Wenye mipango ya kuhama nchi tukutane hapa

Wenye mipango ya kuhama nchi tukutane hapa

Jamani Mimi katika maisha yangu nna ndoto kubwa mbili tuu nikitimiza Hizi asante mungu ndoto ya kwanza ni kuhama nchi natamani nikaishi SA,USA,AU au UK pia ndoto ya pili lazma nimiliki range Rover hata kma ya miaka ya tisini


Jamani huu ni mtazamo wangu tuuu najua MTA ni crash haina shida natamani nikaishi moja ya nchi hizo[emoji115] [emoji115] [emoji115] [emoji115] bila kujari ntaishi maisha gani
Naomba kukuuliza maswali.
1 ushapata passport?
2 unayo hela ya nauli?
3 ushafikia wapi mpaka sasa ili utimize ndoto yako?
4 umejiwekea muda gani uwe ushahama nchi?
5 umebadilisha matumizi yako na kuwa na matumizi ya kusave hela?


Ndukiiiii 🏃‍♂️🏃‍♂️🏃‍♂️
 
Naomba kukuuliza maswali.
1 ushapata passport?
2 unayo hela ya nauli?
3 ushafikia wapi mpaka sasa ili utimize ndoto yako?
4 umejiwekea muda gani uwe ushahama nchi?
5 umebadilisha matumizi yako na kuwa na matumizi ya kusave hela?


Ndukiiiii 🏃‍♂️🏃‍♂️🏃‍♂️




Haya maswali ni nyeti sana kuliko nyeti tulizonazo kwa kila baharia.
 
Kaka huo ni mpango mzuri sana muombe mungu atakusaidia katika hilo,mimi nakumbuka nilikuwa na jamaa yangu nimesoma nae,tulikuwa tukiipanga safari 2012 ya kusepa,tulipita mashirika kadhaa kuulizia nauli ya ndege lakini mwenzangu alikuwa anamishe ingawa pesa ilikuwa ndogo sana.

Huwezi amini alivyokuwa ameshika kalamu na karatasi ananipa mipango kama vile tunapiga pindi nilimuona kama anafanya mzaha vile,alizipanga nchi za kwenda,lakini alisema zikifeli hizi naenda hata south afrika lakini hapa nimepachoka.

Alijitoa sadaka akaacha kazi then akalamba nssf yake ilikuwa kama milioni kadhaa hivi,alisepa nchi moja ya kiaarabu mpaka leo anafanya kazi huko,na mipango yake aende kiwanja kirefu zaidi ya hapo.

Mimi aliniacha kwa sababu changamoto kubwa mno ni nauli kazi ngumu kupatikana na ukipata unapata pesa ya kula tuu.

Ila bado ndoto ninazo katika hilo na hatua mojawapo nimepiga namshukuru mungu kitabu ninacho tayari.

Ila namkumbuka broo mmoja huwa ananiambia safari haipo mdomoni ipo moyoni...weka nia madhubuti muombe mungu,tafuta fursa uchange nauli sepaaaaa.
 
Mimi na mpango wa kuhama Tz.Ila lini na nahamia nchi gani na nauli nta pata wapi Sijui kwa kweli.
 
Mm kuna mshikaji alikua anaenda shopping China,siku moja nikamwambia na mm naitaji kwenda kanambia poa nijiandae na nauli ya ndege+safar ya kwenda Kenya kuanza safar

Nimejiandaa nakuja mcheki jamaa sijui ndio alishayumba ya full changa,ikabid nitulie tu

Ila bado sijapoteza matumaini.. ila mm siitaji kuhama mazima bali kwenda kuchek fursa za kibiashara.
 
Ni ndoto nzuri lakini kuishi na wazungu si unaona walivyo wabaguzi utaweza??
 
Back
Top Bottom