What has Halima Mdee done for Kawe (2010-2015)?

Kwenye miti hakuna wajenzi. Sisi kata ya Kunduchi tunamsubiri aje kwetu ahamasishe maendeleo lakini miaka 2 hatujamuona. Hatuhitaji michango yake tunataka uongozi wake.
 

kuna mwingine au sijui ndio wewe wewe aliibuka hapa na hoja kama hii hii kwa upande wa Mnyika, akimponda kuwa hajali jimbo lake la Ubungo. Leo hii mmeamia kwa Mdee....hamueleweki:A S angry:
 

Nikupe nini mkuu, Umesama yote! TEMEKE, UKONGA, ILALA NA KINONDONI ni ASALI NA MAZIWA!
Na kama mtoa hoja ni mpenda mageuzi kama anavyo taka watu wote tuamini! Angetafuta njia muafaka ya kumshauri kamanda Mdee ambaye mimi naona anachampa kazi kivitendo. Hoja yake Binafsi inalenga kutatua matatizo ya ARDHI si jimboni kwake peke yaka bali nchi nzima. To me Halima Mdee THINKS BIG!
 
Yupo bize na Joshua Nassari kule Arusha si walitangaza jukwaani kwani hamjui kama Nassari ni "open admirer" wake :becky:

Tulieni kwanza atarudi mwishoni mwa 2014
 
Ni kweli. Hata ofisi ya mtaani kwetu haijafunguliwa kitambo.

Ziko wapi ahadi za kuimarisha barabara jimboni? Barabara ya Goba kwenda Mbezi Luis ni mfano wa utendaji wake hafifu.

Uchaguzi Mkuu 2015 ukinikuta Kawe sitamchagua. Wasifanye kosa la kumpitisha.
 
Unataki watu waamini kuwa unaitakia mema CDM,kwa kuanika hapa unadhani umemsaidia?umechukua hatua gani kumwandikia malalamiko haya?umeshindwa pia kufikisha malalamiko yako kwa uongozi wa juu wa cdm?acha kutumika kijana!
Nyie ndio Mnaotetea uwepo wa funza kwenye vyakula
 
Hakuna haja ya kuzungumzia jimbo ambalo halipo mikononi mwa chadema kwa sasa tunachoangalia ni je haya majimbo ambayo tumeyapata tunayatendea haki?Yatakuwa chachu ya kupewa majimbo zaidi?haiwezekani kufagia kwa jirani wakati kwako kuchafu.
 

Sasa hapo ndio pa kueleweshana,kama yapo yanayofanyika na huyu mtoa mada hajayaona ndio pa kusema,lakini sio tutake kuangalia majimbo mengine ambayo hatunayo na sio haya yaliyo mikononi mwetu.
 
Kuna watu wanaendeshwa na hisia badala ya uhalisia,yaan kama jambo likifanywa na chadema tena likiwa la hovyo ndio watu wasiliseme kabisa,tunahitaji kubadilika ili chadema iendelee,palipo na uozo tuseme,alie haeleweki aambiwe kama vipi atoke kwenye chama,Mnafikiri tutaendeleaje bila kurekebishana na kuambiana ukweli?
 
Ooooooooooh Mama Porojo!


 
Lakini mara zote mti wenye matunda ndio hupopolewa na mawe! Cha msingi Kwa Mdee na Makamanda wote ni kukwepa mimawe ya wenye uchu kwa kuwazodoa na hoja nzito nzito! Keep it up lazima mtaandamwa sana!
 
hii ni hoja ya msingi,halima kasaidie kule achana na ushabiki wa wajinga,jimbo linakutegemea
 
Halima Mdee anashughulikia kesi ya LULU kwanza... kawe mbona wanajuta
 
No comment, toa ushahidi, he who goes to equity must do equity
 
Haya ni majungu tu, Mdee ni mmoja wa wabunge bora sio wanawake tu, bali wake kwa waume, nchi nzima; Mimi ni mwana ccm lakini 2015 nitampigia kampeni kwa nguvu sana mbunge wangu huyu apite; kuwatoa Mdee, Lissu, Mnyika ubunge ni wendawazimu; ni muhimu waendelee kuwepo ili CCM ijifunze maana ya kuwa mbunge ni nini; Ubunge sio kuula kama magazeti yanavyoripoti, ubunge sio sawa na ajira Vodacm au Barclays, bali ni kutumikia wananchi, na Mdee has done just that!!!

Kama nia yako ni kutafuta nafasi usimamishwe kawe 2015 na Chadema, kuna njia bora zaidi ya hizi; Mdee ana mapungufu yake kama binadamu lakini ukifanya a cost-benefit analysis, net effect ya ubunge wa Mdee ni HASI, sio CHANYA;
 
Wakati mwingine wabunge huwa mnawalaumu bure. Wananchi wenyewe hawana ari ya maendeleo kwa hiyo hata mbunge akiwa na mzuka vipi unazimika tu kutokana na jinsi jamii ilivyorelax kwenye dimbwi la umasikini...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…