Western Propaganda Turns Mugabe into a Tyrant

Western Propaganda Turns Mugabe into a Tyrant

Fundi Mchundo said:
Shukurani kwa maelezo yako ya historia ya mauaji ya wandebele. Kuna mtizamo tofauti kidogo na hayo uliyoyasema. Silaha kweli zilipatikana katika mashamba ya wakina Nkomo. Kinachobishiwa ni nani aliziweka humo! Inasemekana Mugabe alifanya hivyo ili apate sababu ya kuwashughulikia wandebele.

Fundi,

..nitachimba zaidi suala hili na kuona kama kuna vielelezo vinavyotetea mtizamo wako.

..lakini sioni faida ambayo Mugabe angeipata kwa kuwashughulikia Wandebele kikatili namna ile.

..zaidi wakati ule Mugabe alikuwa anahubiri injili ya reconciliation kwa msingi huo nalazimika kuamini kwamba alitaka Wandebele wawe under his inclusive umbrella.

..kwamba kulitokea maasi MatebeleLand hilo halina ubishi. kwamba kulihitajika nguvu za kijeshi kuzima maasi hayo hilo pia halina ubishi.

..labda tunaweza ku-speculate kwamba ZANU wali-plant zile silaha ili kuwa-discredit Nkomo na wenzake. labda pia walifanya hivyo kuipa uhalali zaidi operation ya 5th brigade. lakini uasi ulikuwepo, na ZANU walikuwa na mashaka kwamba unaweza kugeuka kuwa kama RENAMO ya Msumbiji.
 
Fundi,

..nitachimba zaidi suala hili na kuona kama kuna vielelezo vinavyotetea mtizamo wako.

..lakini sioni faida ambayo Mugabe angeipata kwa kuwashughulikia Wandebele kikatili namna ile.

..zaidi wakati ule Mugabe alikuwa anahubiri injili ya reconciliation kwa msingi huo nalazimika kuamini kwamba alitaka Wandebele wawe under his inclusive umbrella.

..kwamba kulitokea maasi MatebeleLand hilo halina ubishi. kwamba kulihitajika nguvu za kijeshi kuzima maasi hayo hilo pia halina ubishi.

..labda tunaweza ku-speculate kwamba ZANU wali-plant zile silaha ili kuwa-discredit Nkomo na wenzake. labda pia walifanya hivyo kuipa uhalali zaidi operation ya 5th brigade. lakini uasi ulikuwepo, na ZANU walikuwa na mashaka kwamba unaweza kugeuka kuwa kama RENAMO ya Msumbiji.

Faida ni moja. Toka alipowashughulikia kikamilifu wandebele hawaja'recover' mpaka leo! Ukitaka kumtisha kikamilifu adui yako ni kumuonyesha kuwa uko tayari kufanya hata kile kisichokubalika kibinadamu! Ndiyo mantra ya wakina Pablo Escobar. Na ni effective, kama tulivyoona kwa Joshua Nkomo. Soma quotation ya mag3.
 
Fundi Mchundo,

..kipindi hicho Mugabe alikuwa akihubiri injili ya reconciliation. he was trying to be a uniter. he was commited to build a country inclusive of all the enthnicities[white,shona,ndebele,..]

..bench mark kipindi kile ilikuwa ni Mozambique. Yale maneno ya Nyerere kwa Mugabe kwamba "you have inherited the jewel of Africa...." yalikuwa ni maelekezo kwamba usijesambaratisha kiuchumi Zimbabwe kama Samora alivyofanya kwa Msumbiji.

..lengo lilikuwa ni kuhakikisha kwamba kuna stability Zimbabwe ili wazungu wasiondoe vitega uchumi vyao. ndiyo maana 5th brigade wakatumwa haraka, bahati mbaya wakatumia nguvu kubwa kupita kiasi.

..Joshua Nkomo was never a political threat to Mugabe. sababu kubwa ni kwamba kabila la Nkomo ni minority. Mugabe alikataa kuunganisha vyama na Nkomo kwasababu alikuwa na uhakika wa kushinda kutegemea kura za Washona. Which he did.

..threat ilikuwa ni UASI ambao kama usingeshughulikiwa Zimbabwe ingefuata mkondo wa Msumbiji.

..tena unapoangalia matendo ya Mugabe wakati ule ongezea suala la ukombozi wa Afrika Kusini pia. kuna school of thought inayodai kwamba Mugabe angetaifisha ardhi na vitega uchumi wakati ule basi Makaburu wangepata message kwamba wakiachia ngazi basi wata-loose kila kitu. kwa msingi huo basi wahanga wa ukombozi wa SA walimsihi Mugabe asitaifishe ardhi na vitega uchumi na ku-maintain peace and stability.
 
La kujiuliza ni kuwa ni nani alikuwa likely kuasi.

Pengine inabidi tuanze mbali kidogo. Kumbuka amaNdebele kihistoria walikuwa wapiganaji. Hawa chini ya Mzilikazi (aliyekuwa jenerali wa Shaka) walivamia eneo la maShona na kulipokonya na kulifanya lao! Baadae wakiongozwa na lobengula, mtoto wa Mzilikazi, walipambana na mtu mweupe alipoingia Rhodesia kwa mara ya kwanza. Ingawa walishindwa kutokana na watu weupe kuwa na silaha nzito hasa bunduki ya maxim, kiongozi wao hakuweza kukamatwa na hadi leo haijulikani kaburi lake liko wapi. Hivyo kuanzia mwanzo hawa wa amaNdebele walijiona bora kuliko maShona.

Katika vita vya ukombozi wa Zimbabwe, vile vile, vyama vya siasa viligawanyika kwa misingi hiyo hiyo. ZANU ya wakina Mugabe ilikuwa inaonekana ya mashona na ZAPU ya amaNdebele.

Vita ya ukombozi majeshi ya vyama hivi yalitakiwa kuunganishwa kuunda jeshi la Zimbabwe mpya. Hii ilikuwa ngumu maana tayari majeshi haya ya Zipra (ZAPU) na Zanla(ZANU) yaliishapambana mara kadhaa. Wanajeshi wa Zipra hawakuuamini uongozi wa jeshi la Zimbabwe maana walihisi wanawapendelea wenzao wa Zanla (maShona).

Mwaka 1982, zikapatikana silaha katika mashamba ya wanachama wa ZAPU. ZANU ikadai kuwa hizo zilikuwa ni ishara kuwa ZAPU wanakusudui kufanya mapinduzi. Wale ambao silaha zilipatikana mashambani mwao, wakina Dabengwa, Lookout Masuku na wanne wengine wakashitakiwa mahakamani. Kesi ikatupwa nje baada ya serikali kushindwa kuthibitisha madai yao. Hata hivyo Dabengwa na Masuku waliendelea kusota jela kwa zaidi ya miaka minne. Kitendo hiki kikawafanya wapiganaji waliokuwa wa Zipra kuamini kabisa kuwa kuna vendetta dhidi yao, maana hawa walikuwa viongozi wao. Wakaanza kulikimbia jeshi la Zimbabwe.

Mugabe akaomba msaada wa kijeshi kutoka Korea ya kaskazini. Hawa wakafundisha kikosi cha 5th brigade ambayo iliondolewa nje ya mamlaka ya jeshi na kuwekwa moja kwa moja chini ya uongozi wa waziri mkuu Mugabe. Hawa ndio kama ulivyosema ndio waliotekeleza operesheni Gukurahundi ambamo maelfu ya amaNdebele waliuawa kikatili. Mara nyingi walikuwa'executed' wake kwa waume baada ya kulazimishwa kuchimba makaburi yao. Waziri Mkuu Mugabe alipoulizwa akadai kuwa maneno hayo ni propaganda za nchi za magharibi. Baada ya kuona ukatili huo, Joshua Nkomo akaamua kuwanusuru watu wake kwa kupatanishwa na Mugabe. Tokea hapo hatujasikia fyoko kutoka kwa amaNdebele.

Sasa, Mkuu, ukiangalia events zenyewe ni wazi kuwa Mugabe aliishapania kuwashikisha adabu amaNdebele. Ule mwimbo wa reconciliation alikuwa akiutumia kuwazuga watu wengine lakini nia yake ilikuwa ni kuwamaliza wote ambao aliona wana'potential' ya kuja kumpinga. Hivyo hivyo alivyowafanyia wakina Ndabaningi Sithole na wengine. Huyu bwana si wa kumchezea hata kidogo. Msidanganyike na yeye kushika biblia. Ni mtu mwovu sana. Naamini hata huko the Hague hastahili kwenda. Atashughulikiwa nawatu wake kama alivyofanyiwa Samuel Doe. Iko siku wazimbabwe watapumua tena. Unfortunately, si kwa msaada wetu.

Amandla......!
 
..tena unapoangalia matendo ya Mugabe wakati ule ongezea suala la ukombozi wa Afrika Kusini pia. kuna school of thought inayodai kwamba Mugabe angetaifisha ardhi na vitega uchumi wakati ule basi Makaburu wangepata message kwamba wakiachia ngazi basi wata-loose kila kitu. kwa msingi huo basi wahanga wa ukombozi wa SA walimsihi Mugabe asitaifishe ardhi na vitega uchumi na ku-maintain peace and stability.

Hii nadhani ndiyo sababu thabo anapata kigugumizi linapokuja suala la Zimbabwe!
 
Fundi na JK, unajua ndo maana wengine hapa tumesisitiza kwamba utawala wa waafrika especially viongozi wetu waliopigania uhuru huwezi kuwatenga na western powers. Kwa sababu wengi walitaka protection. Na kama ukiangalia kipindi kile cha uhuru kulikuwa hakuna kuaminiana na kiongozi yeyote salama yake ilibidi awe na fall back. Leo Mugabe kutwambia kwamba wazungu ni wabaya kuliko chochote, historia inamuhukumu, Mugabe na wazungu wamegeukana kwa sababu wote wamefikia point no body is serving the other. Sema Mugabe ameamua kuwa katili dhidi ya watu wake. ALL IN ALL, DUNIA IMEBADILIKA SANA, MUGABE HAWEZI KUSHINDA HII VITA. IS FIGHTING A LOSING BATTLE.

Ni kama sisi, generation ijayo, sijui tutaidanganya vipi wakija wakasoma mikataba kama hii tunayosaini kuuza nchi na bado tunabaki maskini 9I HOPE ITAFIKA KIPINDI HII MIKATABA ITAKUWA DECLASSIFIED!). Fundi unavyoichambua historia na sisi tutachambuliwa hivyo hivyo. Tofauti ni kwamba tunafanya wenyewe kwa utashi ila kwa maslahi ya wachache na ya mda mfupi.

I dare say, utawala wa mweusi haujamnufaisha mweusi wa bara letu, zaidi ya vibaraka wachache. Ni jambo la kusikitisha kwamba hatujifunzi kutokana na historia wala makosa yetu. I believe hata kama siyo generation yetu, iko siku bara la Africa litapata ukombozi wa kweli. SADLY, WENGI WETU WONT LIVE LONG ENOUGH TO SEE THAT DAY.
 
Fundi Mchundo,

..maelezo yako ni mazuri lakini umeacha facts muhimu na hivyo kuteleza ktk conclusion yako.

..kulikuwa na matatizo ya uhasama kati ya ZANLA na ZIPRA. nadhani matatizo hayo yanatokana na kutoaminiana kwa viongozi wao wa kisiasa.

..zoezi la kuanzisha jeshi jipya lilikuwa likiongozwa na Wataalamu toka Uingereza. kama kulikuwa na matatizo na manunguniko basi wahusika wakuu wanapaswa kuwa Waingereza.

..kuna matukio ambayo yalitokea kati ya 1980 na mwishoni mwa 1981 ambayo yananilazimisha kuamini kwamba kulikuwa na SECURITY CONCERNS zilizopekea deployment ya 5th Brigade ktk maeneo ya Matabeleland.

..matukio yenyewe kwa uchache ni haya hapa:-

..mapigano at least mara 3 kati ya ZANLA na ZIPRA katika re-deployement centers.

..hujuma ya Afrika Kusini iliyosababisha hasara ya USD 50 million dhidi ya jeshi la Zimbabwe.

..mashambulizi ya makaburu kwenye makao makuu ya ZANU na kusabisha vifo na uharibifu wa mali.

..jaribio la mauaji dhidi ya Robert Mugabe ambapo wahusika walikuwa ni ZIPRA.

..mashambulizi ya makaburu kwenye kambi ya jeshi la anga -- ndege na vifaa viliharibiwa.

..defections za askari wa ZIPRA jeshini na kuongezeka kwa vitendo vya kigaidi.

..kugundulika kwa silaha ktk mashamba ya viongozi wa ZAPU/ZIPRA.

..kwa msingi huo mimi naona tatizo la msingi hapa lilikuwa SECURITY na STABILITY siyo siasa/kukomeshana/kushikishana adabu/kumalizana kisiasa kama ulivyolileta.

NB:

..hivi kwanini unafikiri Mugabe anastahili kupelekwa the Hague? kwanini asishughulikiwe na mahakama za ndani za Zimbabwe?

..mbona lile kundi la Mengistu Haile Mariam limeshtakiwa na mahakama za Ethiopia?

..umeshachunguza na ku-conclude kwamba Watanzania tuko clean ktk hii sakata ya Gukurahundi? hujasikia tetesi na minong'ono kwamba tulitia mguu kule?
 
Interesting Obserever na Kuhani Mkuu,

Jamani sijarudi kusoma maandishi yangu ya nyuma lakini nakumbuka nilichoandika.
Nilichoandika mimi ni ktk kuwaeleza kilichotokea huko Zimbabwe na sio maoni yangu mimi. Bulawayo ama niseme Matabeleland ni sehemu ambayo wazungu walizaa sana na wazalendo hivyo kuwepo kwa mashombe (point five) wengi sio maoni yangu mimi kuhusiana na ushirikiano kati ya wazalendo na wazungu..Na kama sikosei naweza sema ndio ardhi yenye rutba zaidi ktk kilimo kuliko Zimbabwe ya mashariki. Hizi ni facts ambazo hazihusiani na mawazo yangu mimi ama hoja zetu.
Sasa nikirudi kwa Mugabe, nilichosema mimi Mugabe alikuwa upande wa ZANU hao Washona na yeye kama Mshona walikuwa na lengo la kuikomboa Zimbabwe kwa vita tofauti na Nkomo ambaye alitaka zaidi kupitia njia za haki, Hii ni historia ya karibu zaidi na Uhuru wa Zimbabwe.
Hivyo hata baada ya kupata Uhuru, Mugabe kama Mshona aliwaua Wandebele sana tu kwa sababu ambazo mimi siwezi kuzifahamu iwe kisiasa, kikabila au uhusiano wa Wandebele na wazungu... Hilo sipo kabisa!..nachoweza kusema ni kwamba Mugabe alikuwa hasid toka zamani bila ushirika wa mzungu. Na nikasema kuwa mbona alipokuwa akiwaua Wandebele sikusikia kelele za wazungu isipokuwa leo hii imekuwa deal kutupotosha sisi kuwa ARDHI iliyochukuliwa toka kwa wazungu ndio sababu hasa ya kelele hizi za leo..Mzungu hata siku moja haendi citani ama kupiga kelele kama hakupigwa yeye ama maslahi yake kuchukuliwa... never hata siku moja mzungu hana huruma na ngozi ya tako, na kusema kwangu hivyo haipotoshi ukweli kwamba Mugabe ni mtu mbaya hata kidogo... main issue ya mada hii ni kuhusika kwa wazungu!.. tunaposema tusiwalaumu wazungu kwa makosa yetu then pia tukubali kwamba wazungu nao wasiingilie mambo yetu..wanapoingilia iwe hata kuamua ugonvi tunawatazama wanamvuta nani shati huku wanaacha mwanya jamaa apenyeze ngumi. Unajua tena ngumi za mtaani, ukiamua ugonvi watu hutazama uko upande gani!... na unaweza kubeba mzigo wote wa ugonvi huo ukawa wewe unapigwa na watazamaji!
Na wala haiwezi kumpa kura zangu Mugabe kwa mauaji yale ya Wandebele hata kama wangekuwa ni wazungu kwani tayari Uhuru ulikwisha patikana. Hakuna mahala namsifia Mugabe kwa matendo yale hata kidogo na nadhani pengine uandishi wangu ndio tatizo lenu kubwa kiasi kwamba nashindwa kutenganisha matukio na wakati kutokana na nafasi ndigo..
Na kama sikosei nia yangu kubwa ilikuwa kuonyesha kwamba Mugabe hakuwa na ushirikiano na wazungu toka zamani na wala ktk utawala wake hakuwahi kuwa na Muingereza zaidi ya kutegemea kile alichoahidiwa ktk makubaliano ya kuijenga Zimbabwe mpya yenye kuwapenda wazimbabwe wote kwa rangi na makabila yao. Lakini nina hakika Muingereza alijua kabisa Mugabe sio mtu wa kuaminika ni MJAMAA na alikuwa na influence kubwa na Urusi na Cuba zaidi ya nchi za magharibi hivyo sioni ukweli kuwa Muingereza alimbeba Mugabe wakati fulani..
Pia nashindwa kuelewa mnaposema Muingereza alijenga jeshi lao wakati naelewa wazi kuwa Mtawala alikuwa Muingereza!..
Interesting Obserever,
Kuungana kwa Mugabe na Nkono kulikuwa hoja kubwa sana baada ya Uhuru ili kuleta suluhu ndani ya vyama hivi ambayo mimi binafsi siku zote naipinga kwa sababu haitazami wananchi. Kuungana kwa vyama hakuwezi kuwa muhimu ikiwa madaraja ya kikabila bado hayajatafutiwa suluhu kikatiba.. Mkuu utashangaa kuwa hata wakati huo sikumpenda NKONO hata kidogo. Kama unakumbuka siku zote naamini kabisa huwezi ku shake hands na Devil na ndicho alichofanya Nkono.. Mpaka kesho maisha ya wandebele hayakubadilika na hapakuwepo na maendeleo kwa watu wake zaidi ya kuendelea kukandamizwa kama zamani kabla ya muafaka... Ni hatua aliyoichukua Raila na toka hapo nimekosa imani naye! ikiwa mtu umechaguliwa na wananchi leo kuja kubali muafaka ambao unakupa wewe nafasi ndani ya serikali lakini hauwezi kubadilisha maisha ya wananchi waliokuchagua. Kwangu mtu huyu ni MNafiki mpenda madaraka au sifa..
Ndivyo anavyotaka kufanya Morgan sasa hivi na haitawezekana kwa sababu Mugabe ni mjanja kuliko wanavyofikiria. Na hata kama atakubali ku share uongozi basi dunia nzima tutaonekana sisi ni vibaraka vile vile kwa sababu Mugabe ni shetani lazima aondoke lakini hawezi kuwa replaced na shetani mwingine ama ku share madaraka mashetani wawili.. Hili ndilo somo langu kubwa ktk kijiwe hiki..
 
mashambulizi ya makaburu kwenye makao makuu ya ZANU na kusabisha vifo na uharibifu wa mali.

..jaribio la mauaji dhidi ya Robert Mugabe ambapo wahusika walikuwa ni ZIPRA.

..mashambulizi ya makaburu kwenye kambi ya jeshi la anga -- ndege na vifaa viliharibiwa.

..defections za askari wa ZIPRA jeshini na kuongezeka kwa vitendo vya kigaidi.

..kugundulika kwa silaha ktk mashamba ya viongozi wa ZAPU/ZIPRA

JokaKuu! Mbona mengi ya haya nimeyazungumzia? Mshambulizi ya makuburu kwenye makao makuu ya ZANU sina taarifa nayo. Lakini hata hivyo ukiangalia mtiririko wa habari yako ni kuonyesha kuwa muovu alikuwa ZIPRA tu wakati ZANLA nao walihusika katika mauaji ya amaNdebele huko Mutoko, Mount Darwin na Gutu.

Kuhusu jaribio la mauaji dhidi ya Mugabe. Utaona kila huyu bwana akibanwa alikuwa anasingizia kuwa kuna watu wanajaribu kumuua hivyo kumpa carte blanche dhidi ya wapinzani wake. Alitumia kisingizio cha hofu ya coup mwaka 1982 kuwashitaki Lookout Masuku ( huyu alikuwa commander wa ZIPRA na baada ya uhuru akawa deputy commander wa Zimbabwe National Army), Dumiso Dabengwa ( alikuwa Chief of intelligence wa ZIPRA). Kama nilivyosema awali aliendelea kuwashikilia hata baada ya mahakama kuwaachia! Sasa, Mkuu, utawalaumu wale maaskari wa chini kutoka ZIPRA kuamini kuwa kuna witch hunt dhidi yao? Ndiyo maana wakaamua kujitoa. Kumbuka hata mwaka 1997 alidai kuwa Ndabaningi Sithole alikuwa anataka kumuua. Charge kama hizi hizo tena amewahi kuzielekeza kwa Morgan. Si mtu wa kumwamini.

Pamoja na kukana kwake kuhusika katika yaliyofanywa na 5th brigade, Enos Nkala aliyekuwa waziri wa ulinzi wakati ule alishasema kuwa Mugabe ndiye aliyeyaamrisha. Ukiangalia tena kuwa binamu yake Perence Shiri ndiye aliyekuwa mkuu wa 5th brigade na leo ndiye kamanda wa Air Force! Atamzawadiaje mhusika mkuu kama hakuwa anatekeleza amri zake.

Wakati wa utawala wa makaburu, Zimbabwe kama Frontline state walikuwa target halali. Mbona hata sisi yalitukuta? Kwa nini basi aanze kuwashughulikia watu wake kutokana na vitendo vya adui yake?

Ukitaka kujua jinsi alivyo vindictive angalia hatma ya Edgar Tekere aliyempinga sana kutokana na masuala ya rushwa! Angalia jinsi alivyonyang'anya mashamba ya Chikerema na Sithole!

Huyu si mtu wa kutetewa. Ni muovu.

Kama yatatokea mabadiliko ya serikali, nadhani itakuwa nafuu kwake kama atapelekwa the Hague au kwingineko! Wazimbabwe watamfanyia vibaya sana. Yeye na wakina Shiri.

Kabla ya watu kunipa ujiko usio haki yangu, yote haya nimeyatoa mtandaoni. Ni public knowledge.

Amandla......
 
Ningependa kuwaambia wale wote ambao hawajui Mugabe alivyowatumia hao hao wazungu kuimarisha serikali yale baada ya uchaguzi wa mwaka 1980, watafakari hii habari.

The British Governor declared his intention to endorse the result of the election (with the final results due to be declared on 4 March 1980) and a date was set for the independence of the country as Zimbabwe. The situation was now delicately poised, with some whites planning a military coup (Operation Quartz) to prevent Robert Mugabe from taking power. At this point, Smith's son Alec (newly returned from political exile) approached Smith while Joram Kucherera (a senior civil servant) approached Mugabe in order to arrange a meeting to discuss the future of the country. On the night of 3 March 1980 Smith was driven to Mugabe's house by Kucherera. Smith and Mugabe spoke privately for two hours and immediately afterwards Smith met with other senior ZANU figures. The meetings were surprisingly cordial. Mugabe offered key Ministries in the new government to RF MPs and agreed to allow senior officials (such as Lieutenant-General Peter Walls, head of the army) to remain in post. As far as is known, no minutes of the Smith-Mugabe meeting were kept. Both parties have been guarded about what was said and agreed that night.
On 4 March Smith advised the white community to accept the verdict of the election and respond "pragmatically" to events. Specifically, he told the white community to stay in the country and co-operate with the incoming ZANU-PF government. Operation Quartz, scheduled for 4 March, was abruptly called off.
A few weeks later, the co-operation agreement resulted in the Rhodesian army (with white officers) acting to maintain government control of Bulawayo in the face of an attack by ZIPRA dissidents.
Later in 1980, Smith was a member of a delegation making presentations in Europe to international financial institutions regarding investment opportunities in Zimbabwe. The former Rhodesian security forces acted throughout 1980 and 1981 to maintain stability in the country.



RF kilikuwa ni chama cha wazungu watupu wakiongozwa na Ian Smith na ZIPRA kilikuwa kikosi cha wapiganaji chini ya chama cha ZAPU kilichoongozwa na Nkomo. Hii inatupa picha ya halisi ya Mugabe na alivyo tayari kufanya lolote kubakia madarakani.
 
Mkandara!
Hauwezi kulinganisha maovu ya Mugabe na ya Morgan. Mpaka sasa inaelekea mnaogopa kuwa Morgan atakuwa kibaraka. Mikono ya Morgan haina damu za wazimbabwe kama ilivyo kwa Mugabe. Pili kwa mtu kama yeye (kama ilivyokuwa kwa Chiluba) wazimbabwe hawatasita kumtema kama atabolonga!
 
Madai kuwa Mugabe kaitoa ARDHI YAO KUTOKA MIKONONI MWA WAZUNGU NA KUWAPA WATU WAKE WA SERIKALINI.
Na ARDHI YETU PAMOJA NA UHURU WETU VIKO mikononi mwa NANI?
 
Fundi Mchundo,

..habari zote zipo kwenye public domain. unapaswa kuangalia zinatokea wapi.

..kuna ripoti ilitolewa na baraza la maaskofu wakatoliki is a very good source.

..naona tunapata the same information tanatofautiana kwenye conclusion.


mag3,

..hakuna jambo lolote la ajabu kuhusu Mugabe kukutana na Ian Smith kabla ya kutangazwa matokeo ya uchaguzi.

..Mugabe na Smith walishakutana kwa muda mrefu wakati wa mazungumzo ya Lancaster.

..kulikuwa na ulazima wa kuwashirikisha Walowezi ktk vyombo vya ulinzi na usalama ili kuwahakikishia wenzao kwamba hakutakuwa na kulipiza kisasi kwa namna yoyote ile.

..pia iliamuliwa iwe hivyo ili kuzuia jaribio lolote lile la South Africans to go for an all out war against Zimbabwe.

..kuna habari kwamba Walowezi walitaka kumuua Mugabe wakati akielekea Rufaro kwenye sherehe za uhuru. kilichomuokoa ni kuwepo kwa Prince Charles ktk msafara wa magari yaliyokua yakielekea uwanjani.

..habari uliyotuletea haithibitishi uchu wa madaraka wa Mugabe, badala yake unaonyesha umahiri wa INTELLIGENCE ya Mugabe wakati ule. tena nina hakika kwamba yote hayo yalikuwa na baraka za wazee kama Nyerere,Kaunda,Seretse Khama, na Samora Machel.

NB:

..hata Afrika Kusini, Mandela alim-retain Mkuu wa Majeshi ya Makaburu. Pia Benki Kuu iliendelea kuwa chini ya gavana Kaburu. maeneo mengi nyeti yaliendelea kuongozwa na makaburu.

..Mugabe na Mandela walijifunza kutokana na makosa aliyofanya Samora Machel ambaye alitimua Wareno wote matokeo yake nchi ikawa haina wataalamu, na zaidi waka-sponser kikundi cha magaidi.
 
Hawa viongozi wengi Waafrica waliokuwa mbele wakati wa uhuru wengi wao ni worse kuliko hao wakoloni,Mugabe amerudisha Zimbabwe nyuma miaka 100 kuanzia kiuchumi mpaka demokrasi yao,maana hii itakuwa pattern nyingine...kilichobaki ni cronies wake na familia yake kujipanga nani achukue baada ya Mugabe,lazima ZANU ife ili Zimbabwe iende mbele la sivyo wamejichimbia kaburi.
 
Hawa viongozi wengi Waafrica waliokuwa mbele wakati wa uhuru wengi wao ni worse kuliko hao wakoloni,Mugabe amerudisha Zimbabwe nyuma miaka 100 kuanzia kiuchumi mpaka demokrasi yao,maana hii itakuwa pattern nyingine...kilichobaki ni cronies wake na familia yake kujipanga nani achukue baada ya Mugabe,lazima ZANU ife ili Zimbabwe iende mbele la sivyo wamejichimbia kaburi.

Is there any difference to CCM and Tanzania?!!
 
(I am not sure if the guy told the story in full, atleast he tried, though not convinced with title and content)

That Robert Mugabe's regime has brought Zimbabwe to its knees is unquestionable, but the responsibility for creating that regime lies uncomfortably closer to home. Michael Holman, a journalist who grew up in the town of Gwelo in Zimbabwe, explains.

Missing from the acres of newsprint devoted to coverage of Zimbabwe's deepening crisis, absent from the radio and television coverage, is an unpalatable fact: Robert Mugabe is a creature shaped by British colonial rule. And a century after white settlers established the racially skewed land ownership that remains at the heart of the country's turbulent politics, colonial chickens are coming home to roost.

It was British settlers who, in the 1890s, occupied the country soon to be called Southern Rhodesia; nearly a hundred years later, London played midwife to the birth of Zimbabwe, hosting the Lancaster House constitutional conference. With an almost audible sigh of relief, Britain welcomed an independent Zimbabwe.
But its responsibility lives on. Between the arrival of settlers and the handover to Mugabe in 1980, the UK record was a shoddy one.

Three decisions stand out:

* At the break-up in 1963 of the Central African Federation of Southern and Northern Rhodesia (Zimbabwe and Zambia) and Nyasaland (Malawi) in 1963, it was Britain that allocated the bulk of the Federal army to white-ruled Rhodesia. This gave the minority regime of Ian Smith the muscle to make a unilateral declaration of independence two years later, in 1965, and to wage war against black nationalist guerrillas.
*

It was Britain that effectively vetoed landlocked Zambia's request in the early 1960s for World Bank funds to build a railway that would link it to the east African port of Dar es Salaam. The decision forced continued dependence on trade routes through apartheid South Africa – and rebel Rhodesia.

*And it was Britain that reneged on the spirit, if not the letter, of a provision in the Lancaster House settlement intended to tackle the worst feature in the legacy of white rule - half the land was owned by whites. The UK contributed (in real terms) to the buyout of 5,000 white farmers in Zimbabwe just half the amount it had provided for a similar exercise in Kenya in the early 1960s – although its former East African colony had barely a thousand white farmers.

More at; Robert Mugabe: a beast created by colonial Britain?
 
Mag3,
Unachoshindwa kuelewa ama umeacha kuelezea ni jinsi gani Zimbabwe walifikia Muafaka wa kuacha vita kupigana wao kwa wao kama ilivyokuwa South Afrca. Sasa kama kweli mtu atakuja hapa na ku quote mikutano kati ya Mandela na Botha itaonekana wazi kuwa kulikuwepo na uhusiano kati ya vyama hivi..
Yote uliyoelezea yanatokana na Muafaka uliopitishwa kwamba chama kitakachoshinda uchaguzi kitachukua nchi... Sawa na ilivyotokea Tanzania, Zanzibar na nchi nyingine zote zilipopata uhuru wao kutoka kwa mkoloni na wote walizungumza na wakoloni dhidi ya pingamizi zilizokuwepo.. Ni nchi chache sana zilizoweza kumfukuza mkoloni kama Kenya na Msumbiji.. Mkuu kwa taarifa yako hadi leo hii chama cha kina Smith kipo lakini haina maana kuna uhusiano kati ya vyama hivi. Hata Israel hufanya mikutano na Wapalestina haina maana kuna mmoja wao kasalimu amri ama kuna uhusiano...
 
Mag3,
Unachoshindwa kuelewa ama umeacha kuelezea ni jinsi gani Zimbabwe walifikia Muafaka wa kuacha vita kupigana wao kwa wao kama ilivyokuwa South Afrca. Sasa kama kweli mtu atakuja hapa na ku quote mikutano kati ya Mandela na Botha itaonekana wazi kuwa kulikuwepo na uhusiano kati ya vyama hivi..
Yote uliyoelezea yanatokana na Muafaka uliopitishwa kwamba chama kitakachoshinda uchaguzi kitachukua nchi... Sawa na ilivyotokea Tanzania, Zanzibar na nchi nyingine zote zilipopata uhuru wao kutoka kwa mkoloni na wote walizungumza na wakoloni dhidi ya pingamizi zilizokuwepo.. Ni nchi chache sana zilizoweza kumfukuza mkoloni kama Kenya na Msumbiji.. Mkuu kwa taarifa yako hadi leo hii chama cha kina Smith kipo lakini haina maana kuna uhusiano kati ya vyama hivi. Hata Israel hufanya mikutano na Wapalestina haina maana kuna mmoja wao kasalimu amri ama kuna uhusiano...

Mkandara,

Mazungumzo kati ya Smith na Mugabe yalikuwa ya convenience "scratch my back and I will scratch yours". Matokeo yake viti 20 vilikuwa reserved kwa Wazungu in exchange of (a) operation yao ya mapinduzi isitishwe na (b) kwa pamoja waweze kupambana na ZIPRA. Kumbuka hadi wakati huo wazungu wangeweza kumvumilia Mugabe na ZANU lakini si Nkomo na ziko sababu ukizitafuta. Alikuwa wapi Mugabe wakati Nkomo na mwanasheria wake Chitepo walipokuwa wakiongoza mapambano kwenye miaka ya 1950s.

Hata hivyo tuache historia, matendo ya Mugabe kwa Wazimbabwe na ile kauli yake kwamba ni Mungu tu anayeweza kumwondoa madarakani inamtofautisha vipi na Idi Amin na wengineo. Je unajua idadi kamili ya wana Zimbabwe ambao wameikimbia nchi yao kwa sababu ya Mugabe. Je, hawa wote ni vibaraka wa wazungu. Mtu yeyote mwenye akili timamu anaye"endorse" matendo ya Mugabe kwa sababu zozote zile, haitakii mema nchi hiyo. Lakini kwa kuwa wengi humu ndani ni Watanzania, sioni ajabu. Vivyo hivyo na CCM haiondoki mpaka kwa amri ya Mungu. Watanzania (waafrika) ndivyo tulivyo.
 
mag3,

..sina uhakika, lakini nadhani hivyo viti 20 reserved kwa Wazungu vilitokana na mkataba wa Lancaster.

..kulikuwa na matatizo katika kuunganisha majeshi ya Zanu na yale ya Zapu. kulikuwa na uhasama wa muda mrefu na waliwahi kupigana hata hapa kwetu Tanzania.

..matatizo ktk kuunganisha Zanla na Zipra ndiyo yaliyopelekea Zimbabwe kutumia baadhi ya maofisa wa jeshi la Smith.

..kulikuwa na hasara na faida za kuwatumia maofisa wa jeshi la Walowezi. kuna habari kwamba maofisa upelelezi wakilowezi walikuwa wakihujumu serikali huru ya Zimbabwe.

..sifahamu Mugabe exactly Mugabe alikuwa wapi wakati Chitepo na Nkomo wameanzisha chama cha ukombozi. ninachoelewa ni kwamba Mugabe was # 3 by the time Chitepo anauawa.

..Mugabe assumed leadership after that bcuz the # 2 person died in Smith's detention.
 
That's why I love western, when the time aproaching they are always unable to hide their true colour.

After the AU meeting, French Foreign Minister Bernard Kouchner, whose country holds the European Union's rotating presidency, said the EU "will not accept a government other than one led by Mr Tsvangirai".

Source: http://news.bbc.co.uk/2/hi/africa/7485412.stm
 
Back
Top Bottom