The devil wants his hell back!
Ndugu wasomaji najua bado mna hasira na mimi Msomali wenu, mnaniona bandiduuu tu, mnaniona baba ubaya tu, mnaniona mtoto Iddi of which i deserve every part of the anger. Msomali gaidii. I was not planning to come back anytime sooner, ila swala la kuambiwa kuna damu yangu huku liliniharakisha kurudiii. Nilikuwa na mpango wa kurudi baada ya kukamilisha vitu flani flani.
Nilijua kumpata mtoto haitakuwa issue ya siku 1 au 2 huenda hata ingechukua miaka. So na mimi sikuwa na haraka. Its not like she was gonna forget everything and be happy to see me after everything. And i was gonna fight for my baby anyway, hata ikibidi kwenda mahakamani.
Life always makes you to choose between the two things you love most. Always! Life made me choose between my future and the woman i love. And i am sorry to say i dont regret choosing my future. There is always a price to pay and Sally was that price. We all have to make sacrifises to get what we want. Maisha haya bila kutoa kafara kitu unachkipenda sanaa hutokiiii ngooo. Kama huniamini we acha kitu unachokipenda ingia agano na maisha kwamba sababu umeacha kitu flani basi ulimwengu ukufikirie kukufidia. Utafurahi na roho yako. Even in the darkest times i reminded the universe i had sacrfised my love and happiness just to persue greatness it has to make me great. It just has. And it made me greater than my wildest dreams. Milango ilifungukaa, opportunity zilipatikana.
Well i met Sally when i had nothing at all, ila msichojua ndugu wasomaji i might have been poor kwenye mali, ila i had a vision. Sally was smart but not half smarter than me. Nimekaa na kina Sally, Dee, Chriss, Craig i studdied their game and i concluded it was small time. Sawa wanapata pesa ya mboga, maybe kununua old edition second hand japanese cars, kujenga vigorofa vya 200 millions, but lets face it they were going no where in life.
I had bigger dreams, bigger plans, bigger ambitions. And i was gonna persue them either way. I wanted to have multiple homes in multiple countries, i wanted money to work for me, sio kama Sally lazima aamke aende dukani au akapoint ronya ndo aishi. I wanted to drive brand new cars. Wear designer staffs. I wanted to live not survive.
Nilimshirikisha Sally huu mpango once na hakuelewa kitu, she couldnt just get it why i was not happy na kuuza simu. Na sikutaka kumshawishi sanaa cause i knew she was not gifted with my vision. To live my dream i had to go America first. All influential Africans at a point lived in America or UK. Ilipotokea chance la dogo kuolewa na wasomali wale kidogo wanajiweza nikasema it is now or never.
Lets face it, safari ya kutafuta maisha haitaki kadhiaaa, familia wala distractions zozote. Watu wengi wanao oa mapemaa au kuzaa mapema they usually go no where in life. Familia inakubanaaa sanaaa. Huwezi kufanya lolote wala kusapotiwa na yoyote sana sana inakulazimu ukae utunze familia. Na safari ya kutafuta maisha inataka focus, determination, ambition na dedication vya hali ya juu.
Mimi ni msomaliii, na kuwa msomali ni asset kubwa sanaa, it gives you acess to unlimited opportunities kwa wasomali wenzio. Ukiwa na wazo, wasomali wataweka pesaa, ukitaka msaada wowote watakupa just because ni msomali mwenzao. Dont get me wrong kwamba hata ukiwa mjinga mjinga wanaweka tu hela nooo. Ila ukiwa na idea zenye akili they will belive in you and put money to see it mature.
Nimefika US, nikawa nakaa kwa shemeji yangu. Mtu peace sanaaa. Nikaji enrole short course kama 6 kwa mpigo. Raha ya huku kusoma sio bei, haswaa hizi public instituions. Niliamua kusoma course ya Tourism ya wiki 4, inayohusu jinsi ya kumarket tourism, ku draft proposal, kufanya costing. Na kila kitu. Mzungu mzungu tu. I learned so much. Nikasoma course ya madini, jinsi ya kupima grade za madini, kukata madini na basics tu za kujua biashara ya madini. Nikasoma na course ya business adminstration, na basic IT. Miezi mi 3 nasoma tuuu.
Mdogo wangu akawa hanielewi kabisaaa, ananiambia shemeji yako anataka kukufanyia mpango upate kazi za kufanya, huwezi kuishi hapa unasoma soma tu. Nikamwambia mi sio mkaaji hapa, napitaaaa tu. Miezi mi 3 ilipoisha, nikarudi kwanza nyumbani Kenya, Nairobi. Nikaomba kazi kwenye tours kubwa nairobi, sasa sababu nilitoka Us wakanikubalia fastaaa.
Nikiwa pale nikajifunzaa basics, jinsi ya kupata permits, na namna ya kumanuvaa kwenye hio game. Nikausoma mchezo kila kinachotakiwaaa. Nilifanya mwezi tu, nikapata network ya kutosha na kuresign. Nikakaa mezani na wasomali kutoa partnerships tunaanzisha tours. Sasa kuna machali rika langu ila wazee wao wana pesa ndefuuu, ndo wakaniunga mkono. Tukauza shares mimi 60, wao 20, 20. Mimi nilikuwa na hela za mahari, na hela zingine nilifanya fanya vibarua USA, na niliuza sanaa vitu ebay na etsy, biashara ya sally! Nikakodi ofisi ndogo tu, wale machalii mmoja wana kampuni ya usafirishaji, tukakibaliana wageni wakija tutakuwa tuna lease fleet kwao kwa bei ndogo na kulipa ni baada ya kulipwa.
Nikaa chini na kuanza kuandika proposal zilizoenda shuleee, sasa ile course ilikuwa makini sanaa, inakuelekeza likely customers, associations za watalii, exhibitions, membership clubs, na sehemu za kuwanasa wazungu, jinsi ya ku compile economic packages, za safari nzima. Nimepanga na hotel kila kitu, nationa parks, game reserves, fisheries. Kuanzia Nairobi mpaka Lamu. Nimemaliza ku draft nikaanza ku email hizi associations. Nyingi nilikiwa member kitu ambacho wa South wengi wanakifanya ila wabongo na wa kenya bado sanaa. Nika market zile packages zangu. Website iko mahala pake. Bookings zikaanza kumwagikaaa. Sina hata tour guide mmoja. Ofis yenyewe mi ndo secretary, ndo boss, ndo mkoroga chai.
Demand ikawa kubwa kinomaa, mpaka wazee wa wale share holders wenzangu wakaona this is seriou money. Kwanini nipate 60% wakataka kuleta tamaa. Tukakaa tena mezani, nikawakaziaaa, wakakubali na hio 20% wakatoa fleet kama tulivokubaliana. Uzuri watalii wanalipa nusu kabla ya kuja na nusu wakifika. So working capital ilipatikana. Tulifanya kaziiii. Kaziii ilifanyikaaa sio ya kitoto. Tours za nairobi zilishangaa ila kusikia Hussein mwenyewe msomali wakajua tu sekta imevamiwaa ila wafanyaje sasa. Utalii biashara ya msimuuu. Na msimu ukapitaaa. Nikawa pesa nishapata ila ndo mpaka msimu ujao na kama nilivowaambia i wanted to own multiple homes.
Nikaingia Arusha na kufungua kwanza ofisi ya tours. Ili msimu ujao niwe babu kubwa zaidi. Nikaanza kustudy biashara ya maweee. Nikaenda mereranii, matombo wanakochimba rubby, shinyanga kwenye almasi. Nika study bei za wachimbaji wadogo, nikarudi tena USA maana dogo alikuwa ana mimba, afu inamsumbuaaa. Nikafanya na course ya mineral brooker and marketing na kufanya mtihani na kuwa certified mineral brooker. Nikawa nishajua bei za soko la dunia ziko vipi, uuze wapi usitapeliwe. Trick zotr za business nikazisomaa. Nikarudi bongo na kuweka pesa yooote kwenye rubby na saphire. Ambazo nilizi smuggle USA si mnajua mi msomali na smaggling is our birth mark.
Pesa ilipatikanaaa sio ndogo. Na niliuza kwenye black market. Sikuuza njia zinazotakiwa. Nikarudi kufungua kampuni kabisaaa ya kununua na kuuza madini, vibali vyote nililipia, nikaiita Mogadishu Germs. Mi ndo CEO, nikampa na mdogo wangu shares na shemeji yangu shares, na mtoto wa Eva kwa niaba ya mume wa Eva. Na nikafungua kampuni zingine ya utalii Mozambique na South Africa.
Nakutana na Winnie, naenda kwenye tarde fairs Dubai, kumarket Tourism package ya uwindajii, maana nishakodisha vitalu vya kuwindia kwa tours yangu ya Arusha. Nimeenda kukutana na ma mwinyiii wa Dubai waje wawindeee. Na nikatembelea na vyuo vyenyewe Dubai ku market packages za colledge students kwa vyuona associations za wanafunzi, membership clubs. Nilipata biasharaaa sio kidogo.
Nikaenda na London kuwauzia biashara ya utalii kwa English people wenyewe wenye pesa ndefuuu. Kama kawaida yangu, na deal na associations, nawapa comission wao wana comvise member zao. Kama ni colldge wale viongozi nawapa free of charge package kama wakiniletea wanafunzi kadhaaa. Si mnajua dunia inaenda nipe nikupeee. Viongozi wagumu wa his clubs nawaalika na familia zao bureee nawapa goodtime za hatari wenyewe wanajiongezaa. Inshort hii business ya utalii nilishindikanaaa. Kulikuwa na over subscroption mpaka nafunga website sipokei tena watejaaa.
All this was impossible to pull. Nimelala ofisini si mara moja au 2. Nilikuwa busy msisikie. Sally nilimiss sanaa, ila i had bigger purpose. Na ukweli huu ubusy kati kati sikuwa na mwanamke permanent sikuwezaa, nilikuwa chapa ilaleee. Akija mtalii mzuriii kanielewa najipigiaaa siku 2 au 3 imetokaaa. Nikikutana na mdada mzuri kwenye kufatilia vibali akitaka show nampa mambo. Marekani nako nilikutana na wadada nikajilia. Uzuri wazungu haya mambo kwao sio deniiii. Nimekupaa mwili wangu sijui nini. Ni good times baaas. Just the way i liked it for now.
Bongo nimerudi kwanza kufatilia swala la mtoto kwa kina pili kusimamisha business ya madini. Maana yalikuwa hayapatikani kabisaaa. Afu operating cost ni kubwa sanaa. So huu mda kabla ya season ningeutumia kudai mtoto na kusimamia kampuni yangu. Nimefika bongo, nikachukua appartment Masaki. Nikaanza kumtonhoza Sally kwenye meseji.
Alinitukana mitusii si ya nchi hii. Nikawa namuomba tuonane tuongeee, akasema hana la kuongea na mimi. Nikaamua niibuke kwake bila taarifa. Alikiwepo mtoto akamkimbiza chumbani. Katika maongezi akasema mtoto sio wangu wala nini wala nisijisumbue. Nikamwambia watu wanasema msomali. Akaniuliza msomali uko peke yako mjini? Nilitembea na mume wa Eva nae si msomalii pia. Looooohhh! Nyieeee. Uadui uaduiiii. Nikaaga na kundoka.
Nikaja siku nyingine hakuwepo. Ana wasichana wawili. Nikawaomba mtoto wanioneshe, wakagomaaa kabisaaa. Nikaongea kwa herufi kubwa, nikatoa kibunda cha million. Wakaangaliana. Yule ambae inaonesha ana mtunza mtoto akagoma, mwenzie akamuita chember, anamwambia tuchukue pesaa kwani dada atajua? Labda wewe umwambie. Mwenzie akasema anaonekana anzo aongezeeee. Pesa gani ile. Mwenzie mjanja hatariii. Wakarudi wakakuta nimejiongeza bunda 3 jumla million 3. Wakaangaliana tenaaa. Yule mjanja akauliza bei gani hio? Nikamwambia 3 millioni. Akasema ongeza moja, tugawane 2, kila mtu mtoto tunakuonesha, hata ukitaka kupiga nae selfie poaaa tu, hata ukitaka tukupige nae picha oyaaa oyaaa tu. Nikaenda kwenye gari nikaongeza.
Wakanipa mtoto. Dogo hanitakiiii hanitakiiii kama anajua mzee wake nimemfanyia mama mtu ujasusiii. Kwenye gari nilikuwa nimekuja na dereva nikampigia njoo umwone mwanangu. Akaja. Dereva kumbeba anamchekeaaaa kiroho safi. Nikimshika mimi ndo kesi ya jinai analia mpaka anashikwa kwikwi. Kina dada hawana habari wanahesabu pesa tu. Hata ningeamua kumuiba wangesikia mngurumo wa gari tu. Kila nikijathidi kumbeba hanitakiii. Side dereva akasema au unajanaba boss embu nawa mikono. Wapiiii.
Mara tukasikia mtu anatusemesha, mtoto anajua ufilaji ulimfanyia mama mtu, na hawezi kukutaka hata kidogoo, hata uoge na detto uchanganye na Ommo. Sauti tu nikajua ni mama Sally. Bibi ana matusi sio kidogooo. Nikajikosha shikamoo mama. Cha kwanza akapora mtoto, na kumuita dada. Wakaja wanatetemeka. Akauliza mnampa mtoto huyu mnamjua. Mtoto analia nyie hamstukiii? Mtakuja kuwapa mashetani mtoto. Hapo wanamuomba msamaha hatariii. Akakaza kawapa nini mpaka mmempa mtoto? Wakasema tu katupa million 4. Bibi akatabasamu, akasema clearly na mimi miilion zangu zisome kwenye simu lasivo nauza CD kwa mama mtoto na patachimbika hapaaa. Nikasema tu sawa mama.
Nikaaga na side na tuondoke, akanikumbusha tu zisiposomaaa leo hii taarifa zinafikaaa. Nilimuelewa sawa sawiaaa. Nika msort mama mkwe. Pesa mwanaharamuuu baada ya kulipwa ananiambia weekend mtoto yupo kwangu ukitaka kumuona wewe njoo tu pochi yako. Jamaniii. Kwani wewe si baba yake inabidi uwe unakuja kila weekend, mtoto akujue. Yote hio kutengeneza mazingira ya pesa. Ashanigeuza mtaji. Mtoto wangu mwenyewe kwanini nimuone kwa pesa.
Nikaenda kumuona kwa mama yake kama mara 2, ila roho yangu haikiridhika, i wanted to be in my daughters life every facking day. Sally was not making it easy for me. Hataki kuonana na mimi. Na nikifosi kuonana anakua mchungu kama shubiriiii. Hataki kunisikiliza wala kunionaaa. Hatakiii hatakii. She complately shut me out of her life. Utasema sijui nilimfanyia kosa gani labda kumla kibogaaa. Heheheee! Hata kama anacheka akiniona ana nunaaa hapo hapo. It was impossible mimi kuzungumza naye kiutu uzimaa.
Haniuliziiii niko wapi, nafanya nini. Aliacha kuongea na Lidya kwa kushauri tu maybe anisikilizena kuanza kunituhumu natembea na Lidya akamwambia hadi mume wa Lidya alikuta sms za Lkdya kwenye simu yangu vitu vya uongo uongo kutoa funzo kali kwa yeyote atakae nishobokea, ajue yeye Sally hana mipaka katika kumsulubu bila hurumaaa.
Nikawa sina jinsi, nikaenda mahakamani kudai mwanangu. Nilianza ustawi wa jamii kaitwa mara hata 10, hajaaa, anasema hanijui, kwanza hajazaaa, anashangaaa mtoto nae mdai ni yupi? Walivoona anawapasua vichwa wakanipa go ahead nifungue kesi ya kudai visitation rights na kumfosi kutambulika kama baba mzazi wa mtoto.
Wito wa kuitwa mahakamani alitakiwa aupeleke lawyer wangu, ila namjiaa angemtukanaa sanaa, na lawyer angemfungulia kesi ya jinai na tungezidi kuwa maadui. Nikaamua nipeleke mwenyewe. Nagonga anatoka D na taulo. Jamaniiiiii! Dogo ana miezi 8 tu ashaanza kupigwa miti, tena humo humo anamo lala mwanangu. Si ndo kumbemenda mtoto. Nilichukiaaa sanaa, pamoja na ya mtoto na wivu ulichangiaaa kiasi kikubwaaa. Na kama karudiana na Dee shughuli ilikuwa pevuuu. Nikapanic.
Nikamtupia ile mikaratsiiii. Basi alivo mnafiki, anajifanya haelewi nilicbopanic nini, anataka kunipa hug! Yo Hussein!long time no see, whatsup man? Nikasogea pembeni kumkwepaa? Anajifanya kushangaa "Its like that my boy?" Nikamjibu tu yeah! Akaokota zile karatasi na kuanza kuzisomaaa! Si baba wa kambo lazima awe na la kuongezaaa.
Anaa jifanya kuongea taratibu Sally asiskie ananipa ushauri, listen man! Why all this? Huyu si mzazi mwenzio mzungumze tu basi. Mahakama za nini? " Nikamwambia hayakuhusuuu mpe muhusikaaa. Last time i checked ulikuwa na mke na mtoto, mwanao hajakutosha ukaona uje umbemende mwanagu" It was a bit extra ila nilishindwa kujizuia. Likamuingia.
Akapanic! Akarudisha! Last time i checked ulikuwa umetelekeza Sally na mimba yake. Quit the best daddy attitude, mpaka njia tumefungua sisi, labor mkono nilikusaidia kumshikaa, nimelea mpaka leo. So boy show me some respect, i stood up for you"
Hapo ndo uvumilivu uliponishinda na kuanza kupiganaaaa na Dee. Tulizichapaaaa kavuuu kavuuu. Vunja vunja vituuu. Sally hatoki ndani. Majirani wakaanza kujaaa. Nikampora taulo kumuanika kibamia chake bahati ndani alikuwa na boxer. Pigana piganaaa. Watu wakaamuliaaa kututenganishaa. Dee akarudi ndani, nikamfataaa. Lengo langu Dee aondoke na yeye. Haiwezekani tupigane afu akakandwe kandwe na Sally na kumkumbatia kumbatia mwanangu usiku kucha weeee. Ngumi upyaaa.
Mwisho ikaamuliwa Dee aondoke na mimi niondoke hapo baba Sally kaja. Hapo sawaaa. Nimefika home mwili wote unaumaaaa. Nikaanza kuisaka namba ya Pendo mke wa Dee ilikuwa haina namna lazima tukae chini tuyajenge.
ITAENDELEA KESHO.