ndege JOHN
JF-Expert Member
- Aug 5, 2015
- 19,568
- 44,786
Nimeona mimi hapa Dar watu wengi kwenye magari sehemu za biashara wameweka bendera ya taifa la Israel.
Natambua umuhimu wa historia ya dini na mahusiano ya Mungu na watu wa kale hasa Wayahudi. Pamoja na kuwa taifa teule bado sijajua mantiki ya watu kutembea na bendera zake, je ina maana jeshi la serikali ya Mungu bado Israeli ina nguvu kama zamani.
Wenye bendera ni dhehebu gani katika ukristo, kuna nini nyuma ya pazia kuhusu ukweli, watu wenye bendera za Israel wanaamini nini kuhusu hio nchi maana mimi naona nyakati hizi huko Israel maisha ni ya kawaida kabisa kama miji mingine duniani na sala hakuna haja wala sababu ya kuiona kama ni taifa la kipekee mpaka kutembea na bendera yake.