What has Halima Mdee done for Kawe (2010-2015)?

What has Halima Mdee done for Kawe (2010-2015)?

Hata mimi nasikitika Halima Mdee ametuacha amekuwa kimya kama hakuna lilitoke jimboni kwake. mimi nina kiwanja nusu heka na nimejenga kanyumba kangu kadogo jamaa wamekabomoa? wanasema eti sisi ni wakimbizi wanadangany'a public sisi ni wakimbizi kutika Congo mara sijui Burundi ili public iwasupport na kuona imefanya vyema. lakini yote haya yakitokea Halima Mdee amekuwa kimya yani nikikumbuka siku ya uchaguzi mwaka juzi niliamka alfajiri kwenda kumpa Mdee kura yangu yani roho inaniuma. nashangaa kwanini hawa wabunge wanafuatilia mambo ya majimbo mengine alafu yao wanayanyamazia tu. Halima Mdee tunakuomba basi ongea hata neno tukusikia sisi tunajua wewe unaujua ukweli wote dada yetu
Unamlaumu Halima Mdee kwani Chadema ina tinga tinga na polisi wa kusimamia bomoa bomoa, mmeiweka madarakani serikali dhaifu na hayo ndo malipo yenu............................... unamlaumu mkwezi wakati nazi imeliwa na mwezi
 
hebu tuongee ukweli wakuu,Mh Halima Mdee yuko wapi??naombeni jibu hapo,vilevile tunaomba record ya utendaji kazi jimboni mwake,tusiwe tunabisha kila hoja inayoletwa hapa bila kuwa na ushahidi!

Kama unataka kujua yuko wapi, yuko kawe na tangu wiki iliyopita amekuwa akikutana na wapiga kura wake maeneo mbalimbali.

Ni jumamosi tu alikuja hapa kizabizabina mmoja wa huko magamba akijifanya kumlalamikia Halima Mdee ushahidi wa kazi zake ulipofunguliwa hapa aliondioka bila kuaga. Sasa na wewe kama una nia ya dhati ya kutaka kujua mdee amefanya nini unaweza kufanya homework yako vyema kwa kusearch hapa hapa JF utaona thread zote za Mdee na majibu yake.
 
...wakati "wagonga meza"(wabunge wa magamba) wakishirikiana na bi-kiroboto kupitisha sheria kandamizi huwa mnashabikia na kutuzomea...leo hizo sheria mbovu mlizozishabikia wakati zinapitishwa zikianza kufanya kazi(kula kwenu) mnaanza kulia kilio cha mbwa midomo juu...tulieni myolewe ili akili ziwarejee,siku CDM tukisema haya ni mapanya muone japo mikia...
 
Nilikuwa na imani kuwa wabunge wa upinzani ni wabunge mbadala. Mimi ni mmoja wa waathirika wa bomoa bomoa ya Madale ambayo kuna kila aina ya ujanja ujanja lakini tangu tupate matatizo hayo sijawahi kuona mbunge wangu HALIMA MDEE akisema lolote au hata kuwatembelea waathirika kujua shida zao na namna ya kuwasaidia kwani ni wapiga kura wake.

wapo wanaolala nje hadi sasa, wapo walionyang'angwa ardhi kwa nguvu ya fedha lakini Halima ambaye ni mjumbe wa baraza la madiwani la Kinondoni nilitegemea angekuwa na kauli ya kutueleza wananchi tulioathirika na bomoa bomoa hiyo katika eneo la Madale nakalekwa, madale tuaroho na madale nakasangwe. Ni zaidi ya mwezi sasa tangu kupita kwa bomoa bomoa hiyo.

Halima anajua ukweli kwa sababu yuko kwenye vikao vya manispaa ya kinondoni lakini pia niliambiwa kasomea sheria ( i stand to be corrected) ni sheria ipi inaruhusu kumnyang'anya mwananchi aliyekaa eneo kwa miaka kumi bila kuendelezwa hao wamiliki halali akina Michael Chacha na wenzake walikuwa wapi miaka yote. Sheria inatoa miaka mitatu tu kwa ardhi ambayo haijaendelezwa kunyang'anywa au kuwa mali ya yule anayelindwa na sheria hiyo kwa maana kwamba kama mwananchi ameishi hapo kwa zaidi ya miaka mitatu bila mmiliki halali kutokea sheria inatambua na kumpa umiliki yule aliyopo kwa wakati huo.

My take: Halima Mdee acha kukimbilia kigamboni kuwalilia wananchi wake kutokakana na hofu ya mji mpya anza na jimbo lako. Bado tunakusubiri uje kuongea na sisi wananchi wa Madale ingawa umechelewa.

source: Mimi mwenyewe nilikuwa na kiwanja cha nusu heka Madale.

Huyu alima Mdee amejisahau sana, Hata kuanzisha mchakato kwa wakazi wa Wazo na Madale kupata maji ameshindwa. Poleni wakazi wa jimbo la KAWE. Ilitakiwa agombee Kinondoni maana ninamuona anashinda baa za Kinondoni na wapambe wake.
 
Umekosa hela ya bia wewe ndio maana unamuonea donge Mdee kwenda baa na wapambe wake. Kama vipi peleka maombi ya kuwa mpambe ili ufaidi pombe za bure.
 
Umekosa hela ya bia wewe ndio maana unamuonea donge Mdee kwenda baa na wapambe wake. Kama vipi peleka maombi ya kuwa mpambe ili ufaidi pombe za bure.
Mwita! Mwita! Mwita! ukweli tutasema hata kama unaumiza. Punguza jazba.
 
Ingekuwa enzi zile wakati CHADEMA wanaiheshimu Jamiiforums viongozi wake wangekuwa washakuja kutolea swala hili ufafanuzi...

Mkuu nakusahihisha kidogo au kukumbusha,Elimu ya uraia walioitoa CDM inatosha kabisa kwasisi tuliopewa elimu hiyo kutoa majibu madogomado kwaraia wenzetu kama Mama Porojo!Au hata wewe utakapokuja nahoja kama yamama Porojo.
 
Kwanza it is an insult kumwita HARIMA ni HALIMA... Hii inaonyesha jinsi usivyomheshimu... Kwanini ni YEYE ANAYESHAMBULIWA Umeona

Wabunge wa TEMEKE na ILALA na KINONDONI? Hawajawahi kuulizwa CHOCHOTE HUMU ndani na wao ndio MATAJIRI WAKUU zaidi ya

HALIMA... Kafanya kazi kubwa JIMBONI zaidi ya HAO WA CCM yeye ndio wa kutishiwa na wewe?

Kama una jazba ya mambo yako ya kimaisha, haidha huna ajira, umebwaga na kicheche wako au umepatwa na jambo lolote linalofanana na hayo niliyoyaorodhesha basi usitumie uwanja huu wa great thinkes kuja kujifariji kwa kutoa mineno yako ambayo kimsingi haina mantiki katika hoja tajwa hapo juu. Sio lazima utoe maoni wala mawazo kama unajua hayajazi hata kikombe cha kahawa, ni bora ubaki nayo kichwani usubiri yapevuke ndio uyatoe maana ndio yanaweza kuleta manufaa zaidi.

Swala la mwananchi kutoa malalamiko yake kumuelekezea mbunge wake ni jambo ambalo linakubalika kabisa na hapa ndio maala sahihi kabisa kuyaleta ili kundi kubwa la watu waliolewa na mapenzi ya upinzani waamshwe kwa mifano sahihi kabisa, kwamba kuweka chama pinzani sio mwarubaini wa matatizo yanayotukabili wananchi, kama wengi wenu humu mnavyojiaminisha.

Ningependa kumaliza kwa kusema, viongozi wa chadema hawana utayali wa kuona mabadiliko kwa umma wa watanzania, bali wapo tayari kuutumia umma kwa ajili ya mabadiliko yao binafsi, kwenye hili la mabadiliko yao binafsi linajionesha waziwazi kwa kuona viongozi wa chadema wanavyoshinda na kula bata marekani mara kwa mara, wakitembelea magari ya kifahari na kupanga kwenye apartment za gharama kubwa, all in all wanawanyonya wanachama wao effectively na kuwatekenya kwa maneno matamu kama M4C na mengine mengi ya namna hiyo, wewe unaendelea kuenyeka huku wenzako wanapanda pipa tu. Badilika ubadili Taifa.
 
Hivi dada yetu Mh: Mdee huwa sio memba humu?

Angetia timu kwa dakika kadhaa akatuweka wazi kidogo. Nadhani huu ni uzi wa 3 au 4 hivi kumhusu. Najua sio kweli per se haya yaliyoandikwa lakini if she can clear the air please
 
Yaani ukavamie viwanja vya watu kwa mapanga na marungu alafu utegemee Halima Mdee aje kutetea uovu wako?

Apo tunadanganyana!
 
Wakati mwingine tunafikiri wapinzani ni dawa ya matizo yetu kumbe si kweli ukimya wa Halima Mdee kwenye tatizo letu la Madale hakika nimeushangaa sana.

Acha porojo zako wewe, mlimchagua raisi wa ccm na waziri wa ardhi ni wenu pia,wafuateni,wale ndo wanaodhinisha ninyi kunyang'anywa ardhi yenu
 
Duh, kweli mmeamua kumkalia kooni Halima Mdee, lakini hakuwatuma kuvamia mashamba ya watu!
 
Kama una jazba ya mambo yako ya kimaisha, haidha huna ajira, umebwaga na kicheche wako au umepatwa na jambo lolote linalofanana na hayo niliyoyaorodhesha basi usitumie uwanja huu wa great thinkes kuja kujifariji kwa kutoa mineno yako ambayo kimsingi haina mantiki katika hoja tajwa hapo juu. Sio lazima utoe maoni wala mawazo kama unajua hayajazi hata kikombe cha kahawa, ni bora ubaki nayo kichwani usubiri yapevuke ndio uyatoe maana ndio yanaweza kuleta manufaa zaidi.

Swala la mwananchi kutoa malalamiko yake kumuelekezea mbunge wake ni jambo ambalo linakubalika kabisa na hapa ndio maala sahihi kabisa kuyaleta ili kundi kubwa la watu waliolewa na mapenzi ya upinzani waamshwe kwa mifano sahihi kabisa, kwamba kuweka chama pinzani sio mwarubaini wa matatizo yanayotukabili wananchi, kama wengi wenu humu mnavyojiaminisha.

Ningependa kumaliza kwa kusema, viongozi wa chadema hawana utayali wa kuona mabadiliko kwa umma wa watanzania, bali wapo tayari kuutumia umma kwa ajili ya mabadiliko yao binafsi, kwenye hili la mabadiliko yao binafsi linajionesha waziwazi kwa kuona viongozi wa chadema wanavyoshinda na kula bata marekani mara kwa mara, wakitembelea magari ya kifahari na kupanga kwenye apartment za gharama kubwa, all in all wanawanyonya wanachama wao effectively na kuwatekenya kwa maneno matamu kama M4C na mengine mengi ya namna hiyo, wewe unaendelea kuenyeka huku wenzako wanapanda pipa tu. Badilika ubadili Taifa.

BINGO !!! Issue sio HALIMA MDEE Issue ni CHADEMA nakunukuu kwenye Mabano " Ningependa kumaliza kwa kusema, viongozi wa chadema hawana utayali wa kuona mabadiliko kwa umma wa watanzania, bali wapo tayari kuutumia umma kwa ajili ya mabadiliko yao binafsi, kwenye hili la mabadiliko yao binafsi linajionesha waziwazi kwa kuona viongozi wa chadema wanavyoshinda na kula bata marekani mara kwa mara, wakitembelea magari ya kifahari na kupanga kwenye apartment za gharama kubwa, all in all wanawanyonya wanachama wao effectively na kuwatekenya kwa maneno matamu kama M4C na mengine mengi ya namna hiyo, wewe unaendelea kuenyeka huku wenzako wanapanda pipa tu. Badilika ubadili Taifa." Kwahiyo ni VIONGOZI unaowafikiria ndio wana Utayari wa kuona Mabadiliko?
Umeona CHADEMA wanakula BATA MAREKANI; Haukuona JUZI JUZI TU KINANA alikuwa MAREKANI KUFUNGUA TAWI LA

CCM WASHINGTON D.C? Alikuwa anacheza MUZIKI wa hali ya JUU; Wakamleta DIAMOND na ilikuwa ni ZAWADI toka IKULU;

Uliona DIAMOND aliitwa IKULU na RAIS KIKWETE ILI AENDE MAREKANI; Pesa hapo ni za WALIPA KODI; HAUJASIKIA PESA

WAZOZIPELEKA D.C. KUNUNUA WANACHAMA Mpaka wanagombana na Wanashitakiana US-IMMIGRATION ? Sasa NDIO

CCM ya kutawala ? NA INAONYESHA WEWE UNAFAIDIKA na UTAWALA HUU una ACCOUNT USWISI PIA?

MIMI SITEKENYEKI NA CHAMA CHOCHOTE; MIMI NI MPENDA HAKI; no one sided ruling... SINA SHIDA YA KAZI za BONGO.
 
Mama Porojo, Maralia Sugu, tandale one, yaani signature nyinginyingi tu, kesho utasema unaishi tandale kwa tumbo ooh mbunge wangu Mnyika, wiki ijayo utakuja na ile ya kike uliyoweka kapicha ka kuvutia utajifanya unaishi Arumeru. In short hamtawabadili mtazamo watanzania kwa JF, face book na hii mitandao ya jamii. Mwambie nape asimamie serikali yake kutekeleza ilani yao ya 2010. Hilo ndilo jibu, kushindwa hilo ndio anguko lenyewe, kumsakama Halima Mdee haitawasaidia, wapiga kura wameelimika. M4C daima, "Changes are innevitable, if you do not change, change will change YOU". Nape anajua, Mukama anajua, ila wanawaficha tu. Ndio maana leo tuna vyama vingi, unadhani CCM ilipenda vyama vingi, ililazimishwa na wind of change. Mwambie ndugu yako Komba, kama alifikiri alikuwa anaimba tu kuburudisha hadhira, basi hiyo ndio maana yake "The wind of change is sweeping accross the african continent. In fact is in Tanzania for real.
 
Bado hajaolewa, mchumba wake wa mwisho alikuwa Joshua Nasari sijui wamefikia wapi walitangaza hadharani kwenye uchaguzi wa Arumeru Mashariki.

wa kwanza alikuwa yupi we chakubimbi? yaani uvunje sheria halafu upinzani ukutetee we gamba? mbona hamuishi mambo nyie lakini? sasa hapo unataka kusema hafai ubunge kwa kuwa hajaja kukuona baada ya wewe kuvunja sheria? mtajifunza lini kuishi kwenye mstari jamani? mmezoea hadi mnaona kuwa ni utaratibu kuvunja sheria kha!
 
Mama Porojo, Maralia Sugu, tandale one, yaani signature nyinginyingi tu, kesho utasema unaishi tandale kwa tumbo ooh mbunge wangu Mnyika, wiki ijayo utakuja na ile ya kike uliyoweka kapicha ka kuvutia utajifanya unaishi Arumeru. In short hamtawabadili mtazamo watanzania kwa JF, face book na hii mitandao ya jamii. Mwambie nape asimamie serikali yake kutekeleza ilani yao ya 2010. Hilo ndilo jibu, kushindwa hilo ndio anguko lenyewe, kumsakama Halima Mdee haitawasaidia, wapiga kura wameelimika. M4C daima, "Changes are innevitable, if you do not change, change will change YOU". Nape anajua, Mukama anajua, ila wanawaficha tu. Ndio maana leo tuna vyama vingi, unadhani CCM ilipenda vyama vingi, ililazimishwa na wind of change. Mwambie ndugu yako Komba, kama alifikiri alikuwa anaimba tu kuburudisha hadhira, basi hiyo ndio maana yake "The wind of change is sweeping accross the african continent. In fact is in Tanzania for real.

Mkuu natumia kasimu katochi ila NAKUPA LIKE HAPO!Wataelewa tu kuwa kuweweseka nidalili tu yaubongo kutokuwa nautayari!
 
Najua nimewagusa chadema lakini huo ndio ukweli kama tunataka nyota ya Halima Mdee izidi kung'aa tumfikishie ujumbe huu.... haitakuwa na maana kama tutakuwa tunawalaumu wabunge wa CCM tu lakini hao mbadala tukaonekana ni kosa kuwaambia wanapojikwaa.
Sidhani kama issue hapa ni kuigusa CDM. Tambua CDM haipo madarakani ila wananchi kwa mamilioni wameamua kuwaamini. 2015 utayashuhudia haya nisemayo. Mheshimiwa MDEE hahitaji porojo ili nyota ing'ae. Utendaji wake makini ndo unaowafanya wananchi wa kawe waendelee kumuamini,
 
Maajabu saba ya dunia hili nalo liwepo. Yaani leo mama porojo unalia na rafu za ccm selikari.
 
Back
Top Bottom