Je, kipi bora kuajiriwa au kujiajiri?

Je, kipi bora kuajiriwa au kujiajiri?

Mwl Mwakujonga

JF-Expert Member
Joined
Jun 29, 2023
Posts
384
Reaction score
758
Je ni chague kipi kati ya kuajiriwa au kujiajili.

Kumekuwa na majadiliano kwenye mitandao ya kijamii na baadhi ya watu wanapotosha watu kwamba hakuna mtu aliye ajiriwa ambaye ni tajiri?

Ndugu yangu usidangaye na watu ambao hawajui kitu.

Fanya utafiti anzia katika eneo lako usiende mbali.
Kuna watu wanakwenda mbali na kusema hakuna mwajiriwa ambaye anaweza kumiliki Landcruiser V8.

Sio kwamba kuajiajiri ni kubaya hapana , inategemea kati ya mtu na mtu. Kama umepata nafasi ya kuajiliwa usiache hiyo nafasi utajukuja kunishukuru badae

Mafanikio ya mtu ni mchakato, mafanikio sio kitu cha siku moja. Binafsi nimeona watu wengi tu ambao maisha yao walianza kama watumishi wa umma wengine binafsi lakini leo ni mabilionie wakubwa tu.

Unaweza kusema haha hao hiyo haiwezekani au ni wezi tu hapana nasema inawezekana.

Ngoja nikupe shuhuda kadhaa kuna mzee mmoja ambaye alikuwa ni mtumishi wa umma alikuwa ni daktari katika hospitali ya serikali, alifanya kazi miaka kadhaa na baadae akaamua kuanzisha hospitali yake binafsi na kwa sasa hapa mjini hospitali yake ni miongoni mwa hospitali bora na nzuri, hapa kuna shuhuda nyingi tu za madaktari.

Hapahapa mjini kuna baba mmoja ambaye yeye alikuwa ni mhandisi wa mambo ya madini alipata kazi kwenye kampuni moja ya madini alifanya kazi miaka kadhaa na baadae akaacha kazi akaanza na yeye shughuli za madini na sasa ni bilionea mkubwa tu hapa Tanzania.

Kwa hiyo usidanganywe na watu, kwa mtu yoyote anayetaka kuwa tajiri njia zote ni sawa unaweza kuajiriwa ukawa tajiri wamaghorofa na magari na unaweza kuwa mfanyabiashara pia.

Kwa hiyo kama umepata kazi usidharau, kazi yako ifanye kuwa ngazi kuelekea malengo yako.

Faida ya kuajiriwa

Kwanza inakupa fursa ya kujua wateja wako ni watu wa aina gani? Kujua changamoto ya kile ambacho unatarajia kukifanya

Unapata fursa kujua sheria na kanuni mbalimbali ambazo unatakiwa kuzifata ili uweze kufanikiwa

Unapata wateja wako, wewe ni daktari au mwanasheria au mhandisi au taaluma yoyote inakupa nafasi ya kukutana na wateja, wale watu ambao unawahudumia hao ndio wateja wako wabadae

Unapata uzoefu kwa kile unachokifanya, sio rahisi umetoka shule ukaanzisha hospitali au kampuni sio kwamba haiwezekani inawezekana. Ila yule ambaye amefanya kazi kwa miaka kadhaa amejenga jina na sifa ni rahisi sana kupata wateja kuliko yule ambaye amenza tu moja kwa moja.

Yote kwa yote njia yoyote ni sawa ukipata fursa ya kuajiri ni vizuri sana lakini ukipata fursa ya kuajiriwa usiache maoni yangu sio sheria karibu kwa ya kwako
 
Kuajiriwa unadharaulika, unakuwa remote unakuwa kama ng'ombe..... unaweza kugombezwa kama mbwa na mdogo wako kisa kakuzidi cheo ama ni boss wako .......

Kujiajiri kuna presha..... wewe ndio boss, unajiamulia nini ufanye na nini uache! Bali kuna presha zake, ubongo lazima uchangamke, huwi lijinga kama upo ajiran kwamba mwisho wa mwez uwakika unapokea kiasi kadhaa ! Kote huko nipo, nategemea kuachana na kuajiriwa soon, kuna kamradi nafanya, nikiwekeza nguvu na muda ajira nitaiona ni utumwa tu .....
 
Na ukijiajiri ni muhimu kuusisimua ubongo bwashee 🍻
 
Kuajiriwa unadharaulika, unakuwa remote unakuwa kama ng'ombe..... unaweza kugombezwa kama mbwa na mdogo wako kisa kakuzidi cheo ama ni boss wako .......

Kujiajiri kuna presha..... wewe ndio boss, unajiamulia nini ufanye na nini uache! Bali kuna presha zake, ubongo lazima uchangamke, huwi lijinga kama upo ajiran kwamba mwisho wa mwez uwakika unapokea kiasi kadhaa ! Kote huko nipo, nategemea kuachana na kuajiriwa soon, kuna kamradi nafanya, nikiwekeza nguvu na muda ajira nitaiona ni utumwa tu .....
Ni sawa ila kama unataka kujiajiri usisahau utafanya kazi na watu na wengine watakudharau tu hata kama kazi ni ya kwako cha msingi kuwa na moyo mkuu, waulize watu wanoafanya kazi zinazohusiana na watu, kila mmoja analalamika kufanya biashara lazima uwe na uwezo wa kupambana na tabia za watu , waulize wauza bidhaa, usafirishaji hakuba mahali utakosa kufokewa labda kama unataka kukaa nyumbani lakini kwenye shughuli yoyote lazima ujue kuna watu walio na mawazo tofauti na wewe na lazima ujue namna ya kuishi nao kaka
 
Ubora wa Kitu ni ule unaouona wewe ndani yako unaweza kishauriwa ujiajiri Lakini Kuna watu wameajiriwa na wanashauri watu wajiajiri.
 
Back
Top Bottom