What's Politics?

MAMMAMIA

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2008
Messages
3,821
Points
0

MAMMAMIA

JF-Expert Member
Joined Feb 26, 2008
3,821 0
Mtoto mdogo alimsogelea baba yake na kumwuliza, "Baba, nini Siasa?
Baba akajibu, "Subiri nikufahamishe ifuatavyo:
Mimi nikiwa ndiye ninayeleta fedha nyumbani, unaweza kuniita Tajiri.
Mama yako ambaye anapanga matumizi ya fedha, yeye tumuite Serikali.

Bibi yako yeye yupo hapa kuangalia kama kila mtu anatimiza wajibu wake, tumwite Chama cha Wafanyakazi,
Tajiri, serikali na chama cha wafanyakazi, vipo ili kuhakikisha mnapata mahitaji yenu. Nyinyi tunaweza kuwaiteni Wananchi.
Ah! Mhudumu wetu wa ndani yeye ni Mfanyakazi.
Na ndugu yako ambaye bado ni mdogo, yeye ni Hatma.
Umefahamu? Mtot akajibu itabidi aende kulala na kutafakari.

Usiku akamsikia mdogo wake analia, akamkuta yuko peke yake, kajaa mikojo na kinyesi mpaka kichwani.
Kwa hiyo akaenda chumbani kwa wazazi wake, akamkuta mama yake kalala fofofo; akaona hakuna haja ya kumwamsha.
Alipokwende chumba cha mhudumu, akamkuta babake na mhudumu wanavinjari kwenye sita kwa sita, wakati bibi anakwende na kurudi kuchungulia kupitia tundu ya mlango. Kuona vile, akaamua kurudi kitandani.

Asubuhi akamwambia baba yake, "Sasa ninafahamu maana ya siasa, kwani
wakati Tajiri anamnyonya Mfanyakazi na Serikali imelala, Wananchi wanapuuzwa na Chama cha Wafanyakazi kinaangalia tu bila kuchukua hatua na kwa hivyo kuifanya Hatma kuwa ya mashaka.
 

Forum statistics

Threads 1,357,801
Members 519,097
Posts 33,153,476
Top