The Former Minister Affair!
Shostiiiii Joline nimekaaa wimaaa wimaaa nangoja unipeee ubuyu wa mheshimiwa Waziri naniliuuuuu. Nautamaniii huo ubuyuuuu mpaka naumwaaaa. Usipindisheee nipe nukta mpaka nuktaaaa. Jolline akatutizamaaaa, akasema agizeniii bia kwa wingi, ubuyu wenyewe huu wa kitajariii na lazima itifaki ifwatwe manake ni kwamba bia zitiririke huku ubuyu ukitirirka.
Akaitwa waiter akaambiwa kama vipi leta 5 kwa kila mtu kama tunavyokunywaaa, hainaa kujibanaaa, hainaaa kujidhikiiii. Waiter akaleta fastaaaa, akataka kusepaaa, akaambiwa fungua zoteee, hatupelekinyumbaniii. Haya Jolline mwaga huo ubuyuuu na usiache ku drop names pleaseeeee. Jolline akaanza.
Mnakumbuka msibaaa wa K, tuakaendaga kumzika kwako Kamachumu huko Karagwe! Mi nilijitolea pesa ya ndege kwenda, cause tushaishi street moja kule Manchester for more than 5 years couldnt act like i dont know her. So nilivosikia msiba utasafiri na ndege, na mimi kwa gharama yangu kabisaaa, nikajiandikisha, nikaibukaaa huko Kageraaaa.
Tumefika msibaniii, ndo kujua K na familia yake hawakuwa watu wa mchezo mchezo cause kukawa na ugeni mzitooo sanaa, mawaziri, mkuu wa mkoa, mkuu wa wilaya, viongozi wa chama, yaani big names all over. Sasa mimi i was like no body, just moaning the young life gone too soon.
Sina hili wala lile katika kujichanganya nikawa introduced kwa yule waziri kijanaaa, wa awamu ileeee, bata mtuuuu, mzee wa misifaaaaa, misifaniiii. Nikampa heshima yake na nini. He was just being modest akaniuliza a litle back ground about me, nikamwambia just came back not long ago, nimekaaa Manchester for llike 12 years.
Ikawa uchangamfuuu hatariiii, akasema na yeye alikaaa Totenham sanaaa. Akawa ananitaji watu alio waacha kule wazamiaji kina Dora Songambele na wahenga wengine wa UK. He actually knew what went down in Uk sanaa tu. Story zikanogaaa mbayaaa. Umbea kidogooo na nini. Alivotaka kuondoka he asked me for my number. Nikajua tu waziri mtu wa totoz tena zile kaliiiii hatari na anazitatuaga marindaaa, he is never gonna call wala nini, he is just being courteous cause tuem hustle wote UK in different times. Nikampatia hio namba.
Usiku akatuma text, umelala hoteli gani hapa Bukoba? Nikamtaji ingine yenye hadhi ilihali nilikuwa nimelala kwenye guest bubu moja tu ya 15000 kwa siku. Maisha magumu. Akawa analeta story za UK za hapa na pale. We chatted a lot. And i was facinated, huyu ni waziriii jamani tunaemuongeleaaa sio mtu mdogo mdogo. Waziriiiii mkubwaaa sanaaaaaa. Best yake Riz 1, kupika na kupakuaaaa
Kesho msibaniii akanidakaa na kuniambia jioni nitapitiaaa kukucheki we cna hangout na nini cause kesho msiba umeisha tunakianuaaaa. Nikasema sawaaa. Nikaenda kulipa sasa ile hotel ya hadhi kama 80,000 kwa siku. Nimekaaa nawaza yaaani yaaani nimetoa hio 80k afu asilete mapumbu yake haki naenda ofisini kwake kudai refund. Huku najimbia Mungu ni mwema atakujaaa tu, najidharau najishushaaa, kwanini asije.
Saa 2 usiku huyu hapaaa. Akaniltea Jack Danniels blue label which is kind of expensiveee kwa wale mnaozielewaaa. And i was impressed nikasema sasa mi na waziri tunaweza kwenda sawa. Kwa kupenda kuhongwa mimi sina mpinzaniii. Basi story story mpaka saa 6 usiku, he was a gentle man akaaga akaondokaaa.
Kurudi Dar, akafunguka oooh Jolline mimi nina more intrests than being Friends. Mi nakutaka kimapenziii. Fast and foremost nimeoaaa, nina watoto kwenye ndoa, na couple of baby mamas, ila sisi wananume haturidhikiaaa, nimetokea kukutunukuuu. I prefer twende next level, cause hujaolewa na huna mtu anaekufunga, we can actually have fun!
Mmmmmmhhhh! Nikasema have fun???? Okay! Not a bad ideaaaa. Nikamwambia mie pia nimekuelewaaa ni hatariiii, i was afraid you aint gonna ask, lakini kama ulivosemaaa una mke unampendaa sanaa, na wanao. Mie sinaaa mumeee wala mfano wa mumeee. Na hii kazi ya kuwaburudisheni wanaume haina mirathi useme haupo nitarithi kitu, au nimestaafu kuna mafaooo, hakunaaa. Hii kazi ndo baba ndo mama. We mtu mkubwa sanaa nchiii hii mpaka raisi umshakaa naemeza moja mkagonga uongooo?
Oooh kweli kabisaaa. If you need anything ask, kama kuna political favor unahitaji just tell me baby huna haja ya kuzungukaaa. Kama ni nafasi ya mdogo wako utumishi, uhamisho, keshi, anything you want name it, its just one phone call away you have what you need. sipendi utesekeee kabisaaa. Moyoninikasemaaa nyoooo!
Nikampelembaa pale na kuamua kumuingia kwa gear namba 5, Mheshimiwaaa mi sihitaji vingi wala nini, nachoomba ni unipe tu PLOT YA KIWANJA GOBA!!!!!! Nataka nijengeee. I know you politicians you have tones and tones of land. Mnamiliki vijiji sasa mi hata miguu 20 kwa 20 tu inanitoshaaa. Sitaki mambo makubwa ya ma heka aunusu heka walaaaa! Najua wewe mtu mzitooo sanaaa, nakuaminiaaaa. Nitafurahiiii.
Watu wote mezani tukabakia Khaaaaaaaaaaaaaa!!!!!!!!!!!!!? Na kuuliza kwa mpigoo AKATOA? Akaendelea kunywa taratibuna kudakia. Atoe wapiiii. Alichosema apewe mda atalishuhulikia. Nikamwambia mie sina haraka, msaada hauna risitii. Akakaa kama wiki 2, akaja kupiga simu anadai tuonane Serenaaa sijui nini, nikampe mambo.
Nikamuuliza hati za kiwanja uko nazo hapo au inakuwaje? Yuko kiwanja badooo, we just talk. Anataka kuleta ujanja wa kizamaniii. Weeeeeeeeee! Akiingia huku na mimi natokea kuleee. Hatoi uwanja na mimi uchi sitoi ngooo. Basi akaamua kususaaaa. Siku nyege zikimshika anapiga simuuu. Hivo hivo ndo tunavoendaaaa.
Tulichokaaaa. Tukamuuliza sasa wewe kisa cha kumuomba mwenzio kitu kikubwa hivo nini? Kama humtaki si ungemwambiaaa tu, sikutakiii. Ndo nini sasa?
Akasemaa waziri ana mkeweee, anapost mapicha yuko south, yuko Dubai vacation na watoto, mara Paris, anakula bataaa kwenda mbelee, ana wanawake kawaweka kwenye vitengo nyetiii, ofisi nyetiii wanalipwa pesa ndefuuuu, sasa mimi wa kazi GANI? Yaani wooote wamenufaika kuwa nae afu mindo niwe wa KUKOPWA? thubutuuuuuuuuuuuu!
Hawa watu wakubwa wakikutongoza jipimeee tu, je anakuhitaji kwa kazi gani? Kama una thamani atajiongezaa, kama huna ndo ujijue mwajuma nile bureee, atakukula bure not that hana cha kukupa, ila kaamua tu hustahili kupewa lolote, wewe ni mkpo UNTD. We unadhani kashindwa kuninunulia plot Goba kwa 25m Mbona ndogo sanaa kwake? Yule Miss alimpa gari ya million 60. Wkaachana hajampokonya wala nini. Alikuwa ananijaribu, katoa jokeri na mi nimetoa jokeriii.
Tukashusha pumziiii. Jolline akaenda kukojoa, basi huku mdau akadakia, Jolline is hurt, aliumizwaaa sanaa sanaaa na Dulla, so hayuko poaaaa. Mzoeeeni tu. Kichwa yake imepata moto. Wakadakia Dulla ndo nani? Na alimfanya nini? Wakajibu Dulla, mjinga mmoja tu waarabu wa Upanga, alikuwa anashi na Jolline, na ndo alimwambia warudi toka UK cause Jolline hakupanga kurudi kabisaa, akamwambia arudi waoane, wakarudi wakawa wanaishi wotee, siku hio asubuhi Kapigiwa simu Dulla anaoa Upanga, wakati jana yake walilaa wote na mambo alimpaa. Wote tukawa na shauku ya kujua eeeh ikawaje?
Jolline akatokeaaa, ikabidi sasa zianze story zingine zingineee, ila wote mioyo inatuchukutaaa kutaka kujua ilikuwajeeee.
ITAENDELEA KESHO SAA 8 MCHANA