The Palm Tree
JF-Expert Member
- Apr 13, 2013
- 7,951
- 12,535
Mimi nashangaa kidogo jinsi mambo yanavyokwenda dhidi ya mashtaka ya wabunge Mch. Gwajima (Kawe - CCM) na Jerry Silaa (Ukonga - CCM) ambapo mjadala unaendelea hata sasa niandikapo hoja hii...
Tayari m/kiti wa kamati ya "kuhoji" wenzake ameshasoma taarifa ya mahojiano na mapendekezo ya hatua (adhabu) wanayopaswa wapewe wabunge hao "waliokosa"...
Kinachoendelea kwa sasa ni wabunge kuchangia hoja ili kukubaliana au kupingana na mapendekezo ya kamati...
Ila kuna hili la kushangaza kidogo. Karibu 100% ya wanaochangia mapendekezo ya kamati ni wajumbe walewale wa kamati ya "KUHOJI" washtakiwa...
Katika akili ya kawaida, mimi nilidhani kuwa wajumbe wote wa kamati ya "kuhoji" baada ya kuwa wamemaliza kazi yao ya kupata utetezi wa wabunge wenzao wanaowatuhumu na kisha kuwasilisha ripoti yao bungeni, basi wangeishia hapo na kukaa pembeni kabisa na kuwaacha wabunge wengine wasio wanakamati iliyotoa "hukumu" wajadili maamuzi au mapendekezo yao ya adhabu na sababu/ushahidi wa makosa waliyoyaona...
Lakini kilichofanyika leo ni upuuzi mtupu. Yaani Spika awatuhumu wabunge wenzake, akawapeleka kwenye kamati kwa maelekezo yake, kamati hiyo inasikiliza utetezi wa watuhumiwa, inawahukumu, ripoti inapelekwa bungeni/spika, wanachangia hoja na kisha kujifanya wanapiga kura ya kukubaliana na hukumu...
Yaani ni full maigizo mwanzo mwisho!!