Wengine hatumpendi Mungu tunajilazimisha tu

Wengine hatumpendi Mungu tunajilazimisha tu

Shetani ni mtoto wa MUNGU maana alimuumba, sisi ni watoto wa MUNGU maana alituumba, huu ni ugomvi wa ndugu...

Sababu zipi za msingi zinazosababisha BABA awaue watoto wote walioteleza kwa kulubuniwa na ndugu yao? Ndugu ambaye ni mmoja tu? Kwanini maelfu wafe sababu ya ndugu mmoja mkorofi aliyepewa uwezo wa ushawishi na nguvu kubwa ya ulaghai na BABA mwenyewe?

Na ukumbuke hii ni mara ya pili, ya kwanza aliua wote kwa maji, akaacha wachache sana ili wazaliane. Sasa ataua tena kwa moto wa milele, Kwann BABA anafanya hivi?

katika moto wa milele hakuna kifo bali ni mateso ya kuunguzwa milele.

ndugu yetu anatuponza sababu tuna uwezo wa kumkataa na mambo yake yote.
 
hakuna wanachozidiana,wanatofautiama maamuzi tu.

wewe ukiona mtu kaangusha simu,unaona ni sawa kumpelekea,mwingine anaona kapata ya kutumia,mwingine anaona akauze apate hela.

lakini nyinyi wote mna utashi unaoendana,anayefanya vibaya wazo la kwanza humjia,ni taarifa kwamba unachofanya si chema,ila hulipuuza.
Kwanini kuwe na maamuzi tofauti ilihali wote wameumbwa kwa package iliyo sawa sawa?
 
katika moto wa milele hakuna kifo bali ni mateso ya kuunguzwa milele.
Inatisha sana.

Ni ukatili mkubwa kwa binadamu aliyezini kwa sababu ya nyege au aliyeiba sababu ya njaa.

Hakuna upendo hapo na hata wewe unajua hilo sema utakuwa mnafiki sababu huo moto unauogopa sasa unakuwa a coward kusifia usiloamini moyoni mwako.

Imagine unamuoma mama yako mzazi aliyeiba kazini kwake ili usome anachomwa milele na milele na milele halafu eti unasema ni Upendo. MWONGO WEWE ni muoga tu mnafiki ili na wewe usichomwe.
 
haya sasa unasema wewe mkuu.

mwanao anazaliwa ukimwona kwamba mtoto,mnalala naye akiwa busy sana na mambo na michezo yake inayohusu utoto pekee,siku atakayoangalia sehemu yako na kukuhoji baba mbona ya kwako kubwa zaidi,hapa utampa tiketi kwamba sasa anatakiwa akalale peke yake.si kweli kwamba ulikuwa hujui atakuja kukua.

Mungu kamuumba binaadam akijua kabisa siku moja atakuja kudanganywa,ushindi kwa adam ulikuwa kukataa,akashindwa.
Mfano uliotoa ni tofauti na uwezo wa Mungu. Mzazi angekuwa na uwezo asingetaraji mpaka mwanae ahoji maumbile yake kwa kumchungulia, ndio ajue akili yake bali kabla ya chochote kutokea yeye mzazi angeshaanza kutambua na kisha kukiweka sawa. Umetoa mfano ambao unaonesha Mungu ni dhaifu asiyejua kama akili ya binadamu ipoje mpaka pale alipofanya tukio ndio katambua akili ya binadamu ilivyo
 
Sijasema amezaa...

Kwa hiyo tunakubaliana kuwa suala la adhabu alijuaye ni MUNGU mwenyewe? Na pengine tafsiri ya neno moto wa milele inawezakuwa tofauti na tunayoelezwa kila siku?
Adhabu yake imewekwa wazi na inajulikana kama ilivyo malipo adhabu nilazima uipate kwani ndo malipo kwa uliyoyatenda Swala la msamaha iwe kupunguza au kuondoa liko Juu yake Ila ni lazima kwanza utumikie/ulipwe kwa kile ulichochuma.
 
Inatisha sana.

Ni ukatili mkubwa kwa binadamu aliyezini kwa sababu ya nyege au aliyeiba sababu ya njaa.

Hakuna upendo hapo na hata wewe unajua hilo sema utakuwa mnafiki sababu huo moto unauogopa sasa unakuwa a coward kusifia usiloamini moyoni mwako.

Imagine unamuoma mama yako mzazi aliyeiba kazini kwake ili usome anachomwa milele na milele na milele halafu eti unasema ni Upendo. MWONGO WEWE ni muoga tu mnafiki ili na wewe usichomwe.
Umekatazwa usidhini ila ukapewa mbadala wa kuoa sasa kwanini uzini
Iweje ufanye kazi ya kulipwa ujira wako halali alafu ifikie hatua uibe kwa kisingizio cha kusomesha huoni tatizo liko kwako na si kwa Mungu
 
Sawa. Sijahoji uwepo wa adhabu. Nimehoji uhalali wa adhabu kulinganisha na kosa na usawa wa dhambi.

Dhambi zote ni sawa? Muuaji na msengenyaji yaani mmbea wote ni kiberiti si ndio?
 
Uzinzi unaanza na tamaa, na ukitamani hata kabla hujatenda tayari umezini. Kibiolojia wanaume karibu wote kama si wote ni wazinzi kiasili. Hata mkeo kuna kipindi ulimtamani kabla hujamuoa.

Dhambi zote ni sawa, Kiberiti kitakachomchoma mzinzi ndicho hicho hicho kitamchoma mchinjaji na mla nyama za watu. Wewe unaona ni sawa?
 
Sawa. Sijahoji uwepo wa adhabu. Nimehoji uhalali wa adhabu kulinganisha na kosa na usawa wa dhambi.

Dhambi zote ni sawa? Muuaji na msengenyaji yaani mmbea wote ni kiberiti si ndio?
Moto na pepo zote zinadaraja zake kulingana na uzito wa kila dhambi na kila mema utalipwa kulingana na kile ulichokipanda siku hiyo kuna watakaochomwa kila siku kuna watakao pumzishwa katika siku kwa kifupi usitarijie kufanya dhambi ukaona ni ndogo kwamaana adhabu ya mwenyezi haivumiliki cha muhimu ni kuepukana na adhabu hizo ukiwa hapa dunia kwa kufanya yaliyo amrishwa na kuacha yaliyokatazwa kwani ni kwa manufaa yako hapa dunia na kesho akhera.
 
Uzinzi unaanza na tamaa, na ukitamani hata kabla hujatenda tayari umezini. Kibiolojia wanaume karibu wote kama si wote ni wazinzi kiasili. Hata mkeo kuna kipindi ulimtamani kabla hujamuoa.

Dhambi zote ni sawa, Kiberiti kitakachomchoma mzinzi ndicho hicho hicho kitamchoma mchinjaji na mla nyama za watu. Wewe unaona ni sawa?
Ndo mana ikashauriwa watu wavae stara kuficha maungo yao ni bora nusu shari kuliko shari kamili. Pia Mwenyezi Mungu ni mwenye kusamehe unaweza kutubia na akakusamehe soma kisa cha nabii yusufu na hakika utajifunza zaidi.
 
Afande sele alihoji hiki Kitu lakini watu wa dini wakamtishia kifo badala ya kumuelemisha, wengine wakasema watamsomea alibadili ili afe
 
Kama umpendi mbona unaishi kwenye sayari yake wahi kuzimu
 
Sometimes our Imaan/ Faith takes a dive towards a bottomless pit. We feel so devastated and hopeless.

And at that point the devil comes in and whispers such thoughts about God.

Do not allow such thoughts about God. He does not need our love or prayers and beliefs. But we need Him every step of our lives.

Shun the devil and fight these thoughts..... If you are a Muslim listen to the Quran. You will heal instantly.
 
Kwanini kuwe na maamuzi tofauti ilihali wote wameumbwa kwa package iliyo sawa sawa?

ni maamuzi tu maana hakuna makundi maalumu ambayo yameumbwa ili kufanya uchaguzi wa aina fulani tu.
 
Inatisha sana.

Ni ukatili mkubwa kwa binadamu aliyezini kwa sababu ya nyege au aliyeiba sababu ya njaa.

Hakuna upendo hapo na hata wewe unajua hilo sema utakuwa mnafiki sababu huo moto unauogopa sasa unakuwa a coward kusifia usiloamini moyoni mwako.

Imagine unamuoma mama yako mzazi aliyeiba kazini kwake ili usome anachomwa milele na milele na milele halafu eti unasema ni Upendo. MWONGO WEWE ni muoga tu mnafiki ili na wewe usichomwe.

hapana mkuu usinipe sifa za ajabu sababu tu akili yako imefikia tamati katika kuchanganua mambo fulani.

baba yako mzazi alikukanya mambo kadhaa,hukufanya sababu ulijua ni kumkosea baba yako na atakuadhibu,ukatili wa baba yako hauko katika adhabu anayokupa bali upendo upo katika njia mbadala anayokuelekeza kabla hujaamua kushika nyingine.

mama kuiba ili mimi nisome inahalalishaje wizi machoni kwangu!!!wizi ni wizi tu hakuna anayeiba bila sababu za msingi kwake.
 
Back
Top Bottom