Weekend Story! Glory Be To God!

Weekend Story! Glory Be To God!

Damn with all the name tagging and am nt on the list,i feel bad.but that's life it fucks us all sometimes.i better sip some champagne to soothe my heart.good night gal and all.

Post sent using JamiiForums mobile app
Take it easy girl.
 
welcome back sweetheart

Post sent using JamiiForums mobile app
 
Mtumishi atakuwa ibadani mida hii, saa nane dude litaamshwa kweli? sijui

Post sent using JamiiForums mobile app
 
Winifrida!

Jamaniii mimi naona mwenzenu niliandikiwaaa "NA ASILE HELA YA MWANAUME KAMWEEE." Yani kama mtu aliacha laana na hio laana akaitambikiaaa kabisaaa na kuitolea kafaraaa huku akinuiaaa uchi uchi na sio wima wima alichutama mara 7 na kubongoa mara 17 maana zote namba tasa na kunuiaaa juu "Na Winnie ASILE HATA KUONJA hela ya mwanaumeeeee KAMWEEEE" Na hio kamwe aliitamka kwa herufi kubwa KAMWE. Nilibakia tu nacheka peke yang. Si mambo ya kucheka ila nilijikuta nachekaaa.

Nikamwambia Winnie shoga angu, umeolewaaaa, mume unae, anakujaliii, anakupendaaaa, mpaka chooni mnaongozana, sasa sisi ambao hatuna waume tusemaje sasa. Mwanaume anapenda watoto yule mpaka mda mwingine naomba Mungu anipe Mume kama wako.

Weeeeeeeeeeeeeee! Ishia hapo hapoooo mtakuja kuombaaa visivyo omba. Tena kemeaaa, na kanushaaa kabisaaaa kwa damu ya Yesu. Mi ndo nakwambiaaaa. Niamini mimi yale sio mambo ya kuombeaaa kabisaaa kabisaaaa shoga angu. Tema mate chiniiii. Unadhaniiiii. We ndoa zione njeee tu. Wahenga unafikiri kusema ndoa ni ndoano walikurupukaaaaa? Thubutuuuuuuuuu! Donte even dare to think yours will be special or what? Ndoano mwanzo mwisho. We si wazazi wako wana ndoa, na achana na watu wa nje, we si ulikuwa unamjua mdingi wako nje ndani? Was he the man people thought he was? Was he? Was he the man your mom worked so hard to make sure people were convinced people he was? All families have skeletons in the closet. Tena hayo maombi funga siku 40 kukanushaaaa.

I wasnt convised mume wa Winni will be that bad. Come on i knew guy. Winni was just being over dramatic. But she had a point. My dad was an A.ss, and it was no secret, i knew it, Winni knew it too, cause he made a pass at her. But his dad was a religious man. Sitokaaa kimya kumuacha amchafue hivi hivi. I respected that man for crying out loud.

Winnie i know my dad was an A.ss, but come on your father was a good man. He always loved you and your mom. Alwaysss. I always wished your dad was my dad. Hakuwahi kumiss birthday yoyote yako, graduation, any moment in your life he was there. He was involved every single day of his life kujua wanae mmeamkaje, mmeshindaje, what is going on in your life, nani ana kunyapia nyapiaaaa. And you should thank God about that.

Mimi my dad was absent, my entire life except for the envelopes that came coming with money without even a note. Zamani naongea nae kwenye simu ana swear he will show up in my birthday and he never did not even once. Naliaaa hatari. Nimeghairisha kupokea ekarisiti mara 4 so that Dad ahudhurieee, wala haudhuriii,nikaamua tu kupokea mwishoweee. And as i grew older i decided i have waited enough, and i will never even waste 1 second waiting for someone who is never coming.

Fine zamani alikaa nje ya nchi, alivorudi sasa sikuona hata tofauti. He was always on the move, or on a project or on anything that will keep him away from his familly. Nilipolitambua hilooo, aaaah, nikawa hata sijisumbuiii, wala sijiwekei mazingira ya kuwa disapointed. Simuhusishi mambo yangu. Siku akinikumbuka ananicheki, asiponicheki basi. Atajijuaaa mwenyewe. Mpaka leo mtu mzimaaa mwendo huo huo. Tuseme nimejikuza mwenyewe. Hata Dorice anavohaha kumsaka baba yake mzazi, naona anapoteza mdaaa tu, na pesaaa, atachoambulia sana sana ni BIG DISAPOINTMENTS. Anavodhania her dad was not in her life because of situations and circumstances ila niamini atakuja kujua her dad was not in her life because HE MADE THAT CHOICE. Mi nipoooo.

Winnie akanitazama akatikisa kichwaaa na kukaa kimyaa mda. Akaja kusema. "THE GRASS IS ALWAYS GREENER ON THE OTHER SIDE" The only ungrateful person kati yetu ni wewe Sally. Wewe uko focused sanaaa on the fact your dad was not home, your day was never there for you unasahau the bigger fact WHY WAS HE NOT THERE? Hivi ushakaa ukajiulizaa kwa kina kwamba most of the privillages that came in your life came because your dad was not there and he went very far, crossed several oceans, kavuka bahari zaidi ya 5 kwenda kuwatafutieni maisha nyie mbwa, na sio comfortably kwenye ndege labda, amekaa ametulia masaa yake 12, its a done deal, kavuka kwa kuzamia meliii, kajirisk kutoswa bahariniii, kaweka yeye maisha yake rehani hata angekufa in the processs poaaa tu, ila the chance to give you a better life he was gonna take it regardless what hata kama inahusishaaa to give up his own life.

Hivi ushawahi kujiuliza zile bahasha za helaaa alizokuwa anatumaaa anazipatajeee? Watu kibao washua wao walikuwa wako ulaya na marekani ila kuna watu walikuwa wanatumiwa pesa nyingi kama nyie? Mnaishii kwa anasaaa. Hata siku moja mliwahi kujiuliza baba enu huko nje anaishijeee, labda maisha yake yapojeee? You were so focused on spending the money, splashing it all over nonsense to get back at your dad because he didnt show up for your communion.

Sasa mimi Winnie nilimuuliza baba Brenda, si walikuwa nae Ugiriki, kabla hajazamia Monacco. Unaambiwa baba yenu yule alikuwa anajibanaaaa, ni anajibanaaaa anakula makombo ya wateja hoteli anayo osha vyombo. Wateja wakibakizaa anafichaa ndo anarudi getto kula, maana hoteli hairuhusiwiii kula makombo, bora ale mbwa, mzungu hapendi ujingaaa ujingaaa. Wenzie wanaosha vyombo masaa 6 kusudi mikono ikaukee. Yeye kuendekeza njaa anaosha vyombo masaa 18 anakomaa anakazaaa. Mwishowe akaoza mikonooo yoote, fangus, hafai ananukaaa. Mzungu akamstopishaaa. Yote hio awatumie nyie mibahashaa ilio nonaaa.

Kapoteza kazi akawa sasa hana kazi, akaambiwa tuliaa tu utapata ingineee, wapi akaanza kuiba cheni kwenye sehemu zenye vito. Kuiba kwenyewe usidhanie anaficha mfukoni, wana mezaaa, afu wanaenda kuzinyaaa. Siku njaa zake alimeza pete ina kito kikubwaaa hatari isimkabee. Nusu afeee. Akawahi kupigwa bao la mgongo ndo kuikohoa. Na ndo akapata pesa ndefuuu akawatumia mnunue nyumba. Na ndo kupata pesa ya kuhonga kuzamia Monnacco.

Monacco maisha yakamkataaa kabisaaa kabisaaa. Akawa analala nje, hana hela ya ghetto. Akaugua nimoniaaa kwa kupigwa baridi, hana karatasi za kwenda hospital, kuna mama wa kinigeria akamsaidia mi vuduuu na midawa ya kinigeria ya kwao akapata nafuuu. Wabongo na wakenya na watu wengine wanaoongea kiswahili wakamchangia pesaa arudi bongo kufanya maisha mengine, maana afya yake sio nzuriii. Nimonia inarudiaaa, na ikirudia ndo baas. Maana walimwambia akaombe deprtition arudishwe, akagoma kabisaa hawezi kurudiiii hana maisha ya kurudia kama kufa basi afeee huko huko.

Sasa kumuona navosihi kama keshakufa, wakapitisha kapu, apate mtaji wa kurudi, mbona bongo kuna maishaaa piaaaa. Zikapatikana pesa ndefuuuu. Wakamfanyia na party ya kumuaga kabisaaa, maana hali yake haikuwa nzuriii bado mdhaifuuu. Ooooohhhh! Akanunua gari Landcruiser ya mkongaaa, na kuituma Bongo,na hela za kutoleaaa. Watu walikasirikaaaaaa. Walikasirikaaaaa msitake kujuaaaa. Wakasema hata akifa atajijuaaaa.

Kuona wabongo wamemsusaaa akahamia Paris. Bado dhaifuuu. Akapata kazi mgahawa wa wagiriki cause anajua kigiriki, ile ile kuosha vyombo. Ndo lishe kidogo ikawa nzuri makombo yale na kwenda kuonja onja sokoni nyama za kuonja zileee. Akaponaaa. Mda wote anaishi kama MBWAAA. ana kibegi tu cha mgongoniii, suruali 2 na tshirt 2 na chupi 1 kauka nikuvae. Heheheeee. Pesa yoote anawatumia nyie muishi kama mpo ulayaaa. Mnajitanuaaaa mtakavyooo. Mtake nini msipateeee.

Kaosha vyombo kidogo, akapnadishwa mpaka msimamizi wa wafanyakazi cause kujua kigiriki wakaona kama mwenzao sema mweusiii. Wakamtafutia mpaka makaratasiii ya mkimbiziii wa DRC, maana wagiriki nao wazee wa illegal migration hatariii. Akahamishiwa new york kwenye mgahawa wa hao hao wagiriki. Walichomsaidia ni uraia wa ufaransa.

New york nao kaishiii kama MBWA mpaka mwishooo. Kateseka sanaaa mpaka akataka kufa kwa mara ya 2. Yaani story yake ndefu siku we kaa nae siku akusimulieee. Au muulize Jay bahariaaa, ameishi nae ugiriki, Monacco na Paris anamjua fikaaaa. Moral of the story is your dad made so many sacrifices to give you the life you have. Dont focus on hating him so much try to give him a chance and get to know him. The devil is not so black as he is painted.

Nilichokaaaaaaaaaaa! Nikajinyoosha. Ofcourse nilikuwa najua ni baharia huko nje, ila sikujua details huko nje kukojeee. Nilichokaaaaa. Winni anaendelea kubwabwaja tu.

Sally si unakumbuka mi nilitaka kuzamia nje, nikajilipue ukimbiziii, mpaka passport, tiketi, kila kitu nilikuwa nacho, nikaghairi mwishowe, hukuwahi kuniuliza kwanini? Baba, mzee wako alinipigia simu nisiendeee. Nitafute tu maisha hapa hapa Mungu atanisaidia. Kule hamna maisha ya mwanamke. Afterall nitajiziii weee afu nikirudi huku no body will understand the sacrifices i have made, watachukulia easy tu.

Akasisitiza tu niangalie woote waiozamia generation yao wameishiajeee. Sawa maisha walipata ila baada ya kurudi wakakuta mambo sivo walivotarajiaaa, na familia zinavowaelewa sivooo. Wake wamfanya umalayaa mpaka basi kwa pesa walizotuma kwa jasho la damu, kama mama yane kazaa mtoto wa zinaaa. Watoto wake mnamchukiaaa bila sababu mnamuonaa baba katili tu hakuwepo kwenye maisha yenuuu. Malezi mmepewa ya hovyo hovyo tu, mshakuwa maaluni mlioshindikana, la kufanya umri huo mliofikia hana zaidi ya kuwatizameni na kuwaombea Mungu. Dini hamnaaaa. Ndugu nao wanalalamika pesa kapata kampa mkewe zote kafanyia umalaya, hawataki hata kumuonaaa. mradi maisha yanamla Tigo tu. All he did was for nothing! Absolutely nothing. Hata nyumbani alipata shida sanaa kukaa maana angeweza kumua yule mtoto yule mdogo wenu Feisal. Ila baadae kaanza kuswaliiii, kamtafuta Mungu, na Mungu kampa nguvu za kusamehe na kuendelea kuishiii, na kumkubali yule mtoto maana kiumbe wa Mungu hana hatiaaa. Na sahivi roho yake nyeupeeee, hana kinyongo na mtu, na yule mtoto wanaelewana sanaaa tu, ndo kidogo anamsikiliza na kumjali kuliko hata nyie.

Akaniambia we angalia mwisho wa woote, K Boy alishindwaaa kuhimili vishindo karudi mwaka tu, kakuta mkewe kaolewa na wanae wamebadilishwa majina woote, pesa nduguze wamekula zoote hamna walichomuwekezea wala nini na mkewe walikuwa hawampi hata 10 ndo maana maisha kuwa magumu sanaa kaolewa tena. Akajinyongaaa zake. Ilisikitishaaa. Maana kurudi kule haiwezekani umri ushaenda. Macheni ndo yupo Magomeni hapo hamna anachokifanya cha kueleweka. Dulla Smart kawa mleviiii wa gongo Kinondoniii. Anafanya kazi ya ulinzi unaambiwa. Nae hivo hivo maisha yamemla Tigo. Wanae wale mabinti wa 3 hawamjui baba yao kwa chumvi wala sukari. Anajihangaikia atu. Stefano ndo kawa mchungaji njaaa, hawa wanahubiri mabarabarani huku wasio hata na makanisaaa. Na mkewe nae kaolewa na mtu mwengineoo kabisaa. Hussein ndo yuko vizuri sababu anauza substance. Ila usiende mwanangu. Kaa hapa hapa. Mungu yupo utatokaaa.

Jicho likazidii kunitokaaaa. Nikamwambia enough about my dad, now lets talk your dad for a change. Winni akagunaaa!

My dad was a lazy a.ss dudeee. Super lazy! Sijawahi kuona jitu vivuuuu kama lile. Naona hio laana ya "KAMWE WASILE KITU CHA MWANAUMEE" ilianzia kwa mama yangu labdaaa. Mwanaume mvivuuuu yule sijapata onaaa. Niamini mimi. Kuwepo kila mahali ni dalili he had nothing better to do.

Defenc yake kubwa SISHINDANI NA MTU MAISHAA. Hahahaaaa! Zimeingia televison, watu wooote wanazo majumbani mwao, mzee wangu mie anasema anasaaaa hizooo. Sisi sio watu wa mashauziii. Kwanza zinafundisha tabia mbayaaa. Kuna picha zisizofaaa. Atatoa mifano hata 100 kwaniniTv hazifai mradi asinunue. Mama yangu kapambanaaa, kapambanaaa, akaja kununua, YEYE NDO MSHIKA REMOTE MKUU. Humwambii kituanashinda hapo hapo siku nzimaaa.

Watu wakanunua magari, kama kawaida yake, HASHINDANI NA MTU. Kwanza yana ajali sanaaaa. Mfano anaoupenda ooh familia nzima walikuwa kwenye gari lao wakapata ajali ya gari na kupoteza maisha wote. Mmmmmhhh! Shule sasa, watu wanapelekwa English medium ndo zimeingiaaa. Mama kumgusaa aksema SITAKI kusikiaaaa. Mama kakomaa kivyake akatupelekaaa. Akaja kumbwani "UNAJIFANYA UNA HELA KUPELEKA WATOTO SHULE ZA BEI, SITOHUSIKA NA KITU CHOCHOTEEEEEE, TENA USINIHESABIEEE." Mana akamwambia poaaa tu, Mungu wangu ni mkubwa anajua nina nia nzuri na wanangu na hatoacha niaibike milele. Watamaliza tu, nitakosaa vyote ila sio ada, kwa Jina la Yesu watamaliza.

Mtaani watu kuanza kusifiaaa, tunasoma english medium tunapanda school bus, anavojitutumua sasa kidogoo. "Eeeh bwana imebidi tuwapeleke huku English medium hizi za kata hazina kitu kabisaaa". Poor education. Utamjuaaaa? "Ni ghali sanaaa, najinyima sanaaaa huwezi hamini tunalipa 900,000 kila mtoto kwa watoto wa 3 sio mchezoooo" Bsi watu wanamkubaliii na kumiminia sifaaa kemu kemu kumbe hatoi hata 10. Hakulipa hata 10. Mpaka tumemaliza darasa la 7 wote.

Sana sana hivi tumekuwa watu wazima tuna maisha mazuri, kaka zangu wako bank, mi nafanya biashara, tuna maisha yetu ndo siku tu aliamka vizuri akamwambia mama "Mke wangu nashukuru sanaa sanaaa kwa kujifosiiii, kupambana kufa na kupona kuwapeleka watoto English Medium. Wamekuwa tofauti, wameenda mbaliii, na wana comfidence na kujitambuaa kusiko kwa kawaidaaa. Nisamehe mimi sikuwa na vision kama yako mke wangu, sikuona umuhimu kwa wakati ule ila sahivi nakuelewa sanaaaa ulichokionaa. Na kwamba sikutoaga hata 10 ada najisikia aibu kubwaa. Ila i can never be more proudin my life kama kuwa baba wa wanangu." Mama akamtizamaaa tu anavojikosha koshaaa.

Yaaani mzazi wangu yule kitu kinachohusisha pesaaa kwake alejiiiii. Siku kanipeleka shule naenda boarding form 2, mama hayupooo ananipa sh 2000, na sio kitambooo miaka ya 2000 kati kati huko. Sasa sikuelewa ya kula njiani au ya kutumuia shule miezi 6 sikuelewaa. Na anajua mama hayupo na pesa hajanipa. Mama si anamjuaaa aliaachia maagizo nichukue hela ya mchezo anapokea ndo niondoke nayo. Acha tu.

Tangia anafanya kazi seriaklini, kaenda mpaka ulaya kikazi mara kiboa, karudi, kapewa ridanacy sijawahi ona tofautiiii. Siku zoote hana hela ya chochote. Ange oa mtu ambae si zoba kama mama wangesha achana kitambooo. Wewe Sally wewe The grass is always greener on the other side.

Na kinachoniumaaa ule usemi wafanya ufanyavyooo LAZIMA UOLEWE NA MWANAUME KAMA BABA YAKO MZAZI naona ni wa kweliii kabisaaa. Maana huyu baba wa 3 nae yumo muleee muleee kwa mzee baba. Ndomaana napanicccc. Cause i aint my mom, i cant do it forver. Nishachokaaa mapemaaaa.

Nikabakia natoa macho tu.

ITAENDELEA KESHO SAA 4 USIKU
 
Back
Top Bottom