What can you cook best of all

Boflo

JF-Expert Member
Jan 20, 2010
4,384
4,409
What can you cook best of all



Do you know how to cook? If yes, what do you know to cook best of all?

I can cook everything. But best of all, the cakes! Everyone likes them, they are sweet and tasty...so that you will

lick your fingers
smile.gif
. But I won't tell you the secret
langue.gif


cook.jpg
 
ivi kile kipindi cha mapishi ITV kinarushwa alfajiri namna hii...I CAN ONLY MAKE A BLACK TEA...SENKIU!
 
sijui kama ni kweli unajua kupia mbege,
nina wasiwasi,
mm ni mtaalam wa mbege,
nipe matayarisho baada ya
kuchuja ndizi, yaani pale mwishoni mwishoni
ili nikubaliane na wewe mkuu.

Mi naweza pika mbege, in such a way that you will never walk alone..!
 
si unajua wazee ndo tunaona kwa kuwa zamani
kulikuwa hakuna kuchungulia
nyie vijana mnachunguliaga mno
ndo maana macho yanaogopa kuona mapema.

una macho makali....wewe kweli mdaku....umelionaje hilo boflo hapo !!!!!!!
 
sijui kama ni kweli unajua kupia mbege,
nina wasiwasi,
mm ni mtaalam wa mbege,
nipe matayarisho baada ya
kuchuja ndizi, yaani pale mwishoni mwishoni
ili nikubaliane na wewe mkuu.


Mwishoni huwa tunachukua mitungi ile tunaiweka kwa muda wa siku tatu kisha baada ya hapo inakuwa tayari..
kama nimekosea niambie kwa Pii emu.. Lol
 
ngoja nikutafutie kuna mkuu mmoja
alishaomba namna ya kutengeneza mbege
akapata maushauri kibao
naitafuta nitakubandika hapa usoni
ili ukaendeleze ujasiriamali wako mkuu.

Mwishoni huwa tunachukua mitungi ile tunaiweka kwa muda wa siku tatu kisha baada ya hapo inakuwa tayari..
kama nimekosea niambie kwa Pii emu.. Lol
 
hii hapa

quote_icon.png
By mamndenyi
1. Andaa ulezi - anika juani, twanga kwenya kinu, pepeta, osha, loweka maji yaelee mpaka juu, acha kwa siku tatu mpaka tano.
Osha tena, suuza maji safi, tengeneza kitu kama kitanda cha majani ya mgomba chini ili mradi ufunike udongo fresh
mwaga hapo huo ulezi. Funika vizuri na majani ya mgomba, yaani hewa isiweze kupita. Kaa siku tatu hadi nne,
toa ule ulezi utakuta umeota vitu fulani vyeupe, uanike juani, wakati wa kuanika bonda bonda yale mabonge ili kila
punje iwe peke yake. Anika kwa muda wa siku kadhaa hadi ukauke. Pepeta tena ili uchafu utoke. Hifazi kwenye gunia
zuri na safi kwa ajili ya kwenda kusaga hapa baada ya maandalizi ya ndizi kukamilika.

Ndizi - tumia ndizi ng'ombe - siyo bukoba - chagua ndizi zilizo komaa vizuri, vundika, zikiiva vizuri toa maganda, zipike
chombo kigumu, kama sufuria kubwa au chungu kikubwa, tumia kuni ngumu na zilizokauka ili ndizi ziive vizuri
pika hadi ziwe na rangi ya damu ya mzee - ni vizuri usizigeuze geuze sana kwani zinaweza kuungulia chini
epua, ngoja zipoe, hifadhi kwenye chombo kisafi, uchagani wanaweka kwenye pipa maalum lililotengenezwa kwa
miti (sijui kama yapo tena). Hakuna haja ya kufunika juu, ngoja muda wa siku tatu hadi saba inategemea na joto
la mahali ulipo. Utaona kama kuna puvu fulani linaanza kutoka kwa mbali, ujui ndizi tayari zimejisindika.

Utengenezaji wa mbege.

  • asubuhi na mapema jaza maji kwenye chombo kama pipa kisha weka huko zile ndizi ulizovundika, ile leya ya juu haifai hivyo unaweza ukawapa mifugo kama ipo. Koroga, tulia
  • baada ya kusaga ule ulezi - tuliza tu unga pembeni (saga siku ya kutengeneza mbege)
  • ikifika saa kumi jioni chuja zile ndizi ili kutenganisha uchafu na ile juisi
  • pika uji wa ule ulezi, usiwe mwepesi wala mzito sana hakikisha unaiva vizuri siyo kuungulia lakini.
  • changanya huo uji kwenye ile juisi ya ndizi. Koroga. Weka msesewe ambao tayari utakuwa umeutwanga vizuri na kuutenganisha na yale makapi yake (ndicho kilevi cha mbege) kipimo kisiwe kikubwa. Kama una watoto wanaopenda mbege watolee kabla ya kuweka msesewe.
  • ilale hadi kesho, mbege tayari.
ukitaka maelezo zaidi uliza.


Mwishoni huwa tunachukua mitungi ile tunaiweka kwa muda wa siku tatu kisha baada ya hapo inakuwa tayari..
kama nimekosea niambie kwa Pii emu.. Lol
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom