Wengine hatumpendi Mungu tunajilazimisha tu

Kwani yeye si mungu alipaswa kujua mbeleni mwanadamu atakuja kosea. Kwanini aliendelea kumuumba. Na kama alikuwa hataki mwanadamu apotee kwanini amruhusu shetani kumshawishi mwanadamu. Na kipindi shetani anamlaghai mwanadamu yeye mungu alikuwa wapi? Kuna maswali bado hayajibiki

vyema umekiri hayajibiki,mengine anajua yeye sababu.

mfano nikikuuliza wewe ni kwanini hujaugua mwaka mzima huu corona wakati labda hukuwa makini kuchukua tahadhali,hutakuwa na jibu la moja kwa moja.

ndio maana tunasema maamuzi yake au kazi yake haina makosa.
 
kama yapi embu uliza hapa.

NOTE,hakikisha una nia ya kuelewa sio unataka kubishana.
Sawa mkuu. Ngoja nipate darasa.. Ni vipi Adam na hawa wahesabike ni wakosaji na wapewe hukumu ya kifo ilihali wao ni binadamu ambao kimsingi inafahamika kuwa binadamu hajakamilika?
Mungu ni mjuzi anayejua ya mbele ya nyuma na ya sasa, je hakujua kama kwa namna Adam na Hawa pamoja na shetani walivyoumbwa, watakuja kumkosea? Kama alijua je aliwaumba ili wakosee? Kama hakuwaumba ili waje kukosea je ni vipi alifanya ili kuwarekebisha ili wasikosee kwasababu uwezo wa Mungu ni mkubwa kuliko yeyote yule

Kama Mungu hakuwa na lengo la binadamu wafe je kwanini alikiumba kifo?
 
huwezi hitaji msaada wake akakataa kama hakujui.
Kama ingekuwa kila msaada wanaomba watu wanapewa basi tungeona ufanisi wake mkubwa. Unataka kuniambia hakuna wacha Mungu ambao wamekufa ilihali wamepambania uhai wao kwa kila namna hadi kwa dua na maombi lakini mwisho wa siku wamefariki. Kuna wachamungu wameishi kwa ufukara maisha yao yote na wameomba utajiri lakini mwisho wa siku wamekufa wakiwa mafukara. Nimekupa machache kukuonesha kuwa hata uwe na imani kiasi gani kwa Mungu haiwi guarantee ya kupata kila unachotaka
 
kwanini ufikiri utajiri kila mtu anaweza kupewa??

ni kweli si kila unachoomba utapewa,sababu atoaye ana vigezo na sababu zake pia.
 
Sawa mkuu. Ngoja nipate darasa.. Ni vipi Adam na hawa wahesabike ni wakosaji na wapewe hukumu ya kifo ilihali wao ni binadamu ambao kimsingi inafahamika kuwa binadamu hajakamilika?
Mungu ni mjuzi anayejua ya mbele ya nyuma na ya sasa, je hakujua kama kwa namna Adam na Hawa pamoja na shetani walivyoumbwa, watakuja kumkosea? Kama alijua je aliwaumba ili wakosee? Kama hakuwaumba ili waje kukosea je ni vipi alifanya ili kuwarekebisha ili wasikosee kwasababu uwezo wa Mungu ni mkubwa kuliko yeyote yule

Kama Mungu hakuwa na lengo la binadamu wafe je kwanini alikiumba kifo?

hata katika maisha yetu ya kisiasa tunapigizana makelele kila siku,haipendezi mtu kusujudiwa kwa ubabe wake(watu kujipendekeza) bali watu wajikane kwa utashi wao kwa kiongozi husika kulingana na kazi anazozifanya.

Mungu wetu toka mwanzo ni mtu wa kuwapa viumbe wake uhuru,hata shetani alipewa uhuru mkubwa sana mpaka cheo cha juu sana,akaota ndevu.

hata baada ya kifo bado anatutongoza,kuna uzina endapo tutakubali kufuatana naye.
 
kwanini ufikiri utajiri kila mtu anaweza kupewa??

ni kweli si kila unachoomba utapewa,sababu atoaye ana vigezo na sababu zake pia.
Kwa kauli hiyo, basi msiseme kuwa Mungu hajawahi kuwaacha bali mseme Mungu ndiye mwenye maamuzi ya kuwaacha au kutokuwaacha hata kama utakuwa nae bega kwa bega kwa kiasi gani.
 
ni maamuzi ya msemaji tu,kwani hujawahi kukatwa jina ktk interview ya kazi ya kitapeli???utalia ulaumu why Mungu kakuacha maana hujui kitu.soon after ndio unajua kumbe bado una bahati sana.

wengine hupenda kusema Mungu humpa mtu anachostahili sio kila aombacho.
 
hata katika maisha yetu ya kisiasa tunapigizana makelele kila siku,haipendezi mtu kusujudiwa kwa ubabe wake(watu kujipendekeza) bali watu wajikane kwa utashi wao kwa kiongozi husika kulingana na kazi anazozifanya.

Mungu wetu toka mwanzo ni mtu wa kuwapa viumbe wake uhuru,hata shetani alipewa uhuru mkubwa sana mpaka cheo cha juu sana,akaota ndevu.

hata baada ya kifo bado anatutongoza,kuna uzina endapo tutakubali kufuatana naye.
Uhuru, je nini maana ya Uhuru?
Unasemaje kiumbe kiumbe kimepewa uhuru ilihali kuna masharti na mipaka? Kuwa na masharti na mipaka kunaondoa uwepo wa uhuru bali kunakuwa na maamrisho.

Kama kuna uhuru je shetani na viumbe vingine vilipewa nafasi ya kuulizwa kabla ya kuumbwa kuwa wachague kati ya kuumbwa au wasiumbwe?

Umezungumzia utashi.
Je utashi baina ya binadamu na binadamu unalingana?
 
hakuna uhuru usio na mipaka,kama upo basi sio ktk ulimwengu huu wa kutumia utashi.

shetani kama kiumbe mwingine wa Mungu hakuwepo kabla,angeamuaje hatma ya pumzi yake ikiwa hakuwa na uhai,hakuwepo!!

utashi baina ya binaadam na binaadam uko sawa kabisa,labda kama mmoja ana tatizo la akili.
ila utashi kama ilivyo kujua hutakiwi kuvuka barabara bila kuhakiki usalama kwanza,kila mtu anao.
 
Na ndio maana nimeomba unipe tafsiri ya neno uhuru ili tuone uwepo wa mikingamo kunaweza kumpa mtu uhuru ilihali hajapewa uhuru kamili.

Sasa utaumbaje kiumbe au mtu bila ridhaa yake? Kama ni uhuru ilipaswa kiumbe kiridhie, huo ndio uhuru kamili.

Nilikuuliza kuhusu utashi kabla sijaenda mbali zaidi naomba kwanza tuwekane sawa nini maana ya utashi? Kisha tuje tujadili kwenye uumbaji wa Mungu kwa binadamu kwanzia kwenye akili na huo utashi.
 
Back
Top Bottom