What has Halima Mdee done for Kawe (2010-2015)?

What has Halima Mdee done for Kawe (2010-2015)?

MAMA POROJO, ni vema ukarekebisha jina la mbunge wako, km inawezekana. Ni Halima, si Harima. Na naona siku hizi punctuation marks hazina maana tena, au ndio dotcom world!? Compare: Halima Mdee na halima mdee.

Asante nilikuwa na mawazo mengi ya kupoteza mali hii (ardhi) hadi nikakosea.... shukrani.
 
Nilikuwa na imani kuwa Wbunge wa upinzani ni wabunge mbadala. Mimi ni mmoja wa waathirika wa bomoa bomoa ya Madale ambayo kuna kila aina ya ujanja ujanja lakini tangu tupate matatizo hayo sijawahi kuona mbunge wangu HARIMA MDEE akisema lolote au hata kuwatembelea waathirika kujua shida zao na namna ya kuwasaidia kwani ni wapiga kura wake.

wapo wanaolala nje hadi sasa, wapo walionyang'angwa ardhi kwa nguvu ya fedha lakini Halima ambaye ni mjumbe wa baraza la madiwani la kinondoni nilitegemea angekuwa na kauli ya kutueleza wananchi tulioathirika na bomoa bomoa hiyo katika eneo la Madale nakalekwa, madale tuaroho na madale nakasangwe. Ni zaidi ya mwezi sasa tangu kupita kwa bomoa bomoa hiyo.

Halima anajua ukweli kwa sababu yuko kwenye vikao vya manispaa ya kinondoni lakini pia niliambiwa kasomea sheria ( i stand to be corrected) ni sheria ipi inaruhusu kumnyang'anya mwananchi aliyekaa eneo kwa miaka kumi bila kuendelezwa hao wamiliki halali akina Michael Chacha na wenzake walikuwa wapi miaka yote. Sheria inatoa miaka mitatu tu kwa ardhi ambayo haijaendelezwa kunyang'anywa au kuwa mali ya yule anayelindwa na sheria hiyo kwa maana kwamba kama mwananchi ameishi hapo kwa zaidi ya miaka mitatu bila mmiliki halali kutokea sheria inatambua na kumpa umiliki yule aliyopo kwa wakati huo.

My take: Halima Mdee acha kukimbilia kigamboni kuwalilia wananchi wake kutokakna na hofu ya mji mpya anza na jimbo lako. Bado tunakusubiri uje kuongea na sisi wananchi wa Madale ingawa umechelewa.

source: Mimi mwenyewe nilikuwa na kiwanja cha nusu heka Madale nakalekwa.

Kwanza it is an insult kumwita HARIMA ni HALIMA... Hii inaonyesha jinsi usivyomheshimu... Kwanini ni YEYE ANAYESHAMBULIWA Umeona

Wabunge wa TEMEKE na ILALA na KINONDONI? Hawajawahi kuulizwa CHOCHOTE HUMU ndani na wao ndio MATAJIRI WAKUU zaidi ya

HALIMA... Kafanya kazi kubwa JIMBONI zaidi ya HAO WA CCM yeye ndio wa kutishiwa na wewe?
 
Mimi siwasemei wengine hii ni shida yangu na wananchi walioomba nipaze sauti kwa niaba yao kule Madele.
 
kama unaweza kunirudishia fedha yangu ndio inafanya niseme hayo ardhi naweza kupata popote lakini hakuna fidia kwa ujanja janja. Kauli ya Halima Mdee ingekuwa na mwongozo yeye ni mbunge wa wote bila kujali chama so far sheria inamtambua hivyo.

Serikali yenu ya ccm ndio imewanyanganya ardhi kama unalitaka tena eneo lako basi 2015 usifanye makosa tena vote 4 cdm.....m4c with no apology.
 
Mkuu huyo mbunge mbona simfahamu?..haya ndiyo matatizo hata ya kutojua majina ya viongozi wetu.

Najua nimewagusa chadema lakini huo ndio ukweli kama tunataka nyota ya Halima Mdee izidi kung'aa tumfikishie ujumbe huu.... haitakuwa na maana kama tutakuwa tunawalaumu wabunge wa CCM tu lakini hao mbadala tukaonekana ni kosa kuwaambia wanapojikwaa.
 
Serikali yenu ya ccm ndio imewanyanganya ardhi kama unalitaka tena eneo lako basi 2015 usifanye makosa tena vote 4 cdm.....m4c with no apology.

Baada ya uchaguzi kuisha Halima Mdee ni wetu sote, hakuna mbunge wa CCM kawe
 
Mhhh sidhani kama sheria inasema kama unavyo tueleza hapa. Kama ingekuwa ni hivyo basi watu wengi wangepoteza maeneo yao. Mi navyofahamu si kweli kuwa kama eneo halijaendelezwa kwa miaka mitatu basi watu wavamie na kujigawia. Kwa case ya maeneo ya hao akina Chacha na Prof maeneo yao mmeyavamia yakiwa yanamimea ya kudumu kama miembe na michungwa ambayo wavamizi mmeikatakata na kuiharibu. Ati leo unasema Mbunge aje kukutetea, kwa lipi?? Uharibu mali ya watu kwa kisingizio cha kutoendelezwa then useme mbunge aje akutetee?? NO Way. Mbunge yupo kusimamia haki na sheria, maadamu hamkutenda haki, mnastahili kubomolewa!!!
 
Wakati mwingine tunafikiri wapinzani ni dawa ya matizo yetu kumbe si kweli ukimya wa Halima Mdee kwenye tatizo letu la Madale hakika nimeushangaa sana.

Kuwa mpinzani sio kupinga kila kitu serikali ya ccm imeshabomoa hata akipiga kelele haisaidii kesi bado ipo mahakamani serikali imetumia nguvu unataka yeye mdee afanye nini zaidi kwenye serikali hihi hihi inayosema utii wa sheria bila shuruti wakati yenyewe inauwa na kunyanyasa wananchi wake .....
Subiri cdm wachukuwe nchi ndio ulalame
 
Mhhh sidhani kama sheria inasema kama unavyo tueleza hapa. Kama ingekuwa ni hivyo basi watu wengi wangepoteza maeneo yao. Mi navyofahamu si kweli kuwa kama eneo halijaendelezwa kwa miaka mitatu basi watu wavamie na kujigawia. Kwa case ya maeneo ya hao akina Chacha na Prof maeneo yao mmeyavamia yakiwa yanamimea ya kudumu kama miembe na michungwa ambayo wavamizi mmeikatakata na kuiharibu. Ati leo unasema Mbunge aje kukutetea, kwa lipi?? Uharibu mali ya watu kwa kisingizio cha kutoendelezwa then useme mbunge aje akutetee?? NO Way. Mbunge yupo kusimamia haki na sheria, maadamu hamkutenda haki, mnastahili kubomolewa!!!

Halima Mdee anaweza kuja ama kutusaidia au kutueleza ukweli kuwa sisi ni wavamizi yote ni wajibu wake.

acha uongo kama hujawahi kufiki madale hakuna kitu kama hicho kwa miaka 7 sijawahi kuona miembe wala machungwa kama ni hivyo mbona hawajadai fidia ya mali yao tuliyoharibu.... labda kama ni wewe uliyetunyang'anya unaleta ujanja hapa. MTu hawezi kuweka makazi kwa miaka 10 eneo moja kisha unakuja na maneno hayo ya wajanja wa mjiji.
 
Bado Kesi iko mahakamani lakini tumebomolewa nyumba na kunyang'anywa ardhi tulitegemea mbunge ungekuja kusaidia namna ya kutafuta haki mahakamani lakini uko kimya. Wananchi masikini wamefungua kesi lakini kabla ya hukumu tumeondolewa kwa nguvu.

Mkuu MAMA POROJO, pole kwa yaliyowakuta, lakini ni vema kufahamu hii ndio serikali yetu hata sheria ikikiukwa namna gani bado wao ndio wanawahi huko mahakamani, ..
-Lakini pia put yourself in her shoes( Halima Mdee,(MP) ungefanya nini ili kesi iharakishwe?
-Ingekuwa hakuna kesi, ningesema ,mfungue kesi...lakini kesi ipo mahakamani je, atoe rushwa??

NB:next time check the spellings before you post(esp majina ya watu) bse hata mbunge wetu huyu huyu anaweza kukataa si yeye ingawa mimi na wewe tunajua ndiye ulim-maanisha.
 
Imekuwa jambo la kawaida kwa wananchi kuwaomba viongozi wao, hasa wabunge wawasaidie kugharamia miradi ya maendeleo. Mazoea haya yametufanya tusahau majukumu halisi ya wawakilishi wetu na pengine jukumu letu la kuwawajibisha pale wanapokwenda kinyume na wajibu wao.
Wabunge wamesahau majukumu yao ya msingi, badala yake wanajitwika majukumu ya serikali. Hali hii pia inasababisha wananchi tusahau vigezo muhimu vya kuchagua viongozi na kutumbukia kwenye mkumbo wa kuchagua viongozi matajiri-ambao nao wanaitumia fursa hiyo vilivyo kuimarisha utajiri wao pamoja na kuulinda.

Ieleweke kuwa sio wajibu wa wabunge kulipia/kugharamia miradi ya maendeleo majimboni mwao. Wabunge wengi wamekuwa wakitoa ufadhili mbalimbali katika majimbo yao, na kusahau majukumu yao ya msingi ya kuwawakilisha wananchi na kuwasilisha mawazo yao Bungeni ili yapatiwe ufumbuzi na kuisimamia, kuishauri na kuikosoa serikali katika kutoa huduma za jamii na kufanya miradi ya maendeleo.Y
Aidha, mfuko wa jimbo ambao, wabunge wa upinzania na chama tawala, CCM walisahau tofauti zao na kuupitisha kwa kishindo umekuwa nao ukitumika kama mali ya mbunge na katika kutafuta wema kwa wapigakura, wamekuwa wakiahidi mambo kadhaa huku wakiacha kuwaweka wazi wapigakura. Mwishowe wananchi wanaamini hizo ni huruma za mbunge wao.
Hali hii hakika umetupeleka pabaya kwani umesababisha na unaendelea kusababisha yafuatayo:
Mosi, hali ya wabunge kulipia miradi ya maendeleo kunavuruga utaratibu wa mchakato mzima wa mipango ya maendeleo. Tunazo sera nzuri za kusaidia jamii kuibua miradi ya maendeleo na fursa za hiyo miradi kuweza kugharamiwa. Hivyo wabunge wanapochukua jukumu la kugharamia miradi hiyo, kunafanya wananchi wanakosa imani/hawaoni umuhimu wa kufuata mchakato uliwekwa kwa ajili ya kuwaletea maendeleo na badala yake wanatupia jukumu hilo kwa wabunge.
Pili, hali hii inapunguza uwajibikaji wa pande zote mbili hasa uwajibikaji wa wananchi. Mradi unaogharamiwa na wabunge, unakuwa mradi wa mbunge. Hivyo wananchi wanakosa umiliki wa miradi hii kitu ambacho kinafanya miradi hii isiwe endelevu, na zaidi isiwanufaishe wananchi kwa upana wake.
Wakatiw mbunge kwa upande wake anashindwa kutumia nafasi yake ya uwakilishi kwa kujenga hoja kwa lengo la kupata fedha kwa ajili ya kugharamia miradi ya wananchi. Hatima yake ni kwamba serikali haioni umuhimu wa kutenga fedha kwa ajili ya miradi ya wananchi kwani mbunge anazo hela na hataki ibainike kwamba serikali/wananchi wanaweza kuendeleza miradi yao wenyewe.
Pia, mwenendo huu wa wabunge husababisha migongano kwenye Serikali za Mitaa; hii hutokea pale panapokuwepo fedha ambazo tayari zimeshatengwa kwa ajili ya miradi husika, ambapo fedha hizo zinaweza kuishia mikononi mwa wajanja. Wajibu wa mbunge katika hili ni kuwahamasisha wananchi kushiriki katika utekelezaji wa miradi hii na kusimamia matumizi ya fedha ya miradi hii.
Tatu, wabunge kugharamia miradi ya maendeleo inachochea hali ya utegemezi ndani ya jamii zetu. Serikali kupitia sera ya ugatuzi wa madaraka inalenga kuijengea jamii utamaduni wa kujitegemea kwa kuitaka jamii ishiriki moja kwa moja katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo ikiwa ni pamoja na kuchangia gharama. Sasa mbunge anapofadhili hii miradi, inafanya wananchi wajijengee utamaduni wa kusubiri kufanyiwa kila kitu. Na ndiyo hali ilivyo sasa kwani mara nyingi wenye fedha ni rahisi kupata madaraka.
Nne, wananchi wanajikuta wanapima viongozi wao kwa ufadhili waliotoa badala ya kutathmini utekelezaji wa majukumu yao kama wabunge. Hii inasababisha watu wasiokuwa na uwezo wa kifedha kukosa nafasi za uongozi hata kama wanao uwezo wa kuongoza vizuri. Hali imesababisha wananchi wengi kukosa uwakilishi na kuongezeka kwa matatizo makubwa ya uongozi mbovu, ufisadi, rusha na hali ngumu ya maisha huku wachache wakiendelea kunufaika na rasilimali za nchi hii.
Tano, wabunge wanaelemea katika kutafuta fedha za kugharamia miradi ya maendeleo badala ya kufanya majukumu yao ya msingi. Hii imesababisha wabunge kutoonekana majimboni kwa sababu inawabidi watafute mbinu mbalimbali za kupata fedha badala ya kutumia muda wao kutimiza majukumu yao ya msingi.
Badala ya kuwapigania wananchi ili kuwakwamua kutoka hali waliyonayo, wabunge wamejikuta wakipigania maslahi yao binafsi mfano wa sasa wa wanavyopambana kufa na kupona kuhalalisha kupanda kwa posho kwa madai ya kuwa wanatoa hela nyingi kwa wapiga kura kufadhili shughuli mbalimbali za maendeleo. Amenena mtu mmoja kuwa wanatumia fedha za walipa kodi kuwahonga wapiga kura.

Najua nimewagusa chadema lakini huo ndio ukweli kama tunataka nyota ya Halima Mdee izidi kung'aa tumfikishie ujumbe huu.... haitakuwa na maana kama tutakuwa tunawalaumu wabunge wa CCM tu lakini hao mbadala tukaonekana ni kosa kuwaambia wanapojikwaa.

Mkuu MAMA POROJO ,niliposema "viongozi wetu" nina maanisha kiongozi wa serikali (maana mimi pia ni mbunge wangu) lakini sijasema "viongozi wetu wa chadema"..

Please read between the lines before posting.
 
Mkuu MAMA POROJO, pole kwa yaliyowakuta, lakini ni vema kufahamu hii ndio serikali yetu hata sheria ikikiukwa namna gani bado wao ndio wanawahi huko mahakamani, ..
-Lakini pia put yourself in her shoes( Halima Mdee,(MP) ungefanya nini ili kesi iharakishwe?
-Ingekuwa hakuna kesi, ningesema ,mfungue kesi...lakini kesi ipo mahakamani je, atoe rushwa??

NB:next time check the spellings before you post(esp majina ya watu) bse hata mbunge wetu huyu huyu anaweza kukataa si yeye ingawa mimi na wewe tunajua ndiye ulim-maanisha.

Sina maana kuwa halima atatue kesi anatakiwa kuja kutuambia nini anakijua juu ya mgogoro huu kama kuna haki yetu basi tuendelee kudai na kama hatuna haki ni wajibu wake kama mbunge.
 
wananchi wanamwitaji Halima Mdee kama tunaona haina haja pia ni sahihi anaweza kuendelea na maisha yake kama hatuoni mantiki katika thread yangu
 
Back
Top Bottom