Wenje asakwa kwa uchochezi....adaiwa kutimkia Dar! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wenje asakwa kwa uchochezi....adaiwa kutimkia Dar!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rutashubanyuma, Dec 9, 2010.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Dec 9, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,345
  Likes Received: 418,711
  Trophy Points: 280
  Gazeti La CCM Uhuru la leo linatuhabarisha ya kuwa Wenje ametimkia Dar akikimbia mkono mrefu wa dola ambayo inamsaka kwa kuhamasisha machinga kufanya vurugu endapo Chadema haitanyakua nafasi ya umeya wa jiji la Mwanza......

  Wenje asakwa kwa uchochezi

  Thursday, 09 December 2010 14:23 newsroom
  * Adaiwa kutimkia Dar
  NA PETER KATULANDA, MWANZA
  POLISI mkoani hapa inamsaka Mbunge wa Jimbo la Nyamagana kupitia CHADEMA, Ezekia Wenje kwa tuhuma za uchochezi.
  Aidha, limemuonya mbunge huyo pamoja na wafuasi wa chama hicho kwamba wasithubutu kuvunja au kuchoma mali za halmashauri ya Jiji la Mwanza na mali za wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM). Akitoa onyo hilo, Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Simon Sirro aliwataka wafuasi wa chama hicho pia kutothubutu kuvamia kituo kikuu cha polisi kwa lengo la kukomboa pikipiki zilizokamatwa kwa mujibu wa sheria, vinginevyo watakiona cha moto. Wenje katika mkutano wake alioufanya katika viwanja vya Sahara mjini hapa Desemba 6, mwaka huu, alihamasisha wanachama wa chama hicho kuharibu mali za jiji na za wanaCCM.

  ìPolisi tuko imara, ole wao watakaothubutu kufanya hayo watakiona cha moto maana tulikuwa tunapima kujua tunashughulika na watu wa aina gani, lakini sasa tumegundua ni wahuni na vibaka,î alisema Sirro. Alisema: ìIkifikia kiongozi kama Mbunge unasema maneno kama hayo ina maana haujui utawala wa kisheria, lakini pia kutojua kwako hakutafanya tusikuchukulie hatua za kisheria, hivyo tumefungua jalada la uchunguzi, tunamtafuta tumhoji.î Alisema baada ya Wenje kupata taarifa kuwa anasakwa, inadaiwa amekimbilia mjini Dar es Salaam, na kwamba atakapopatikana atahojiwa kuhusiana na kauli hizo.
  Kamanda Sirro alifafanua kwamba alipata taarifa kuwa Wenje katika mkutano huo alikuwa akihamasisha wananchi, wakiwemo wafuasi wake kwamba Desemba 17, mwaka huu waende katika ofisi za halmashauri hiyo kusubiri matokeo ya Meya wa Jiji la Mwanza na iwapo hatatoka katika chama chake, wachome viwanda na hoteli za matajiri zinazomilikuwa na wana CCM.
  Katika uchaguzi mkuu uliopita Oktoba 31, mwaka huu, jijini Mwanza, CCM ilipata viti tisa vya madiwani, CHADEMA 11 na CUF kimoja ilichoambulia Novemba 28, mwaka huu, wakati wa kukamilisha uchaguzi wa madiwani kwenye kata za Mirongo na Mkuyuni.
  Aidha, katika jimbo la Nyamagana pekee, CCM ilipata viti sita, CHADEMA vitano na CUF kimoja, wakati Ilemela, CCM ilipata viti vitatu na CHADEMA sita.
  Alidai pia kwamba Wenje alikaririwa akisema pikipiki za baadhi ya watu zinazoshikiliwa kwa makosa mbalimbali katika hicho, watazitoa kwa nguvu ya umma.
  Sirro alisema juzi saa 12.40 jioni wafuasi wa CHADEMA walifunga barabara za Makongoro na Nyerere wakati wakiandamana kutoka eneo la Magomeni Kirumba kwenye mkutano wa wabunge Wenje na Hines Kiwia wa jimbo la Ilemela hadi maeneo ya kati kati mji na kusababisha usumbufu.
   
 2. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #2
  Dec 9, 2010
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 443
  Trophy Points: 180

  This is where I tend to say no! Give the source plse.
   
 3. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #3
  Dec 9, 2010
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  Mkuu this shows kwamba haukusoma habari yenyewe umesoma heading tu.... Soma first line ya habari
   
 4. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #4
  Dec 9, 2010
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,663
  Likes Received: 21,887
  Trophy Points: 280
  Gazeti la Uhuru! hivi halijajifia tuu? maana haliuziki kwa vile linaandika sana unazi/uongo uliopitiliza unaowauzi hata wana CCM. Au linapata ruzuku ya serikali?
   
 5. Ally Msangi

  Ally Msangi Verified User

  #5
  Dec 9, 2010
  Joined: Jun 29, 2010
  Messages: 581
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  hizi habari si za kweli, hilo gazeti limeandika kwa uchochezi tu
   
 6. samirnasri

  samirnasri JF-Expert Member

  #6
  Dec 9, 2010
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 1,377
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Wewe unayepata muda wa kusoma gazeti la UHURU inabidi tukupime kwanza akili. Tangu lini gazeti la uhuru likaandika mazuri ya CHADEMA !! Walishindwa hata kuipa uzito habari ya jk kususiwa bungeni. Siku zote gazeti la uhuru linaandika habari za kuiponda chadema au zile zinazoeelezea kile wanachokiita "mpasuko". ndani ya chadema.. Mimi nikisikia habari imeandikwa na uhuru, RAI mtanzania na habari leo ,I dont BOTHER..
   
 7. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #7
  Dec 9, 2010
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,908
  Likes Received: 12,066
  Trophy Points: 280
  Hivi u analyst wako ni wa kukopi na kubadilisha heading za magazeti tu huna kazi zingine mara Wenje mchochezi mara Shibuda matatani, na mara nyingi huwa unatafuta habari za uchochezi za CDM ndizo unazikopi. Stop distorting informations.
   
 8. kilemi

  kilemi JF-Expert Member

  #8
  Dec 9, 2010
  Joined: Mar 13, 2009
  Messages: 520
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35

  Bado kidogo utaenda kutafuta habari chooni!!
   
 9. samirnasri

  samirnasri JF-Expert Member

  #9
  Dec 9, 2010
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 1,377
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Wewe unayepata muda wa kusoma gazeti la UHURU inabidi tukupime kwanza akili. Tangu lini gazeti la uhuru likaandika mazuri ya CHADEMA !! Walishindwa hata kuipa uzito habari ya jk kususiwa bungeni. Siku zote gazeti la uhuru linaandika habari za kuiponda chadema au zile zinazoeelezea kile wanachokiita "mpasuko". ndani ya chadema.. Mimi nikisikia habari imeandikwa na uhuru, RAI mtanzania na habari leo ,I dont BOTHER..
   
 10. M

  Miruko Senior Member

  #10
  Dec 9, 2010
  Joined: Feb 8, 2008
  Messages: 173
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35

  Sources zangu zinasema kuna mkutano wa wabunge wa CHADEMA Dar, ulianza jana na unaendelea leo, yawezekana amekuja kuhudhuria mkutano, au kweli kakimbia.
   
 11. Isaac

  Isaac JF-Expert Member

  #11
  Dec 9, 2010
  Joined: Jan 4, 2009
  Messages: 627
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 45
  Kwahiyo, Dar na Mwanza polisi wao ni tofauti? Bahati yako umeanza na Gazeti la CCM Uhuru....
   
 12. tanga kwetu

  tanga kwetu JF-Expert Member

  #12
  Dec 9, 2010
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 2,165
  Likes Received: 1,124
  Trophy Points: 280
  ...yupo kwenye kikao cha wabunge wa CDM, jijini Dar!
   
 13. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #13
  Dec 9, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,345
  Likes Received: 418,711
  Trophy Points: 280
  Angalau sasa tumejua ukweli kuwa hajatoroka polisi..........................
   
 14. Kamakabuzi

  Kamakabuzi JF-Expert Member

  #14
  Dec 9, 2010
  Joined: Dec 3, 2007
  Messages: 1,499
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Chadema viti 11, ccm 9 na cuf 1. Hakuna kuchakachua hapo, ni wazi CDM itachuka umeya, labda kama baadhi ya madiwani wa CDM watahongwa!
   
 15. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #15
  Dec 9, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Ushauri/ombi kwa kakangu Rutashubanyumba, kama unaweza jaribu tu kuwapotezea kabisa uhuru, habari leo na daily news kwenye mpango wako kamambe wa kutuhabarisha... wanatuharibia siku tu
   
 16. Kagemro

  Kagemro JF-Expert Member

  #16
  Dec 9, 2010
  Joined: Jan 11, 2010
  Messages: 465
  Likes Received: 50
  Trophy Points: 45
  kama wana akili timamu wamfuate bagamoyo kwenye retreat.
   
 17. m

  matawi JF-Expert Member

  #17
  Dec 9, 2010
  Joined: Mar 29, 2010
  Messages: 2,055
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Mwacheni Rutashubanyuma awe anatuhabarisha maana vinginevyo tunaweza tusijue wapinga maendeleo wana mpango gani maana wengine huwa hutuyasomi haya magazeti
   
 18. Bams

  Bams JF-Expert Member

  #18
  Dec 9, 2010
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 3,599
  Likes Received: 2,984
  Trophy Points: 280
  Gazeti La CCM Uhuru la leo linatuhabarisha ya kuwa Wenje ametimkia Dar akikimbia mkono mrefu wa dola ambayo inamsaka kwa kuhamasisha machinga kufanya vurugu endapo Chadema haitanyakua nafasi ya umeya wa jiji la Mwanza...

  Haifai kutumia gazeti la Uhuru kama chanzo cha habari. Hakuna mtu yeyote sasa hivi, hata wana CCM wanaolitumia gazeti hilo kama chanzo cha habari. Leo nilikuwa naongea na Kiongozi mmoja wa CCM kuhusiana na wahisani kutoa tamko kuhusu msaada wao kwa Tanzania. Akaniambia kuwa, 'nimesoma kwenye gazeti la uhuru wameandika maneno fulani kuhusiana na wahisani lakini siwezi kusema chochote maana huwezi kuamini habari yoyote kwenye gazeti hili mpaka uone hiyo habari imeandikwa na magazeti mengine kama Mwananchi'. Kwa ushauri tusipoteze kuongelea habari zinazoandikwa na magazeti kama Uhuru ambayo waandishi wao hawaelewi hata maana ya 'HABARI'.
   
 19. m

  muje Member

  #19
  Dec 9, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 12
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Uhuru nimetoa offer kwa wakinamama wafungie maandazi!
   
 20. N

  Njaare JF-Expert Member

  #20
  Dec 9, 2010
  Joined: Sep 26, 2010
  Messages: 1,075
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135

  Mkuu hapo kidsogo umepotoka. Ni muhimu kujua maadui zako wanakuchukuliaje ili ujihami. Usiposoma hayo magazeti hutajua wanakuchukuliaje na wao wanajivunia nini. Heko Ruta kwa kupata huo moyo wa kuyasoma maana yanakera ila ni muhimu kuyasoma ili kujua jinsi ya kupambana na CCM
   
Loading...