Wenye familia na watoto mnawezaje kutazama Runinga nyumbani?

Ncha Kali

JF-Expert Member
Sep 19, 2019
14,535
27,069
Eti?

Unarudi nyumbani unakuta watoto wanatazama katuni zao kwa raha zao, au tamthilia pendwa za kike unawezaje kubadili chaneli bila kuonekana katili?

Tuseme muda wa Taarifa ya Habari, au hata mechi pendwa za soka..... ukibadili channeli watoto hao wanakukimbia sebuleni unabaki mwenyewe.

Hujisikii vibaya?

Hapa ndo umuhimu wa kupitia maeneo fulani kabla ya kurudi nyumbani, wenzetu mnawezaje?
 
Screenshot_20240328-191222.png
 
Nikishakubali matokeo kuwa kwangu Tv ya sebuleni sio mali yangu.

Nashukuru Mungu niliweka TV chumbani. Ninachotaka kuangalia nakiangalia chumbani kwangu. Huko sebuleni ni Nickelodeon na Cartoon Network.

Ningeweza kutumia ubabe wa ubaba lakini sioni faida yake. Ikiwa nipo hai acha wanangu wa enjoy nyumbani kwa baba yao.
 
U
Eti?

Unarudi nyumbani unakuta watoto wanatazama katuni zao kwa raha zao, au tamthilia pendwa za kike..... unawezaje kubadili chaneli bila kuonekana katili?

Tuseme muda wa Taarifa ya Habari, au hata mechi pendwa za soka..... ukibadili channeli watoto hao wanakukimbia sebuleni unabaki mwenyewe.

Hujisikii vibaya?

Hapa ndo umuhimu wa kupitia maeneo fulani kabla ya kurudi nyumbani, wenzetu mnawezaje?

Ukiwa na watoto basi hata hiyo tv ni mali ya watoto lazima wafurahi wakiwa home mzazi anapaswa kujali furaha ya watoto sio kujijali yeye kama vipi anunue nyingine aweke chumbani
 
Nikishakubali matokeo kuwa kwangu Tv ya sebuleni sio mali yangu.

Nashukuru Mungu niliweka TV chumbani. Ninachotaka kuangalia nakiangalia chumbani kwangu. Huko sebuleni ni Nickelodeon na Cartoon Network.

Ningeweza kutumia ubabe wa ubaba lakini sioni faida yake. Ikiwa nipo hai acha wanangu wa enjoy nyumbani kwa baba yao.
Safi sana nimeipenda hii 👏👏👏👏👏
 
Eti?

Unarudi nyumbani unakuta watoto wanatazama katuni zao kwa raha zao, au tamthilia pendwa za kike..... unawezaje kubadili chaneli bila kuonekana katili?

Tuseme muda wa Taarifa ya Habari, au hata mechi pendwa za soka..... ukibadili channeli watoto hao wanakukimbia sebuleni unabaki mwenyewe.

Hujisikii vibaya?

Hapa ndo umuhimu wa kupitia maeneo fulani kabla ya kurudi nyumbani, wenzetu mnawezaje?
Una tivii moja nyumbani?

Kama unayo moja tu, ndo muda wa kuwekeza katika tivii chumbani, jikoni, ofisi ya nyumbani, sun room, na streaming apps kama Sling TV, Peacock, YouTube TV, etc.

Sihitaji kuwa nyumbani kuangalia TV.

Hata nikiwa Maswa, bado naangalia NFL football kila Jumapili.

Zama hizi huna haja ya kuwa mateka wa runinga.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom