Bad Addictions.
My name is Jolline, na Lidya ni dada yangu. Unaweza kuona nimetajwa tajwa juu juu tu katika hii story tena kwa mambo mabaya mabaya tu ukaniona namna gani vipi, walaaaa, hujanijuaaa tu ndugu msomaji na ukinijuaa utanifurahiaaaa sanaaaa.
Well nimekaa sanaa UK, sanaaa almost 8 facking years kwenye nchi ya mzungu. Kukaa kule sanaa kuna side effects pia, huwezi kurudi bongo na kuwa regarded as normal. Bongo normal is over rated. After some time unazoea kuwa treated as if kuna fuse zimeungua kichwani pako. I know and i dont care.
Sikupanga kurudi kabisaa Bongo, sababu mimi na Bongo we are kind of antagonistic. Uk is the land of the free. Niko mbali na wanafiki woteee, na most of all niko mbali na Lidya. I just cant stand her. She is my sister and everything but i simply cant stand her. The queen of perfection and hypocrisy. I enjoyed UK and i should have stayed there.
I had a life in UK. I was not just living, i had a life. Not until some fake ass shit nigga happened in my life. Before i was bailing high. Mimi na wabongo tofautiiiii kabisaaa. Na deal na wapopo tu. Nikapataga bwana mpopo, ana hela ni hatariii. Hauzi unga wala nini. Anauza vitu Ebay na Amazon, Etsy na ALi express. Kwa siku anaingiza pesa ndefuuuu hatariiiii.
Afu wa nigeria wanajua kujaliiii. Wanajua ku care. Atakuhudumia kilaaa kituuu. Kwa UK ni ngumu kupata mtu wa hivo. Maana Mzungu mwenyewe hataki ujinga, mzee wa cost sharing. Ilikua bahati yangu kwa kweli. Nimempata, nikayapatia maisha. Nikapata na kikazi changu cha uzushiii. Na hela za Da Lidya mambo bam bam UK inogileeee.
Wabongo sikuwa na mda nao kabisaaaa. Wala party zao sikuwa naenda, hata dinner sijui mikusanyiko gani nikawa sina mda huo. Kwanza mnigeria ni mtu wa kutokaaa hatariii, mtu wa kuyafaidi maishaaa. Mimi ni ku party na mnigeria kwenye cycle zao za wa west mda wote. And life was good, so good nikawa nishaamua Bongo mimi bahati mbaya hapa UK sibandukiii.
Siku hio niko shopping kwenye malls nikakutana na Susan rafiki yangu wa kitambooo sanaa, tumesoma nae Primary, tukasalimiana na nini. Sasa nisingeweza kumpotezea, tukabadilishana adress, na namba za simu. Kila mtu akasepa zake. She kept in touch.
Uswahili ukaanza sasa kama asili yetuuu, nisindikize huku mara nisindikize kule. Ukikataa basi kufika UK anajidaiiii, maisha yake mazuri sijui nini. Jamaniiii. Nikawa nakataa 90% ikibakia 10% nakubali. Sasa hamuwezi amini hii 10% ndo ilioniponzaaa.
Siku kanimbia kuna even ya wabongo twende, nikakubali shingo upande kwendaaa. Kwenda huko si ndio nikakutana na kijanaa Rama, ana asili ya upemba pembaaa na warabuu warabuuu. Alinivutiaaa sanaaa. Sema fahari ya macho. Kumbe na mimi nimemvutia. Kuja kuniomba namba nikatoaaa. Kosaaaaaa! Tena kosa lenyewe la uhainiiii.
Akaanza kunitokeaaa. Yeye anakaa mji mwingine, ili aje napokaa mimi anapanda treni. Akija najiiba kwa mnigeria naenda kuonana nae. Haramuuu tamuuu. Penzi likanogaaa hatariii. Mimi pale Sally namuelewaaa sanaa anachopitiaaa. Penzi lilinogaaa, mahaba niteketezeeee.
Hajui kama nakaa na mnigeria anajua naishi na Suzy, tuna share studio appartment. Akaniambia we should move in together , sasa mimi nikakataa kwanza sababu kubwa bado sijaamua namtokaje mnigeria. Nikamwambia ni mbali, ni sehemu ya kupanda train. Mi siweziii. Hapo Suzy partner wake asharudi bongo kuwaka jua, na Suzy nae in 2 month anarudi bongo.
Rama sijui aliongea nini na Suzy akajua Suzy anaondoka, akanimbia akiondoka Suzy yeye ndo atahamia mji huu sasa, na atakuwa anapanda train kwenda kazini kwake. Nikamkubaliiiaaa. Ikabidi niachane na Mnigeria fastaa fastaaa bila sababu. Mnigeria alinibembelezaa nibakieee. Nikagoma.
Hapo ujinga wa ndoa ushaniingia, naolewaa na Rama, nakuwa mimi peke yangu, na mume wangu na watoto wetu. The dream is so sweet. Kuhamia pale nikaonja joto ya jiwe ya UK. Bills bills and more bills. Hapo bado Suzy hajaondoka. Maana nilitaka nikae japo mwezi majirani wanijueee kabla Rama hajahamia jumla.
Suzy kaondoka leo, kesho Rama kahamia, sasa ndo mimi kujua ukweli kwamba Rama hana kazi, hana scholarship. Anategemea hela za kaka yake mwenye maduka Kariakoo ambazo ni kidogo. Huko kwenyewe kwenye huo mji mwingine alikosema anaishi alikuwa anaishi kwa ndugu zake, wapemba wapemba wenzie.
Nikajutaa kumuacha mnigeriaa, nikaanza kuwaza hivi kweli napendwa mwenzenuuu au nimetumika ndivo sivo hii UK. Mimi ndo baba yake ndo mama yake afu UK. Ikabidi sasa nianze kuliaaa na Lidya, na alivo mgumuuu. Lidya simpendi ndio ila namuheshimu sanaa sanaa kaniweka mjini tena UK. Nikatafuta more paying job kuweza kumeet bills. Atleast baada ya 6 months tukaanza kuwa stable.
Rama mvumilivu nikiwa sina hela nakuwa in bad moods za hatariii. Namfokeaa, namgombaaa hata kwa vitu vidogo sanaa. Sema mwenyewe muelewaaaa. Akawa anapotezea tu. Nikiwa nimeanza kurelax, kaka mtu akapata matatizo aliyumba kibiashara so mara ada atume nusu, mara asitumee. Nilikuwa na kiakiba changuuu cha kurudia bongo niliapaga sikigusiii hata itokee nini. Ikabidi nikitumie kumpiga tough. Acheniii.
Nimishi na Rama miaka miwili ananitegemea mimi 100%. Kama kujitolea nilijitoleaaa sanaaa. Sema alikuwa ananipenda sijui ndo ananipelembaaa anichuneee hata sielewiii. Rama alikuwa anasoma Medicine, mwaka wa 3 wa kusihi nae akapata kazi ya kutibu ngombe na mifugo kwenye ranch. Kama staff wa vetenary.
Kazi alikuwa analipwa hela ndefuuu sanaaa. Akaniambia niache kazi niliokuwa nafanya, cause nilikuwa naumia basi tu njaaa. Tukahama studio apartment kwenda apartment kubwa zaidiii. Maisha yalikuwa mazuriii. Napewa pounds za matumizi ya ndani. Za shopping. Nachotaka.
Mwanaume hana mambo mengi, akitoka shift yuko ndani, tunakaa tunaongeaaa, tunapangaaa maishaa. Walionicheka wakaanza kunitamaniii. Ana mipango ya maana hatariii. Akaanza kujenga ghorofa Mbezi Beach, ananionesha ramani, our future home. Mipango ya mbele ya maana. Nilijiona na bahatiii sio ya dunia hiii. Mwananume HB, pesa kaikamataaa kisawa sawa, ananipendajeeee yaani idont even have to try hard. Nikawa nasema Lidyaaaa dada yangu UMEKWISHAAA.
Mama Rama alishakujaga kipindi mimi ndo namtunza Rama, tukakaa nae wiki 3, yuko vizuriii sanaa, mtu safiii. Sema aliniuliza swali moja tu la uchokozi. Dini utabadilishaa? Nikamjibu sina nenooo, mi nabadili tuuu. Tukawa tunaishi vizuriii sanaa, nikirudi kazini nakuta kapikaaa, kasafishaaa. Nikiwepo tunakwanguana mmba, tunasukana mabutu. Yeye anajua kusuka rasta za mabutu ananisukaaa. Tunapendana sanaaa. Akaniambia Rama anapenda snaa chapati za kusukuma, akanifundisha kupika mpaka nikaweza.
Akaja tena Rama hela imekubali, mi sina hata mia, nimekaa nyumbani tuu. Wala hakubadilika bado vile vile mkarimuu. Alipelekwa na mwanae kwa sonara, akaniambia shoga nimekuchagulia na wewe mwali wangu, sasa sijui nimepatia maana nyie wasichana mna mambo mengi. Nikamshukuruuu. Akinunuliwa kitu ananichukulia na mimi. Mpaka unafarijika mama mkwe wangu mtu mzuriii.
Rama akamaliza shule, akaniambia turudi bongo, maana ile kazi ilikuwa anaruhusiwa kufanya endapo tu ni mwanafunzi wa hiko chuo. Kama field. Akaniambia nyumba yetu iko kwenye finishing, UK bila kazi tutateseka. Twende bongo we will make it. Nikarudi bongo kwa moyo mmoja, najua Rama si yupo.
Tumekaa bongo miezi 6, tumepanga Sinza, mi kazi sijapata bado, na yeye kazi bado hajapata. Akaanza kupata yeye , mi sina shakaaa, nishazoea kulelewa. Oooohooo. Siku hio sitakaa nije niisahau napigiwa simu mie na mama angu mdogo anaishi Upanga. Njoo Jolline, kuna watu wamekuja kuoaa, mbona kama yule kaka uanemuweka facebook? Tumeulizana wote ndieee kabisaaa. Nikasema haiwezekaniii, Rama nimelala nae jana usiku mimi, asubuhi kaenda kazini. Mamdogo akasema njoo tu bwanaa uhakikishe.
Kwenda NDIYEEEE haswaaaa. Tena yuko na mama yake. Mama mnafiki yule sijapata onaaa. Nikataka nivamie, kina mamdogo wakanidakaaa. Wakasema Jolline acha, utazidi kujiaibishaa. Utatolewa kwenye magazetiii, kama kaamua kuoa ataoa tuuu. We achaaa. Nililiaaaaa. Nililia mpaka homa.
Usiku katuma sms leo sirudi, nimesafiri ghafla. Nikamwambia safari njema. Asubuhi ananitafuta umeamkaje mke wangu? Nyokooo kwelii. Mi namjibuuu. Mpaka honey moon ikaishaaa. Akaja kuniambia naomba tuongee kitu. Nikamwmabia haina haja najua sana kama umeoaa, nilikuwepo kwenye harusi yako. Akadai ooh sio kama unavoolewa, its complicated. Nikamla Block. Sasa alitaka abishe hajaoa wakati nimemuonaaa mwenyewe live.
Baada ya hapo nikawa naranda randaaa, Lidya yupo kunisemaa kutwa mara 3. Sijui nilimkosea nini. Kanipeleka UK la maana nililo rudi nalo ni mwananume, mwanaume mwenyewe kaoa. Nilikondaaaa nikabakia mifupaaa. Mungu si athumani nikapata kazi kwenye kampuni ya mafutaaa. Ila bado wanaume mimi wakawa wamenitumbukia nyongo kabisaaaa.
Kwanza nikaanza tabia ya kuwa na mabwana hatariii. Sijibaniii. Nina bwana anafanya kwenye gas Mtwara, huyu senior bachelor alioa wakashindwana na mkewe sasa anatanga tangaaa. Tunapigana mechi za kiutu uzimaaa. Analipa kodi na kutoa house maintainance, akitoka Mtwara nampozaa kishkajii.
Nina bwana yupo USA, ni black America, nilikutana ane Amsterdam, nae yuko busy sanaa tunapiga show tu za msimuu. Uzuri ana mihelaa balaaa. Hanipi ila akikuhitaji good time utazopewa sio za nchii hii. Dubai, Paris, atakulipia kila kitu mpaka Visa. Asema anataka anioeee atiii. Najua sound tu.
Hao ndo permanent acha hawa wa short time. Sijibaniii kabisaa kabisaaa. Sijui laana zangu au nini Rama na mkewe walipeana talaka 3 hata mwaka haukuishaaa. Alishakuja kuniambia upuuzi wake kwamba alilazimishwa na mama yake amuoe yule mwanamke, na yeye alipanga kumuoa ili mama aridhike, afu akiona ambavo hawaendani aje anioe mimi mke wa pili. Mmmmmmmmhhh! We ndugu msomaji linakuingia akilini hilo kweli? Mimi liligoma mwenzenuuuu.
In short siku hizi mwenzenu mshipa wa kupendaa ulishakatikaaa, nipo kimaslahiiii tu. Nipe changuu nikupe papa. Huna anza mbeleee. Sicheki na kima, sitaki ujingaaa. Kama Kupenda ishakula kwangu. Kitu kinachoweza kufanya niloweee pesaaa tu hamna kingineeee.
Ila siku ile namuona yule msomali wa Sally, roho ilinilipukaaa paaaaah! Sijalipukwa roho hivo tangia siku ya kwanza kumuona Rama. Na mimi wakati namuona msomali hakuwa na Sally, nikafurahiii, nikasema finally a new face maeneo hayaaa. Nikawaza yule kaka jamaniii mbona ananitia majaribuniii. And it was nice to have feelings again. Mara namuona Sally anambusu busu yule Msomali khaaaaa! Jamaniiiiiii! Yuko fastaaaa. Nikajua kamkuta pale pale.
Kuulizia nikaambiwa hata usisogee. Kamtoa Somalia mwenzioo huyo msomali. Nikashangaaaa? Sikuelewa ina maana wanaume wamemvuruga Sally mpaka kaamua kwenda Somalia kujichukulia bwana wake peke yake sikuelewaa. Naambiwa ndo hivooo. Huyu msomali hana ndugu yoyote hapa Dar zaidi ya Sally. Na roho yakee hiooo. Invosemekanaa kamtoaa Mogadishuuu, anakaa nae kwake, anambana kwapani masaa 24, Winni haoni ndaniii.
Hataki ushogaaa siku hizii, hataki ubest, hataki chochote zaidi ya kukaa na huyo Msomali. Hata ukitaka kwend akwake hatakiii, atakwambia hayupooo. Kwa jinsi Sally alivo kichwa ngumuuu, sio kunyooshwa na msomaliii kirahisi rahisiii. Hapa wooote tunataka tupige na msomali walau show mojaaa tu, ya kuonjaaa kujua kilicho mdatishaa shosti wetuuu hivooo. Sema ndo bado tunausomaa mchezooo.
Dada yako Lidya naona hakopwagi, anamuuzia mpaka mumewe ila kwa msomali anajigawa sandakalaweee. Umri ule msomali atuachie sisi. Atakuja kauchika aanze kutanga tanga. Nikastukaaaaaaaaa na hizi habariii. Ina maana mna uhakika Lidya anamtaka Msomali? Kumbe jeeeee? ANgekuwa hamtaki angemuharibia Sally? Mimi mwenyewe nimemsikia kwa masikio yangu anamwambia Msomali mambo ya Dee na Kinshasa.
Siku nyingine anamwambia mbona huji saloon kunisalimia, mara mbona msomali hampigii simuuu, mara kamtafutiaa msomali dili la kuspply simu kwenye bank yao, msomali hana kampuni bado, Lidya akawa anamsisitiza watumie kampuni ya Chriss, hana shidaa, na Chriss akamkubalia wapitishe hio transaction kwenye kampuni yake sababu wao ni general traders.
Everything is so open, Lidyaaa ana nyegeee, tena nyege mbayaa za damu changaaa. Kiharage kitakuwa kina mpwitaaa sio kidogooo. Sally tu kawa Sloppy siku hizi. Angeshausoma mchezo siku nyingiii sanaaa. We Lidya kazaa juzi au jana, mwanae mdogo si ana miak 9? Jioni hii ndo anaenda gym, anafunga tumbo kwa kwenda mbele, anataka amrudishie nani shape kama sio msomali! Mxieeeeeeeeewww! Si tunamchoraa tu mtu mzima asietuliza kiharage chake chini akatulia na mume, hivi kucheat ukachanganye damu na wasomali damu yao ilivokuwa kali. Heheheeeeee!
Taarifa zilinimalizaa nguvu zooote. Mpaka Lidya???? Alivokuwa against free P, Haaaaaaaaa! Sikutaka kuamini nikasema nitampeleleza Lidya kidogo kidogo. Mpaka niupate ukweli mwenyewe. Na lengo haswaaa ni mimi roho iliniuma kashaniwahiii kwenye moves. Na mimi sikuwa na lengo la kukubali kabisaaaa kutompata msomali kama tutashea poaaa tu.
Nikarudi kukaa kwa Lidya kwanza, namjua ndugu yangu kama ana mshawasha haewezi kujibanaga. Nimemkuta anakula sit ups. Nikashangaaa. Jioni kabla hajalala akajipaka manjano na Riwa. Nikamuuliza vipi? Aaaah uzee wanijia kasi. Mmmmhhh! Raha ya Lidya ni kumsema Sally asubuhi mpaka jioni na mimi. Ila siku hio hakumzungumzia kabisaaa utasema hamjui kabisaaa. Nikaanza kushikwa mashaka huenda kweliii. Tumbo lilinichezaaa. Nikaamua kuchokoza nyuki.
Da Lidya! Yule msomali wa Sally unamuonaje? Akastukaaaa kama kashikwa ugoniii. Na kuhamaki, namuonaje vipi? Kivipi yaani, sikuelewiii? Mi mke wa mtu. Khaaaaaaaaa! Kama nimemsoma roho vileee. Nikambadilishia gia, unamuonajeee kiumbeaa, mimi na wewe dada yangu wambeaaa. Akapoa kidogo. Ahaaaaaaaaa! Mi naona Sally kapotea njia tu. Free P tu yule. Ila ana roho nzuriii kweli, rafiki yangu hatariii, nakapendaaa kweli kama mdogo wangu. Mmmmhhh! Nikatabasamu. Nikampelekea B52 mtu mzima kileja yule. Kwani dada Lidya mara ya kwanza ulijua nimemaanisha nini nilivokuuliza unamuonaje? Akasambaratikaaaa! "Hivo hivo ulivomaanisha kwani ulitaka kumaanisha nini?
Mmmmmmhhhhhh! Nikaona kiharageee kinampwitaa sio kidogoo. Ndugu yangu yuleee kaishaaa habari yake. Nikapata uhakikaaa kabisaaa Lidya tuko nae kwenye ligi bila hata upinzaniii wala utata, kibaya mwenzetu ana resources za kutosha. Sasa kama Lidya tuko nae kwenye ligi ina maana nani hayupo sasa? Maana Lidya sio mwepesi mjueee. Yaani mpaka stage hii sitoshangaa kama Winni nae tuko nae njia moja ya kumnasa msomaliii. Nikamsikitikia tu Sally.
Mdomo koma nikajikuta naongea haya mambo kwa Chriss. Sijui ndo kiharage kunipwita na mimi sijui. Ila nikajikuta tu, naenda kwa Chriss anishauriii. Nikamsimuliaa yote kasoro ya Lidya, yule ndugu yangu, mama angu kwanza yule manake kanileaaa. Naanzaje kwanza kumsambazaa? Aibu yake, aibu yangu. Nilitegema Chris astushwee na hizi taarifa ila tofauti na matarajio yangu walaaa hakustukaaa.
Akauliza tu kwa masikitiko WHAT DO YOU PEOPLE SEE IN HIM? WHAT DO YOU LOSERS SEE IN HIM I CANT UNDERSTAND. Unajua wewe ni mtu wa 3 unaniomba ushauri kuhusu huyo boyaa, hao wa 2 siwezi kukutajia cause mmoja wao nampendaa sanaa na kumjaliii mnooo. Nikashangaaaa sanaaa! Ina maana huyo anaempenda na kumjali aliemuomba ushauri kuhusu msomali sio kewe kweliii? Makubwaaaaa! What type of marriage are they having? Au ndo open marriage mnashauriana ucheat na nani? Whatever!
Chriss akawa analalamika tu, hana gari, hana nyumba, the dude has nothing, completely nothing. He has accomplished nothing mpaka umri ule, he has been no where, he knows nothing is is known by no one, yaani ni hopeless case. Ila the speed women mnajirusha kwake is alarming. Very frustrating and shameful.
Ukizingatia principles zinakiukwaa kabisaa. Accomplished men like myself, i am PHD, i have a very big role in this country, i am well paid, nimetembea dunia, i have savings in my bank account, i have investments, i have everything he doesnt have will probably never have. Kushindania wanawake na yeye is a complete mediocrity. Sielewi.
Time will tell. Binafsi mimi Chriss lazima nikae nae chini, i might learn a thing or 2 about women toka kwake. Really. Kwanza kula hela za Sally uwe na zaidi ya PHD. Tukacheka tuuu.
ITAENDELEA KESHO SAA 4 USIKU