Wenyeviti wa mitaa kutolipwa mishahara ndio chanzo cha Rushwa katika kutoa Huduma, na pia kukosa ofisi ya kufanyia kazi

Bushmamy

JF-Expert Member
Aug 18, 2019
8,848
15,252
Wenyeviti wa serikali za mitaa, wamekuwa wakiweka mazingira ya Rushwa katika utendaji wao kwa madai kuwa wanafanya kazi ya bure na hakuna malipo yoyote wanayopata kutoka serikalini.

Hali hii ni tofauti kutokana na kuwa kuna baadhi ya halmashauri wenyeviti wa mitaa wanalipwa na Halmashauri nyingine viongozi hao wakiwa hawapati chochote kitu toka serikalini.

Hii imepelekea huduma muhimu za kijamii kutoka kwa viongozi hao kuwa katika mazingira ya Rushwa kwa madai kuwa bila chochote toka kwa Mwananchi katika kutoa huduma mfano wa muhuri au mashauri ni swala la kupoteza muda. Hili. Nalo limekuwa kero kwa wananchi.

Kwenye baadhi ya Halmashauri ambazo viongozi hao hawapati mishahara au posho yoyote wamekuwa wakifanyia shughuli za kuhudumia wananchi majumbani kwao kwa maelezo kuwa kupangisha ofisi ni gharama hivyo hawana pesa ya kodi.

Muda mwingi kuwa kwenye shughuli zao binafsi badala ya huduma kwa Wananchi kutokana na kuwa ndizo zinazowasaidia kujikimu kimaisha hii nayo imekuwa Kero kubwa kwa wananchi.
 
Kwa Tanzania mtu alipwe mshahara asilipwe rushwa ipo palepale maana ipo kwenye damu, wanaongoza kwa rushwa ni wale wanaolipwa mishahara mikubwa
 
Back
Top Bottom