Wewe na simu yako ni nani anayemiliki mwenzake?

Wewe na simu yako ni nani anayemiliki mwenzake?

Sio simu ni internet ama online platforms/social media,

Nikipata internet hata kwenye laptop. Hii simu naiweka pembeni .
hapa uneiweka kitaalam zaidi, kuna kamsemo kua smartphone bila internet ni kitochi
 
Tuseme ukweli bila kupepesa macho
  • Unalala nayo kitandani
  • Ukiamka kitu cha kwanza ni kuiangalia
  • Ukiisahau nyumbani, siku yote unakuwa kama umetupwa kisiwa cha peke yako
  • Battery ikishuka chini ya 20% moyo unaanza kukudunda kama una deni.
  • Bundle likiisha kwa baadhi ya watu bora asinunue chakula anunue bundle.
Sasa swali ni moja tu: Wewe ndio unamiliki simu, au simu ndio inakumiliki wewe?

Na unapokosa muda wa kuishika, unahisi kama vile kuna mtu amekuondoa kwenye “group la maisha”😂😂


NI SWALI LA KIPUMBAVU. KAMA NIMEINUNUA MIMI, NAWEZA IZIMA NA KUIWASHA, NAWEZA ICHARGE, NAWEZA KUONGEZA AIRTIME N. K. NI WAZI KUWA MIMI NDO NAIMILIKI. SIMU HAIWEZI MILIKI MTU NA HAITATOKEA. HATA SIKU MOJA. IT DOESNT MAKE SENSE.
 
Mzungu ana akili sn akita kuua ashushe na bando uone addiction itakavyo kuwa kubwa zaidi
kuna binti mmoja atamaliza kazi zake mapema ofisini ila ataendelea kukaa mpaka jioni aendelee tu kutumia free internet ya ofisi
 
NI SWALI LA KIPUMBAVU. KAMA NIMEINUNUA MIMI, NAWEZA IZIMA NA KUIWASHA, NAWEZA ICHARGE, NAWEZA KUONGEZA AIRTIME N. K. NI WAZI KUWA MIMI NDO NAIMILIKI. SIMU HAIWEZI MILIKI MTU NA HAITATOKEA. HATA SIKU MOJA. IT DOESNT MAKE SENSE.
addiction ya simu inawezekana
 
Mwaka Jana nilienda mafunzo kwa miezi 5 (Off the Grid) kipindi chote hicho.
Callous ur Mind ndio wimbo wangu ktk kuanza pattern mpya .
Simu kwangu muhimu pale ntakapo ihitaji tu.
safi sana kama wewe ndo unaamua lini na wapi utumie simu
 
Tuseme ukweli bila kupepesa macho
  • Unalala nayo kitandani
  • Ukiamka kitu cha kwanza ni kuiangalia
  • Ukiisahau nyumbani, siku yote unakuwa kama umetupwa kisiwa cha peke yako
  • Battery ikishuka chini ya 20% moyo unaanza kukudunda kama una deni.
  • Bundle likiisha kwa baadhi ya watu bora asinunue chakula anunue bundle.
Sasa swali ni moja tu: Wewe ndio unamiliki simu, au simu ndio inakumiliki wewe?

Na unapokosa muda wa kuishika, unahisi kama vile kuna mtu amekuondoa kwenye “group la maisha”😂😂
Ajsee wacha inimiliki tuu. Raha sana kuperuz mitaaa ya jf na kucheki warembo wanatingisha matakoz kule tiktok
 
Sio simu ni internet ama online platforms/social media,

Nikipata internet hata kwenye laptop. Hii simu naiweka pembeni .
Tena kwenye laptop ndio balaaaa kwa sir wenye uraibu wa pilau....mpaka shemeji anajiuliza mbona kela leo mnapika ugali mlenda
 
nilikua nawaza hapa kutengeneza dawa ya watu wenye uraibu wa simu
Usipofanya deep analysis unaweza fikiria ni uraibu (addiction) lakini ukweli simu inatumika sana kwasababu ya mabadiliko ya teknolojia. Simu ndo kila kitu kwa sasa, huwezi kaa mbali na simu. Mfano mdogo majuzi kupitia simu nimetafuta,nime bargain, nimenunua, nimesafirisha mzigo kutoka sehemu tatu tofauti kwa wakati mmoja. Simu tu hiyo. Mimi nikiwa nimetulia zangu ofisini. Meanwhile mambo mengine nikiendelea nayo ndani ya simu hiyo hiyo. So matumizi ya simu yamekuwa makubwa kutokana na technology transformation na simu hazifumiliki bali upepo wa teknolojia ndo tunavuma nao. Mobile phone is everything.
 
Back
Top Bottom