Tangu achaguliwe kuwa mbunge Halima Mdee amefunguliwa threads nyingi sana. Baadhi tu ya threads hizo ni hizi.
Kwako Mbunge wangu Halima Mdee.....!!!!
What has Halima Mdee done for Kawe in the Last 3 years?
Halima Mdee (Mheshimiwa sana)
Mbunge wetu Halima Mdee, njoo utuokoe Kunduchi Machimboni
Report card ya wabunge wa Dar: Halima Mdee
Mheshimiwa Halima Mdee Kulikoni???
Mheshimiwa Halima Mdee Karibu Tegeta Namanga
Kipindi kigumu jimboni Kawe
Pamoja na hii inayoendelea.
Nadhani ndiye mbunge aliyefunguliwa threads nyingi zaidi ya kuuliziwa utendaji wake, na anayefuatia kwa wingi wa threads ni John Mnyika.
Kutokana na wingi wa threads hizi kuna uwezekano wa mambo kadhaa, lakini mie nataja mawili.
Kwanza. Kwamba Halima Mdee hatimizi wajibu wake.
Hapa kwanza itabidi tuainishe wajibu wa mbunge ni upi? Katika kupitia katiba nimeona haya hapa:
Kazi kuu za Bunge
· Kutunga sheria
· Kujadili mipango ya maendeleo na kupitisha makaridirio ya fedha za matumizi ya serikali kupitia Wizara husika.
· Kudhibiti mwenendo wa serikali, wakati wabunge wanapouliza na kuhoji mambo mbalimbali ya serikali. (maswali na majibu Bungeni).
Nini kazi za Wabunge?
Kazi za Wabunge ni pamoja na:-
· Kuwakilisha wananchi na kuwasilisha mawazo yao Bungeni ili yapatiwe ufumbuzi.
· Kuhoji utendaji wa serikali
· Kuchangia uboreshaji wa miswada kabla haijawa sheria, na kuipitisha miswada iliyoboreshwa
Kitu gani kitarajiwe kutoka kwa mbunge?
Mbunge anatarajiwa:-
· Awe muelewa wa mahitaji na matatizo ya raia wake
· Ashirikiane kwa karibu na raia wake katika kutatua matatizo yao na kuleta maendeleo kwa kusikiliza wananchi juu ya kero zao, kusimamia utendaji wa halmashauri, kwa kutetea mgao wa bajeti ya serikali (si kwa kutumia pesa zake binafsi)
· Awawakilishe kikamilifu katika Bunge.
Je Halima Mdee anatekeleza haya? Kila mmoja anaweza fanya tathmini yake. Lakini mimi binafsi naona anatoa mchango mkubwa sana katika majukumu haya ya kibunge.
· Anachangia sana miswada mbalimbali ya kutunga sheria mpaka Mwanasheria mkuu na Mh. Lukuvi wanamwona kama anawasumbua.
· Anawatetea sana wananchi kwa maswali anayouliza bungeni, pamoja na michango anayotoa katika kuchangia mijadala ya bajeti. Hii hapa ni baadhi ya michango na maswali yake.
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...years-post4518750.html?highlight=#post4518750
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...years-post4518392.html?highlight=#post4518392
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...years-post4518191.html?highlight=#post4518191
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...years-post4518111.html?highlight=#post4518111
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...years-post4518061.html?highlight=#post4518061
· Hata hivi sasa ametayarisha hoja binafsi itakayotetea wananchi wa Kawe na Watanzania kwa ujumla juu ya masuala ya ardhi.
· Anafanya pia vikao na wananchi wake. Hapa ni mfano mmojawapo.
Lakini tukirudi jimboni Kawe kuna mambo yanayoonekana ambayo yameshafanyika kwa juhudi zake:
1. Barabara toka Millenium Tower, kupitia Chekechea ya Hindu Mandal hadi Shoppers Plaza inawekwa lami.
2. Daraja la njia fupi toka Rose Garden kwenda School of Journalism Mikocheni limejengwa.
3. Amesaidia kuhamisha soko la Tegeta na Stendi ya Daladala Tegeta toka barabarani kwenda sehemu nzuri zaidi.
4. Amesimamia vema ujenzi wa barabara toka Tegeta Nyuki hadi Bahari Beach kiwango cha lami. Ujenzi umekamilika.
5. Amesimamia vema ujenzi wa New Bagamoyo road na upgrade ya Old Bagamoyo Road.
6. Amepambana sana na uvamizi na ubadilishaji holela wa matumizi ya ardhi iliyotengwa kwa matumizi ya kijamii (KUNDUCHI, WAZO, MADALE n.k.) na kubatilishwa na kupewa watu wenye pesa. Katika hili kikwazo ni madiwani (wa CCM), ambao ndio wawakilishi wa maeneo husika kwenye vikao vya halmashauri pamoja na maafisa wa Halmashauri (inaongozwa na CCM) ambao ndio watekelezaji na ambao hawampi ushirikiano. Hapa ushirikiano wa Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ulihitajika sana.
7. Amekusanya data za viwanda na mahoteli yote ya jimboni kwake ili kuhakikisha wanalipa kod inayoongeza pato kwa shughuli za maendeleo ya jimbo la Kawe.
8. Ameshiriki unanzishaji na uendelezaji wa vikundi vya kina mama Kawe.
9.Amepigania chuo cha IMTU Kilikuwa kinatoza ada kwa dola za marekani sasa kinatoza kwa fedha za TZ, pia ada ya imeshuka na kuwa fixed.
10. Eneo la Tegeta amesimamia ujenzi wa Shopping mall ya kisasa. Imekamilika.
11. Amehamasisha na kuamsha ari ya vijana na kina mama katika kushiriki kwenye siasa na ameonyesha umahiri na kujiamini kwa hali ya juu jambo ambalo lemesaidia sana kubadili mtazamo wa wamama na wasichana walio wengi kwamba wakina dada nao wanaweza.
12. Amekuwa na mchango mzuri sana katika kujadili miswada bungeni, na katika kuibua hoja za kitaifa.
Na mengine mengi sana mnisaidie kuongeza.
Ameyafanya yote haya licha ya juhudi za makusudi za Halmashauri inayoongozwa na CCM (ambao ndio wanapokea fedha za maendeleo za jimbo) na madiwani (ambao ndio wawakilishi wa wananchi wa kata zao kwenye halmashauri) kumkwamisha. Masuala ya ardhi ni mfano wa kukwamishwa na madiwani wake.
Pili, kwamba, huyu mtu anaikera system. Inawezekana anaikera system kwa michango yake bungeni ambayo huhoji ubadhirifu, ufisadi, kutowajibika kwa viongozi wakubwa wa serikali. Kumbuka hata uvunjaji wa baraza la mawaziri wa mara ya mwisho, ulichochewa katika hatua za mwanzo na Halima Mdee. System ina namna yake ya
kunyamazisha wenye kelele. Mifano ipo mingi tu Tanzania sihitaji kutaja. Inawezekana kuna watu hutumika humu na system kwa ajili ya kutekeleza hilo. Mfano: threads nyingi hapo juu zimeanzishwa na
MAFILILI.
Kama hili ndilo, sisi wananchi wa kawaida tuwe makini kuangalia na kutokurupuka kumshambulia bila kutafakari vizuri. Nasema hivi kwa kuwa mtu anayeikera system kwa kutetea masuala yenye maslahi kwako mtu wa kawaida, huyu hayuko kinyume chako.
Mwisho najiuliza swali: hivi sisi watanzania tunatamani bunge letu liweje?
· Bunge lililojaa wabunge wa chama kimoja ambao wameapa kulinda maslahi ya Chama chao hata kama inabidi mwananchi wa kawaida apigwe teke?
· Bunge ambalo kazi yake ni kupigia makofi mawaziri, au bunge linalowawajibisha mawaziri?
· Bunge lililojaa wabunge matajiri ambao wana uwezo wa kuwahonga fedha zao binafsi, au wabunge wenye uchungu na wananchi na japo hawana uwezo wa kutumia fedha zao binafsi, lakini wanaibana serikali kuhakikisha kodi yako wewe mwananchi inakufanyia kazi wewe mwananchi?
Ndio maana wanasema akili za kuambiwa changanya na za kwako.
Mie ni mchanga sana hapa jamvini lakini huu ndio mchango wangu katika maswala ya demokrasia ya vyama vingi.