Wewe una watu au watu wana wewe?

Wewe una watu au watu wana wewe?

Kikawaida kwenye maisha watu tunategemeana

Iwe kwenye afya au ugonjwa, kuna muda kila mmoja wetu huhitaji watu. Kuna msemo unasema watu ni mtaji

Lakini utakuta wengine wanasema, Mimi nipo kivyangu, sijui cha ndugu wala marafiki

Wengine huamini ukipata pesa watu watajitokeza wenyewe, kana kwamba pesa ni sumaku inayovuta kila kitu pesa subuni ya roho

Ukweli ni kwamba, watu tunahitajiana kwa namna nyingi sana

Unaweza kuwa umefungua mradi wako, lakini ili ufikie malengo lazima uwe na team ya watu wa kushirikiana nao

Kuna wakati unaweza kuumwa mpaka ushindwe hata kujisogeza hapo utahitaji watu wakusaidie

Ukiwa mahabusu, utahitaji mtu wa kukutolea dhamana

Ukiandaa sherehe, ili ifane na iwe na furaha lazima watu wajitokeze kulingana na mialiko uliyoitoa

Maana yake ni kwamba, watu tunahitajiana
Swali ni je, wewe una watu?
Una watu ambao ukiwaita wanaweza kuja?

Ukipata matatizo unaamini watakuwa pembeni yako, au ni watu wa misimu leo wapo, kesho hawapo?

Na moja ya watu tunaowazungumzia hapa ni ndugu
Ndugu zako ukiwaita watakuja? Au ni wewe ndiye unayewakimbilia kila wakati? ndugu vichomi

Hivi una mtu anayoweza kukukimbilia maji yakizidi unga?
Au upo kwenye kisiwa chako mwenyewe, lonely 🙁

ShesRise_1
Kuna member amekutumia barua ya wazi.
Kamjibu
 
Nakuonea wivu, pia nafurahi kwa ajili yako muombee sana

Unavyo vingi vya kumpa sio lazima iwe pesa dear tena yeye ndio anaejua anachopata kwako na thamani yake ukiachilia mbali undugu wenu
Yeye sio muda wote unipa pesa na shida sio pesa tu kuna kuumwa atakusindikiza hospital.
Anaweza kutuma msg nikajibu baada ya wiki
 
Mimi sina watu ila kuna watu walifanya niwe wa kwao ila baadae nikatoroka nikakataa kwa sababu walitaka niwe wao huku wao hawakutaka wawe wa kwangu pia ili mzani u balance

Sasa hivi nina mtu/watu ila na wao wakileta ubinafisi nao nitawatoroka kwa amani🙏

Soma vizuri usichanganyikiwe 😁
Tawiree!!!
 
Nje ya mada,

Hii comment imenifanya kuijua ID uliyokua unaitumia mwanzo kabla ya kubadili,kisha ukabadili tena na kua na hii ID ya sasa,yani hii ID ni third generation.

Ndani ya mada,

Watu wangu ni familia yangu,marafiki ni watu wakupita tu na huwezi ukawaamini sana.
 
Nje ya mada,

Hii comment imenifanya kuijua ID uliyokua unaitumia mwanzo kabla ya kubadili,kisha ukabadili tena na kua na hii ID ya sasa,yani hii ID ni third generation.
I'd ipi ile ya hata najua basi?
Kama ni hiyo kila mtu anajua sio jambo la siri hata kaka

Ndani ya mada,

Watu wangu ni familia yangu,marafiki ni watu wakupita tu na huwezi ukawaamini sana.
Ni sa hihi kabisa watu huja na kuondoka
 
Back
Top Bottom