Weka sifa ya mke umtakae hapa.!

Dam55

JF-Expert Member
Oct 8, 2015
3,626
2,000
Wiki iliyo pita niliwahoji wadada kuhusu sifa za mume, wao kwa kuwa imethibitika kuwa ni watu wasio na msimamo japo si wote, niliwataka waweke sifa kuu moja.

Sasa leo zamu yetu vidume.
Sasa kwa kuwa sisi ni vichwa na ndivyo tulivyo hilo halina ubishi hata hawa warembo wetu humu wanalijua hilo japo wengine watabisha wakipigania usawa lakini mioyoni wanakubali. Mfano Dada Yangu EMMYTA.
Hivyo sisi tutaweke sifa tatu muhimu kwasababu wao wapo chini yetu.

Karibuni muweke sifa hapa.
Na kwa wale walio oa tayari basi watuambie ni vigezo vipi walivizingatia hadi kuwapata hao wake bora walio nao.

Tukianza na mimi.
1; Awe mzuri nimpende( haijalishi rangi wala umbo, kikubwa nimpende)

2; asiwe mtu wa tamaa( kumtunza ni jukumu langu kama mwanaume, hivyo nitawajibika katika nafasi yangu)

3; aliyefunzwa maisha na familia( ajue nini maana ya kusimama kama mama wa familia na kuilea kuanzia watoto, ndugu, mumewake na mazingira yate ya familia kwa ujumla.
Japo hawezi kukamilika kwa 100% kwasababu ni binadamu)

Haya kazi kwenu vidume.
Wadada mkuje mjionee hapa.

Nawasilisha.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom