Wewe una watu au watu wana wewe?

Wewe una watu au watu wana wewe?

Mimi nilijifunza kua mbinafsi maana nilijikuta najitoa kwa watu Ila sasa hao watu nikiwahitaji mbinde kuwapata nikajifunza kua mbinafsi
 
Mimi nilijifunza kua mbinafsi maana nilijikuta najitoa kwa watu Ila sasa hao watu nikiwahitaji mbinde kuwapata nikajifunza kua mbinafsi
Umefanya vizuri wewe sio mtakatifu
Kupoteza nguvu zako au kujipa umuhimu kwenye maisha ya watu wasio na shukrani
 
Kikawaida kwenye maisha watu tunategemeana

Iwe kwenye afya au ugonjwa, kuna muda kila mmoja wetu huhitaji watu. Kuna msemo unasema watu ni mtaji

Lakini utakuta wengine wanasema, Mimi nipo kivyangu, sijui cha ndugu wala marafiki

Wengine huamini ukipata pesa watu watajitokeza wenyewe, kana kwamba pesa ni sumaku inayovuta kila kitu pesa subuni ya roho

Ukweli ni kwamba, watu tunahitajiana kwa namna nyingi sana

Unaweza kuwa umefungua mradi wako, lakini ili ufikie malengo lazima uwe na team ya watu wa kushirikiana nao

Kuna wakati unaweza kuumwa mpaka ushindwe hata kujisogeza hapo utahitaji watu wakusaidie

Ukiwa mahabusu, utahitaji mtu wa kukutolea dhamana

Ukiandaa sherehe, ili ifane na iwe na furaha lazima watu wajitokeze kulingana na mialiko uliyoitoa

Maana yake ni kwamba, watu tunahitajiana
Swali ni je, wewe una watu?
Una watu ambao ukiwaita wanaweza kuja?

Ukipata matatizo unaamini watakuwa pembeni yako, au ni watu wa misimu leo wapo, kesho hawapo?

Na moja ya watu tunaowazungumzia hapa ni ndugu
Ndugu zako ukiwaita watakuja? Au ni wewe ndiye unayewakimbilia kila wakati? ndugu vichomi

Hivi una mtu anayoweza kukukimbilia maji yakizidi unga?
Au upo kwenye kisiwa chako mwenyewe, lonely 🙁

ShesRise_1
1003445747.gif
 
Back
Top Bottom