Napendekeza wenyeviti wa mitaa, vijiji na vitongoji kulipwa mshahara

ichumu lya

JF-Expert Member
Aug 11, 2016
2,605
2,729
Kwa mujibu wa taarifa ya Tamisemi 2014 Tanzania bara ina jumla ya mitaa 3, 741
Vijiji 12, 423

Vitongoji 64, 616 ukijumlisha vyote unapata jumla 80, 780 idadi hii nisawa na wenyeviti wa mitaa, vijiji na vitongoji kama kutakuwepo na utashi wa kisiasa tukaamua wenyeviti awa kuwalipa mishahara Tsh, 200, 000/@ maana yake tutatumia Tsh, 16, 156, 000, 000/ ( Kumi na sita bilion milion mia moja hamsini na sita) kwa mwezi kwa mwaka Tsh, 193,872,000,000/ zikitengwa fedha hizi tutakuwa tumewaajili wenyeviti wa mitaa, vijiji na vitongoji maana yake bajeti ya Tamisemi itatakiwa kuongezeka kwa fedha hizo nje ya bajeti kuu.
Sasa mala nyingi uwa najiuliza ivi serikali kuu inajua umuhimu wa watu awa? Kwanini mbunge apate Tsh, 12, 000, 000 kwa mwezi na marupurupu kibao uku wawajibikaji wakiishia kupewa posho ya Tsh, 20, 000 kwa mwezi au kwa miezi mitatu?

Ni aibu kwa Taifa kuona watu wanao angaika na wananchi mchana kutwa kuhakikisha nchi inatawalika wanaonekana makarai wanakumbukwa kwenye chaguzi baada ya uchaguzi wanatelekezwa kama mjenzi na karai baada ya nyumba kuisha. Awa ndio ushinda wanakimbizana na uharifu mitaani, ndio uimiza wananchi kutunza mazingira, ndio usuluhisha migogoro midogo midogo, ndio upunguza kesi nyingi mahakamani ambapo kama kila kesi ingekuwa inapelekwa polis na mahakamani sijui kama pangetosha kwa uwingi wa kesi, awa ndio uhimiza wananchi kulipa kodi na shuru mbalimbali, awa ndio usuluhisha magomvi ya kifamilia yasiyo na sababu za kwenda kwenye majukwaa ya kisheria, awa ndio uhimiza watoto kupelekwa shule wasishinde mitaani nasema awa ndio wasimamizi wa sheria ndogo ndogo lakini pia awa ndio walinzi wa mali ya umma ikiwamo ardhi na miundombinu kibao.

Pamoja na umuhimu huu bado ndio watu wasio na thamani katika serikali na vyama vya siasa sio CCM wala CHADEMA wala ACT wala CUF wala NCCR wala chama chochote cha kijamii badala yake mzigo wa WENYEVITI awa umeangushwa kwa walipa kodi kila mtu ale kulingana na urefu wa kamba yake maana yake kila huduma wanayotoa kwa walipa kodi watozwe posho kulingana na maamuzi. Mimi Katikabakama na wananchi wote wa nchi hii tunapinga kwa nguvu zote uonevu si tu tunaofanyiwa kupitia Wenyeviti awa bali SERIKALI.

Inakuaje Serikali ishindwe kulipa Wenyeviti wetu ambao kwetu tunawaona kama watendaji wakuu katika maeneo yetu. Sisi wananchi tunatambua umuhimu wao ni wasaidizi wa serikali ivyo tunaona ni busara wakalipwa nankodi zetu wanazosimamia.

Kama CAG anatwambia upotevu wa fedha kwenya idara moja ya serikali kwamba Bilion 600, 000, 000, 000/zimepotea au hazijulikani matumizi yake kwanini tusiwalipe Wenyeviti wetu wa Mitaa, Vijiji na Vitongoji Tsh, 200B ili wafanye kazi kwa utulivu japo kidogo? Swali kwa TAMISEMI nani alipendekeza posho ya Tsh, 20, 000/ kwa kila mwezi? Je akipewa yeye ataifanyia nini?

Narudi kwa Wabunge nyote mnajua bila wenyeviti ninyi hamuwezi kufanya lolote ata diwani anamtegemea Mwenyekiti na wajumbe wake. Mnashindwa nini kuwatetea Wenyeviti awa mnapokuwa mnaishauri serikali?
Nimalize kwa kuishauri serikali, Vyama vya siasa na taasisi nyingine wakati tunapeleka mapendekezo ya mabadiliko ya Katiba ya nchi na mabadiliko ya sheria chonde chonde kumbuka Wenyeviti wetu awa tunataka watambuliwe rasmi kimaslahi na Katiba itamke kwamba wanastahili kulipwa vinginevyo hatuwatendei haki wenye nchi (walipakodi)

@Katikabakama.
View attachment 2707702
 
Umesikika mwenyekiti
Ila wanatakiwa wawe wameenda shule na wengi ni darasa la saba.
 
Sasa hio bajeti si Bora wawaongezee walimu na watendaji mishahara
 
Kuchukuwa form za utambulisho kutoka kwa serikali ya mtaa Ni sh 2000.

Ikifanyika biashara yeyote ndani ya ofisi ya mwenyekiti mtaa Ni 10%.

Bado Kuna Kodi za viduka pamoja na vibanda wanakusanya kila siku,
Taka Taka malipo 10000 kwa mwezi kwa kila kiduka na mwenye biashara ktk mtaa husika


Bado hawapati pesa?
 
Kuchukuwa form za utambulisho kutoka kwa serikali ya mtaa Ni sh 2000.

Ikifanyika biashara yeyote ndani ya ofisi ya mwenyekiti mtaa Ni 10%.

Bado Kuna Kodi za viduka pamoja na vibanda wanakusanya kila siku,
Taka Taka malipo 10000 kwa mwezi kwa kila kiduka na mwenye biashara ktk mtaa husika


Bado hawapati pesa?
Kwa huo mchanganuo utafanya sisi majobless mwaka kesho tushindane na wazee
 
Back
Top Bottom