Ushawahi kuona wapi mfupa uliomshinda fisi, mbwa akauweza?? Yaani suala la Tundu Lissu, naona Wema analichukulia kama suala rahisi saana. Anaifahamu Singida vizuri au anasukumwa na uroho wa madaraka?
Hapo kwa Lissu walishaenda akina Chiligati, Kikwete, Mwigulu na wengine wengi lakini matokeo yake waliyaona. Asije akadhani mambo ya siasa ni kama yale mambo yao ya mara sijui Diamond kafanyeje, mara Zari imekuwaje. Asije tu akajikana baadae.
Huko maji ya shingo na ndo maana hata yeye mara ya kwanza aliamua kwenda kwenye viti maalumu vya chama chake, nahofia mwisho wa siku atajikana.