bintimacho
Member
- Apr 25, 2008
- 41
- 1
Mkuu Fundi Mchundo,
Naamini kwamba uwezo wako wa kuelewa ni mkubwa. Lakini nashindwa kuelewa unapojifanya kutokuelewa nini hasa maana ya rangi NYEUPE!!
Rangi NYEUPE kamwe haimanishi UZUNGU! ALMASI na PAMBA zote zina rangi NYEUPE lakini zinapatikana hapahapa Afrika ya WEUSI, tena Tanzania kwa WASUKUMA walalahoi wa nchi hii. Wasukuma huiita PAMBA kwa jina la DHAHABU NYEUPE kwa sababu ya WEUPE wa RANGI yake ya ASILI. Inamaana tuwambie hao wasukuma waache kulima pamba(dhahabu NYEUPE) kwa sababu FUNDI MCHUNDO anaamini WEUPE ni UZUNGU??!! Au tuwalazimishe waamini kwamba PAMBA ina RANGI NYEUSI wakati ni NYEUPE! Ajabu!
RANGI NI RANGI TU WALA HAINAUHUSIANO NA TAIFA AU DINI YA MTU!
MUNGU WASAIDIE WALIOATHIRIKA KISAIKOLOJIA KIASI CHA KUWAABUDU WAZUNGU!
ZNI ujinga mkubwa kuamni kwamba Wazimbabwe hawawezi hata kulima mahindi wakati ni hao hao Wazimbabwe waliokuwa wakilima Mahindi kwa mzungu.. Hakuna mzungu aliyeingia shambani kuzalisha mahindi peke yake wote hao walikuwa na wafanyakazi Wazimbabwe..
Mkuu endelea kuamini unavyoamini lakini mimi binafsi naamini kabisa kuwa kinachofanywa na nchi za magharibi ni kikubwa kuliko tunavyosoma. Binafsi nilitaka kununua Chicken egg incubator na hatchery machine toka Zimbabwe nilikataliwa na bank yangu kufanya transaction kwa sababu ya sanctions.. Kuna mshikaji wangu ambaye anasafirisha Pamba toka Zimbabwe nje kwa kupitia South Africa na kanihakikishia kwamba ni lazima deal lipitie Suoth laa sivyo hakiuziki kitu.
Wazungu mtawalaumu mpaka YESU arudi without Africans getting any better!
Humility, Humility, Humility!. Mugabe anataka kushindana na wazungu, kuwaonyesha kwamba yeye ni kidume!. Kiongozi ni lazima uwe tayari kusacrifice kwa ajili ya watu. kuna raha gani kudindiana na wazungu wakati watu wako wanakufa kwa njaa, ukosefu wa dawa, na pia kuzidi kudidimia katika shimo la umasikini?.
hata kama Mugabe ana haki ya kutawala, lakini yeye binafsi ilibidi ajiondoe kwa sababu yeye ndo imeshafahamika kwamba amekuwa tatizo. ilibidi afikirie kwa moyo na akili aone kwamba kuwepo kwake kunasolve tatizo au kunazidisha tatizo?. umwamba wakati mwingine hausaidii!.
sasa kama Mugabe anadhani hali ngumu inatokana na vikwazo vya west, na wakati huo huo anafahamu fika kwamba vikwazo hivyo vimewekwa kwa sababu yake, kwa nini sasa asiondoke ili hivi vikwazo viondoke. na kama ni kuhusu hii land reform, mtu mwingine anaweza kuendelea na hiyo programu kwani lazima iwe Mugabe?
Mugabe anataka kushindana na wazungu....
sasa kama Mugabe anadhani hali ngumu inatokana na vikwazo vya west...,
Sio kweli kwamba Mugabe anataka kushindana na Wazungu, au anaamini hali ya Zimbabe inatokana na nguvu za nje. Hana hiyo dhati.
Anachofanya Mugabe ni sawa na Osama bin Laden anaposema ujasusi ni juhudi za kutetea Uislamu unaotishiwa na Wamagharibi ikiongozwa na US. Hiyo inamsaidia kupata sapoti ya wapenda Uislamu, na wachukia ukoloni mamboleo wa US na siasa zao za kibeberu (imperialism). Kama unachukia ubeberu, na ukoloni mamboleo na pia ni mpenda Uislamu unaweza kujikuta unajiunga na kambi yake ya mafunzo, kumbe ukweli ni kwamba mzizi wa fitina haswa ni bifu yake na watu wa kwao huko Uarabuni ambao walikataa mawazo yake fulani fulani miaka kibao iliyopita.
Anachofanya Mugabe kunyooshea kidole Magharibi ni pretext kama hiyo hiyo ya kumsaidia kupata hurumu ya wote tusiopenda Ukoloni mambo leo na ubeberu wa Wamagharibi. Ni usanii wa kisiasa.
Asante mkuu! Ungekuwa karibu ningekupa hata bia moja pale Rose Garden kesho!
Binafsi simpongezi Mugabe hata kidogo isipokuwa mnashindwa kusoma between the lines...Hivi kama Wazungu wangekubali matokeo ya kuchukuliwa ardhi bado mnafikiri kuwa Mugabe angekuwa huyu wa leo?... Na ilikuwaje ktk miaka yote toka 1982 hadi 2000 (18 yrs) Alikuwa akiitwa kiongozi bora Africa...While watu kama mimi nilifahamu kabisa kuwa Mugabe ni mmoja kati ya NDIVYO TULIVYO!
Kilichochukuliwa ni ardhi ambayo ilikuwa inamilikiwa na wazungu, hilo la mashamba ni lugha ya mzungu!...ardhi ambayo sio laqzima ilikuwa ikitumika ktk kilimo..
Kisha mnafikia kuamini ati vikwazo ni kuhusiana na vifaa vya kijeshi, lini Zimbabwe wamenunua vifaa vya kijeshi toka nchi za magharibi na hununua vifaa hivyo mara ngapi kwa mwaka! mara ati oooh kazuiwa kusafiri, Sii huyu Mugabe alikuwa New York (UN) na Italia majuzi tu..
Fundi Mchundo,
Mkuu endelea kuamini unavyoamini lakini mimi binafsi naamini kabisa kuwa kinachofanywa na nchi za magharibi ni kikubwa kuliko tunavyosoma. Binafsi nilitaka kununua Chicken egg incubator na hatchery machine toka Zimbabwe nilikataliwa na bank yangu kufanya transaction kwa sababu ya sanctions.. Kuna mshikaji wangu ambaye anasafirisha Pamba toka Zimbabwe nje kwa kupitia South Africa na kanihakikishia kwamba ni lazima deal lipitie Suoth laa sivyo hakiuziki kitu.
ZNI ujinga mkubwa kuamni kwamba Wazimbabwe hawawezi hata kulima mahindi wakati ni hao hao Wazimbabwe waliokuwa wakilima Mahindi kwa mzungu.. Hakuna mzungu aliyeingia shambani kuzalisha mahindi peke yake wote hao walikuwa na wafanyakazi Wazimbabwe..
Kisha kuhusu habari ya kuwekeshga Cuba nakuomba soma vizuri habari nzima usichague kipande cha NIKE... na lauikama ingekuwa rahisi kama unavyozungumza basi Tungeona maduka kama hayo Tanzania ambako kila kitu ni ruksa isipokuwa tunaona mitumba na vitu fake..
Mugabe ni kiongozi mbaya sana lakini hadi sasa hivi hamjatoa suluhisho zaidi ya kulaumu tuuuu. nimeomba maoni yenu toka jana nachokiona ni kuzunguka mbuytu hakuna mwenye jibu zaidi ya kulaumu...kitu ambacho hakuna anayekataa.. Huyo Morgan kajificha kwa wazungu, Ubalozi gani vile?...
ahsante Lakini Hapana Ahsante.
Unajuaje Mimi Ni Mlevi Kama Wewe Kunikaribisha Kilevi?
J/k
naomba Radhi Mkuu! Tafadhali Nisamehe Sana! It Was Just A Simple Gesture Of Appreciation! I Withdraw My Statement Ya Mwaliko Na Kukubali Kwamba Mimi Ni Mlevi As You Faithfully Branded Me.
Peace
..kiongozi yeyote yule wa dunia ya tatu akiwekewa VIKWAZO na wakubwa na akajaribu kuendesha UCHUMI kivyake-vyake matokeo yake ni hayo tunayoyaona Zimbabwe.
Mugabe alifanya nini cha "kuendesha UCHUMI kivyake-vyake" mpaka akawekewa vikwazo?
Na alianza lini?
Mimi nawapa changamoto wale wote mnaobisha kuwa Waafrika Ndivyo Tulivyo kunionyesha mifano ya Sivyo Tulivyo na nitatoa ya kwangu ya Ndivyo Tulivyo ili kulinganisha lipi ni zaidi. Nawahakikishia mkinionyesha mifano kumi ya Sivyo Tulivyo mimi nitawaonyesha mifano 10,000 ya Ndivyo Tulivyo. Haya kazi kwenu......let's go for it.