Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,470
- 911,173
Gazeti La CCM Uhuru la leo linatuhabarisha ya kuwa Wenje ametimkia Dar akikimbia mkono mrefu wa dola ambayo inamsaka kwa kuhamasisha machinga kufanya vurugu endapo Chadema haitanyakua nafasi ya umeya wa jiji la Mwanza......
Wenje asakwa kwa uchochezi
Thursday, 09 December 2010 14:23 newsroom
* Adaiwa kutimkia Dar
NA PETER KATULANDA, MWANZA
POLISI mkoani hapa inamsaka Mbunge wa Jimbo la Nyamagana kupitia CHADEMA, Ezekia Wenje kwa tuhuma za uchochezi.
Aidha, limemuonya mbunge huyo pamoja na wafuasi wa chama hicho kwamba wasithubutu kuvunja au kuchoma mali za halmashauri ya Jiji la Mwanza na mali za wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM). Akitoa onyo hilo, Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Simon Sirro aliwataka wafuasi wa chama hicho pia kutothubutu kuvamia kituo kikuu cha polisi kwa lengo la kukomboa pikipiki zilizokamatwa kwa mujibu wa sheria, vinginevyo watakiona cha moto. Wenje katika mkutano wake alioufanya katika viwanja vya Sahara mjini hapa Desemba 6, mwaka huu, alihamasisha wanachama wa chama hicho kuharibu mali za jiji na za wanaCCM.
ìPolisi tuko imara, ole wao watakaothubutu kufanya hayo watakiona cha moto maana tulikuwa tunapima kujua tunashughulika na watu wa aina gani, lakini sasa tumegundua ni wahuni na vibaka,î alisema Sirro. Alisema: ìIkifikia kiongozi kama Mbunge unasema maneno kama hayo ina maana haujui utawala wa kisheria, lakini pia kutojua kwako hakutafanya tusikuchukulie hatua za kisheria, hivyo tumefungua jalada la uchunguzi, tunamtafuta tumhoji.î Alisema baada ya Wenje kupata taarifa kuwa anasakwa, inadaiwa amekimbilia mjini Dar es Salaam, na kwamba atakapopatikana atahojiwa kuhusiana na kauli hizo.
Kamanda Sirro alifafanua kwamba alipata taarifa kuwa Wenje katika mkutano huo alikuwa akihamasisha wananchi, wakiwemo wafuasi wake kwamba Desemba 17, mwaka huu waende katika ofisi za halmashauri hiyo kusubiri matokeo ya Meya wa Jiji la Mwanza na iwapo hatatoka katika chama chake, wachome viwanda na hoteli za matajiri zinazomilikuwa na wana CCM.
Katika uchaguzi mkuu uliopita Oktoba 31, mwaka huu, jijini Mwanza, CCM ilipata viti tisa vya madiwani, CHADEMA 11 na CUF kimoja ilichoambulia Novemba 28, mwaka huu, wakati wa kukamilisha uchaguzi wa madiwani kwenye kata za Mirongo na Mkuyuni.
Aidha, katika jimbo la Nyamagana pekee, CCM ilipata viti sita, CHADEMA vitano na CUF kimoja, wakati Ilemela, CCM ilipata viti vitatu na CHADEMA sita.
Alidai pia kwamba Wenje alikaririwa akisema pikipiki za baadhi ya watu zinazoshikiliwa kwa makosa mbalimbali katika hicho, watazitoa kwa nguvu ya umma.
Sirro alisema juzi saa 12.40 jioni wafuasi wa CHADEMA walifunga barabara za Makongoro na Nyerere wakati wakiandamana kutoka eneo la Magomeni Kirumba kwenye mkutano wa wabunge Wenje na Hines Kiwia wa jimbo la Ilemela hadi maeneo ya kati kati mji na kusababisha usumbufu.