na je, hii ndio
kazi ya group ya familia? Nilishatoka katika hii group kwa vile yeye ni
creator akanirudisha tena, sasa nashindwa kumuelewa ananilazimisha
kukaa kwenye hii group ili kunipa stress?

Hivi wenzangu mnamtafsiri vipi mwanaume mwenye tabia hizi? Naona yuko
tayari niwe stressed na yeye kwake ikawa burudani.

Naombeni mtazamo wenu, lakini nahisi maisha ya ndoa yananishinda maana
hayana starehe zaidi yana stress.

======================

Hii ndio picha iliyotumwa kwenye hilo Group la Whatsapp:
attachment.php
View attachment 204120

maskini! ivi mme utajiskiaje mkeo kusimangwa!! ila vumilia kila lenye mwanzo lina mwisho
 
Kuishi na Mwanaume anaye entertain whatssap , sijui anarusharusha picha FB na vistatus vya kitotototo , sijui Instagram yataka moyo maana wengi wanakuwa kama Ma SHE tu .:sorry:....pole mwanamke mwenzangu ....
 
Nimeshajaribu hivo my ila inakuwa ngumu kidogo wakati mwingine unajikuta umesoma japo si yote
Wewe unapenda shari, na from maelezo yako uko arrogant sana!Unataka usikilizwe wewe tu, na umejaa ubinafsi uliopitiliza!Bila shaka mumeo ni mtu wa watu na hilo linakukera sana, it is obvious usipobadilika utaishi kwa shida sana!Vinginevyo u better quit the marriage!
 
Nimeshajaribu hivo my ila inakuwa ngumu kidogo wakati mwingine unajikuta umesoma japo si yote
pole ila mimi najuavyo hakuna raha ya kumpuuza mtu au watu, yaani hata kama moyo wako unavuja dam, ila ukatabasam watajiona wajinga.
 
Kuishi na Mwanaume anaye entertain whatssap , sijui anarusharusha picha FB na vistatus vya kitotototo , sijui Instagram yataka moyo maana wengi wanakuwa kama Ma SHE tu .:sorry:....pole mwanamke mwenzangu ....

Umeona eehhh...wanaume ni wachache sana these days...wavulana ndio wengi...
Hizi sijui IG na whatsapp zilivyo time consuming mume wa ukwee muda atautoa wapi...?

Mimi japo siko huko najua sababu rafiki yangu ana complain daily jinsi anavyosumbuliwa sababu kajiunga na haya mauchafu...maana ndugu jamaa na marafiki wanamuona hewana na kwa kuwa hawana shughuli wanadhani na yeye ana muda wa chatting....na akichuna ugomvi....
 
Kwa tabia hizi za kike mumeo atakuwa mtu wa Pwani ama Zenji.

pwent of correction: tabia za kiswazi, si za kike. Ina maana na wee unayo? mi sina, au ngoja nikamuulize mama jinsi yangu.
 
Back
Top Bottom