Wezi wamenitenda vibaya, Msaada

Wezi wamenitenda vibaya, Msaada

Ndakilawe

JF-Expert Member
Joined
Jul 6, 2011
Posts
4,815
Reaction score
2,832
Habari za Asubuhi wadau,

Juzi jumamosi maeneo ya Tabata Liwiti, majira ya saa kumi alfajiri nimestuka kuona mlango wa chumbani kwangu upo wazi, niaamka fasta, kufika sebuleni nikakuta milango ipo wazi, nikatoka nje fasta nikaona pochi ya honey imetupwa, geti lipo wazi, nikatoka speed nje nikawaona vibaka wanakimbia na pikipiki huku wamekumbatia TV Singsung Inch 42, nikawakimbiza bila mafanikio.

Hawa jamaa waliingiaje ndani? Ndio swali ninalojiuliza mpaka sasa, maana hakuna mlango uliovunjwa wala kitasa cha mlango.

Walichukua TV, wakachukua wallet yenye kilo 6, na kilo 6 ingine ilikuwa mezani (nilikuwa niende site kuwalipa mafundi hivyo nilidroo pesa kiasi bank), simu aina ya Blackberry i10, wakanywa na Heinken 1 kwenye friji na maji ya baridi (manina zao).

Hasira zinanipanda kila nikifikiria walivyomkuta honey kalala naked, bora mm nilikuwa na bukta. Nimejaribu kuwasiliana na jamaa zangu ambao nao wamewahi kupatwa na dhahama kama hii wanasema jamaa wanatumia ushirikina.

Popote mtakaposikia mtu anauza TV, tafadhali mdau wangu, uje inbox fasta unistue...!

Natangaza rasmi, Kuanzia leo popote nitakapokuta mwizi/kibaka anapigwa, lazima nimmalizie.
 
Pole sana ndugu yangu kwa tukio la kuhuzunisha.
Kwa sasa tuliza akili wezi huwa hawatoki mbali. Kama hawakufahamu basi wamepata msaada kwa anayekufahamu.
Badala ya kufikiria wezi fikiria watu waliowapa msaada na taarifa wezi juu ya pesa ulizotoa benkiNimeshiriki kwenye upelelezi wa kesi nyingi za wizi hasa za majumbani na zote zinafanana kwenye jambo moja tu; unaibiwa na anayekufahamu au aliyepata taarifa zako kutoka kwa mtu anayekufahamu.
 
sio bure Huyu atakua mhaya huyu ukisoma uzi wake utaelewa uhaya wake ila ana bahat sana hawajamlawiti
Acha ujinga mkuu, mimi naelezea hali halisi unaleta masihara mkuu. Ukisikia popote TV inauzwa aina iyo niliyotaja , tafadhali usiache kuniambia...!
 
sio bure Huyu atakua mhaya huyu ukisoma uzi wake utaelewa uhaya wake ila ana bahat sana hawajamlawiti
KWELI KABISA! Maana huu Uzi ukiusamalaizi hauwezi kuzidi mistari mitatu; "cha ajabu tumeambiwa mambo kibao! Ninacho wapendea wahaya ukiwa naye anataka ujue anavyomiliki vyooote!
Kuna siku nilipanda gari ya Mhaya mmoja aroooh! Alikuwa na gari ndogo lakini kiila alipokuwa akigonga bonde lazima aseme; " bora ningekuwa na ile vogue Yangu !
 
KWELI KABISA! Maana huu Uzi ukiusamalaizi hauwezi kuzidi mistari mitatu; "cha ajabu tumeambiwa mambo kibao! Ninacho wapendea wahaya ukiwa naye anataka ujue anavyomiliki vyooote!
Kuna siku nilipanda gari ya Mhaya mmoja aroooh! Alikuwa na gari ndogo lakini kiila alipokuwa akigonga bonde lazema aseme; " bora ningekuwa na ile vogue Yangu !
Mkuu umenifurahisha sana..'eti bora ningeenda na ile vogue yangu'...wahaya bana
 
kuna mmoja mtaalam wa makufuli ukipiga picha kufuli yoyoye duniani kisha umuonyeshe picha ya kufuli anakupa funguo yake hapohapo!huyo yeye huwa haendi kuiba ila akikupa funguo huwa haigomi na haitakuja kutokea.huyu unamlipa laki 3 ya kukukodishia huo funguo.alikuwa anatafutwa na dola akakimbilia hukohuko daslinga.huyu jamaa kila sehemu ikipigwa kazi watu wakishikwa wanamtaja yeye kama master key
 
Kwanza pole sana kwa yaliyotokea jaribu tu kuwatrace kwa simu waliyoiba. Kwenye huu Uzi nimevutiwa na huu uandishi yaani walikunywa Heineken yangu kwenye fridge hatari
 
kuna mmoja mtaalam wa makufuli ukipiga picha kufuli yoyoye duniani kisha umuonyeshe picha ya kufuli anakupa funguo yake hapohapo!huyo yeye huwa haendi kuiba ila akikupa funguo huwa haigomi na haitakuja kutokea.huyu unamlipa laki 3 ya kukukodishia huo funguo.alikuwa anatafutwa na dola akakimbilia hukohuko daslinga.huyu jamaa kila sehemu ikipigwa kazi watu wakishikwa wanamtaja yeye kama master key
Huyo mtu anapatikana wapi...
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom