Wenye bendera za Israel wanamaanisha nini?

ndege JOHN

JF-Expert Member
Aug 31, 2016
8,833
2,000
israe.jpg

Nimeona mimi hapa Dar watu wengi kwenye magari sehemu za biashara wameweka bendera ya taifa la Israel.

Natambua umuhimu wa historia ya dini na mahusiano ya Mungu na watu wa kale hasa Wayahudi. Pamoja na kuwa taifa teule bado sijajua mantiki ya watu kutembea na bendera zake, je ina maana jeshi la serikali ya Mungu bado Israeli ina nguvu kama zamani.

Wenye bendera ni dhehebu gani katika ukristo, kuna nini nyuma ya pazia kuhusu ukweli, watu wenye bendera za Israel wanaamini nini kuhusu hio nchi maana mimi naona nyakati hizi huko Israel maisha ni ya kawaida kabisa kama miji mingine duniani na sala hakuna haja wala sababu ya kuiona kama ni taifa la kipekee mpaka kutembea na bendera yake.
 
Perfectz

JF-Expert Member
May 17, 2017
7,150
2,000
ULIMBUKENI TU MKUU NA KUTOKUWA WAZALENDO.HIZI DINI TUMELETEWA MKUU.
PIA SABABU NYINGINE INAWEZA KUWA NI NAMNA WANAVYOLIKUBALI TAIFA HILO,KIMBINU,KIMKAKATI NA ULE USEMI KUWA NI TAIFA TEULE.
 
Aug 2, 2017
21
75
View attachment 573252 nimeona mini hapa dar watu Wengi kwenye magari sehemu za biashara wameweka bendera ya taifa la israel.natambua umuhimu wa historia ya dini na mahusiano ya mungu na watu wa kale hasa wayahudi.pamoja na kuwa taifa teuli bado sijajua mantiki ya watu kutembea na bendera zake.je ina maana jeshi la serikali ya mungu bado israeli ina nguvu kama zamani.wenye bendera ni dhehebu gani Katika ukristo kuna nini nyuma ya pazia kuhusu ukweli..watu wenye bendera za israel wanaamini nini kuhusu hio nchi maana mimi naona nyakati hizi huko israel maisha ni ya kawaida kabisa kama miji mingine duniani na sala hakuna haja wala sababu ya kuiona kama ni taifa la kipekee mpk kutembea na flag yake
Ni kweli na si tu hizo bendera,pia wengi wamekua wakidai wanaenda kuhiji kwa maana kwamba kuna nguvu ya kiMungu ndani yao, na baraka tele!!!,lakini ukweli ni kwamba watu wanafikiri Mungu yupo katika baraka za vitu,kwa sasa Yesu yupo mioyoni katika yohana 4:20-27,na pia baraka zitatokea pale utakapofanya mapenzi ya Bwana wetu Yesu Kristo,kumbukumbu 28:1-14,neno linasema mkitii sauti na amri za Mwenyezi-Mungu ,Mungu wenu baraka hizi zitawajilien,mtabarikiwa mashambani na mijini nk.......!lkin hii hutokana na kwamba watu hawajui nguvu ya Yesu kwamba ipo kwao na kwa watu wa mataifa mengine !!!!hvo nguvu ya bendera au kuhiji haimsaidii mtu chochote km asipoangalia kutimiza mapenz ya Mungu na kuacha dhambi mfn hasira,uzinzi,uasherati,uongo,wivu,usengenyaji,chuki,matusi,uchu ,shauku na mengine kama hayo,(galatia 5:16-21)!!#

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ELI-91

JF-Expert Member
Aug 24, 2014
3,591
2,000
Utumwa wa kifikra na athari za ukoloni. Itachukua miaka mingi watu kujitambua na kuthamini asili zao.
 
imali

JF-Expert Member
Sep 4, 2013
476
500
Ni kweli na si tu hizo bendera,pia wengi wamekua wakidai wanaenda kuhiji kwa maana kwamba kuna nguvu ya kiMungu ndani yao, na baraka tele!!!,lakini ukweli ni kwamba watu wanafikiri Mungu yupo katika baraka za vitu,kwa sasa Yesu yupo mioyoni katika yohana 4:20-27,na pia baraka zitatokea pale utakapofanya mapenzi ya Bwana wetu Yesu Kristo,kumbukumbu 28:1-14,neno linasema mkitii sauti na amri za Mwenyezi-Mungu ,Mungu wenu baraka hizi zitawajilien,mtabarikiwa mashambani na mijini nk.......!lkin hii hutokana na kwamba watu hawajui nguvu ya Yesu kwamba ipo kwao na kwa watu wa mataifa mengine !!!!hvo nguvu ya bendera au kuhiji haimsaidii mtu chochote km asipoangalia kutimiza mapenz ya Mungu na kuacha dhambi mfn hasira,uzinzi,uasherati,uongo,wivu,usengenyaji,chuki,matusi,uchu ,shauku na mengine kama hayo,(galatia 5:16-21)!!#

Sent using Jamii Forums mobile app
Maneno mengine ni kama mtu anawaza na makalio. Upuuzi mtupu. Waafrika ni wakuburuzwa tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kivava

JF-Expert Member
Apr 2, 2013
5,783
2,000
Google ; Why Jews don't accept Christ
kama utapandisha bendera ya mayahudi tena!
 
Victor wa happy

JF-Expert Member
Apr 24, 2013
11,675
2,000
Atakayeibariki Israel nami nitambariki

Atakayeilaani Israel nami nitamwadhibu

mchana toch ,usiku magogo tufanyaje?
 
Automata

JF-Expert Member
Mar 3, 2015
2,706
2,000

Wengine tena hubandika stika za hilo bendera la kijani kwenye daladala na maroli yao na wengine huchora kabisa hilo li bendera la kishetani kwenye majengo yao

Tutaheshimiana tu
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom