Weekend Story! The Workaholics Silence

Weekend Story! The Workaholics Silence

Wakafika akaanza kuingia Gillbert, wakati Stacy kabakia kwenye gari. Akapita ki boss, walinzi full kumsalimia. Mapokezi akamkuta mlinzi akamuuliza za kwako? Nzuri shikmoo Boss, hel hizi wakati mlinzi mkubwa kwa Gillbert basi heshima za rejareja. Gill akaitikia marahaba, vipi kazi? Mlinzi akajibu njema tu boss. Gill akajisemesha kijanja kama kupeleleza, nimewahi leo wa kwanza, nataka kuona wachlewaji usiniambie kuna binti au mwanamke kaniwahi? Moyoni ankagua kama Stacy hajamchezea picha la kumtuma shoga ake yoyote aweke chupi chooni kumuingza kingi.

Mlinzi akaabasamu hamna mmama wala madada aliekuwahi, akataka kusema kuna mkaka keshaingia ila roho ikasita manake mkaka kaja saa 10 yule, akajiongeza ukute kaja kuwanga au kufanya dawa mule ndani kujitengenezea mambo yake ya kikazi, manake kazi hizi ukiwa mwepesi hufanikiwi. Labda mgang kampa dawa au kombe la kuja kunuia sasa ofisi zingine pool ukichelewa uawanga saa ngapi watu wamejaa. Akajiongeza tu kukaa kimya. Kwanza akamtilia shaka boss huenda na yeye wale wale wa kuplizaaa kaja kufanya nini usiku huo wote? Akamjibu tu hamnaaa mtu we ndo wa kwanza boss.

Moyoni mlinzi anatetemeka mara yule kaka atokeee mbona itakuwa mambo ya aibu. Isitoshe kapita juu sasa hivi dakika 10 nyingi mpaka boss anaingia pale anamsemesha yeye anamuona anangoja lift pale haijatengamaa, kumsikia boss akamuona anakimbilia ngazi akawange fasta fasta, ukute kapewa dawa ya kuitupia kwa boss hahaaaaaaaaa, ndo atapofumwa. Akawaza wale lazima wabambane leo.

Boss akaweka finger prints akapita, kama bahati akakuta lift imetengamaa, akapanda na lift. Mlinzi akasema wale lazima wabambaneee, labda kama hawapo floor moja. Vinginevo booooom! Boss break ya kwanza chooni kwa wanawake. Akakuta choo cha kwanza kimefungwa kwa nje bila kufuli akataka kukifungua akasita huenda kibovu kimejaa mavi, akachungulia tu chini hakuona miguu na kwamba kimefungwa komeo kwa nje akajiridhisha. Akaingia cha pili hakina chupi, cha tatu akaikuta chupi kwenye kidude cha toilet paper, kama imesahaulika kabisa. Na chupi hio anaijua alimpa yeye ina sidiria yake. Akamuamini, akasikitika sanaa kumpeleka mzobe mzobe ilihali kafiwa, akajilaumu hivi kwanini hawezi kumuamini kwnini ana muhisi hisi mda wote. Akatoka nje, akagongana na Stacy akamuuliza umeikuta?

Gillbert ikabidi awe romantic ghafla manake chupi ipo kweli, basi anajisemesha achana na chupi twende tukajadili msiba. Stacy akajua ameikuta roho ikamtulia. Akamjibu acha chupi yangu bwana kabla hawajaanza kufanya usafi. Gillbert akasema uje ofisini tujadili hilo swala. Akawa kaondoka kuelekea ofisini kwake.

Huku Stacy kaona choo cha kwanza kimefungwa kaingia cha pili chupi hamna, cha 3, chupi ipo Akaikunja, akaiweka kwenye rambo, akaitia kwenye pochi. Akajisemsha duuuuuuuhhhh! Mungu mkubwa, ambariki tu yule kaka, leo nilikuw naachika. Akasikia mtu mwanaume anamsemsha nifungulieee,Akastukaaaa maana choo cha kike kile. Kidogo akimbie. Akakumbuka atakuwa yule kaka aliemtuma, akastuka zaidiiiii kumbe bado alikuwepo chooni alivoingia Gillbert. That was a close one. Akamfungulia kome kile choo cha kwanza. Yeye kweli. Akajikuta tu wanacheka wote. Wakatoka wakawa wamesimama corridor ya chooni kabla ya junction ya choo cha kike na kiume.

Stacy akamuuliza hajakuona kweli? Harris akasema nusra nusra alamanusraaaa anione. Nimeweka chupi namsikia hatua zake anakuja nikasema leooo. Nikafunga choo cha kwanza kome nje nikaingia cha pili, nikaruka juu kuingia cha kwanza chenye komeo nje nikawa nimechuchumaa juu ya sink ili miguu sionekane na kachungulia miguuu. Daaaah! Hatari sanaaa. We mwanamke umejua kuniweza na ningekuwa jana sijala mzigo roho ingeniuma sanaaa, inabidi unipe mechi ingine sio kwa mission impossible hili. Stacy akajibalaguza tutaongeaaa, usijaliii kabisaa lazima nikufikirie wewe wangu si kwa msaada huu. Asanate sanaa tutaongeaaa.

Akaelekea kwa MD kujadiliana. Confidence zikawa zimemrudi zote sasa, akajiambia ama kweli siku unayotembea uchi ndo unakutana na mkweo. Siku zote yuko commited kwa Gill, miaka yote, juzi tu kusema achepuke mara moja dno matukio yote hayo ya kumkamatisha yametokea. Arobaini yake haipo mbali. Akaingia kwa MD sasa wayaongeee ya msiba akawa hajajua atamwambia nini.

Amefika pale Gill sababu ya kuzodoka mda si mda anajitia gentlemen hakuna mfano wakati alimkokota mzobe mzobe. Akamuuliza embu nisimulie imekuwaje. Akamsimulia kuanzia kuipasua simu, dogo kuja ofisini, akamgea million 5 ajikatae na asimtafute tenaaa. Na kuja kuwasha simu namba aliompa dogo ambayo ndo aliipasua baada ya siku kama 5 na kukuta sms jana yake. Gill akamuuliza kwa hio mwili uko mochwari au? Stacy akamwambia walishazika bwana.

Gill akamwambia inabidi twende tukaonanae na huyo mtu, huwezi kuaha haya mambo hivi hivi, yatakuletea matatizo makubwaa, yule dogo ana mji wake, ana watu wake, anatakiwa akazikwe kwao, mila zifanyike, akutaniswe na ndugu zake wa ukoo wake. Asipozikwa na wazee wake atakusumbua. Stacy akaona sasa complications za Gill zshaanza. Akataka kusimplify mambo, akamwambia sasa Gill, wameshazika, msiba wame umaliza labda kutoa tu taarifa na kuanua matanga arobaini ikifika.

Gill akamuuliza "Unabishana na mimi? mimi nakupenda nakujali na naelewa hivi vitu, haviwezi kuishia hivi hivi, tunaenda huko wanatuonesha walipozika, tunafukua, tunasafirisha, anaenda kuzikwa kwenu, kwa misa na padri, na mila zote kama inatakiwa ngombe wengi au mbuzi wengi aende nao atachinjiwa. Tunafanya hii kazi mara moja kwa uhakika ili isje kusmbua huko mbele, na hio barua lazima ichukuliwe. Unajua alizikwa hata na padri au alizikwa kama ngombe tu?. Stacy akamuona kweli Gillbert ni zaidi ya mzazi wake kwa kweli. Pamoja na kwamba hajamuoa wala anaweza asimuoe ila mambo anayomfanyia na kumsaidia ni mengi mnooo, kama asingekuwepo hajui angekuwa mgeni wa nani. Akamgea ile namba iliotuma sms.

Akampigia, ikapokelewa. Hallo! Gillbert akaanza kujieleza, "Hallo, sisi ndugu wa Traves ndo tumepata ujumbe wako tunahitaji kuja kuchukua mwili tusafirishe, sasa tunaomba msaada wako ukatuoneshe kaburi alipozikwa" James akawajibu "Sawa kuna barua na mzigo mwingine aliuacha mkija tutawapa vyote." Akamwambia Stacy watumie ujumbe nyumbani kuna msiba unakuja. Akatuma sms kwa baba yake mdogo, ikabidi ajitambulishe yeye nani, mtoto wa nani manake, mda sanaa hajawatafuta ndugu zake. Akampigia, akamuelekeza unakuja usiku huo huo utafika kesho. Ba mdogo akasema sawa atawaambia watu.

Gillber akawakodi Corona kwa shughuli nzima ya mazishi na kusafirisha. Wakaenda kukutana na James. James akashangaaa kumbe ndugu wa Traves ni watu wenye uwezo mkubwa wamekuja na kampuni professional, wamejaa hela, mbona Traves alikuwa anaishi kama mbwa tu enzi za uhai wake? Mpaka akawa mwizi wa magari, au sababu alikuwa shoga ndo maana wakawa wamemtenga? Akawa haelewi. Wakafukua pale, wakatoa jeneza, wakazika mgomba na kuna mzee Gillbert alikuja nae wa kimila walie elekezwa na baba yao mdogo yupo huku Dar, akafanya mila kabla hawaja fukua, mila tena wlivofukua, kuiomba mizimu kwamba wanazika mgomba ili kaburi lischukue mtu mwingine na kwamba makosa yalitokea, akawaomba msamaha kwa kushindwa kumzika na wazee wa ukoo wake kwa kuanzia, wakafukia mgomba, kafanya mila tena. Wakawa tayari kwa msafara. Na watu wengi walikuja kumsupport Gillbert kumsindikiza mpaka Moshi. Ukiwa boss mjini hukosi support.

Wakaingia chemba Gillber, James na Stacy akawapa ile barua na ile bahasha yenye hela akawaambia million 1 na nusu walitumia kumzikia. Gillbet akasema haina shida hizo hela alishapewa marehemu kama aliziacha ndani kwake manake alitaka yeye James azipate kwa hio watamuongezea 1.5 ingine kukamilisha 5m aliyoachiwa na marehemu. James akawa anashangaaa. Wakamtumia kwenye simu. Gillbert akaichukua ile barua wakaanza kwenda Moshi kuzika. James akabakia anashangaa sanaa kwanini Traves alikuw anaishi vile wakati ndugu zake wapo vizuri sanaa. Akajiambia ushoga kitu kibaya sanaaa.

Safarini anamuuiza Stacy husomi hii barua? Stacy akamwambia siisomi, Gill anamwambia ujue marehemu hawezi kuzikwa bila hii barua kusomwa, jikaze uisomeee. Huwezi jua labda ana matakwa yake yanayotakiwa kukamilishwa kabla ya mazishia acha utoto soma hii barua. Stacy akamwambia siwezi kuisoma sababu najua alichoandikaaa. Najua atakuwa kanitupia mimi lawama zote za yeye kufeli maisha. Bora nisijue kaandika nini. Gillbert akaifungua ile bahasha na kuanza kuisoma yeye ile barua.

Akaisomaaa, akawa anafuta machozi mara adhaa. Stacy akawaza mpaka Gill amelia yatakuwa yameandikwa mazito humoo.Akapawa shauku ila akajiona hana nguvu za kuisoma. Hii kumfanyia mdogo wake proper mazishi ikawa ime easy guilty yake kidogo. Akamaliza kuisoma akairudsha kwnye bahasha na kuiweka kwenye briefcase. Stacy anmuuliza kimeandikwa nini? Gill anamwambia kama unataka somaaa. Huwzi kusomaaa basi. Akaitoa tena barua ile akachukua namba akaanza kuipiga, ikawa inasema namba unayopiga haipatikaniiii. Stacy akawaza namba ya nani? Kwanini iwemo mwenye barua ile.

Ukapita ukimyaaaa. Baadae Gill akamwambia hivi unajua kaka yako ameacha mtoto wa kiume. Stacy akastukaaaa! Mtoto? Yule si alikuwa gay? Akamwambia ndo maana inabidi usome hio barua uelewe na umjue kaka yako. STacy akashusha pumzi, kwa hio huyo mtoto yuko wapi? Gill akajibu ndo namba naipiga hii haipatikani. Na tukifika mpakani nyie mtaenda na maiti kijijini mi nitachua tax, kwenda Arusha kwenye chumba chake kuvunja, kuhesabu mali, na itu vingine ili siku ya arobaini vigawanywe kwenye ukooo. Stacy ndo akaona kweli mdogo wake kafa kweli. Maana bado ilikuwa haimuingii akilini kabisaa.

Wakafika pale, wakapoklewa vizuriii, kesho Gillbert akarudi kuungana nao msibani na wakazika hio hio kesho. Siku ya tatu wakanua Tanga. Ukoo ukaa kujadili, wakamsuta Tracy kwamba walijitenga na mdogo wake yamewafika ndo wamerudiii kwenye familia. Tracy akakaa kimya tu msiba upite. Ila moyoni akawa anajisema hana ndugu pale sio kwa waliomfanyia. Akawataarifu tu kuwa marehemu kaacha mtoto mmoja ambae hawajui alipo na mali nyingi tu. Mengine yalikuwa yajadiliwe siku ya 40. Kutokana na maneno yalioongelewa juu marehemu na tabia zake za kishoga inabidi aondoke na ngombe wengi kumuombea msamaha kwa mizimu kwa mambo yake hayo. Tracy akasema sawa nitatoa hela ngombe mpaka 40 kila wiki anatakiwa achinjiwe ngombe 3 wanaukoo wagawane wamuombee msamaha kwa mizimu. Hela ya ngombe ikatolewa. Wakaondoka kurudi DSM mpaka siku ya 40 kumaliza msiba.

Njani Stacy akawa anawaza Gill asingekuwepo sijui angefanyaje, kambeba sanaa maishani mwake, nyakati zake zote ngumu yupo bega kwa bega nae, hajawahi kumuangushaaa. Alivokumbuka juzi ali mcheat oho ikamuuma sanaa, akasema harudiii tena huo ujingaaaa. Njiani Gill akamwambia Stacy ujue Traves nimeenda kuchukua balance kwnye account yake ATM kaacha 50m utaamini? Kweli ushoga na ujambazi vinalipa. Stacy akastukaaaa. Akasema ndo maana ile 5m niliompa ilimuuma sanaa kumbe alikuwa na hela zake all he wanted was his sister. Jamniiiiiii. Akajisikia vibaya sanaaa. Akataka kuisoma ile barua akakosa ujasiri kabisaaa.

Wakarudi ofisini kuendela na kazi, Gillbert akampa zile strategy zote na action plan, Gillbert kichwa sanaa, Stacy alivo zipresent board nzima ikakubali she is worth the money anayolipwaaa. Team yake yenyewe wakakubali kuwa Stacy ni revolutionary sio degree ya chupi. Wakaona kabisaa the future of the company can never be brighter.

Siku ya 40, wakarudi Moshi, na Gill alimpeleka tenaaa, marehemu kaacha nyumba 1 Arusha na million 50 na gari 1. Kaacha na mtoto mmoja Arusha. Ikaamuliwa gari achukue bamdogo sababu ndo baba yake mlezi, nyumba tafutwe mwanae apewe, million 20 wagawane ndugu wote, na hizo 30 achukue Stacy kumlea yule mtoto na kumsomesha. Arobaini ikaisha salamaaa.

Wakiwa wamerudi Stacy anawaza akamtafutie wapi yule mtoto, Gill akamwambia nishampata, huko Arusha. Ile namba nilienda Voda nikatumia connection zangu, nikampata huyo mwanamke picha yake, na mnara alikuwa anatumia kuwasiliana ambao ni Unga limited. Nikaenda kumsaka na picha yake, ni punda huyo dada na addict, akaniambia hata Traves alikuwa anatumia unga sanaa na amesafrisha sanaa, walisafirisha wote. Mtoto ukimuona huulizi wamefanana balaa, copy. Kana miaka 2. Akagoma kuachia mtoto na anamlea mazingira hatarishi sanaa. Tumejadiliana kakubali million 20 ndo aachie mtoto. Ila alikuwa anaachia kwa shida sanaa na uteja wake ila unaona kabisaa anampenda mwanae, na kumtoa anaumia sanaaa. Kasema hio pesa akipokea atamtoa basi tu manake kwa kazi yake anaweza kufungwa mda wowote, nchi yoyote.

Sasa mtoto mimi Gill kwa nilivoona malezi aliokulia na afya yake ilivo na tabu amabazo amesha pitia wakimchukua tampeleka kwa Marie amlee, atamwambia kamu adopt na anajua Marrie ana upendo na atamlea vizuri sanaa, na takuwa mtu huko mbele. Stacy akastukaaaa! Atampeleka kwa Marrie???????????? Mxiuuuuuuuuuu! Sasa hayo mazooooooea. Akagoma mtoto hakuna kupelekwa kwa Marrie yeye ni shangazi yake na atamlea yeye. Alishindwa kuishi inavotakiwa na kaka yake ila uncle wake atamlea mwenywe. Ukatokea majibizano makali sanaaaa baina yao. Pakageuka alshabab, ila hitimisho Gill kasimamia msimamo wake mtoto atapelekwa kwa Marrie mkewe.

Stacy akawa hajakubaliana na hilo swala hata kidogo, ila Gill ndo baba yake ndo mama yake, atafanyajeeee. Wakaachana hawasemeshani kabisaaaa. Akarudi nyumbani akakumbuka hajaingia MP miezi 2. Akastukaaaa, msiba ulimtinga na karuka sindano miezi 2. Na kauza mechi kavu kavu. Akachanganyikiwaa. Akaenda kununua kipimo. Akapima Kitu na box! She wa pregnant. Akaona hata akaenda hospital akaambiwa habai njemaa kabisaa wako wawili kutu kina mweiz na siku kadhaa. Hesabu zikaja siku ile ile alio lala nao wote wa 2 yule kaka wa ofisini na Gillbert. Akawa hana uhakika who is who manake alilaa nao tofauti ya masaa tu.

Ngachokaaaaaaaaaaaaa!

ITENDELEA SAA 2 USIKU.
 
Uwiii mbavu zangu Mie Nimeishia hapa kwenye kelele za harry za nifunguliee ngoja nicheke kwanza lol si utamu wa lara1jfstorues mweh! Khakhakhaaaaaa
 
Sasa Traves kampataje huyo mtoto wakati ni shogga? Huenda hakuwa shogga maskini ya Mungu. Duuuh! Kweli wewe n kubwa la maadui.
 
Duh stancy stancy stancyyyyyyy hapo lazima jicho limtoke hapo kitu mbaya sana hio usiombe ikukute uvushe siku Halafu mambo hayaeleweki dah stancyyyyyyy
 
Duh stancy stancy stancyyyyyyy hapo lazima jicho limtoke hapo kitu mbaya sana hio usiombe ikukute uvushe siku Halafu mambo hayaeleweki dah stancyyyyyyy
Umeona eheeee akili ajipi kabisa bora awe 1 wawili on the same time lazima udate
 
daah pole ya stacy kama mimba si ya gill maana si kwa wivu wa gill akijua alimegewa
 
Nyengne sa ngap Lara nikatafute na kinywaj tunywe
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom