Wema arudi Singida kushindana na Tundu Lissu

Wema arudi Singida kushindana na Tundu Lissu

hesalieyo

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2012
Posts
378
Reaction score
416
Baada ya Wema kuukosa Ubunge, sasa amerudi rasmi Singida kumng'a Tundu Lissu. namaanisha anagombea ubunge wa kuchaguliwa na wananchi.

Tumuombee katika safari yake hii ya siasa.

Kila la kheri Sepetu.

=============


MSANII maarufu wa filamu nchini,Wema Sepetu, amemtangazia kiama mbunge wa jimbo la Singida mashariki Tundu Lissu wa CHADEMA, kwamba siku zake za ubunge zinahesabika.

Wema miss Tanzania 2006, aliyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya safari yake ya kisiasa ambayo ameianzisha baada ya kushindwa kwenye uchaguzi ubunge viti maalum (CCM) mkoa wa Singida uliofanyika hivi karibuni.

Alisema matunda ya safari yake ya kisiasa yataanza kuonekana kuanzia oktoba mwaka huu baada ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu, kwani jimbo la Singida mashariki,litakuwa mikononi mwa CCM chama tawala.

"Mimi nimerudi Singida kwa kazi maalum, nimekuja kushiriki upigaji kura za maoni CCM.Tumemchagua mgombea wetu Jonathan Njau&[HASHTAG]#8230[/HASHTAG];..tutahakikisha Njau anamgaragara Tundu Lissu",alisema Wema kwa kujiamini.

Akifafanua,alisema hivi sasa maandalizi ya kuing'oa CHADEMA jimbo la Singida mashariki,yameanza na yanaendelea vizuri.

Wema alisema kazi ya kuing'oa CHADEMA mwaka huu, itafanywa kwa ushirikiano wa karibu na wana CCM wote na kuungwa mkono na kundi la wasanii maarufu kutoka jijini Dar-es-salaam.

Kwa upande wake katibu wa CCM wilaya ya Ikungi, Aluu Segamba,amesema Wema ameonyesha amekomaa kisiasa kwa kitendo chake cha kurudi Singida mapema,licha ya kuangushwa kwenye uchaguzi wa ubunge viti maalum CCM hivi karibuni.

"Tunaendeleaa kushuhudia wana CCM wengi wanaoangushwa kwenye chaguzi mbalimbali,huwa na chuki na chama na wangine wamefikia uamuzi wa kukihama chama. Lakini Wema ndio kwanza mapenzi yake kwa chama yameimarika na sasa anaelekeza nguvu zake kulikomboa jimbo la Singida mashariki kutoka CHADEMA na kulirudisha CCM", alisema Segamba.

Chanzo:
dewjiblog.com
 
Hakuna lisilowezekana chini ya jua,na kama ameandikiwa kupata atapa na kama ameandikiwa kukosa hata aungane na Simba hapati.......
 
mleta uzi hakueleza vizuri. wema anakwenda kumsaidia mgombea ubunge kwa tiketi ya ccm jonathani njau ili amuangushe tundu lisu. ndivyo ilivyoandikwa kwenye baadhi ya mitamndao.
 
mleta uzi hakueleza vizuri. wema anakwenda kumsaidia mgombea ubunge kwa tiketi ya ccm jonathani njau ili amuangushe tundu lisu. ndivyo ilivyoandikwa kwenye baadhi ya mitamndao.

Njau yule wa DSE (aliyekuwa) hamuwezi Lissu

Alishamshindwa na hatakaa amuweze
 
Baada ya Wema kuukosa Ubunge, sasa amerudi rasmi Singida kumng'a Tundu Lissu. namaanisha anagombea ubunge wa kuchaguliwa na wananchi.

Tumuombee katika safari yake hii ya siasa.

Kila la kheri Sepetu.

Acha uongo kura za maoni zimeshapita na yeye alishiriki kura za viti maalum, sasa tuambie amagombea kwa chama gani au TLP?
 
Mleta thread hebu tuweke sawa anagombea kwa chama gani maana kule kwa Maghufuri alishakatwa ????????????????
 
Hii nchi vituko haviishi,huyo anajua kabisa hashindi ila anataka wamkumbuke hata ukuu wa wilaya,na akipewa ndio maajabu Saba ya Tz.
 
Mmmmh nachelea kuiamini hii
Juzi hapa ccm walipoga kura za.maoni kuchagua wawakilishi

Wema atarudije ilhali uchaguzi umefanyika???

Au mwamsingizia tu binti wa watu???



Baada ya Wema kuukosa Ubunge, sasa amerudi rasmi Singida kumng'a Tundu Lissu. namaanisha anagombea ubunge wa kuchaguliwa na wananchi.

Tumuombee katika safari yake hii ya siasa.

Kila la kheri Sepetu.
 
Shigongo kawaharibu! hata uandishi wenu wa kikuda kuda utadhani kuna baadhi ya topic mwalim wako wa Kiswahili aliruka!
 
Back
Top Bottom