Weekend Story! Glory Be To God!

Weekend Story! Glory Be To God!

Kosa la Defence Bao!

Hakuna mtu aliekiwa anamsubiria mtoto wa Sally kwa hamuuu kama mimi Dee! Utasema mke wangu ndo alikuwa mjamzito. Hapo kati Tonny alinisumbuaaa jamaniii! Alijua kunisumbuaaa kichwa yuleee mpuuzi, khaaaa, khaaaaa acheni tu ndugu wasomaji.

Alikuwa ananibanaaa kwenye korodani sina pa kuhemea. Bora angefanya ligi ya man to man asingeweza kunishinda ila alikuwa analeta umama na mambo ya kike kike kwenye ligi mradi tu kunimalizaaa. Yaaani! Mambo ya umama si kitoto. Na alikuwa amenipaniaaa.

Sawa wote tunamzengea Sally ila wanaume tunatakiwa tuwe na mipakaaa. Sio kuleteana compeee za kike. Unaweza kuta kuna ka function, akiona tu niko na Sally lazima anyeee aseee yule chalii sio. Utasikia "Dee mkeo anasikia baridiii, mwanao leo kakuona mwisho saa ngapi? We mume wa mtu haipendezi kukaa nje mpaka sahizi" Mambo ya umama mama mtupuuu. Sasa msomaji kauli kama hizo za kike unadhani mi najibu nini? Kwamba sina mke? Au sio mume wa mtu. Namtizamaa tu anavojiaibishaaa.

Mwanzo na mimi nilimletea ligiii sio ya kitoto. Yeye hela hanaa, afu mi ninazoo. Kumkomeshaaa mi nilikiwa nasimamia hio hio fact atampa nini Sally mbwa kachoka yule, anaacha kupambana na hali yake anakomalia wanawake wa mjini kina Sally.

Nikimuona naanzisha mazungumzo flani amaizing ambayo labda level za mume wa Lidya hivi, Chriss, na watu amazing kama hao. Nazungumzia Car Rallies sababu wote wa 3 tuna own sporting gears, sio za bei kubwaaa, visubaru tu ndugu msomaji roho isikutoke. Naongelea magari sio usafiriiii. Najua yeye mtumishi tena kijakazi wa kumbebea boss mikoba, level hizi za entrepreneurs hagusiiikabisaa tunaziweza wanaume wa shoka.

Msimuonee hurumaaa, mgumu yule kama pakaaa, ana roho 9, hana sporting gear ila Rally zote hakosiii. Anakuja na Chriss. Mwanaume kujikomba kwa mwanaume mwenzio kiasi hiko haipendeziii kabisaa, ila yumooo. Ishu ya magari maongezi yake kama Baba Winny. Atatafutiza vi article cya kupondea hio edition ya gari kama mtu vile.

Na alikuwa ana cpunter attack sio kidogo. Mda mwingine anatumia hizo hizo risasi zangu kunimaliza mwenyewe. Kauli anayoipenda ni "Mwisho wa siku wote tuko hapa hapa tinakunywa bia, we una vote hivo mi sina chochote yet mwisho wa yote wote tuko hapa hapa isint God amaizing" Na nyingine anayoipenda "Sawa wewe una vyote ila ukinya yananuka vile vile siajabu kushinda hata yangu" Hahahaaaaa! Mxiuuuuu.

Siku alionikeraaa kuliko zote ni siku ya jumapili nakumbukaaa. Nilishaamua kujitoa tu akili nimvishe Sally pete. Ilikuwa birthday yangu. Nikajua hawezi kukataaa mbele za watu. Lengo ni kwamba mke wangu akija kusikia nimemvisha mtu pete labda atasusaaa aondoke mwenyewe. Si mnajua mtu mwenye visaaa ndo mimi.

At this stage nishaongea na mke wangu nimgaie hata mali tuachane kiroho safi kagomaaaa kabisaaa. Anadai anajua nimelogwaa atamuomba Mungu wake iko siku atamsikia. Kuachana hakupooo. Labda mimi nimuache yeye. Sasa hapo ndo paliponitia simanzi kweli kweli. Maana pamoja na yote sitaki kuonekana mkoraaa nimetelekeza familia. Yaani nimetumia all diplomatic mediation and abtration kukubaliana na huyu mwanamke kagomaaa. Na anavosema nikiondoka niondoke jumlaaa familia atalea mwenyewe. Nikawa nipo kama mfungwa huru. Anachosimamia yeye huwezi kumpenda mtoto wangu na kunichukia mama ake. We ukiamua kunyea kambi nyea jumlaaa sio kubeep.

Sikukubaliana na ishu ya kuspend the rest of my life unhappy sababu ya mistakes i made in the past. Na mimi nikaamua kufanya visa. Yani na mke wangu nyumba ikageuka uwanja wa vita. Visa juu ya visaaa. Ndo nikaamua tu, it just came in my mind and i did it kwamba namvalisha pete hivo hivo kwani nani ananidai? Nikawashirikisha kina Chriss tu na mume wa Lidya. Na uhakika aliemwa!bia Chriss ni Tonny.

Nikawa nafanya sherehe ya kimya kimyaaa, watu wachache tu, marafiki nikawaalika. Japo watu wengi hawa ku approve my actions ila its not like i needed any approval anyway. Some hawakujaaa sio kwamba ni mashost na Pendo or something ila basi tu it was against their principle.

Tonny alivonyapia nyapia akanifata na kuniambia sio poa! Nikamwambia watch me! Analalamika tu, nikamwambia its a FREE COUNTRY, stop me if you can. Bwana weee kumbe nikawa nimempa go ahead.

Party iko kati kati, wakaja Pendo, mwanangu, mama yangu, mama Pendo na baba Pendo waone kama kweli nitafanya niliofanya. Hapakutoshaaa. Ikabidi nikae na Mc chemba na kubadili game plan. Ni mu acknowledge mke wangu na wenye sherehe yao wazee.

Umama aliuendeleza through out mimba. Mpaka nikaanza kuamini yeye ndo baba, naweza ku!wambia Sally nimekumiss yeye akatia "Mkeo hio taarifa anayo? Kama una miss wanawake wengine? " Basi wanawake wanamuunga mkono hatariiii. Utasema sijui kaongea point gani nyama yuleee.

Siku ameenda kujifungua sikusumbuka maana toto lingekuwa lake angefanya umama sijui wa aina gani. Napata sms usikuu toto somaliiii. Weeee! Mbona niliamka saa 8 hio nikaogaaa na kwenda disco kusherekea na kucheza Azontooo. Aaaaaaaaaah! Yaaaani acheniiii tu. Niliogoma kiwakopesha mchana niliwakopesha woteee kwa furaha tu.

Nikajua tu zama zake zimekwishaaa. Alinishikia bango sanaa mimi na mtoto sijui nini haya sasakamaSally nae ana mtoto. Yeye ndo mgumba peke yake. Play date hazimuhusu kabisaaa, birthday nazo atakuwa anapiga dash kama kawaida. Inshort the award has outgrown the competitor. Woyoooo woyooooo.

Sio viziriii, ila i couldnt resist kumpigia simu Tonny kumdhihaki tu. Na hakupokeaaa hio simu yangu kabisaaa. Nyamaffff! Mi hospital nikarnda kiroho safiiii. Huu mda defence Tonny alikiwa anataka kujipanga mi ndo nautumia kufunga goli la hattrick!

Nothing serious just the normal done in extra ordinary way. Kila asubuhi lazima fresh roses ziende hospital, na mtip na nurse kabisaa ile verse isitoke mle ndani, kadi ya kishkaji anas hizo zonakuja kwa hisani ya baba la baba Dee. Afu mi mke wangu si ashazaa so haya mambo naajua kinomaaa.

Nikajua mtoto hana nguo, nikajiongeza fasta fastaaa, only the best quality, pure cotton. And nobody thought about it kabla yangu. Si mnajua wabongo hawanunui vitu mpaka mtoto azaliwe. Nikajiongeza kumnunulia stroller moja stress sana! Kila mtu ana admire. Na mwenyewe alishukuru.

Alivoanza kupona tu sikujikawizaaa kabisaa kitangaza niaaa. Akawa ahana uhakika na mimi nikamwambia ujueulivonifanyia mimi sio vizuri kuninyima nafasi sababu ya mtoto. Haya sasa n wewe umezaa unaujua uchungu wa mtoto vizuri sanaa je upate mwanaume unaempenda afu akushikie bango inakuwaje kuhusu huyu mtoto as if umeyapanga haya yote yatokee utajisikiaje?

Ulikosea sanaa kunihukumu mimi kwa vitu vilivotokea kabla na kuvichukulia kiwepesi wepesiii tu. Ila mimi sijamind wala nini. Sasa wote tuna watoto cha kufanya tuoane tuzae mtoto mmoja tumemaliza kazi. We utadeal na msomali, mi nitadeal na Pendo.

Akasema nipe mda kwanzaaa, maana dunia inavonipenyaaa bila KY wala Mate sitopenda kufanya maamuzi yatakayo nipeleka chaka kuliko hili situ la equator nilimo maana sio kwa bakora hizi na mijeledi dunia inayonichapa. Nipe mdaaa. Mi nikamwambia usiwazeee, mda nitakupaaa unaohitajiii. Ila iingie kwenye rekodi za maktaba nishatangaza niaaa. Sio baadae anarudi Tonny kiholela holela patachimbikaaaa hapa. Akawa anachekaaa tu.

Stress zilimzeesha! Alizeeka as if hakupanga afu ikawa kama pigo kwake. Pendo alisikitika sanaa mtoto sio wa Tonny. Mnoo mnooo. Utase!a ana undugu na Tonny. Mxiuuuuu! Upambe tu. Mi kwa kujua ana stress nikawa sina mkono wa birikaaaa.

Kumtongoza mzazi sio kazi sanaaa kama kumtongoza msichanaa. Mzazi ni kama ngombe mwenye ndama tu. Ukimbeba ndama ngombe atakufata kokote unapoendaa. Simple like that. Mi ndo nikawa nampenda yule mtoto kama baba mzazi. Na Sally is not a good mother. Hana patience. Ni yule mtu ana mambo mengiiiiii so anaona dogo kama anambanaaa.

Kuna siku kapiga simu usiku, mwanao halali huki, niko na Feisal tu, wote na dada tumechoka fanya uje umfanyie maarifa. Mie tenaaa, father of the year! Ukiacha mke wangu kuzaa pia niliwalea wadogo zangu wa 2 so i am good with babies. Nimefika pale hajamtoa gas, nikamtoa dogo gesi, aka burp mara 2 usingiziii.

Sally mkaliiii mpaka mda mwingine anakuwa mkatili. Mtoto akilia mara moja atambe!beleza kwa upendo, akigoma si mnajua venye mda mwingine vina visaa tu vinakuwa havinyamaziii. Anaanza ku loose temper. Anaweza kumuacha kitandani akaenda kukaa njee, alie tani yake akichoka atanyamaza mwenyewe. Mpaka nikahisi hasira za msomali anammalizia mtoto.

Nikaanza kumshauri aende counceling, she was loosing it. Sasa namshaurije bila kunyosolewaaa. Sio mtu wa kumuingia kichwa kichwaa. Siku nimeanzaa tu akahamaki so you are insinuating i am a bad mother? Najitetea. Nikaambiwa you are no longer welcome in my house. You are too judgy, kwanza mkeo kakushindaa mwanao kakushinda who are you to tell me how to raise my daughter. Ilikuwa balaaa.

Nikaenda kumsemea kwa mama yake. Mama yake anammudu na ndo kiboko yake. Ugaidi wake wote hawezi kumjibu mama yake. Baba anamjibu kunya kama kawaida ila mama atakaa kimyaaa tu. Mama yake akamchanaa, una hasiraaa za nini? Bwana kila mtu alikwambia sio bwana yulee, ukajitia nundaa sasa maisha yamekula Tigo, hasira za nini kwa mjukuu wangu, si raha zenu ndo zimemleta duniani? Ulitumwaa uzae. Badilikaaa.

Nikiona au hata kuhisiii unamfanyia huyu mjukuu mahasira hasira nampiga baba ake aje adai custody ya mwanae. Weee ! Mama gaidi lileee, Sally akasome upyaa chekechea. Na anamjua atafanya kweli. Ndo kuwa kavurugwa zaidi. Huku bibi kahamia kumsimamiaaa, sio kumsaidiaaa kumsupervise tu malezi yake.

Akilalamika anaambiwa keleleee, si umetaka kuzaaa, mi niliwazaa wa 3 nililea mwenyeweee hio ndo kwanza asubuhiii. Bado mchana bado jioni zinakuja huko. Akazidi kukaukaaa. Nikamhurumia kuna kadada kalisoma nursing hakana kazi,nikaongea nacho kama kataweza kulea nikape pesa kidogo, kakasema kataweza. Nikakapeleka kwanza course Nairobi ya u nanny ya 30 days maana bila hivo wiki tu angetimuliwaa.

Na hasira zote, Sally msafiii, afu hapendi mambo loko loko kwenye malezi sijui mafuta ya nazi, mara mtoto kajojo unampa mafuta, mambo yetu wa swaziii. Kimerudi kule nika ka jazaa, wewe mlele mwanae vizuri atakutoa kimaisha kawaroa watu kibaooo. Give it your all. Ana kisirani flani ila ni mtu mzuriii tu ukimzoeaaa. Dada njaa imembana akakubali.

Kumpeleka Sally akawaanaleta nyodo nyodo haitajii, namwambia mimi nitamlipa kama ishu hela. Akawa anadengua tu. Mtoto akalia, dada yupo shapuu, kanawa mikono fastaaa na sabuni akamchukua mtoto, Sally akamuwakia nani kakwambia ushike mtoto wangu? Dada hajapanick akambembelezaaa, akachukua vifaa akambadilisha professional.

Sally akauliza kwani mshahara bei gani? Nikamwambia 200,000 maongezi yapo. Akasema sawa si unamlipa wewe, nikasema ndio ila ndo nifikiriwe na mimi mambo yangu nilio yaombaaa. Akacheka tu. Yule mdda yuko vizuriii. Ndo akawa kila kituuu. Bibie akaanza sasa kurelax. Namtoa out na nini.

Siku ya siku tuko nae out mchana, ikaingia sms akaaga. Namuuliza nini akanianganya na!uona live kabisaaa ananidanganya. Nikasema Mafaaan! Nikampigia yule msichana nurse achunguze anipe feedback. Akanipa feedback alivomsikia Sally mwenyewe anasema msomali karudi Tanzania anataka waonane. Ndo anajishauri aende au asiende.

ITAENDELEA
 
Tonny mjinga sana,hivi huwezi jitengenezea njia hadi ubomoe ya Dee,mwanaume farao huyu sijapata kuona...
Ila Dee nimecheka alivyoamka sa8 kwenda kucheza azonto hahaa
Sasa na huyu mkimbizi ndo nini kuja kuunguza picha hivi,mfyuuu zake...
So far story bado inaendelea na chochote chaweza kutokea...lara 1 ubarikiwe na uwe na safar njema
 
Tonny mjinga sana,hivi huwezi jitengenezea njia hadi ubomoe ya Dee,mwanaume farao huyu sijapata kuona...
Ila Dee nimecheka alivyoamka sa8 kwenda kucheza azonto hahaa
Sasa na huyu mkimbizi ndo nini kuja kuunguza picha hivi,mfyuuu zake...
So far story bado inaendelea na chochote chaweza kutokea...lara 1 ubarikiwe na uwe na safar njema
Father of the year
 
Back
Top Bottom