Wengine hatumpendi Mungu tunajilazimisha tu

hujakubaliana na mimi popote kwamba anayetenda maovu kuwa sio mkamilifu.

niambie kwanza tafsiri ya neno udhaifu,ni kutenda dhambi umeitoa wapi??ili twende vizuri.
Unataka tafsiri ya neno udhaifu? Au unataka ufafanuzi juu ya udhaifu ni kutenda dhambi? Nyosha kwanza maelezo
 
nataka uhusiano uliopo kati ya neno udhaifu na binaadam kutenda dhambi.

kwanini kwa makusudi kabisa linataka kufanwa ni neno lenye maana moja???
 
Nimelizungumzia hilo kwenye post 249.

unasema mtu mwovu ana mapungufu katika akili na utashi,.kitu ambcho ni udhaifu katika maumbile ya kibinaadam.
hii sio kweli.tuanze darasa kidogo.

mtu mwovu hana mapungufu yoyote katika uumbaji,anapungukiwa uchaji wa Mungu,ambao huusababisha mwenyewe kwa kujitenga na muumba wake kwa makusudi kabisa akiwa na akili timamu.

hali hiyo hutokea wakati ambao mwili wa mtu unakuwa master wa kila kitu unajiongoza wenyewe,na si nafsi ya mtu au roho yake.nafsi ya mtu ina uungu ndani yake,ina nguvu kamili ya Uungu,ila inachafuliwa na mwili huu wa kibinaadam.
 
Watu hamna shukrani,badala uombe akupeleke waliko vpenzi wako mkapendane unalaumu huku jf! Ubinadam kazi kwelikweli
 
Wengine hatuna tu option kulingana na vitisho tulivyopandizwa tangu utotoni ila huyu Mungu hatumpendi haswa
Mkuu shukuru sana umeumbwa na una akili timamu pambana sana umjue aliyekuumba akupe michongo,uhai siyo kiatu rahisi ,usikate tamaa mapema yupo aliyekuumba na ana program zako nyingi ,mtafute utafanikiwa
 
Hofu ya uwepo wa Mungu Ipo kwa kila Binadamu ndugu yangu

Ndio maana hata kama Mtu hajawahi kufundishwa au kushuhudiwa habari za Mungu utakuta anajua kabisa kuwa mema ni yapi na mabaya ni yapi, na anajua kuwa kumfanyia mtu hivi ni vibaya na hivi ni vizuri

Mathalani katika jamii za kiafrika hata kabla ya kuja kwa Wazungu na Waarabu tayari walijua kuua ni dhambi, kubaka, kusema uongo, kuroga n.k

Kwahiyo, watahukumiwa kwa kile walichokifahamu wakakaidi.

Walifahamu kuua ni jambo la kawaida hadi waliweza kuvamia tawala zingine na kuua. Watahukumiwaje
 
unasema mtu mwovu ana mapungufu katika akili na utashi,.kitu ambcho ni udhaifu katika maumbile ya kibinaadam.
hii sio kweli.tuanze darasa kidogo.

mtu mwovu hana mapungufu yoyote katika uumbaji,anapungukiwa uchaji wa Mungu,ambao huusababisha mwenyewe kwa kujitenga na muumba wake kwa makusudi kabisa akiwa na akili timamu.

hali hiyo hutokea wakati ambao mwili wa mtu unakuwa master wa kila kitu unajiongoza wenyewe,na si nafsi ya mtu au roho yake.nafsi ya mtu ina uungu ndani yake,ina nguvu kamili ya Uungu,ila inachafuliwa na mwili huu wa kibinaadam.

Kwanini unasema makusudi?

Je watu wote waliokaribu na Mungu hawafanyi makosa?
 
watu walio karibu na Mungu hawafanyi makosa.

kuna watu waliwahi kuwepo na imani kali sana,kama ayubu.
Nimekuuliza swali haujanijibu kwanini unasema makusudi?

Mimi kuhusu Ayoubu sijui alikuwa na imani kiasi gani kwasababu sijamshuhudia, wewe Ayoubu umepata kushuhudia imani yake zaidi ya kusoma hadithi tu? Na je huyo Ayoub ndio mtu pekee alikwa na imani kali sana kuliko binadamu wote?
 
ni makusudi kwa sababu hakuna kitu ambacho binaadamu hakijui kuhusu makosa kwa muumba wake,nasema uongo!!!
utazini makusudi,utaroga makusudi,utasengenya makusudi,utadanganya makusudi nk.

hata mimi ayubu sijawahi kumwona,nafanya rejea ya kitabu biblia na hadithi yake mojawapo ni hii ya ayubu,kama una mtu mwingine umesimuliwa au umewahi kumwona alijaribiwa kama ayubu na hakubadili msimamo wake,sio mbaya ukimtaja hapa,atahesbiwa tu kama ushahidi pia,sijasema ayubu ndiye pekee nimetolea mfano tu.
 
Kujua makosa ni swala moja na kujizuia kutofanya kosa ni swala lingine tofauti unalijua hilo?

Rejea zinazotumika hazina ukweli kwa asilimia mia kuna kujipinga na kujichanganya kwa mambo mengi. Na pia Mungu hakuwahi kuandika vitabu hivyo ni maneno ya watu.

Nimekuuliza kama kuna mwingine zaidi ya Ayoubu nina maana yangu hivyo kama unawajua wengine wanaofanana au kumzidi Ayoub wataje kulingana na hiyo rejeo unayotumia ila kama hakuna mwingine pia sema
 
at least umekiri kwamba kuna kujizuia kufanya makosa,nikadhani ni swala lisilomhusu binaadam mwenyewe,linategemea kiumbe mwingine nk.

hakuna sehemu nimesema au kuandika Mungu kaandika kitabu furani.

wapo ndio,yupo Nuhu,ayubu,stephano nk.
 
Hoja yangu ilikuwa ni binadamu kutokuwa na ukamilifu. Wewe umesema binadamu anafanya makosa makusudi nikakuuliza kwanini useme makusudi ukanijibu kwavile anafanya kosa huku anajua ni kosa. Nikakwambia kujua kosa ni kitu kimoja lakini kujizuia ni jambo lingine tofauti. Hapa kwenye kutokujizuia ndipo penye msingi wa upungufu wa binadamu.

Naomba niambie ni wapi ambapo kumesimulia maisha ya kila siku ya huyo Nuhu, Ayubu, Stephano, n.k ili namimi nikasome nione maisha yao kila siku wakiamka mpaka wanalala wanaishi vipi, wameongea kipi mbele za watu. Hiyo rejea ieleze maisha yake yote kwasiku zote alizoishi dunia ili nihitimishe kweli hakiwahi kukosea.walivyokuwa duniani, na sio kuelezea matukio kadhaa na kufanya hitimisho kuwa hakuwahi kufanya makosa ina maana hao watu wako level moja Mungu?
 
ninakuuliza,kujizuia ni jukumu la binaadam mwenyewe au napo mpaka msaada!!!sijui uliona hili swali??

hakuna sehemu palipoandikwa historia ya kila siku ya nuhu,stephano wala ayubu.
 
Back
Top Bottom