miss chagga
JF-Expert Member
- Jun 7, 2013
- 57,805
- 49,109
sa utaolewa mara ngapi kila unakoenda unakutana na taahira?uvumilivu unahitajika ila oooh uwe na kikomo kuna yasiovumilika
uvumilivu una mwisho mamy ..
sa utaolewa mara ngapi kila unakoenda unakutana na taahira?uvumilivu unahitajika ila oooh uwe na kikomo kuna yasiovumilika
Kwenye settings za WhatsApp kuna kitufe kimeandikwa "Mute".
Wewe bonyeza kitufe hicho kisha waache waendelee na maneno yao, wapoteze muda wao. Kwani wahenga walisema "Maneno matupu hayavunji mfupa!"
Mungu atakusimamia na mwisho huyo mume wako atajirudi mwenyewe.
Daima usibishane na mjinga!
Maisha bana ......
Dada pole kwa changamoto ambayo unakumbana nayo,hakuna changamoto ambayo inasumbua kama hii yako kwasababu iko pale ambapo unatarajia kutuliza misongo na vurugu za mawazo ambazo unaweza kuzipata mahali pengine,hapa panapokuwa ndio kikwazo maisha huwa magumu kidogo
Kwanza labda nianze kukuambia tu kuwa mumeo ameshindwa kutimiza jukumu lake kama baba na kiongozi wa familia anazoziongoza,baba unatakakiwa uwe mtu wa kuondoa matatizo kwenye familia na sio wa kuongeza matatizo kwenye familia,huyu wako inaonekana ni wa kuongeza matatizo badala ya kuyaondoa
Mumeo inaonekana kuna mambo mawili,huenda amekuchoka na ndio sababu ya kuacha yatokee yanayotokea na kama ukiamua kuondoka basi pakacha litakuwa limevuja na faida imekuwa kwa mchukuzi,nasema hivi kwasababu ni ngumu sana mtu kufurahia kuona mtu ambae aliapa kumlinda maisha yake yote awe ana huzuni kwenye mambo ambayo anaweza kabisa kuyaondoa,wakeze pamoja na mama yake wako chini ya himaya yake na anaweza kukemea na hayo yakaisha,lakini kwasababu hii ya kukuchoka [kama ndio sababu] anaamua tu kukuacha na utaamua wewe mwenyewe
Jambo la pili ambalo naliona hapa ni mumeo kuwa na malezi ya kipwani hivi,yaani hapa namaanisha kuwa amelelewa nae kuwa na tabia kama za kike za kupenda umbea na kupashana,huyo angekuwa huku usukumani kwetu tungemuona kama ana tabia za kike kabisa,sasa basi wewe unaona ni tatizo wakati mwenzako anaona ni kawaida tu,hapo kazi ipo sana tu,lakini pia inawezekana pia hajui hata daraka la mume kwenye familia ni lipi na mwanaume anatakiwa aweje hii nayo inasababishwa na malezi na kama ni hivi huyu kuwa sawa ni kazi kidogo
Sasa basi kwasababu hiyo kila jambo huwa lina namna yake ya kulitatua,kama mumeo ana tatizo la kwanza hapo unatakiwa ukague ni kwasababu gani amekuchoka na ukijua sababu naamini utajua cha kufanya,tatizo linaweza kuwa halijaanzia kwake [kama amekuchoka] bali limeanzia kwako na unashindwa kuliona kwasababu unatazama upande wake zaidi,chunguza na ukijua sababu utajua na na namna ya kufanya
Kama ana tatizo la pili la kulelewa kike hapo itakubidi umkubali kama alivyo kama misingi ya ndoa inavyoagiza na uwe unajitahidi sana kumpenda kwa namna alivyo,tafuta masomo ya utambuzi ujifunze namna ya kuishi na watu wa namna hiyo na utakuwa na amani na hata kusumbua,lakini pia kama utafanikiwa kujua namna ya kuishi nae taratibu utamvuta kujifunza namna ya kujitabua nae atabadilika tu
Kama atakuwa ni mt ambae ameathiriwa na malezi na kushindwa kujua majukumu yake utaweza kumsaidia kwa kumpenda zaidi na kuwa unajaribu kmuelekeza kwa upendo na utulivu nae atakusikia
Pole sana dada ....!!
Za siku wana MMU?
Ni hivi; kwa kifupi mimi na familia ya mume wangu hatuko vizuri sana kama mwanzoni, na hii yote imesababishwa na fitina ya mmoja wa mke wa mdogo wa mume wangu kuwa na mambo ya umbea, urongo na unafiki na anapenda kutupaka matope wake wenzake siku zote.
Kwa vile ni familia ya kusikiliza maneno, huwa wanampokea vizuri na wanamfurahia, sasa mimi sikulelewa katika maisha hayo nilichoamua kuwa mbali kidogo na maneno yao yaani ni pamoja na kupunguza sana visiting ya ukweni maana wenzangu wengine watatu wote wanakaa pamoja na mama mkwe yaani bado hawajaamua kutoka nyumbani.
Sasa nyumba imekuwa na matatizo, yaani wengine hapo hatufai kabisa na anaefaa ni huyo mwenye hulka ya maneno, hii imeweza kutujengea ukorofi kwa kila tunalolifanya liwe zuri liwe baya utaonekana mbaya tu mzuri ni huyo mmoja.
Tukija katika point ni hivi, mume wangu ame-create family group whatsapp. Hiyo group ni mipasho, manyanyaso na masimango tu, sio group ya kupeana taarifa muhimu. Kukiwa na shida ndani basi sehemu ya kukusemea ni katika group. Sasa jana ka-share hiyo picha hapo na ndugu zake wote wakawa wanaisupport na kuifurahia, na hiyo yote kwasababu pia hawanipendi na wananisemea vibaya kila siku japo nasikia ila nanyamaza kwa vile sitaki shari.
Mume wangu anafahamu hayo yote, mimi binafsi nimeona hii ni kejeli kubwa kwa sababu waliomo kwenye group ni watu ambao wanatamani nipate shida, watafurahia wakisikia nanyanyasika, watafurahia wakisikia nimeyumba.
Sasa kwa mfano ningeweka mimi picha labda inasema husbands are always selfish and cheaters, vipi yeye asingeona namdhalilisha? Na je, hii ndio kazi ya group ya familia? Nilishatoka katika hii group kwa vile yeye ni creator akanirudisha tena, sasa nashindwa kumuelewa ananilazimisha kukaa kwenye hii group ili kunipa stress?
Hivi wenzangu mnamtafsiri vipi mwanaume mwenye tabia hizi? Naona yuko tayari niwe stressed na yeye kwake ikawa burudani.
Naombeni mtazamo wenu, lakini nahisi maisha ya ndoa yananishinda maana hayana starehe zaidi yana stress.
======================
Hii ndio picha iliyotumwa kwenye hilo Group la Whatsapp:
View attachment 204120![]()
Asante sana mkuu nimekuelewa vilivo ubarikiwe sana
Nimeshajitoa katika hiyo group najua atanirudisha tena maana ana makusudio yake
Kwa sababu hajatumia akili yake bali kaquote wimbo.. angetumia yake bado hangemake sense.. hahaha no insult lkn.
Za siku wana MMU?
Ni hivi; kwa kifupi mimi na familia ya mume wangu hatuko vizuri sana kama mwanzoni, na hii yote imesababishwa na fitina ya mmoja wa mke wa mdogo wa mume wangu kuwa na mambo ya umbea, urongo na unafiki na anapenda kutupaka matope wake wenzake siku zote.
Kwa vile ni familia ya kusikiliza maneno, huwa wanampokea vizuri na wanamfurahia, sasa mimi sikulelewa katika maisha hayo nilichoamua kuwa mbali kidogo na maneno yao yaani ni pamoja na kupunguza sana visiting ya ukweni maana wenzangu wengine watatu wote wanakaa pamoja na mama mkwe yaani bado hawajaamua kutoka nyumbani.
Sasa nyumba imekuwa na matatizo, yaani wengine hapo hatufai kabisa na anaefaa ni huyo mwenye hulka ya maneno, hii imeweza kutujengea ukorofi kwa kila tunalolifanya liwe zuri liwe baya utaonekana mbaya tu mzuri ni huyo mmoja.
Tukija katika point ni hivi, mume wangu ame-create family group whatsapp. Hiyo group ni mipasho, manyanyaso na masimango tu, sio group ya kupeana taarifa muhimu. Kukiwa na shida ndani basi sehemu ya kukusemea ni katika group. Sasa jana ka-share hiyo picha hapo na ndugu zake wote wakawa wanaisupport na kuifurahia, na hiyo yote kwasababu pia hawanipendi na wananisemea vibaya kila siku japo nasikia ila nanyamaza kwa vile sitaki shari.
Mume wangu anafahamu hayo yote, mimi binafsi nimeona hii ni kejeli kubwa kwa sababu waliomo kwenye group ni watu ambao wanatamani nipate shida, watafurahia wakisikia nanyanyasika, watafurahia wakisikia nimeyumba.
Sasa kwa mfano ningeweka mimi picha labda inasema husbands are always selfish and cheaters, vipi yeye asingeona namdhalilisha? Na je, hii ndio kazi ya group ya familia? Nilishatoka katika hii group kwa vile yeye ni creator akanirudisha tena, sasa nashindwa kumuelewa ananilazimisha kukaa kwenye hii group ili kunipa stress?
Hivi wenzangu mnamtafsiri vipi mwanaume mwenye tabia hizi? Naona yuko tayari niwe stressed na yeye kwake ikawa burudani.
Naombeni mtazamo wenu, lakini nahisi maisha ya ndoa yananishinda maana hayana starehe zaidi yana stress.
======================
Hii ndio picha iliyotumwa kwenye hilo Group la Whatsapp:
View attachment 204120![]()
Miss Chagga nimeshajitoa huko lakini najua atanirudisha tena, ila hii hali tu inanikwaza sana, yaani sijui niseme nini nieleweke lakini maisha ya ndoa yamekuwa magumu
Ngoja tumpatie mhanga hiki kiburudisho.
Pole mdada.
uvumilivu una mwisho mamy ..