Nadharia zako umeziweka kwa kuelemea upande mmoja kuonyesha kana kwamba binadamu ni kiumbe dhaifu na si kweli. Embu turudi kwenye mfano wako kwa kusema Mungu kakwambia kabisa kuna nyoka msimsogelee na akiamua kuwasogelea amewapa na uwezo wa kumwondoa huyo nyoka kwakuwapa kila aina ya silaha ya kumuua huyo nyoka, nyoka mwenyewe ni mmoja na nyie mpo wengi tena mna silaha hapo mnamwitaji mungu wa nini tena ikiwa uwezo huo kawapa mnao wenyeweUmejenga nyumba,
Hapo ndani kwako anaingia nyoka,
unawaambia wanao kuna nyoka humu msimsogelee kaeni mbali atawauma,
nyoka anawauma wanao mmoja mmoja,
nyoka uwezo wa kumwondoa unao ila humwui unasubiri siku ya mwisho uchome wote wanao waliumwa na nyoka kwa kosa la kuruhusu nyoka awaume na nyoka mwenyewe.
Hizi hadithi za wachungaji kuna mambo hayapo sawa.
MUNGU yupo ila nina wasiwasi na haya mahubiri tunayohubiriwa.
Kuna uwezekano huyu MUNGU si huyu wanayemuhubiri.
Na ndio maana nimeomba unipe tafsiri ya neno uhuru ili tuone uwepo wa mikingamo kunaweza kumpa mtu uhuru ilihali hajapewa uhuru kamili.
Sasa utaumbaje kiumbe au mtu bila ridhaa yake? Kama ni uhuru ilipaswa kiumbe kiridhie, huo ndio uhuru kamili.
Nilikuuliza kuhusu utashi kabla sijaenda mbali zaidi naomba kwanza tuwekane sawa nini maana ya utashi? Kisha tuje tujadili kwenye uumbaji wa Mungu kwa binadamu kwanzia kwenye akili na huo utashi.
Kwenye hiyo maana ya uhuru uliyotoa hakuna neno masharti walaneno uhuru kwa tafisir ya moja kwa moja,ni nafasi ya mtu kufanya mambo yake bila kuingiliwa.
Kwenye hiyo maana ya uhuru uliyotoa hakuna neno masharti wala
Vigezo vya kuzingatiwa. Hivyo kama Mungu angekuwa ametoa uhuru kusingekuwa na sheria.
Yupo sasa? 🙆♂️🙆♂️🙆♂️
Waafrika tunapigwa sababu tumeachana na miungu yetu tukaambatana na miungu mfu ya kigeni
Sitarajii nieleweke leo
Hakuna uhuru ulio na masharti. Ukipewa masharti au mipaka inaitwa ni maamrisho au maagizo nawala sio uhuru. Uhuru maanake unafanya unavyotaka au unavyojisikia pasipo na katazo lolote.uhuru ukiwa na mashart au mipaka unaitwaje???
GreatKwamba?
Kama tatizo ni Hela Sasa hivi Dunia nzima inapitia kipindi kigumu kiuchumi.
Tunapaswa kuwa Na Subra. Mungu yupo Na anatupenda sana
Tunapaswa kumshukuru Kwa Kila Jambo.
utashi ni akili za kawaida kabisa kutambua mazingira yanayokuzunguka.
Everything happening for reason ukijua hili wala hutasumbuka na hutoweza kumchukia Mungu.Katuondolea vipenzi vyeti ametuacha na majonzi yasiyoisha
AiseeNamchukia sana
Hakuna uhuru ulio na masharti. Ukipewa masharti au mipaka inaitwa ni maamrisho au maagizo nawala sio uhuru. Uhuru maanake unafanya unavyotaka au unavyojisikia pasipo na katazo lolote.
Mungu wakati anamuumba binadamu A si anajua fika kuwa huyu mtu A nayemuumba kutokana na akili na utashi alionao, akienda duniani atakuwa ni mwizi je inawezekana vipi mtu huyu A akaja dumiani akawa tofauti na vile Mungu alivyotaraji?
2) je mtu A aliyekuja duniani akawa muovu na mtu B ambaye kaja duniani akawa mwema wanazidiana kipi kwenye vichwa vyao mpaka kila mmoja afanye chaguzi tofauti ilihali wote wameumbwa na mmoja?
Hili swali haujanijibu. je mtu A aliyekuja duniani akawa muovu na mtu B ambaye kaja duniani akawa mwema wanazidiana kipi kwenye vichwa vyao mpaka kila mmoja afanye chaguzi tofauti ilihali wote wameumbwa na mmoja?mimi nimesema utashi wa binaadamu wote ni sawa,labda mmoja awe na matatizo ya akili.
Mungu alitupa akili za kutambua mema na mabaya mara baada ya adam kula tunda,tulikabidhiwa haki hiyo ambayo haikuwa yetu.maana yake sasa hapa kila aliyechuma janga ikaanza kuhesabiwa kwamba ni kwa akili zake zote kafanya kosa husika akijua kabisa.
kwa sasa wewe ni rahisi sana kuvunja sheria ya mamlaka kwa kutojua lakini sheria za Mungu siku akili imekomaa tu zote umeshazijua.
Ina maana Mungu alipomuumba Lucifer hakujua kuwa ataharibu mpango wake mwema?mkuu kumbuka wakati Mungu anamuumba mwadamu haikuwa lengo lake mwanadamu kufa ila alimwambia utakapo kula mtu huo ni hakika utakufa.
Na mimi na wewe tunajua kabisa kuwa shetani ndio sababu ya mwanadamu kula lile tunda kwa maana yeye ndie alie washawishi hivyo ni Lucifer anapaswa kulaumiwa juu ya vifo vya wanadamu.
Kwahiyo unamaana wakati Adam wakati anaumbwa hakuwa na utambuzi wa mema na mabaya ila baada ya kula tunda ndio akapewa hiyo akili. Inamaana Mungu anabahatisha hakujua yaliyo mbele yake kuwa itatokea nini ili ampage kabisa binadamu hizo akili kabla hata ya kula tunda.Mungu alitupa akili za kutambua mema na mabaya mara baada ya adam kula tunda,tulikabidhiwa haki hiyo ambayo haikuwa yetu.maana yake sasa hapa kila aliyechuma janga ikaanza kuhesabiwa kwamba ni kwa akili zake zote kafanya kosa husika akijua kabisa.
.
Nadharia zako umeziweka kwa kuelemea upande mmoja kuonyesha kana kwamba binadamu ni kiumbe dhaifu na si kweli. Embu turudi kwenye mfano wako kwa kusema Mungu kakwambia kabisa kuna nyoka msimsogelee na akiamua kuwasogelea amewapa na uwezo wa kumwondoa huyo nyoka kwakuwapa kila aina ya silaha ya kumuua huyo nyoka, nyoka mwenyewe ni mmoja na nyie mpo wengi tena mna silaha hapo mnamwitaji mungu wa nini tena ikiwa uwezo huo kawapa mnao wenyewe
Mungu hakuzaa sisi ni viumbe vyake. Mwenyez Mungu anahuruma na viumbe vyake ndo mana anatupa nafasi ya kutubia matendo yetu na hakika ni msamehevu. Moto ni adhabu kwa wale wenye kuasi na kwenda kinyume, ukomo wa adhabu hiyo anaijua mwenyewe Muumba.Shetani ni mtoto wa MUNGU maana alimuumba, sisi ni watoto wa MUNGU maana alituumba, huu ni ugomvi wa ndugu...
Sababu zipi za msingi zinazosababisha BABA awaue watoto wote walioteleza kwa kulubuniwa na ndugu yao? Ndugu ambaye ni mmoja tu? Kwanini maelfu wafe sababu ya ndugu mmoja mkorofi aliyepewa uwezo wa ushawishi na nguvu kubwa ya ulaghai na BABA mwenyewe?
Na ukumbuke hii ni mara ya pili, ya kwanza aliua wote kwa maji, akaacha wachache sana ili wazaliane. Sasa ataua tena kwa moto wa milele, Kwann BABA anafanya hivi?
Hili swali haujanijibu. je mtu A aliyekuja duniani akawa muovu na mtu B ambaye kaja duniani akawa mwema wanazidiana kipi kwenye vichwa vyao mpaka kila mmoja afanye chaguzi tofauti ilihali wote wameumbwa na mmoja?
Kwahiyo unamaana wakati Adam wakati anaumbwa hakuwa na utambuzi wa mema na mabaya ila baada ya kula tunda ndio akapewa hiyo akili. Inamaana Mungu anabahatisha hakujua yaliyo mbele yake kuwa itatokea nini ili ampage kabisa binadamu hizo akili kabla hata ya kula tunda.