Hupotezi watu ila wao ndio wanakupoteza wewe

Hupotezi watu ila wao ndio wanakupoteza wewe

Wakusolve

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2020
Posts
561
Reaction score
992
Hupotezi watu ile wao ndio wanakupoteza wewe.

Binadamu mara nyingi utambua thamani ya mtu na ata vitu baada ya kupotea, Kama wewe ni mtu mwenye pure heart(moyo wa upendo) una toa upendo kwa watu au jamii

Mfano marafiki bila kutarajia chochote kutoka kwao na wanashindwa kuthamini mchango wako jiondoe kwenye mfumo wao wa maisha ili universe iwafundishe.

Kuna muda universe(God) anaondoa watu kwenye maisha yako usijihisi kama kuna kitu unakosea ni kwamba watu wanao ondolewa wameshindwa kuweza kukumiliki(handle),

Wameshindwa kutambua thamani yako, wameshindwa kutambua upendo wako hivyo Mungu anaamua kuwaondoa ili wajifunze kupitia absence(kutokuepo) kwako kwenye maisha yao .

Unapokubali kuondoka kwenye maisha yao unarudisha energy back kwenye maisha yako itakusaidia kuendelea kung'ara sababu umetambua thamani yako.

Hii pia inaweza wasumbua maana ule upendo uliokuwa unawapa awawezi upata kwa mtu mwengine sababu Mungu akikupa baraka ukashindwa itumia hatakupa mtu mwengine ili ujifunze.

Hii pia hipo kwenye mahusiano unapo toa muda wako, nguvu zako na upendo kwa mtu lakini yeye ajali chochote na kuthamini kile unachotoa.

Jiondoe kwenye hayo mahusiano usiogope itakuaje omba Mungu akupe nguvu maana inawezekana una maumivu lakini ukiwa na Mungu atakusaidia kuweza kuondoka kwenye hali hiyo.

Mathayo 19:26
Yesu akawakazia macho, akawaambia, Kwa wanadamu hilo haliwezekani; bali kwa Mungu yote yawezekana.


Ukishaondoka na kutoangalia nyuma unafanya karma ifanye kazi yake atapata kile alichokuwa anakitoa ili ajifunze na akitaka kurudi usimpe nafasi utapata mtu mwengine ambayo atatambua thamani yako.

Kama unapitia kipindi cha kupoteza watu tambua sio mwisho , watu wanao ondoka tambua wakati wao umeisha,

Watu sahihi wataendelea kuwepo na wewe nyakati zote na pia watakuja watu wapya watakao endana na wewe mpya.
 
Back
Top Bottom